Freeman A. Mbowe
New Member
- Dec 2, 2006
- 2
- 36
Salaam Wana JF.
Kwanza kabisa naomba niwapongeze wale walioanzisha forum hii kama sehemu ya matumizi ya uhuru wao binafsi. Aidha, niwapongeze kwani forum hii ni sehemu ya harakati muhimu ya kujadili mustakabali wa nchi yetu.
Nimesoma maoni, pongezi, malalamiko, hofu, ushauri na mambo mengine kadhaa katika forum hii. Nimejadiliwa mara kadhaa katika hoja tofauti. Nawapongeza wote waliochangia mada zilizonihusu hata kama wamenipinga au kuzusha. Nitoe pongezi zaidi kwa wale walioonyesha kuipenda nchi yetu na kuitakia mema kwa mijadala mbalimbali.
Leo naandika kwenye forum hii kwa mara ya kwanza. Siyo kusudio langu kujibu hoja zinazonihusu moja kwa moja. Aidha, siyo nia yangu kuingia kwenye malumbano ya aina yeyote na wachangiaji. Naheshimu sana uhuru na mawazo ya wote hata kama kwa makusudi au bahati mbaya yanapotosha. Binadamu tunatofautiana katika fikra, uelewa na malengo.
Siasa na uongozi wa Taifa letu vina mahusiano ya moja kwa moja na maisha yetu ya kila siku.Tanzania ni nchi yetu sote. Hatuna sababu ya kufanya masihara na siasa wala viongozi wetu wote. Walio madarakani na wale wenye nia hiyo.
Mara nyingi, binadamu ni wepesi wa kulaumu na kuhukumu. Tunapenda kadhalika, kudai haki pengine bila kutafakari kwa kina tumetekeleza wajibu wetu kwa kiasi gani.
Tupende tusipende, Tanzania ina kilio. Wote tusipojiuliza na kutekeleza wajibu wetu, kila mtu na nafasi yake kukabiliana na msiba huu, kamwe kilio hakitaisha. Muda wetu wa kuishi maisha haya ni mfupi sana na kila mmoja wetu anastahili kujiuliza amechangia nini katika wajibu wa kumaliza msiba huu?
Naamini, tatizo kubwa la kwanza la kukabiliana nalo nchini mwetu ni WOGA na HOFU. Naamini Wana Jambo forum wengi ni watu wenye uelewa wa kutosha. Kwa nchi yetu iliyo hoi kielimu na hata kiuwezo, hawa ni watu wa "kutumainiwa" na familia zao na hivyo nchi yao kwani familia ni sehemu ya nchi. Napenda kuamini ni sehemu ya "cream" ya Taifa letu nanyi kwa kutoa mawazo yenu, mmekuwa sehemu ya harakati.
Nasikitika, wengi wa wana forum wanatumia majina yasiyo ya kweli. Sina hakika kama siyo ishara ya woga! Na kama wasomi, waelewa, wenye upeo wanakuwa hivyo, Watanzania wa kawaida wategemewe wawe vipi? "Authenticity" ya tunayoyaandika inafifishwa na hali hii?
CHANGAMOTO: KWA KUFICHA MAJINA YETU UJASIRI WETU WA KUHOJI, KULAUMU NA KUHUKUMU UNAPINGANA NA DHAMIRA YA HARAKATI? HARAKATI NA WOGA VINAENDANA? WOGA UNAWEZA KUOKOA TAIFA?
By concealing our identity, are we truly living to our motto which says "Where we dare talk openly?"
"The only thing we have to fear is fear itself" - President Franklin Delano Roosevelt, Washington DC, 4th March 1953
Nawashukuru na naomba kutoa hoja!!
Freeman Mbowe