The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

This seems to be the reasonable analysis ya kinachotokea huko majimboni.

Inakuwa vigumu kuamini kuwa watanzania ni wajinga kabisa kabisaaa na kushindwa kuona ukweli wa mafisadi kama wanavyotakiwa kuonwa.

Mtizamo huu ni tumaini kuwa wanajamii wanaamka na pengine kuna mwelekeo sahihi toka kwao.

Kwani ni kwa wanajamii wenyewe kuona hali halisi na ukweli wote bila kutegemea viongozi waliopo na hasa hawa waliojiuzulu kuwaonyesha cha kuonwa kwani almost all of them wameshaadhirika.
 
According to the dataz, Chenge sasa yupo London akiwa chini ya ulinzi wa makachero wa UK, akiwasaidia kuhusiana na uchugnuzi wa Radar. Habari nyeti nilizozipaata jana ni kwamba Chenge aliondoka kwa siri hapa nyumbani bongo kuelekea London, majuzi usiku ambako alikuwa akitakiwa kisheria na wachunguzi wa huko ambao ndio walioibua kashfa ya zile "Vijisenti". Huko London, alipokewa na makachero hao mara tu alipofika kwenye uwanja wa ndege, ambao walimpokea na kutokomea naye kusikojulikana.

According to more dataz, ni kwamba Muungwana was approached na makachero hao wa UK, hata kabla ya kikao cha CCM Butiama, na kwamba hata alipokuwa anachagua baraza la mawaziri tayari alikuwa anazo habari za Chenge na "Vijisenti", lakini hakutaka pupa. Dataz hizo zinasema kuwa hata kabla ya kwenda India, muungwana alikuwa tayari ameshawapa makachero wa UK, kibali cha maandishi cha kumshika, na kum-search Chenge, as much as they wanted or see fit!

Kabla ya kwenda Butiama, Chenge was approached na makachero hao wa UK lakini akawajibu kijeuri sana kuwa yeye ni mtu mkubwa sana hawezi kutishwa na wakoloni, ndipo wazungu walipomuonyesha warrant maalum iliyoandikwa na kusainiwa na Muungwana, Chenge almost fainted, lakini akakubali na kuchukuliwa na makachero hao, walioi-search nyumba yake upside down kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa mbili suiku, na kupata ushahidi mwingi waliokuwa wakiutafuta na kuondoka nao, na muungwana alimpa order ya kuendelea kuwasaidia hadi watakapomaliza uchunguzi wao, na baada ya kujiuzulu Chenge aliambiwa ajitayarishe kwenda UK kushiriki kwenye kuwasaidia zaidi makachero hao wakizungu, ambako ndio alienda rasmi majuzi na yuko huko bado.

Halafu dataz zaidi pia zinasema kuwa mapesa mengi na mali za mafisadi zimeszuiwa na serikali kwa siri kubwa sana, the matter of fact hata nyumba za mafisadi wengi zilizoko SA ikiwemo ya Mkapa pia zimeshikwa na serikali tayari, ikiwa ni pamoja na mapesa yao yote yaliyopo hapa bongo.

Mafisadi wengi wamejaribu kumfuata Mkono ili awasadie, akiwemo Chenge pia, lakini according to the dataz hata Mkono amewaruka wote, baada ya kupewa a very strong warning na muungwana kuwa akae mbali nao, now mnyonge anyongwe, lakini haki apewe on this.

....More Dataz to Come Soon....
 
Sioni sababu ya kumpa JK point kwa hatua za sasa ambazo ni za awali ,akichukua hatua basi ataweza kupewa haki yake , kwani kuonyesha nia na kutenda ni vitu viwili tofauti sana.

Amehojiwa ni kweli na pia wapo watu waliowasaidia makachero hao kuwaonyesha baadhi ya mali za Chenge Bongo pamoja na jijini mwanza na hata kule Arusha alikoandikisha mali hizo kwa jina la mkewe.
 
Asante sana Mkuu ES .Leo nilikuwa najiuliza ES yuko wapi sasa mbona hasemi lolote kuhusu wapemba kukamatwa ? Mara umeibuka .Hii ni habari nyeti wacha niingie mtaani kujua kulikoni na kunani .
 
lots of reasons to be skeptical - one of them: JK hana ujasiri moyoni wa kihivyo - running roughshod treatment to mafisadi! I wish this was the case.
 
I will be devils advocate hapa...

