According to the dataz, Chenge sasa yupo London akiwa chini ya ulinzi wa makachero wa UK, akiwasaidia kuhusiana na uchugnuzi wa Radar. Habari nyeti nilizozipaata jana ni kwamba Chenge aliondoka kwa siri hapa nyumbani bongo kuelekea London, majuzi usiku ambako alikuwa akitakiwa kisheria na wachunguzi wa huko ambao ndio walioibua kashfa ya zile "Vijisenti". Huko London, alipokewa na makachero hao mara tu alipofika kwenye uwanja wa ndege, ambao walimpokea na kutokomea naye kusikojulikana.
According to more dataz, ni kwamba Muungwana was approached na makachero hao wa UK, hata kabla ya kikao cha CCM Butiama, na kwamba hata alipokuwa anachagua baraza la mawaziri tayari alikuwa anazo habari za Chenge na "Vijisenti", lakini hakutaka pupa. Dataz hizo zinasema kuwa hata kabla ya kwenda India, muungwana alikuwa tayari ameshawapa makachero wa UK, kibali cha maandishi cha kumshika, na kum-search Chenge, as much as they wanted or see fit!
Kabla ya kwenda Butiama, Chenge was approached na makachero hao wa UK lakini akawajibu kijeuri sana kuwa yeye ni mtu mkubwa sana hawezi kutishwa na wakoloni, ndipo wazungu walipomuonyesha warrant maalum iliyoandikwa na kusainiwa na Muungwana, Chenge almost fainted, lakini akakubali na kuchukuliwa na makachero hao, walioi-search nyumba yake upside down kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa mbili suiku, na kupata ushahidi mwingi waliokuwa wakiutafuta na kuondoka nao, na muungwana alimpa order ya kuendelea kuwasaidia hadi watakapomaliza uchunguzi wao, na baada ya kujiuzulu Chenge aliambiwa ajitayarishe kwenda UK kushiriki kwenye kuwasaidia zaidi makachero hao wakizungu, ambako ndio alienda rasmi majuzi na yuko huko bado.
Halafu dataz zaidi pia zinasema kuwa mapesa mengi na mali za mafisadi zimeszuiwa na serikali kwa siri kubwa sana, the matter of fact hata nyumba za mafisadi wengi zilizoko SA ikiwemo ya Mkapa pia zimeshikwa na serikali tayari, ikiwa ni pamoja na mapesa yao yote yaliyopo hapa bongo.
Mafisadi wengi wamejaribu kumfuata Mkono ili awasadie, akiwemo Chenge pia, lakini according to the dataz hata Mkono amewaruka wote, baada ya kupewa a very strong warning na muungwana kuwa akae mbali nao, now mnyonge anyongwe, lakini haki apewe on this.
....More Dataz to Come Soon....
Es
Pamoja na habari hizi mimi sioni sababu ya JK kuficha kile ambacho anakifanya, yeye amepewa dhamana na WTZ kwa nini kufichaficha mambo kama haya na kwa nini hao makachero wa UK wasingemuhoji Bongo? Chenge ni raia wa Tz wao wangefanya upelelezi hapa hapa nyumbani hii kasumba ya kuwatosa raia wetu kwa hawa waingereza tumeipata kutoka wapi? Uhalifu huu umetokea Tanzania na ni jukumu la serikali ya Tanzania kumshitaki Chenge na kundi lake lote la wezi na Mafisadi kwa sheria zetu.
Je Jakaya anaogopa nini kutangaza haya ambayo ameyafanya? Mali yetu ndio inateketea na rasilimali ya Tanzania hawa Waingereza wanaangalia maslahi yao hawawezi hata siku moja kutetea maslahi yetu.
Je, ni lini tutawashikisha adabu hawa wezi kutoka nje ambao wanashirikiana bega kwa bega na wazaledo?
BTW tunasubiri kuona Che-Nkapa, EL, Karamagi, Mramba na wezi wengine wote koko wanashitakiwa kwa sheria zetu.
Mkuu hii nimeipenda,msikonde JK anatupeleka Sinai kwa mbwembwe tukale mkate kwa asali
Sijui kama kuna kesi hapo. Sifahamu international law lakini can someone tell us kama UK wana jurisdiction ya hiyo kesi. I don't see the legel aspects kwenye hiyo kesi, they can't lock him down.
