Dstv naona local channel moja tu yaani TBC, zingine sioni na wala sijawahi ona hata siku moja, please anayejua namna ya kufanya hata nione Star TV tu. Msaada please
Mkuu DSTV bana haipo kwenye michakato ya TCRA, utaishia kuiona TBC tu
Dstv naona local channel moja tu yaani TBC, zingine sioni na wala sijawahi ona hata siku moja, please anayejua namna ya kufanya hata nione Star TV tu. Msaada please
me mbona nina cha startimes na local chaneli zote tano nazipata though bado nasubiri vingine nihame.elfu kumi na nane then chaneli zenyewe za kizushi tu.kwa anayetumia zuku anaweza tupa data zake?
Mkuu DSTV bana haipo kwenye michakato ya TCRA, utaishia kuiona TBC tu
Kwa sheria, walitakiwa waoneshe local channels zote - free. DSVT ni scandal mwanzo mwisho.
Na hii switch-over imeenda vibaya sana, na naona ni failure ya Wizara na TCRA kutofanya maandalizi ya kutosha ili kuhakikisha local channels zinapatikana.
kwani ni lazima sana muangalie TV? Hamna shughuli zingine za kufanya?
Kwa mwendo huu wa hawa TCRA tutajikuta tuna ving'amuzi zaidi ya viwili kupata local Channels..... Gharama zaidi kwa mwananchi....
Natumia Startimes; nipo mby city; naona local channel zote 5; ITV, STARTV, EATV, TBC & CHANNEL 10. Ila nitahama vikija ving'amuzi ambayo package zake zina ridhisha, coz ktk startimes kifurushi cha bei rahisi (9,000) channel za ziada nyingi hazina mvuto sana!
Siyo viwili ila tegemea sebule nzima, am tired!Hivi hawa jamaa TCRA si wao ndo wangeuza hivyo ving'amuzi na sisi tukawafuatehao jamaa wengine ili tulipie hizo chanel zingine za movie?Yaani ni usumufu kweli
nunua satelite dish
Mkuu uko nchi gani wewe?, yaani matangazo yote yale yaliyotolewa na TCRA wewe bado hujaelewa!.Naona usanii unaendelea kulitafuna taifa!kwa waelewa wa mambo tumeshanusa harufu chafu ya ufisadi ndani ya TCRA.nisiseme mengi bali nijikite kwenye swali langu au letu!
Ili niweze kuona local channels zote ninunue king'amuzi kipi?
This is a very serious question from the common mwananchi.
Wakuu dunia ya leo hakuna kitu inaitwa bure tena, huku nchi za dunia ya tatu ndio tunaona mambo haya maajabu na hii inatokana na kulemazwa na mfumo wa kizamani wa bure bure
Labda tuangalie mfumo wa urushaji matangazo kwenye mfumo huu wa dijitali ili tuelewane
Zamani mtu yeyeto anaweza kuanzisha tv station yake labda akaiita miningits tv akawa anafanya vipindi vyake na kwa mfumo wa analojia maana yake alikuwa anaweka dish lake na kurusha na wenye tv zao za analogi wanadaka na kuendelea na maisha
mfumo wa dijitali umekuja kivingine maana sasa meningits tv atahitaji mtambo mkubwa wa kurusha matangazo kwa digitali kitu ambacho ni kigumu kwake
kinachofuatia ni watatokea watu wenye uwezo wa kurusha matangazo kwa dijitali na watakuwa wanakusanya tv station kadhaa za nje na ndani na kuziweka kwenye ving'amuzi vyao kisha kivirusha kidijitali na hii hufanyika kwa makubaliano ya kibiashara zaidi, hapa inabidi meningits tv aende kwa hawa jamaa ajiunge nao wamrushie matangazo yake
Hadi sasa tuna Ting, Startimes, Zuku na Easytv kama sijakosea, hawa ndio wanarusha matangazo kidijitali kupita vingamuzi vya fta na setelaiti
sasa wenye tv stations wanayo haki ya kuchagua kufanya kazi na nani kati ya wenye ving'amuzi hawa kulingana na offer zao, lakini ikaibuka hoja inamaana mtu atalazimika kununua ving'amuzi vingapi kuona local channel mbalimbali?
hapo sasa TCRA ikaja na ubabe kwa manufaa ya mwananchi kwa kuwalazimisha wenye tv stations 5 walizoita za kitaifa kuingia mikataba na wenye ving'amuzi wote.
