Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 57,155
- 128,815
Mkuu FP, asante kwa heri ya mwaka mpya heri na wewe!Pasco,
Saa nyingine kaka UNAANDIKA (unaongea) kama hawa watalawa wa sasa wa Tanzania!, Inasikitisha na sijui kama ni wewe yule yule wasiku zote.
Nina maswali Pasco ,
1. Mkuu yule mama anayeuza mama nitilie anayeishi Buguruni malapa na yule msukuma mkokoteni wa Kwa Mtogole waliokuwa na TV yao wakanunua antenna ya mwiba uliotengenezwa kwa tubelights mbovu na waya mbovu wakawa wanashika Local TV kwa sasa ndio basi UNATAKA wasione tena TV au mpaka waende Bar Sinza?. Na je wana uwezo wa kwenda Bar?
2. Yule mzee kule Mwanerumango naye vipi? alipie elfu 10 kila mwezi? akanunue vifaa elf 62 kisha alipie kila mwezi?
3. Mkurugenzi wa TCRA aliwahi kusema kuwa kuna king'amuzi utanunua elf 39 kisha utaona channels ulizokua anaona bure! yaani sio unajiunga na kampuni flani kwa mpango wa subscription flani NO, unanunua basi. Alizungumza hayo Power breakfast ya clouds fm. Imekuaje
Pasco nahisi harufu ya Ufisadi katika wizara ya "RAIS" "wao" mtarajiwa.
Mbongo mpe nafasi ya mabadiliko lazima atavuruga au kunukisha Rushwa.
Hivi nishakwambia, happy nyu year?. basi hepi nyu yiaaa dear Pasco
FP
Sisi watu wa media pia ni watawala!, yaani sisi ni ule mhimili wa nne baada ya ile mitatu ya kawaida ya The Executive, The Judiciary, The Legislature na sisi ndio "The Fourth Protocal" hivyo tuu watawala, tatizo letu hatuna budget, hivyo kutegemea zile bahasha na matangazo!.
Tukirudi kwenye mada, yule mama wa Buguruni malapa na yule wa Manerumango, kama waliweza kununua TV kwa 150,000/=, hawawezi kushindwa kununua king'amuzi kwa elfu 39,000/=!. Tena pita Buguruni, Temeke, Ilala na Kinondoni, kila baada ya nyumba ni kibanda cha chips kuku na kila kona ni bsar na zote zinajaa!. Kila mtaa ni maduka na kila kanga mpya zikitoka zinagombaniwa zinakwisha!, Na kila baada ya mtaa, ni gest za "wageni wenyeji", huko masikioni ni matundu matatu matu na hereni za dhahabu tena siku hizi ile mikufu ya dhahabu sio shingoni tuu!, ndio maana hata ununuzi wa zile sh.. za wamasai umepungua!. Hivyo kisingizio cha Uswazi ndiko kwa walala hoi, doesn't hold water!.
Nenda Mikocheni, Osterbay, Masaki na Mbezi Beach, tafuta vibanda vya chips, tafuta bar, tafuta gest, tafuta maduka?!. Hakuna!. Ikifanyika survey kuangalia watu wa maeneo gani wanakula kuku zaidi, wanajirusha zaidi, wanastarehe zaidi na kuvunja ile amri ya 6 zaidi kwenye magesti!, kuhonga zaidi, kuvaa zaidi etc, utakuta ni watu wa Uswazi!, hivyo hiyo elfu 39!, wanayo!.
Alichosema Mkurugenzi wa TCRA ni sahihi kabisa!, baada ya kukinunua hicho king'amuzi kwa hiyo elfu 39, utapata zile stesheni 5 za bure bila hata kufanya subscription!. Hiyo ndio basic!, sasa ukiamua kulipia ile subscription fee ya elfu 10 kwa mwezi ndio unapata kila kitu, sasa hii ni kwa starehe yako!. Starehe gharama!.
Kingine Mkuu FP, Watanzania ni wavivu ila tuna tabia ya kulalamia tuu sometimes without any reasonable cause, ni kulalamika tuu bila sababu yoyote ya msingi ali mradi tulalamike tuu. Nakumbuka nimeshawahi kukaa bar fulani Sinza na kimwaga fulani "anazungusha" ile mbaya huku tumezungukwa na vimwana, ni kula kunywa kwa raha zetu!. Siku ya siku nilikuja kukutana na wife wa jamaa na mtoto akiwa na uniform ya shule!, machozi yalinilenga!. Kuna watu wanastarehe huko familia zao zikinyanyasika!, hawa watalaaniwa! na ndio wa kwanza kulalamika!.
Tubadilike, mtambo wa analogia ndio umeishwazimwa, sasa dawa ni kununua king'amuzi tuu hakuna dawa nyingine!.
Pasco.