Yaliyojiri Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi kwenye kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake, kesi imeahirishwa hadi - Nov 10, 2021

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,191
4,104
Kesi ya mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe inaendelea kuunguruma leo mahakamani baada ya kuahirishwa jana. Leo Jaji atatoa maamuzi ya mabishano ya kisheria yaliyotokea jana kati ya mawakili wa Utetezi na Jamhuri.

Leo Jamhuri inaendelea na shahidi yule yule Jumanne Malangahe.

Kuwa nami.

========

Jaji ameingia

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa

Robert Kidando anatambulisha Jopo la mawakili wa serikali..

Peter Kibatala anatambulisha Jopo la mawakili wa utetezi..

Jaji anaita washtakiwa wote wanne na wote wanaitika wapo...

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Shauri limekuja kwa jili ya Kusikiliza Uamuzi wa Mahakama na tupo tayari kwa ajili ya yote

Jaji: Utetezi

Wakili Peter Kibatala: Na sisi tupo tayari kwa ajili ya Ruling

Jaji: Jana Mahakama ilihairisha Shauri hili na Maamuzi yapo tayari

Jaji: Maamuzi haya Madogo yamekuja baada ya Upande wa Utetezi Kupinga Kielelezo Cha Hati ya Kukamata Mali, Ambapo ASP Jumanne aliyekuwa Kwenye Timu ya Kuwakamata washitakiwa huko Rau Madukani, Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro

Na alikuwa anatoa Ushahidi, Katikati ya Ushahidi wake aliomba kutoa Kielelezo Cha Hati ya Kukamata Mali, Na Mawakili wa Utetezi Wakapinga, Kwa kuanzia na Wakili Nashon Nkungu na wengine wote.

Na Kwamba Kifungu namba 38 (3) Ndiyo I naelekeza Namna ya Kuchukua Mali, Na Kwamba Hati hiyo ni ya Kisheria na lazima Sheria ifuatwe. Na Kwamba Upande wa Mashtaka hawakuomba Nafasi ya Kutibu Mapungufu.

Jaji: Hoja zao ilikuwa kwamba Kielelezo ambacho Kilikuwa kinaenda Kutolewa hapa Mahakamani na Kilikuwa tayari kimeshafanyiwa Utambuzi. Kwa Mujibu wa Maelezo Yaliyitolewa ni kwamba hakuna Kifungu cha 38 kilicho fanyiwa Marekebisho Mwaka 2018, na Kwamba hatuna Sheria hiyo

Jaji: Na Kwamba Kesi Nyingine ya Mahakama Kuu Chini ya Jaji Malimbe Yapo Maamuzi Kwamba Kuto Kurejea Vizuri Vifungu Vya Sheria kunaathiri Kesi, Na Kwamba tutupilie Mbali kwa kutumia Kanuni ya Overriding Principle, Hizo ndiyo zilikuwa hoja In chief kwa Upande wa Utetezi

Jaji: Na Kesi Ya Mwenderosi katika Mahakama Ya Rufaa, Kwamba Overriding Principle haitaji Kuachiwa kwakuwa itaharibu kabisa Mwenendo wa Kesi, Wakaomba Mahakama itumie Maamuzi ya Mahakama Kuu kutupilia Mbali.

Au anaweza Kurejea Sura ya Sheria hiyo, Kina Inavyoonekana Katika Sheria hiyo, Wao wanasema Kielelezo Kimekidhi Vigezo cha Sheria hiyo kwa Sababu imetajwa Jina la Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Wametaja Mwaka, Wametaja Sura,

Jaji: Kwa Upande wa Mashitaka Walikawakilishwa na Robert Kidando na Pius Hila, Hoja zao ilikuwa Wa naomba Mahakama iongozwe na Sheria ya Tafsiri ya Sheria chini ya Kifungu cha 20 (1) kwamba Mtu anaweza Kurejea kwa Kifupi, Mtu anaweza Kurejea Mwaka au Namba ya Sheria

Jaji: Na Kwa mujibu Wa sheria wamekiri ni kweli hakuna marekebisho ya sheria hiyo, hapakuwa na marekebisho ya kifungu hicho mwaka 2018, Na pamoja na kutorekebishwa kwa kifungu hicho lakini sheria yenyewe iliwahi kurekebishwa

Admisive, Kielelezo ni Competence na Kwamba Kielelezo ni Relevance. Kwa Mambo hayo, Pingamizi, hayaonyeshi Kwamba Kielelezo hicho kimekosa Sifa hizo