Najua Chenge inabidi achnguzwe lakini hivi sisi tunayo extradition treaty na UK? Je Chenge alipata legal representative? Je na sisi tukitaka kumhoji aliyekuwa waziri wa DFID wana Hilary Benn kuhusus kasfa za ma consultants wa kiingereza walivyochoata pesa Tanzania serikali ya UK itakubali?

Ndio I am all for wanaotuhumiwa kuchunguzwa lakini nina wasi wasi namna MUUNGWANA aka JK aka ZE COMEDY alivyowapa SFO carteblanche huko Tanzania. Kama unayosema ES ni kweli then hii ngoma ni nzito kwani kuna mengi tuu kuhusus SFO ambayo yenyewe credibility yao iko questionable

Anyway hizo ni two cents zangu lakini kutokana na mentality ya baadhi ya wana JF this will be good news na sitoshangaa watakavyokuja kushangilia hili bila kuuliza hard questions
 
Muungwa akifanikiwa atakuwa ameongeza kura moja kutoka kwangu 2010

Akifanikiwa kufanya kitu gani? huu ni uchunguzi wa waingereza wanataka kuwachukulia hatua watendaji wa BAE waliohusika na huyu ni shahidi tuu kuwa alipewa kitu kidogo vijisenti.

JK kama anataka awaamuru TAKUKURU =ILE Taasisi ya Kulea na Kubatiza Rushwa / imfungulie mashtaka .
 
Hiyo sasa ishu....mungwana lazima anyooshe makucha yake lasivyo wadau watajua anadeal nao..lazima awatose.Ili aweze kuaminika kwa wananchi kwani wameanza kukosa imani nae.
Kama haya maneno ni ya kweli basi hatua imepigwa zidi ya mafisadi,
 
Hiyo sasa ishu....mungwana lazima anyooshe makucha yake lasivyo wadau watajua anadeal nao..lazima awatose.Ili aweze kuaminika kwa wananchi kwani wameanza kukosa imani nae.
Kama haya maneno ni ya kweli basi hatua imepigwa zidi ya mafisadi,

Hapa hakuna hatua kwani SFO wanafanya kwa ajili ya kuwachukulia hatua watendaji wao , huyu ni shahidi tuu wa kesi hiyo, tuendelee kuamini kuwa JK anaweza kumtosa Mkapa? kwani hili dili mzee na mramba yule aliyetishia kuwa wakimwaga mboga anamwaga ugali yumo.
 
Great, but there isn't much to be cheerful about

Habari njema hizi. It sends a strong signal to all mafisadi nchin mwetu.

Lakini hatuna sababu ya kujimwagia sifa sisi maana hao SFO wanafanya kazi ya nchi yao na wala sisi hatukuwatuma. Hii ndio kusema kama wizi huo ungekuwa haujagusa maslahi ya UK na kama usingehusisha kampuni ya UK akina Chenge wasingeguswa kama vile ambavyo tumeshindwa kuwagusa wale majambazi wa pesa za EPA. Pengine credit pekee aliyo nayo JK ni kutoweka vizuizi vya huyu bwana kuchunguzwa. Hata hivyo sijui kama alifanya hivi kwa kuwa anakerwa na ujambazi wa fedha za nchi yetu au kwa kuogopa kwamba kuzuia uchunguzi huu ungeharibu uhusiano wa nchi yetu na UK na kwamba aliogopa nchi yetu kunyimwa misaada na hawa jamaa ambao yeye huwaita "bwana mkubwa".

Hii pia inatukumbusha udhaifu mkubwa uliopo miongoni mwa vyombo vyetu vya kusimamia usalama wa taifa na sheria za nchi. So, miaka miwili ambayo JK amebakisha angejitahidi kutumia mamlaka aliyo nayo kuona kwamba vyombo vyetu hivi vinaimarika kiutendaji na kitaasisi. Ni aibu kwamba aliyekuwa waziri wetu anakuja kusachiwa na makachero wa Uingereza!
 
Mkuu Field Marshal ES,

Na wakuu wengieneo,

Hii habari ni nyeti sana na SFO wamepania kuhakikisha wanaondoa jeuri zote kuhusiana na mambo haya.

Ikumbukwe kwamba SFO ni moja ya organs za Usalama wa UK lakini jukumu lao likiwa ni kushughulikia masuala yote ya UFISADI na hasa FRAUD.

Katika moja ya funtions zake kimataifa wanaeleza kama ifuatavyo, nanukuu,

International fraud prevention.

To combat fraud, criminal justice authorities around the world share information and use their national powers to help each other.