The only thing watakachofanya ni kumtumia ili kuwaprosecutes watu wao. I need more explainations kwenye legel aspects ya hili swala.
Lord Justice Moses and Lord Justice Sullivan ruled that the SFO had betrayed the rule of law when his predecessor, Robert Wardle, allowed a foreign potentate, Prince Bandar of Saudi Arabia, to dictate that its bribery investigations into him should be called off.
17 March 2008
NEW DIRECTOR OF THE SERIOUS FRAUD OFFICE APPOINTED
[The following press release has been issued by the Attorney General's Office today]
The Attorney General, the Rt. Hon Baroness Scotland QC, has appointed Richard Alderman to be Director of the Serious Fraud Office. Mr Alderman will succeed the present Director, Robert Wardle, on 21 April 2008.
Mr. Alderman is currently the Director of the National Teams and Special Civil Investigations at HM Revenue & Customs.
In making the appointment the Attorney General said: I am delighted to announce the appointment of Richard Alderman. I look forward to working with him and I am sure all at the Serious Fraud Office are delighted that someone with such experience and strong expertise in complex fraud investigations, including notable work at Her Majesty's Revenue and Customs, will be leading them in to the future.
Kwani si tuliambiwa chenge ni shahidi tu, sasa kwa nini akamatwe?
Sifahamu international law lakini can someone tell us kama UK wana jurisdiction ya hiyo kesi. I don't see the legel aspects kwenye hiyo kesi, they can't lock him down
The only thing watakachofanya ni kumtumia ili kuwaprosecutes watu wao. I need more explainations kwenye legel aspects ya hili swala.
lots of reasons to be skeptical - one of them: JK hana ujasiri moyoni wa kihivyo - running roughshod treatment to mafisadi! I wish this was the case.
I will be devils advocate hapa...
Najua Chenge inabidi achnguzwe lakini hivi sisi tunayo extradition treaty na UK? Je Chenge alipata legal representative? Je na sisi tukitaka kumhoji aliyekuwa waziri wa DFID wana Hilary Benn kuhusus kasfa za ma consultants wa kiingereza walivyochoata pesa Tanzania serikali ya UK itakubali?
Ndio I am all for wanaotuhumiwa kuchunguzwa lakini nina wasi wasi namna MUUNGWANA aka JK aka ZE COMEDY alivyowapa SFO carteblanche huko Tanzania
kutokana na mentality ya baadhi ya wana JF this will be good news na sitoshangaa watakavyokuja kushangilia hili bila kuuliza hard questions
Mmh, ES nikitumia ruga ya nyumbani nitasema "wakora" tata ingawa chumvi na pili pili vimefanya Matoke na Rubisi zikolee na kuonekana kama ni kitu kimoja.
Lakini ukiangalia scenario zote hizo mbili, sidhani kama Serikali ya URT (United Republic of Tanzania) ilikuwa inamhisi mtu yeyote katika Serikali yake kuhusika na "uhujumu" au kushiriki katika "rushwa" ya Radar hii.
- SFO wanafanya uchunguzi wao kwa manufaa ya Uingereza dhidi ya BAE ili kujua na mwishowe kuwaadhibu/kuliadhibu BAE kwa kutumia rushwa katika miradi yake na mauzo ya silaha zake. Radar ya Tanzania ni sehemu ndogo ya "uhujumu" na "Rushwa" ambazo BAE wanatuhumiwa kuzifanya. Tunajua SFO wanachunguza jinsi BAE walivyouza silaha Saudia Arabia, Tanzania, South Africa na nchi nyingine kwa kutoa hongo ili bidhaa zao zinunuliwe. Chenge yeye ni shahidi kwa niaba ya SFO na si mtuhumiwa (kwa sasa). Amepelekwa Uingereza ili akatoe maelezo upya na ya ziada ili SFO wajue ni nani kutoka BAE na serikali ya Blair walihusika na rushwa hii. Sasa wakishamaliza uchunguzi wao, na kesi kupelekwa mahakamani, Chenge anaweza kuwa shahidi na hata kuwa mtuhumiwa ikiwa ni kweli yeye alihusika kikamilifu kuchonga hiyo dili ya rushwa na zaidi ikiwa yeye ndiye mhusika mkuu kwa upande wa Tanzania.
