The Only Thing We Have to Fear is Fear itself

Freeman A. Mbowe

New Member
Dec 2, 2006
2
36
Salaam Wana JF.

Kwanza kabisa naomba niwapongeze wale walioanzisha forum hii kama sehemu ya matumizi ya uhuru wao binafsi. Aidha, niwapongeze kwani forum hii ni sehemu ya harakati muhimu ya kujadili mustakabali wa nchi yetu.

Nimesoma maoni, pongezi, malalamiko, hofu, ushauri na mambo mengine kadhaa katika forum hii. Nimejadiliwa mara kadhaa katika hoja tofauti. Nawapongeza wote waliochangia mada zilizonihusu hata kama wamenipinga au kuzusha. Nitoe pongezi zaidi kwa wale walioonyesha kuipenda nchi yetu na kuitakia mema kwa mijadala mbalimbali.

Leo naandika kwenye forum hii kwa mara ya kwanza. Siyo kusudio langu kujibu hoja zinazonihusu moja kwa moja. Aidha, siyo nia yangu kuingia kwenye malumbano ya aina yeyote na wachangiaji. Naheshimu sana uhuru na mawazo ya wote hata kama kwa makusudi au bahati mbaya yanapotosha. Binadamu tunatofautiana katika fikra, uelewa na malengo.

Siasa na uongozi wa Taifa letu vina mahusiano ya moja kwa moja na maisha yetu ya kila siku.Tanzania ni nchi yetu sote. Hatuna sababu ya kufanya masihara na siasa wala viongozi wetu wote. Walio madarakani na wale wenye nia hiyo.

Mara nyingi, binadamu ni wepesi wa kulaumu na kuhukumu. Tunapenda kadhalika, kudai haki pengine bila kutafakari kwa kina tumetekeleza wajibu wetu kwa kiasi gani.

Tupende tusipende, Tanzania ina kilio. Wote tusipojiuliza na kutekeleza wajibu wetu, kila mtu na nafasi yake kukabiliana na msiba huu, kamwe kilio hakitaisha. Muda wetu wa kuishi maisha haya ni mfupi sana na kila mmoja wetu anastahili kujiuliza amechangia nini katika wajibu wa kumaliza msiba huu?

Naamini, tatizo kubwa la kwanza la kukabiliana nalo nchini mwetu ni WOGA na HOFU. Naamini Wana Jambo forum wengi ni watu wenye uelewa wa kutosha. Kwa nchi yetu iliyo hoi kielimu na hata kiuwezo, hawa ni watu wa "kutumainiwa" na familia zao na hivyo nchi yao kwani familia ni sehemu ya nchi. Napenda kuamini ni sehemu ya "cream" ya Taifa letu nanyi kwa kutoa mawazo yenu, mmekuwa sehemu ya harakati.

Nasikitika, wengi wa wana forum wanatumia majina yasiyo ya kweli. Sina hakika kama siyo ishara ya woga! Na kama wasomi, waelewa, wenye upeo wanakuwa hivyo, Watanzania wa kawaida wategemewe wawe vipi? "Authenticity" ya tunayoyaandika inafifishwa na hali hii?

CHANGAMOTO: KWA KUFICHA MAJINA YETU UJASIRI WETU WA KUHOJI, KULAUMU NA KUHUKUMU UNAPINGANA NA DHAMIRA YA HARAKATI? HARAKATI NA WOGA VINAENDANA? WOGA UNAWEZA KUOKOA TAIFA?

By concealing our identity, are we truly living to our motto which says "Where we dare talk openly?"

"The only thing we have to fear is fear itself" - President Franklin Delano Roosevelt, Washington DC, 4th March 1953

Nawashukuru na naomba kutoa hoja!!

Freeman Mbowe
 
Mheshimiwa Mbowe:

Naandika hii nikiwa naamini wewe kweli ni Mh. Mbowe. Nadhani kwanza nikukaribishe. Karibu sana bodini. Nilivyokuelewa umetoa changamoto kwa wanabodi humu watumie majina yao ya kweli. Hilo silo lengo letu humu. Nadhani hata wewe nikikuuliza kuna viongozi wangapi wa upinzani waliorudi CCM kwa kutopenda unaweza ukanijibu hilo swali. Kutumia majina yetu yasiyo ya kweli kunaweza kuwa ni uoga bali ni uoga wa maendeleo. Watu waliomo humu ndani wengi wana connections na viongozi wa serikali kwa kutumia majina yao kutawafanya wawe limited na utoaji wa mawazo yako.