Approximately 65% of our cases have an international dimension. National borders rarely prove to be barriers to determined fraudsters. Money is channelled through overseas banks and offshore companies, victims can reside anywhere in the world and suspects and evidence can hide behind the laws of different jurisdictions. The unscrupulous try to exploit the size and reputation of the UK financial markets to disguise their criminal activities and launder the proceeds of their crimes. mwisho wa kunukuu


Halafu pia hawa jamaa huwa kabla ya kushughulikia kesi kama hii huwa wanaangalia vitu kama ifuatavyo:

Je value ya fraud imezidi £1 million?
Je kuna international dimension?
Je kesi inaweza kusababisha widespread public concern?
Je kesi inahitaji highly specialised knowledge, e.g. of financial markets?
Na mwisho kuna haja ya kutumia SFO's special powers, such as Section 2 of the Criminal Justice Act?


Kwa hio hapa Chenge anaweza akaorodhesha watu wote waliohusika na ndio songombingo litakapoibuka.

Na tusubiri.

Halafu mkuu GT wewe unaelewa mfumo wa sheria wa UK lakini inategemea unamaanisha nini kuhusu CREDIBILITY ya hawa jamaa-SFO

Kumbuka hawa pesa wanayopewa inatosha kukidhi maisha yao. Waache wafanye kazi yao.
 
Jibu analo Gigo...
Kosa lenu Mme mfungia....!!Sasa Mbona wano fanya kazi ni Genius wa nje...--
how wakwenu hamwapi kazi-
 
Kama JK kafanya hivyo, kura ndio kwanza zipungue maana yeye ni amirijeshi mkuu, vyombo vyote vya dola viko chini yake, idara ya polisi, magereza, TAKUKURU nk ana mamlaka navyo, yaani anaifanya nchi ni tegemezi hadi kushughulikia waarifu (sorry- watuhumiwa)!!!
 
I will be devils advocate hapa...

Najua Chenge inabidi achnguzwe lakini hivi sisi tunayo extradition treaty na UK? Je Chenge alipata legal representative? Je na sisi tukitaka kumhoji aliyekuwa waziri wa DFID wana Hilary Benn kuhusus kasfa za ma consultants wa kiingereza walivyochoata pesa Tanzania serikali ya UK itakubali?

Ndio I am all for wanaotuhumiwa kuchunguzwa lakini nina wasi wasi namna MUUNGWANA aka JK aka ZE COMEDY alivyowapa SFO carteblanche huko Tanzania. Kama unayosema ES ni kweli then hii ngoma ni nzito kwani kuna mengi tuu kuhusus SFO ambayo yenyewe credibility yao iko questionable

Anyway hizo ni two cents zangu lakini kutokana na mentality ya baadhi ya wana JF this will be good news na sitoshangaa watakavyokuja kushangilia hili bila kuuliza hard questions

GT hizi arguments zako nyingine are they meant to apply in our REAL WORLD or they are just for academic and intelectual fanfare? ni kama kuuliza kwa nini Iraq isiwachukulie hatua CIA au Afghanistan isifanye hivyo...man..ndo maana nasema itatuchukua mda waafrika kukombolewa na wasomi kama akina GT..they are so intelectually higher up there, but too abstract in their thinking..hence unable to connect to the real word of common men and women.

Otherwise its agood argument for the forum!
 
Es

Pamoja na habari hizi mimi sioni sababu ya JK kuficha kile ambacho anakifanya, yeye amepewa dhamana na WTZ kwa nini kufichaficha mambo kama haya na kwa nini hao makachero wa UK wasingemuhoji Bongo? Chenge ni raia wa Tz wao wangefanya upelelezi hapa hapa nyumbani hii kasumba ya kuwatosa raia wetu kwa hawa waingereza tumeipata kutoka wapi? Uhalifu huu umetokea Tanzania na ni jukumu la serikali ya Tanzania kumshitaki Chenge na kundi lake lote la wezi na Mafisadi kwa sheria zetu.

Je Jakaya anaogopa nini kutangaza haya ambayo ameyafanya? Mali yetu ndio inateketea na rasilimali ya Tanzania hawa Waingereza wanaangalia maslahi yao hawawezi hata siku moja kutetea maslahi yetu.

Je, ni lini tutawashikisha adabu hawa wezi kutoka nje ambao wanashirikiana bega kwa bega na wazaledo?


BTW tunasubiri kuona Che-Nkapa, EL, Karamagi, Mramba na wezi wengine wote koko wanashitakiwa kwa sheria zetu.
 
Back
Top Bottom