Naanza kuona hasa ni akina nani "wanashinikiza" Gesi ya Mtwara iletwe Dar es Salaam, wakati gharama za kutandaza mabomba hayo ya usafirishaji wa gesi kutoka huko ingetosha kujenga vinu vya kuzalisha umeme huko huko Mtwara na kutandaza mfumo wa usambazaji umeme karibu maeneo mengi nchi nzima na kiasi kidogo cha gharama kingetumika kutandaza mabomba madogo sana ya kusafarisha kiasi kidogo cha gasi kwa matumizi mengine ya Dar es salaam!!!.
--MpigaKeleleee...ee!,
Kwanza nianze kwa msisitizo kuwa jemeni, mimi sio mtu wa TCRA!, naona maswali yanazidi kuelekezwa kwangu!.
Lile la gesi ya Mtwara, mimi ni mmoja wa masupporter wakubwa ile gesi ije Dar kwenye viwanda na magari na majumba ya watumiaji!. "You can never miss what you never had!". Kuna kampuni moja ya Waholanzi, waliamua kugharimia solar panels na biogas kwenye shule, zahanati, na nyumba za ibada za kujiji cha Itonjanda, huko Tabora Vijijini ili kuwahamasisha wanakijiji wengine kuchangia kidogo tuu wawekewe highly subsdized solar pannels! na mitambo ya biogas ili kukoa mazingira!. Amini usiamini, wananchi wale hawakuchangia!. Nikiwa JET,(Chama cha waandishi wa habari wa Mazingira) tukapewa tenda ya kufanya research kwa nini?!. Tulipozungumza na wanakijiji, wao wakasema shida yao kubwa sio nishati, kuni zipo za kumwaga, wala sio umeme, wameziea chemli, bali shida yao kubwa ni barabara na maji!. Mradi ended up to be a "white elephant!".
Mimi binafsi nimepeleka solar na jiko la gesi ule mtungi mkubwa kwa mama yangu kule kijijini!, huu ni mwaka wa pili sasa, mtungi mmoja haujaisha na kila nikifika, tv ina vumbi tuu kuonyeshwa haiwashwi!. Nikimuuliza mother kwa nini hupikii gesi?, sikuzoea!, chakula cha gesi sio kitamu kama cha kuni!, halafu nimeambiwa siko moja italipuka!, hivyo gesi inatumika tuu wakija wageni!. Na TV jee, hatukuzoea kuangalia! eti pia inakula umeme mwingi hivyo tunakosa mapatio ya kuchajisha simu za watu mchana!. Ile tv ni pambo tuu!. Hivyo ndivyo ilivyo gesi ya Mtwara!, hawajazoea!, na viwanda si mpaka vijengwe?!. Kazi ya kuestablish "petrochemical industry" hiyo Environmenta Impact Asssessment yake tuu yenyewe!, inachukua mpaka 5 years!, sasa wakati tunasubiri hivyo viwanja vijengwe huko, gesi iliyopo iletwe Dar ambapo viwanda tayari vipo na wa`tumiaji tupo!.
Kuna watanzania wako Nyaminywili-Rufiji, Omukihisi- Bukoba,
Muhukuru-Songea vijijini,
Mwazye-Sumbawanga vijijini, Oldonyo-Sambu, na kadhalika na kadhalika; hawa nao wanahitaji kupata matangazo ya Televisheni kwa unafuu kulingana na kipato chao.
Pasco kwa utaratibu huu unaoupigia 'chapuo', ni wazi unataka kuwanyima fursa watanzania wenzako haki ya kupata habari kwa njia bora kabisa, kwani kwa taaluma yako ya masuala ya habari unajua kabisa wananchi wa maeneo nliyoyataja na mengine yanayofanana nayo hawaweze kumudu gharama za ving'amuzi/visimbuzi ulivyovitaja.
