Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 64
Wakuu,
Kwa kifupi ATCL haikopesheki wala haiminiki kutokana na financials zake mbovu. Mi navyofahau mpaka mwaka jana walikua na accummulated loss of Tzs. 15 Billion.Tetesi zinasema they make more money kwenye kukodisha majengo kuliko kwenye mauzo ya air tickets.
Sasa hii kampuni haiwezi kuipa hiyo ndege bila kuwa na guarantee ya serikali ya Tanzania maana wanaogopa kuwa ATC wanaweza kushindwa kulipa hizo dola laki 5 kila mwezi. Kama ATCL ingekuwa ina cashflow nzuri na good financials, mibenki kibao ya bongo ingeweza kuwapa hiyo line of credit au Standby Letters of Credit(SBLC) ili kumpa aliyekodisha comfort.
Utamu unakuja pale ambapo BOT ndio wanatakiwa kuissue hiyo guarantee, na sasa hivi Prof. Ndullu anaangalia duka liko vipi maana Don Ballali alikuwa anazitoa kama nyungu hizo guarantees na nyingi zimetolewa kwenye project feki(ie Star Apparrel,Kagera Sugar,Mtibwa Sugar, Mzindakaya Meat Farm etc)
Kikwete anamwogopa Chenge big tyme na usishangae mabilioni yakatumika hapa kama kawa huku Chenge akicheka all the way to the bank!