Kuna watu ambao wako usalama wa taifa wameamua kusaliti masharti ya kazi zao na kuamua kuchangia humu ndani. Huo ni uoga ambao unakubalika katika jamii. Lakini zaidi ya yote lengo la hii forum siyo kutafuta marafiki au kuunda chama cha siasa, hapa tunakata issue bila kujali unaamini nini au wewe unaitwa nani.

Kwa mfano, wewe mwenyewe ulinukuliwa na vyombo vya habri ukisema Richmond inauhusiano na mmoja wa watoto wa vigogo lakini hukumtaja jina na sidhani kama uko tayari kutaja jina humu ndani hata kama ni kweli, huo ni uoga ambao unaruhusiwa wewe ukiwa kama Mbowe. Unatambua madhara yake vizuri sana. Ila ukiwa kama Fikiraduni au DrWho unaweza kulitaja na tukajadili ukweli wa madai yako.

Anyway, this is sam mmoja wa seniors kwenye hii forum. Karibu sana.
 
Freeman Mbowe


Thanks for joining us

Maswali machache tu.

Unapokuwa na njaa na kuomba chakula ukipewa huuliza nani amekitoa? Utakula baada ya kushiba ndio utaanza kutafakari nani alikupa kile chakula etc.

Tanzania leo hii kuna matatizo lukuki hata wabunge wanaambiwa wafyate mkia kuuliza maswali ambayo ni ya msingi kutoka majimboni kwao na wanakubali. (maswala ya umeme n.k. hata opposition walinyamaza)

Sasa je watu wadogo ambao hata sio wabunge wanawezaje kujiweka hadharani kuuliza, maana bado tuna wasiwasi ikiwa hata rais tuliyemchagua anaogopa kutoa majina hadharani ya wauza unga? Pamoja na kashfa kibao za mikataba?

Tujibiwe maswali yetu halafu tukifika mahali kila mtu anajiona yuko free kueleza mawazo yake bila kubughudhiwa na vyombo vya usalama tutaweka majina yetu. Tanzania ikishashiba ianze kuuliza nani aliuliza lipi?

Vilevile labda unasahau forum ya kwanza ilisambaratishwa kwa kutoa ukweli, je kwa maana hiyo tutafika kweli?

Wabunge maswali yapo mengi tu ya msingi yameelekezwa kwenu hapa kwenye hii forum mbona hamjafuatilia? Au ndio EL na JK wamewaweka mfukoni?
 
Mheshimiwa Mbowe:

Kwanza napenda kukukaribisha kwenye Jambo Forums,kwani ndio sehemu pekee unayoweza kupata ukweli wa dhati kuhusu masuala yote muhimu yanayohusu maendeleo ya Nchi yetu na watu wake!.Mimi ni mgeni mno humu,lakini kwa kipindi kifupi tu,nimeweza kujua mengi hata kuliko nilipokuwa ndani ya serikali na sehemu nyeti ya "Usalama".Nimetoa mwaliko kwa waliopo serikali pia waingie humu ndani ili waone "Uzuri na uozo" wa sekta mbalimbali za umma.

Waliokwishapita humu wameniambia kwamba kweli "Jambo" ni kiboko!. Napenda kukuthibitishia tu, kwamba, kinachosemwa humu kipo! Kkwa maana hiyo kila thread ina manufaa kwa jamii husika.Kuja kwako humu ni kioo kingine ktk kupambanua mambo yanayotokea kwenye Taifa letu Gonjwa (Tuna miaka 45 lakini bado tunatambaa).

Tunaomba ujadiliane kwa hoja na sio nguvu wala Ubabe,tunahitaji sana hekima yako humu! Tuelimishe na pambanua kila unalolijua kwa kina,nawe kubali kukosolewa na kuelekezwa.

Nina Imani ipo siku tutaijenga Tanzania kwenye misingi ya Uwazi,Haki, Ukweli na Uhuru wa vyombo vya Habari bila kusifu au kupendelea wanaotuongoza!Kusifu tu bila kukosoa kunapotokea makosa hiyo sio ethic ya uwanahabari. Angalia suala zima la Richmond limefumbiwa macho na kila aliyekuwa madarakani,sasa nani atawapa ukweli wapiga kura?