Nilitarajia kwa kalamu yako upaze sauti zao za kuona namna serikali kupitia TCRA na Wizara husika kushusha gharama za kupata vifaa hivi na kuhakikisha wanasimamia suala la kuhakikisha televisheni zote za 'bure' zinapatikana kwenye ving'amuzi hivi ili watanzania wote tufaidike.
Ahsubuhi njema.
--MpigaKelele
Hili nalo neno!, vituo vya TV kama yalivyo makampuni ya simu , mabenki au miradi yoyote, inapelekwa kule kwenye faida!. Ndio maana kuna baadhi ya maeneo reli imepita kungine hata kichochoro hakuna!. Kuna baadhi ya maenneo kumepita mabarabara ya lami mpaka vijijini, wakati kungine hakufikiki kabisaa! hakuna hata hiyo barabara ya uchochoro!, kisa hakuna shughuli yoyote ya maana ya kiuchumi, hivyo hakuna biashara, hakuna pesa, nani aende?!.
Wakati nikiwa mtangazaji mchanga pale RTD, nilitupa jicho langu mahali kwa kabinti fulani, kumbe cha "wenyewe" ma bisi, hivyo dawa yangu ni kutupwa kituo cha Nachingwea kama adhabu!. Kule nikashangaa kukuta hakuna hata hoteli moja ya maana! hivyo nikafikia guest!. Chakula nikaagiza kuku, nikaambia hapa hakuna kuku!, nikauliza hakuna hata hoteli yoyote yenye kuku?, nikaambiwa hakuna kwa sababu hata ukuchinja kuku, hakuna wateja!, wakasema ukitaka kuku, unaagiza asubuhi ndipo tunakununulia, kukuchinjia na kukupikia ila lazima utamla wote maana watu wa kule hawana purchasing power ya kula kuku!. Ukiuliza hiyo bei yenyewe ya kuku!, nilikula kuku mpaka!, ukijumlisha na kale kajiukarimu ka watu wa "ntwara!" almanusura ningelowea, ila kiukweli kimaendeleo hakufai kabisa!. Watu wenye pesa walikuwa ni wajeda pekee kwenye kambi yao ya Fort Koma" nao kila kitu ni barracks!.
Vivyo hivyo kwa makampuni ya simu, hayawezi kupelekja huduma zake mahali amba hapalipi, so do banks na vituo vya TV are no exception!. Kwa taarifa yako, mpaka leo kwa Tanzania nzima, hiyo coverage area ya TV Ωote zilizopo ukizijumlisha pamoja na cable na wanaotumia ma dish yao, hawafiki 30% ya Watanzia wote!, hivyo hapa unawazungumzia hao Watanzania 70% ambao are still living in the dark!. Kumbuka "you can never miss what you've never had!". Kwao life is as usual!.
Kati ya hawa asilimia 30% wanaopata TV signal, only 15 % ndio wanatumia antenna waliobaki wanatumia either cabla au dish, hivyo hao wa cable na dish huu uhamaji hauwahusu, bali wale 15% waliotegemea antenna kama za Chadema etc ndio wanahusika!.
Kwa vile kupata habari ni miongoni mwa haki za msingi za binaadamu, serikali haiwezi kuziachia tuu hizi kampuni za simu na mawasiliano kuwekeza kwa wenye pesa tuu!, hivyo imeanzisha mfuko wa Universal Communications Access Fund (UCAF) na unagharimiwa kwa kiasi kikubwa na TCRA kupitia wizara ya Mawasiliano ambao utatoa fungu la ruzuku kuwafidia makampuni ya simu na vituo vya TV kufika hata yale maeneo ya pembezoni ambako ni hasara tupu! so that hatimaye, kila mahali patafikiwa japo sii leo wala kesho ila one day kote kutafikiwa!. Hivyo soon the problem will be solved!.
Nawaombeni msiniulize maswali zaidi, mimi sio mtu wa TCRA!
Pasco.