Kwa Maana hiyo Mahakama Itupilie Mbali Pingamizi Hilo. Na Kwa namna hiyo Wameomba Mahakama Irejee Kesi ya Athuman Sharif iliyoketi Katika Mahakama Ya Rufaa ya Rufani ambapo Kesi hiyo ilitaja Kanuni tatu za Kufuata Na Kwamba Wameomba Kielelezo hicho Kichukuliwe Kama Shahidi ni

Jaji: Na Pamoja na Kutorekebishwa Kifungu hicho lakini Sheria Ya yenyewe uliwahi Kurekebishwa, Maamuzi yaloyorejewa Kwa Upande wa Kesi Ya Mwenderosi haishahabiani na Kesi iliyopo Mahakamani kwakuwa Kesi ya Mwenderosi ilikuwa ni Juu ya Kukosekana kwa Barua ilikuwa Kwenye kesi hiyo.

Wakati Nyaraka hiyo ilikuwa ni ya lazima, Na Kwamba Kesi hiyo ni Tofauti na Kesi hii, Kuhusu Kesi ya John Marco Na Malimbe ni kwamba Kesi hiyo ilikuwa inahusu Maombi ya Nyaraka ya Kesi iliyopo Mahakamani Wakati Kesi hii kinacho zungumza ni Kurejewa tofauti kwa Sheria tofauti

Jaji: Na Kwa sababu hiyo Kielelezo Kinatupeleka kupokelewa, Na Kwamba Siyo Sheria Moja tu ambayo imetejwa katika Kielelezo Bali pia Kuna Sheria ya The Police Force and auxiliary Act, Na Kwamba Mahakama Itupilie Mbali pingamizi hilo

Na Kwamba Wamesahau Kwa Makusudi Kusoma Kifungu cha 20 (3,) kwamba Sheria inapaswa Kurejewa Kama ambavyo imepigwa na Mpiga Chapa wa Serikali, Mahakama ufahamu kwamba Kifungu cha 35 kuwa inapaswa Kusomwa Kwa Pamoja Kifungu cha 38 na Kwamba Vifungu hivyo Vinafanya Kazi kwa pamoja

Jaji: Kwa Upande wa Utetezi Walikuja na Ufafanuzi wa Kifungu hicho cha Sheria, Wao hawapingi Kifungu Cha Sheria ya Tafsiri ya Sheria, Na Kwamba Kifungu hicho Kipo Upande wao, Na Kwamba Wao Marejeo yao hayarejei Kurejea Kwa Ukamilifu kama Sheria Inavyotaka

Marejeo ya Kesi Kwa Ujumla, KESI YA MWENDEROSI inatoa Kanuni ambayo Mahakama hii naiomba kuitumia, Na Kwa sababu Ilitakiwa Irejee kwa Mujibu wa Sheria ambayo Ilitakiwa Kuwa Ipo, Basi wa naomba Mahakama ikatae Nyaraka hiyo, Kimsingi hizo ndizo hoja za Pamoja nimejitahidi Kufupisha

Jaji: Na Kwamba Kukosewa Kwa Sheria Moja hakuiganyi Nyaraka hiyo kuwa hai, Hawakuomba Mahakama Irekebishe Kabla, na Kwamba Kurekebisha wakati Nyaraka Ipo Mahakamani Haikubaliki hata Kidogo, Hawana eleza Kwamba Wametumia Short title, Kwamba wanatumia Namba na Sura

Jaji: Kwa Pamoja kuna Hoja ambazo haina Ubishi, Pingamizi lilikuwa la Moja kwa Moja, Kwamba Nyaraka haiku nukuu Sheria Kwa Ukamilifu, Na wameitambua Wakati wa Kutaka Kuingizwa, Mambo waliyoongea kwa Upande Mashtaka ni Mambo ya Statutory na siyo Hoja ya Msingi iliyopo Mbele yake

Sheria inatoa Namna ambavyo Sheria za Nchi yetu zinaweza Kutafsiriwa. Na Kifungu cha 38 na Kifungu cha 35 Ndiyo zinatoa namna ya Kuchukua Mali kwa Mtuhumiwa. 38(3) inatoa Umuhimu wa Kuchukua Hati ya Kukamata Mali

Jaji: Niwapongeze mawakili wote ambao wameisaidia Mahakama kufika maamuzi yake, Na kwa sababu hiyo nitajitahidi kwenda kwenye hoja ambazo zinahusu pingamizi na hoja ambazo sijazitumia sijazipuuza Hapana, Kwa kuanza pande zote mbili wanakubaliana Kwa 20(1) ya Sheria ya Tafsiri ya