Karibu Mzee hapa Kijiweni!
 
Mheshimiwa Freeman,
Karibu sana kwenye forum yetu. Kama alivyosema Sam, woga wetu wa kutumia majina bandia si woga wa kusema ukweli.Kwa mfano, kama wewe utajua my true identity labda kitu utakachofanya ni kucheka. Lakini that is not the point. Kivuli hichi cha undercover kinatupa sisi wengine ambao kwa kweli ni "high profile" uwezo wa kusema tunachokiona bila hofu . Kwa hiyo ni wogo positive na si woga woga. Karibu sana!
 
Mbowe karibu sana .

Kwa kuanza tu tafadhali katika nia ile ile ya kutaka kujenga Tanzania , tunaomba ujibu kwa jini hata Upinzani uko kimya sana juu ya maswala ya Richmond ?

Asante
 
mheshimiwa mbowe karibu sana ,kwa kweli jambo ni sehemu pekee ambapo hoja za msingi zinajadiliwa bila woga ,nafikiri bora sisi wengine tufiche majina ,huku nyie makamanda mtapata mambo mengi ya kuiweka sawa nchi ,ni matumaini yetu kuwa hoja ZETU HUKU ZITAPATA mbebaji.

muheshimiwa huku tuna uchungu sana na nchi yetu ,mara nyingi nakaa najiuliza tungepata hata asilimia 10% ya wananshi wawe na ufahamu kama wa wana forum ,tusingekuwa tunaletewa mikataba kama ya kina cifu mangunga,ea richmond.naomba kutoa changamoto ya kupatikana gazeti lisilohitaji faida na radio [mf butiama ] ambayo itakuwa funded ili maono kama haya yawafikie wananchi wengi wale wa vijijini ,tatizo kubwa haya magazeti mengi yanayotegemea matangazo ya serikali na hata lile RAI tuliloliamini sasa yamegeuka ya mtandao,hata lile la kwako ukitaka kuliendesha kibiashara ni vigumu kama utakuwa too critical....

la mwisho mmenisikitisha sana CHADEMA na wapinzani kwa ujumla kutokwenda mahakama ya east africa kupinga ule uchaguzi ,,,bado muda upo naomba tuitumie mahakama ile ,hii ni mara ya pili ccm kupitisha wapinzani dhaifu kumbuka ya zitto kabwe kukosa ubunge wa africa na sasa hili.

karibu sana!!!
 
freeman,
kwanza ningependa kujumuika na wanabodi wengine kukukaribisha katika forum hii,

pili napenda kukupa hongera kwa uamuzi wako wa kuamua kurudi shuleni,ili uweze kuongeza ujuzi wa kwenda sambasamba na karne hii ya utandawazi,sayansi na teknolojia.

tatu natumaini kujiunga kwako na bodi hii kutaleta changamoto nzuri kwa kuwavutia washikadau mbalimbali wakiwemo wa upande wa ccm nao kujibu hoja mbalimbali na hivyo kuifanya hii forum siyo kijiwa cha kupiga soga bali ni mawasiliano ya moja kwa moja kati ya waongozaji na waongozwaji.

kama ulivyosema hapo kwa maneno ya blue umuhimu wa kila mtanzania kwa nafasi yake kushiriki katika siasa na demokrasia katika tanzania.
Mimi nakuunga mkono kwa dhati kabisa NI LAZIMA WATANZANIA TUSIMAME KIDETE KATIKA KUHOJI MASUALA MUHIMU YA TAIFA HILI.

Madhara kama ya umeme ni matokeo ya kutokuwa na viongozi makini na wasionauchungu na taifa hili, aibu kubwa sana katika karne hii tanzania hakuna umeme wa uhakika,
Tanesco imefisilika kwa kulipa mabilioni ya pesa kwa kampuni ya IPTL , serikali mpaka leo imekaa kimya kuhusu suala hili na hakuna hata mtu mmoja amechukuliwa hatua za kinidhamu.

Kila siku tunasoma kwenye vyombo vya habari kuhusu madhara yanayopatikana kutokana na mikataba iliyosainiwa kienyeji na wahusika hawaonyeshi responsibility yeyote.
Hii inatokana na ukweli kuwa viongozi wa ccm wamefanya kuwa taifa hili ni mali yao na familia zao na ndio maana wanaweza kufanya lolote lile bila mtu kuhoji,
ndio maana ni muhimu kwa watanzania kwa ujumla kuweza kujenga uwezekano wa kuwa na political alternatives wakati mambo yanaharibika.