Wakatoa agizo kwamba lazima ITV, EAT, STARTV, TBC na CHANNEL10 ziingie mikataba na wenye ving'amuzi wote na pia ikatoa amri wenye ving'amuzi warushe chaneli hizo tano bure hata kama muda wa package ya kawaida ukiisha basi chaneli hizi ziendelee kuonekana
Hadi hivi sasa kampuni zote zinarusha chaneli hizo tano lakini bado hawajaafikiana vizuri kibiashara kwasababu ya ulazima waliopewa na TCRA
Sasa hizi tv station zingine kama DTV, clouds nk wanalazimika kutafuta kampuni moja ya kufanya nayo kazi au kama wakiweza basi wataingia mkataba hata na kampuni zaidi ya moja, kwataarifa nilizo nazo Clouds tv wameshindwana na Startimes na wamekwenda Zuku
Kama hutaki usumbufu wa kulipia kwa mwezi walau kwa muda huu wakati bado tupo ugenini kwa dijitali basi unaweza kufunga dish la free chanel na utaweza kuona baadhi ya stations zinazorusha matangazo kwa setelaiti....na hii ni kwa muda tu maana biashara ikichanganya watazitoa na utalazimika kuziangalia kupitia ving'amuzi
Mkuu uko nchi gani wewe?, yaani matangazo yote yale yaliyotolewa na TCRA wewe bado hujaelewa!.
King'amuzi ni kimoja tuu utaona TV zote tano za "free to air" bure!.
Mpaka sasa kuna makampuni matatu ya kurusha matangazo, Star Media, Agape Associets "ting" na kampuni ya Mengi na Dialo ambayo king'amuzi chao bado hakijaingia sokoni, ila kimeanza kutangazwa!.
Ukishanunua king'amuzi chochote, hizo TV tano za bure utaziona bila kulazimika kuzilipia na zitaonekana kwenye ving'amuzi vyote vitatu, hivyo uko huru kuchagua kununua kingamuzi chochote kati ya hivyo!.
Mfano kingamuzi cha Star media hawana chanel ya movie ya HBO, kama wewe ni mpenzi wa HBO, huna jinsi, lazima ununue king'amuzi cha Agape!. Huko pia utaziona bute zile tv tano za bure!.
By choice, kama unataka usipitwe kitu, na unapenda mambo mazuri yote, then utavinu nua ving'amuzi vyote vitatu?.
Mimi nilianza na kingamuzi cha Easy TV, nikaja cha DSTV, Sasa ninacho cha Star Media, my boys wanapenda movies za HBO hivyo soon nitanunua cha Agape!.
Wengi wa Wakazi wa Dar, tunapenda zaidi starehe kuliko kuzijali familia zetu!, mimi nakunywa Sinza, kuna bar 250 na zote zinajaa, kwa nini tushindwa kulipia king'amuzi elfu 10 kwa mwezi?!.
Heri ya Mwaka Mpya.
Pasco.
Mkuu Namungula Jr, DSTV ni foreign channel, iko Africa ya Kusini, hii itaonyesha TBC tuu, tena hiyo TBC iliingia enzi za Tido, sijui kama itadumu!. Hizo TV tano za bure zinaweza kujiunga na DSTV ila kiukweli, kama kujiunga Star media ni issue, DSTV itakuwa ndio kabisa hawawezi kuigusa!.Mkuu nashukuru kwa ufafanuzi,vipi kuhusu Dstv wataonyesha hizi 5 local channels?
itv na star tv unazipata?
Kwani siku hizi upo Kenya Yo Yo??bongo mna kazi kweri kweri kudadadadeki kwa hiyo jana wengi wenu bila bila tv bwahahahaaha
Awali tulielezwa kuwa tv zitakazoathirika kwa kutokuonyesha ni zile za analogy ambazo ndiyo zitahitaji visimbuzi! Sasa inaonekana kila mtu amekuwa affected na inafanywa bihashara. Hivi nchi zingine waliotutangulia nazo unahjitaji visimbuzi kuona channel ambazo si za kulipiwa? zaidi kwa nini mtu ununue visimbuzi vinavyoonyesha vituo vya ajabu usivyotaka kuangalia ilimradi tu upate TBC na Channel ten?