Nimeona Mahakama iemde Moja kwa Moja kwenye Fomu hiyo, Kama ambavyo imeandikwa Kwa Lugha ya Kiswahili, Imeandikwa Hati ya Kuchukua Mali, Na Kwamba Imetolewa kwa Kifungu cha 38 na Kifungu cha 35 cha Sheria ya Polisi na Polisi wasaidizi, Iliyorekebishwa Mwaka 2018

Jaji: Lakini haijapingwa kwamba Ni takwa Kisheria Kwamba Fomu hiyo ni lazima ikidhi Kisheria, Ambapo Pande zote Mbili wamekubalina, Na mimi naona hivyo, Niende Moja kwa Moja kwenye Pingamizi, Pingamizi hili linaonyesha Kwamba Sheria ambayo imenukuliwa na Kwamba imekosewa Kurejewa

Kitu ambacho nimepata Kwenye kamusi hiyo ni Neno REKEBISHA, Kwamba ni Adjusted or amended, Which was Adjusted Or was amended, Hivyo kwamba Kilichopo Mbele ya Mahakama Siyo Iliyo Rekebishwa Mwaka 2018,

Mahakama ikasema iendelee na hii sintofahamu?, Mahakama ikaona Hapana ishughulike na neno hili, Mahakama ikapata kamusi ya Kiswahili TUKI Toleo la UDSM la Mwaka 2001, Rekebishwa Siyo Jina 'Waka' Kitenzi ambacho linaweza kusimama pekee yake

Jaji: 2018 Kwamba Ndiyo limeleta Ubishi Mbele ya Mahakama, Imetumika Kama sheria ambayo Imerekebishwa Mwaka 2018, Maana halisi iliyorekebishwa Mwaka 2018 halikuwa imeelezwa inamaanisha nini, Mahakama Ikaona ni Vizuri kama Kweli Sheria hii ilirekebishwa Mwaka 2018,

Jaji: Mahakama inaona Kifungu hicho cha 38 hakikuwahi Kurekebisha Mwaka 2018 Bali Kuna Ushahidi Wa Kutosha ambapo Sheria hiyo ilirekebishwa l Mwaka 1993, Na Wote tunakubaliana kwamba imekosewa Kurejewa Kimakosa, Sasa baada ya kurejea Sheria hiyo Kimakosa nini Kinafuatia??

Jaji: Ni wazi kwamba sheria inapokuwa imekosewa kurejewa katika Kesi ya MALIMBE kwamba nyaraka ambayo imekosewa inakuwa DEFECTIVE inakosa nguvu za kisheria. Na kubaliana kwa Pamoja Na Maamuzi ya JOHN MARCO Na Kwamba huo ndiyo Msimamo wa Sheria.

Kutoa Maagizo Juu ya mamlaka, Maombi Kama haya yalilejewa Katika Maombi ya Jinai namba 3 ya Mwaka 2012, Imeelezwa Kwamba Pale ambapo Kunakosewa Kurejea Sheria Vizuri Kunifanya na Kuinyima Mahakama Kufanya Maombi Mahakama.

Jaji: Na kwamba kanuni hiyo kwamba kukosa nguvu Kwa Nyaraka inafanya Ife maamuzi hayo hayaingii kote bali kuna sehemu mbalimbali, Mahakama Imeona Kwamba Yapo Maamuzi ya Mahakama Ya Rufani Kwamba Kukosewa Kurejea Sheria Mbalimbali Kunifanya MAHAKAMA kutoa Nafuu kwenye Kesi hiyo na

kwa Mazingira ya Kesi ya JOHN MARCO ni Tofauti kabisa na Kesi iliyopo Mbele yetu, Mahakama Inapofanya Maamuzi iangalie haki zaidi, Mahakama Imeamua Kuangalia Mapungufu Yanayokuja na Masuala ya Kisheria

Yametajwa Vizuri Kwenye Rejea ya Kesi ya SAIDI KINDAMBA dhidi Ya Jamhuri na Maamuzi ya Seleman Abdallah Dhidi Ya Jamhuri, Ambapo Kote walieleza kwamba Dhumuni la Nyaraka ni CERTIFICATE OF SEIZURE ni Malengo yanayotofautiana, Kwa Maana hiyo na kubaliana na na Upande wa mashitaka

Jaji: Nyaraka yoyote ambayo inafanya MOTION ya kuomba Mahakama ifanye Maamuzi Inafanya Mahakama Ifanye Maamuzi, Na Kwamba Nyaraka Iliyopo Mahakamani siyo Nyaraka Inayofanya MAOMBI Mahakamani, MAZINGIRA haya ni Tofauti na Mazingira Niliyoyataja hapa Juu

Sheria Vizuri kumemuathiri Vipi, Kwa Mtizamo huo huo nitaona Kwamba Kwamba Mahakama Kuu kwa kutokurejewa Vizuri kwa Mashtaka kama hakutoonyesha Kumeathiri Vipi, Mahakama hii Inakubali Mambo yafuatayo...