Kama ulivyosema freeman, taifa hili ni letu wote na kila mtanzania anahitaji kufaidika na kinachopatikana kutokana maliasili tulizonazo na sio wajanja wachache.

Kuna wakati nilifanya utafiti kuhusu ni kwa vipi nchi ndogo ya japan imeendelea sana kuliko hata mataifa makubwa duniani kama ajentina na brazil,
nilipata jibu moja kuwa ni utamaduni wa wajapani ndio siri ya maendeleo yao.
Wajapani wao wote kwa pamoja wanaishi kama familia moja, wote kama familia wanashirikiana kujenga taifa lao.
Why not us?
Mimi naamini tukishirikikana tunaweza kuleta mabadiriko katika taifa hili, tunaweza kukabiliana na matatizo sugu ya rushwa, uzembe,ubadhirifu wa pesa, nk.
Aluta continue...
 
Mheshimiwa Mbowe karibu kijiweni ,

Sitaki kurudia sababu zilizokwisha tolewa na wajumbe hapo kwa juu kwa nini watu hatutaki kutumia majina yetu ya kweli kwani nadhani wamezielezea vizuri tuu kwa hiyo sina sababu yoyote ya kulizungumzia hilo ! Mheshimiwa nchi yetu ina matatizo makubwa na kipindi kama hiki Upinzani ulitakiwa usimame kifua mbele na kuexpose uozo na usanii unaofanywa na chama tawala lakini cha kusikitisha ni kuwa upinzani nao umekaa kimya !

Tatizo la umeme wa Richmond alihitaji Phd kujua ya kuwa rushwa ilitembea . Ili ni jambo ambalo nyie wapinzani mlitakiwa mlivalie njuga na kuwaweka hao CCM katika defensive side lakini hamfanyi hivyo mnasubiri mpaka uchaguzi ndio muanze kuzungumzia mabaya ya hawa watu . Pili, suala la EAC na kuingizwa kwa Rwanda na Burundi bila ridhaa ya bunge ni matuzi makubwa kwa watanzania . Wakati tume ikizunguka kukusanya maoni wether tujiunge na jumui au lah ..marais wameamua kuongeza nchi nyingine kinyemela , huu ni uhuni na inaashiria ya kuwa bunge letu lipo pale ku=rubber stamp tuu maamuzi ya serikali .

Tatu , ni lazima wapinzani mfanye mpango muanzishe radio ...haya mambo ya kuassume watu wanawajua yamepitwa na wakati . Radio ni chombo muhimu katika kuwa impower wananchi.

Mheshimiwa karibu sana .
 
MR MBOWE

As much as i have my objections with Politicians but i have to admit that you sure have some "guts" and secondly i got abit curious with your FDR quote...i dont have any particular problem with it but i have some serious objections with FDR's liberalism in IR which in 2006 is disgused as Realism

Now my question to you Hon Mbowe,Are you by any chance a REALIST?
 
Comred,

Duh!

Lakini nadhani utakubaliana na wanachangiaji kwamba wengine nafasi zao haziwaruhusu kuwa wazi. Lakini pia wapo wenye woga wa kweli. Anyway,naamini ujumbe umefika.

Nimesoma katika ujumbe wako kwamba hukuingia kwa ajili ya majibishano. Kama naweza kusoma katikati ya mstari ni kwamba si kila hoja utajibu wewe labda ikiwa ila inayohitaji jibu toka juu kabisa.

my argument here is-pamoja na nia njema ya kuwa karibu na umma mwenyekiti wa chama ni mtu senior, anapaswa kunyamaza zaidi na kusema pale inapobidi na kwa yanayobidi. Lasivyo inakuwa kama Mrema ambaye anarukia kila ajenda au Kikwete anazungumzaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!( nawaomba radhi kwa ku-cross z line, nilitaka nieleweke)


Umetupa kazi ya ziada kwa kweli. Maana sasa itabidi ku-keep tract ya hoja na kuzijibu zilizopo katika ngazi yetu.

Again, I can't do that 4 now. Mpaka nifike DSM. Ila taarifa tu kwa mjumbe mmoja-wapinzani walifungua kesi kuhusu uchaguzi wa EAC. Tofauti yetu na wakenya ni kuwa wao walifungua EAC court wakati hapa wamefungua mahakama ya Tanzania. subject matter za cases zilikuwa tofauti.(But its debetable). Lets cross our fingers.