- Serikali ya Tanzania na Takukuru, hawafanyi uchunguzi wowote kuhusu Radar na mazingira ya rushwa yaliyohusika. Serikali ya URThaimchunguzi Chenge au watanzania wowote waliohusika na hili suala la Radar. Serikali yetu inasubiri kulipwa "fidia" au kizungu tunasema refund ya kuuziwa Radar kwa bei zaidi ya ile bei halali. Kwa kauli za viongozi wetu na hasa "Kisura", sidhani kama Serikali ya URT ilikuwa na nia yeyote kufanya uchunguzi kuhusiana na suala hili zima la Radar na mazingira yake. Serikali yetu imelifanya tatizo hili kuwa ni la UK na si Tanzania. Tanzania inasubiri maafisa wa BAE wawekwe ndani na hukumu itolewe, ndipo Serikali i-idai Serikali ya Uingereza refund kwa "overpayment".
Kutajwa kwa Chenge katika kesi hii kama shahidi na huko tunaokoelekea kuwa ni mtuhumiwa bado hakujaiamsha Serikali kwa makini ianze kufuatilia na kuchunguza mikataba yote ambayo iliingia wakati Chenge akiwa Mwanasheria Mkuu na ama aliidhinisha au aliandika mikataba hii.
Ndio maana sishangai tena kwa yeye Chenge kurudi Bariadi kwa madaha na mbwembwe, kwa kuwa hakuna uchunguzo wowote unaofanya na Serikali yetu. Sisi tunasubiri Waingereza wakamilishe kesi yao, ndipo tutangazie umma kuwa "tulidhulumiwa" wakati ni sisi wenyewe tumejidhulumu kwa Chenge kupokea rushwa ili Tanzania iuziwe hiyo rada kwa bei mbaya.
Nisichokielewa ni hili, kwa nini BAE walikuwa tayari kutoa rushwa ya $12m ili Radar inunuliwe. Je ni nani kwa suala la Tanzania walipokea rushwa hiyo? Tunajua dalali Vithlani ana mgawo wake, sasa Chenge naye ana mgawo, je ni nani hao wengine waliobakia? je ni maafisa na watendaji wa BAE? Ni maafisa na viongozi wa Serikali ya Uingereza? je kuna maafisa na viongozi wengine wa Serikali ya Tanzania ambao wamo ndani ya huo "mugawo"?
Chege pamoja na kuwa ni shahidi kwa kesi ya Serikali ya UK dhidi ya BAE, anaweza kuwa mtuhumiwa katika kesi hiyo na pia anaweza kushitakiwa na Serikali ya Tanzania katika mahakama zetu kwa kujihusisha na rushwa. Hili la yeye kushitakiwa na Serikali ya URT litawezekana ikiwa Serikali ya URT itaamua kufanya uchunguzi wake na hata kutokana na matokeo ya uchunguzi wa SFO, Tanzania iamue kuwafikisha mahali pao wale waliohujumu kwa makusudi mambo ya mkataba huu wa kununua Rada.
La mwisho, ni kwa nini Tony Blair na sasa Brown wanaelekea kushinikiza SFO waachane na uchunguzi? je ni kuficha makucha yao ya ulaji rushwa au ni kuogopa kujulikana kuwa Serikali yao na makampuni yao bado yanatumia rushwa ili kujiimarisha kibiashara?
Au ni kweli wamedindiwa na Saudi Arabia ambao wametishia kusitisha kufanya biashara na mahusiano ya kijeshi na ulinzi kama SFO wataendelea na uchunguzi ambao utaonyesha kwa dunia nzima (na hasa Ali Keda) kuwa nyumba Saud (mfalme na familia) ni wala rushwa na si safi na bora kuongoza nchi ambayo ni makao na nyumba ya Mtume Mohamed SAW?
Halafu pia kuna the X-factor wa hizi kesi zote zinazowahusu mafisadi, anaitwa Mary Kejo ninataka kuamini kuwa anayajua yanayokaribia kumkuta hivi karibuni.........!