Makosa na ikasema Maneno Yafuatayo.. Majaji katika Maamuzi hayo walisema Maamuzi ya Charles Mwinyichande Dhidi ya Jamhuri na Said Ally Dhidi ya Jamhuri wakasema Kwa sasa Mahakama Imekuwa na Maamuzi tofauti na Kwamba Kwa sasa lazima Mtu aeleze Mtu kwamba kutokurejewa Kwa

Jaji: Ambapo imekuja na Kanuni kwamba Sheria Kunukuliwa Vibaya haitoshi Kwamba KutoKurejea Kwa Sheria hiyo Kunafanya Nyaraka hiyo iwe imekufa, Lazima aeleze ni Kwa namna gani Kwa Kukosewa Kwa Kesi hiyo Kuna fanya Nyaraka hiyo Kuwa Imekufa, Mahakama ya Rufani iliona Kwamba Kuna

Katika hali hiyo basi Mahakama Inaona Katika Shauri hili kwamba Kuwepo Kwa Mwaka 2018 Kimakosa hakujaelezwa kwamba Kunaathiri Vipi Upande wao, Kwa namna hiyo basi natupilia mbali Pingamizi na Mahakama Inapokea Kielelezo Cha Seizure Certificate....

Jaji: Hakuna Ubishi Kwamba Kukosewa Kwa Kurejea Kwa Sheria Kwa Nyaraka Ambayo inaleta Maombi Mahakamani Kunafanana na Seizure Certificate, Katika Mazingira hayo ni wazi Kwamba Kwa Kanuni hiyo ambayo Nyaraka ambazo Kesi Mahakamani lazima zifuate Utaratibu huu

Jaji: Shahidi wenu yupo wapi upande wa mashtaka?

Jaji: naomba sasa shahidi apokee nyaraka hiyo na asome mahakamani.. Shahidi anachukua na kuanza kusoma maelezo yake..

Shahidi kamaliza kusoma maelezo yake..

Wakili wa Serikali: Shahidi Kwa Mujibu wa Fomu hiyo, Hati ya Kukamatia Mali ilikuwa inamhusu nani?

Shahidi: Adam Kasekwa Alimaarufu Adamoo

Wakili wa Serikali: Wakati Unatoa Ushahidi Wako Mwanzoni Ulisema Unampekua Mtu anaitwa Adam Kasekwa Je Adamoo inatoka wapi

Shahidi: Wakati najaza Fomu hii kwa Ukamilifu ndipo alinitajia Majina yake, alimaarufu Adamoo

Wakili wa Serikali: Wakati Unajitambukisha Mwanzoni Unajitambulisha ASP Jumanne Malangahe

Shahidi: kwa Ukamilifu naitwa ASP Jumanne Shaban Malangahe. Kwa Kuandika Kwa Kifupi au Kama Sehemu ni Kubwa inatosha naandika yote Matatu, Ni Mimi yule yule..

Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa Kielelezo hicho hebu elezea Vitu Ulivyo vikamata Adam Kasekwa

Shahidi: Ni Silaha aina ya Luger ikiwa na Magazine yenye Risasi tatu

Shahidi: Kwa Mujibu Wa Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai, Sura ya 20 iliyorekebishwa Mwaka 2018 Na Chini ya Sheria ya Polisi na Polisi wasaidizi Iliyo fanyiwa Marekebisho Mwaka 2002

Shahidi: Simu na Laini za Simu Ni sababu Ya Kufuatilia na Kupata Ushahidi Wa Mawasiliano ya Miamala ya Fedha au Mawasiliano ya Ujumbe wa Simu ambao ungeweza Kusaidia Katika Upelelezi

Wakili wa Serikali: Na Upekuzi huo Ulifanya kwa Sheria gani

Wakili wa Serikali: Baada ya Kufanya Upekuzi huo wa Adam Kasekwa Vipi Kuhusu Vile Vitu?

Shahidi: Nili Sogea Kwenye Gari Nikaanda Hati ya Makabidhiano na Goodluck ambaye nilikuwa nampa tangu Mwanzo

WS: Leo hii hiyo Hati ya Makabidhiano ukiiona unaweza Kuitambuaje

Shahidi: Naweza Kuutambua kwa Mwandiko wangu, Majina yangu na Sahihi yangu Pamoja na Jina la Askari niliyemkabidhi, katika Makabidhiano hayo niliandaa Hati mbili tofauti

WS: Utofauti wake ni nini?