Kuhusu Richmond, CHADEMA ilitekeleza wajibu wake wa awali. Tumewapa muda. Tukiliendeleza tena hili suala ni 'nguvu ya umma' kwa kwenda mbele.(na hapa ndio tatizo la forums, wakati mwingine unajikuta una-disclose clues za kufanya dola ijiandae ku-pre empty, ndio maana wakati mwingine huwa sipendi kutoa kila facts upenuni).

Catch u all soon

JJ
 
Mbowe
karibu sana mheshimiwa.
wewe unajua wazi kuwa forum hii inatumiwa na wafuasi wako kama sehemu ya kujitangaza na kueneza sera za chama chako.
lakini cha ajabu wanachama wako mwenyewe wanatumia majina ya bandia wako wengi.mfano quartz, mwanasiasa na wengi.
ukija kwetu akina chinga hatujulikani na hatuna haja ya kutaja majina yetu sababu tunafanya kwa nia njema wenye kusikia wasikie vilio vyetu na wao wana vyanzo vya kujua kama kweli au pumba. sasa hatuna nia ya kutaka kuleta au kutumia hii forum kwa ajili ya umaarufu au kukipatia chama au NGO fulani umaarufu.
tunachofanya kama kutoa sadaka hatuhitaji saana kushukuriwa na binadamu mtoaji mzuri wa sadaka anatarajia malipo kwa Mwenyezi mungu.
kadhalika hapa tunapeleka vilio kwa wahusika wa nchi yetu wakiona yanafaa wayachukuwe.
Onyo langu kwako
forum hii au nyingine haziwezi kutumiwa kufuata matakwa ya chama chochote cha siasa au NGO yeyote kwani nimeona wapambe wako kila tamko la chadema linaletwa humu itakuwa sio fair play hata Mrema naye matamko yake yanatakiwa yaje humu.
huu ni ukumbi wa kuelimisha na kuongoza jamii sio sehemu ya kupiga chapuo au ujiko.
 
Mheshimiwa Mbowe,

Mimi nilifuatilia sana kampeini zako wakati ule na ninakiri kwamba niliona kuwa ulifanya kjampeini ya kistaarabu na yenye mantiki sana bila kutoa ahadi za kigagagigikoko kama tulizopewa na JK za kuletewa ajira na kujengewa shule za sekondari kwa idadi ya kufikirika. Kwa jumla kama wanasiasa wetu wengi wangekuwa na mtazamo wa kina na ustaarabu kama wako, bila shaka wasingeukwa wanakula rushwa za asilimia 29 bila hata kunawa mikono, na nchi yetu isengekuwa kwenye ufukara tulio nao leo. Hivi majuzi niloposikia umekwenda kusoma nikasema ni uamuzi mzuri kuliko watu wa CCM wanaojichotea digrii za bandia kutoka PWE, COU, WIU n.k. na kuzitumia kudanganya wananchi. Ni kutokana na digrii hizi za bandia, jamaa hawa huwa hawana uwezo wa kuchambua mikataba na hivyo kudanganywa bila kujua na kusababisha nchi yetu kumalizwa na wageni mbele ya macho yetu hivi hivi. Baada ya kusema hayo sasa naomba nijibu hoja yako kama ifuatavyo.


Forum zote za kwenye internet zinatumia "nicknames" au "aliases" siyo kwa sababu ya woga wa kutoa hoja ila ni njia mojawapo ya kusaidia kuficha identity za wanaforum. Kwa nchi kama marekani identity theft ni jambo kubwa sana na watu wanachukua tahadhali nyingi ikiwa na kuficha majina yao halisi yasionekana kwenye forums kama hizi. Kwenye dunia ya leo kuna baadhi ya watu ambao wanaweza kutumia jina kamili la mtu kufanya uhalifu wa kielectronik na kumsababisha mwenye jina awe matatizoni. Kwa vile internet inasomeka duniani kote basi ni vizuri tuendeleze hizo tahadhali hata kama forum yenyewe ni waswahili kama hii.

Vile vile faida nyingine ni kwamba matumizi ya aliases huwezesha wapiga filimbi waliomo serikalini kutoa data za mambo haramu yanayofanywa na serikali bila kujulikana na wakuu wao wa kazi, jambo ambalo ni zuri kwa forum.

Kwa kawaida kazi ya forum ni kujadiliana mada mbalimbali bila kujali zimetolewa na nani. Ninakushauri kuwa kila upatapo nafasi, ingia kwenye forum hii na kupata mawazo tofauti. Chambua yote kwa mapana na marefu hata kama kuna yanayokuchoma hasa kwa vile yale yanayokuchoma ndiyo yanaweza kuwa ya maana sana katika kukusaidia kupigania nchi hii. Mada zote zenye uwongo huwa zinachambuliwa na wanajumuia wengi na mwishoni kutupiliwa kwa mbali, kwa hiyo mada za namna hiyo usizijali sana na utazigundua tu.


Nakutakia kila la kheri na vita ya ukombozi.
 
Hon. Freeman Mbowe, Chairman CHADEMA.

I feel honoured to respond to your 'fears' of us using assumed names when making any presentations to the media. Don't worry honorable Mbowe, these names are simply "PEN NAMES", used to hit hard the nail where it would had been otherwisely difficult to do so.

So, whatever the name a column presenter would use it does nevertheless affect the real contents of the message.

If you are a keen follower and enthusiast of die hard column presenters you'd definetely have had noticed the embarrassments these wrtiters faced - not only to themselves, but to the entire family. How would you explain to your young adult son that the governemnt has stripped the citizenship from all of you? So in order to avoid this, go about using the pen name.

In as much as we all are aware, you, as a chairman of opposition party, can not be touched - whatever the case - because those in the saddle are wise enough to know that tides might change the course to make them find themselves the other side os the ocean....

Therefore, the quote made above can not be accepted in our country where leaders make good decision in the conference rooms but to perform quite differently altogether when it comes to implementation.

I will maintain my pen name to mock president with his empty promise regarding corruption and shady tender award. What can the president tell the Tanzanians regarding the Richmond Scandal? THIS COMPANY WAS AWARDED TO SUPPLY A LEASED POWER GENERATORS to TANSECO while it was not dully registered with BRELA. Kikwete hana lolote jipya, zaidi ya kumsema KANZU JIPYA LAKINI SHEKH YULE YULE.

That is all for now, I think the msg has been delivered.

Kaiba
 
mnyika nimekusoma,

tunasubiri kwa hamu hiyo kesi ya mulpractices za east africa legislative...tutafurahi haki ikitafutwa hadi mahakama ya EA si mnajua mahakama zetu???
 
Bw. Mbowe, karibu sana hapa.. kwa kuweka jina lako wazi kunakunyima uhuru fulani wa kuzungumza mambo fulani ambayo yanaweza kuja kukugeuka baadaye!! kwani hii ni public forum, na chochote utakachosema humu chaweza nukuliwa!!
 
Mheshimiwa Mnyika,

Ninakushauri si wakati wote ni kuongelea politics au kuwa kwenye kampeni.

Kwenye ujumbe wako hapo juu umeanza vizuri sana lakini ukaja kusea ulivyo
amua kuwa tempted na kurusha vijembe kwa Mrema na JK. Najua wanasiasa
bila vijembe ni kama hawajaenda kazini lakini kwa wananchi wengi wenye uelewo wa mambo kama wasomaji wa hii forum, vijembe kama hivyo havikusaidii.
Kila chama kina strategies zake na kuna viongozi wa vyama ambao wanatoa misimamo yako kwenye kila jambo na kuna wale ambao wanafumba midomo yao ili hizo comments zao zisije zikajichanganya zenyewe.

Kila mmoja wa hao viongozi ana nafasi katika jamii yetu na siku ikifika sisi wananchi tutaamua nani anatufaa.

Jitahidi sana kuongelea Chadema inafanya nini au itafanya nini bila kuingiza vijembe kuhusu vyama vingine.

Mtanzania.
 
Mtanzania,

Naelewa hilo ndio maana nikaomba radhi mwishoni kwa kutumia mfano halisi ili nieleweke.

Asante kwa ushauri. Point noted!

Narudia tena: si vibaya kutumia pen name kama nia ni 'kusema ukweli, fitina mwiko'. Nadhani concern inakuja pale zinapotumia pen names nyingi kwa lengo tu la kutoa fitina zisizo za kweli. Kwa hiyo kuna makundi mawili. Kundi la kwanza ni wale wanaotumia pen name kwa nia njema- kuibua uozo ulioko bila kuingia matatani na watu wanaowafahamu ambao wanashiriki uozo huo. (hii ni kazi yenye maslahi kwa taifa), kundi la pili ni watu wanaotumia pen name kwa ajili ya kuandika uzushi. Hawa wanachohofia ni heshima yao kushuka kama wakijulikana ni wao ndio wanameandika.(hii ni kazi ya maslahi binafsi).

anyway, nadhani wanasiasa hatujaingia humu kuifanya hii forum ya chama fulani. Tumeingia kwa ni ya kushiriki kwenye mijadala kuhusu hatma ya nchi yetu. Binafsi niliingia humu baada ya hoja nyingi kuelekezwa kwenye mashambulizi kwa CHADEMA na nikaingia kutoa ufafanuzi. Toka wakati huo mpaka leo nimeendelea kuwa mwanachama wa kijiwe hiki. Kila kiongozi binadamu ana haki ya kuingia au kutoka katika kijiwe hiki. Mwambie chinga awaambie viongozi wake nao waingie. As a matter of fact matamko mengi yanayojadiliwa humu ni yale yaliyotolewa na serikali zaidi.

Tuendelee kujadiliana. Tanzania ni yetu sote, ikididimia sote tunadidimia bila kujali dini, rangi, kabila ama chama cha siasa.

Keep writing, as a promise-niko njiani, nikifika bongo nyumbani nitajibu kwa kina. Yaliyoandikwa mpaka sasa ni mengi. Yanahitaji siku nzima huru kuyajibu.

Mbarikiwe!

JJ
 
Add: 'nadhani kauli yako kwamba si wakati wote ni wa kuzungumzia siasa au kuwa kwenye kampeni' inahitaji kujadiliwa!

Je, siasa ni nini?Nini kati ya mipaka ya siasa na maisha yetu ya kila siku?

Je, kampeni ni nini? Je, kuchambua masuala ya kitaifa na kutoa hoja mbadala bila kusema nichague mimi ni kampeni?

Jj
 
Mheshimiwa Mbowe umenikuna. Umetuthibitishia kama alivyosema Mzee ES kuwa forum hii inapitiwa na watu wazito! Ahsante sana kwa kuingia hapa. It has boosted the profile of the forum, but of course, of our party as well! Najua hakuna kiongozi wa CCM anayeweza kuthubutu kutumbukia humu. Kwanza wale jamaa wana allergy na kusoma. They just dont even read! Chinga waamushe hao wenzako waanze kutafuta maarifa katika maandishi!

Sasa tuwaonye akina Nungwi kuwa hapa hakuna nafasi ya longolongo, hoja zenye akili tu zinatakiwa. Sio blabla na propaganda ya kutetea mambo ambaye hayateteeki.

Nyongezea katika majibu ya kutumia pen names: Binadamu tunahlika wakati mwingine wa kuangalia 'nani amesema badala ya amesema nini'. Kwa hiyo tuliona ili to-focus kwenye hoja tukakubaliana tangu enzi za BCS kwamba tutumie pen names. Ila nakuhakikishia sio kwa sababu ya woga hata kidogo. Hatukuogopi maana mambo mengi humu ndani hatuzushi hata kidogo.

JJ: ni vizuri kwamba kuna kesi Dar kuhusu ubunge wa EAC. Lakini unajua kinachokosekana katika siasa za upinzani TZ na hasa katika CHADEMA ni militarism. We need millitant politics. Hii ya Zitto peke yake anapiga kelele wakati wengine wanaendelea na business as usual inaturudisha nyuma. Bado hatujawatia jambajamba CCM. Na ukiona CCM wanatusifia kuwa ni chama cha wastaraabu, ujue hatujafanya kazi yetu vizuri. Kuna mambo mengi ya ku-capitalise on. Inasikitisha kwamba wabunge wetu hawakulibebea bango suala la Richmond katika bunge lilipita. Hatuku-capitalise pia katika tatizo la wamachinga na wewe kama Mkurugenzi wa Vijana nafikiri hili linakuhusu moja kwa moja. In short, we must miliitarise our political party. Hawa jamaa ni mafia hasa, watatusogeza hadi uchaguzi watakuwa hawajafanya kitu lakini na sisi pia tutakuwa hatuna cha kuonesha kwamba wa are an alternative. Safari njema Dar.
 
Back
Top Bottom