Shahidi: Niliandaa Fomu ya Kumkabidhi Silaha, Pamoja na Magazine na Pia Fomu ya Kumkabidhi Simu na Laini Yenye Namba A5340 Lakini pia ilikuwa na Simu Ndogo ya Itel aina ya, Aina ya 2160, Yenye IMEI namba 353736289120265/353736289120273, Kulikuwa na Line Ya Vodacom, ICC ID 89255044105294533187 Kulukiwa na Airtel Sim Card yenye ICC ID namba 89250509095499322.

Wakili wa Serikali: Ilikuwa je Mashahidi hawa Anita na Esther Wakapatikana,

Shahidi: Nikingakia Sehemu tuliyopata watuhumiwa hawa wawili, Ni wakina nani walikuwa wameona Watuhumiwa Wakikamatwa, Kwani Majengo yale yalikuwa wazi, Ni Wazi wangeweza Kuona Ni nini Kinafanyika

Shahidi: Ningependa Mahakama Ipokee Kama Sehemu ya Ushahidi Wangu

Wakili wa Serikali: Wanaipeleka Nyaraka kwa Mawakili wa Upande wa Utetezi Wanainamia na Kukagua pamoja, Wanaijadili na kuigeuza geuza Wote wanasema hawana pingamizi, na Mahakama inapokea

Shahidi: Nimeitambua Ni Hati ya Makabidhiano Baina yangu na Askari Detective Constable Goodluck WS: Umeitambuaje Shahidi: Kwa Majina Yangu, Sahihi yangu Pamoja na Askari niliyemkabidhi WS: Ungependa Mahakama ifanye nini katika hiyo Nyaraka

Wakili wa Serikali: Hiyo fomu na Risasi 3 Ukiiona Utaitambuaje

Shahidi: Kwa Majina Yangu Pamoja na Sahihi yangu, Pamoja na Jina la Askari niliyekuwa namkabidhi

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Naomba Kumuonyesha Kielelezo

Wakili wa Serikali: Angalia Kama Umeitambua

Shahidi: Nimeitambua Ni Hati ya Makabidhiano Baina yangu na Askari Detective Constable Goodluck

Wakili wa Serikali: Umeitambuaje

Shahidi: Kwa Majina Yangu, Sahihi yangu Pamoja na Askari niliyemkabidhi

Wakili wa Serikali: Ungependa Mahakama ifanye nini katika hiyo Nyaraka

Shahidi: Ningependa Mahakama Ipokee Kama Sehemu ya Ushahidi Wangu

Wakili wa Seriklali: Wanaipeleka Nyaraka kwa Mawakili wa Upande wa Utetezi Wanainamia na Kukagua pamoja, Wanaijadili na kuigeuza geuza Wote wanasema hawana pingamizi, na Mahakama inapokea

Jaji: basi Mhakama inaipokea na Inakuwa Kielelezo namba 12 cha Upande wa Mashtaka Shahidi anasoma upya hiyo Hati ya Makabidhiano...

Shahidi: Nilienda Moja kwa Moja Kwa Mtunza Vielelezo pale Kituo cha Polisi Kati Moshi

Wakili wa Serikali: Sasa Baada ya Kukamilisha Upekuzi Kwa Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya nini Kilifanyika baada ya Upekuzi huo

Shahidi: Tuliondoka na Watuhumiwa kwenda Kituo cha Mjini kati Moshi

Wakili wa Serikali:Shahidi Ulifanya nini Vitu Ulivyo kamata Kwa Adam Ling'wenya, Vitu Ulivyo kamata Kutoka Kwa Mohammed Ling'wenya ulivipeleka Wapi

Shahidi: Nilimkabidhi Constable Goodluck, Simu pamoja na Laini, Kete sikumkabidhi WS: Zile Kete Ulipeleka wapi

Wakili wa Serikali:Kwa Mujibu wa Hati hiyo ya Makabidhiano ni Nani uliyemkabidhi Vitu Ulivyo Vikamata kwa Adam kasekwa

Shahidi: H4347 Detective Constable Goodluck

Wakili wa Serikali: Na Ulimkabidhi nini

Shahidi: Pistol yenye Namba A5340 aina ya Luger pamoja na Risasi tatu ndani ya Magazine

Tukiwa kwenye Gari Afande ACP Aliwauliza Mwenzetu Watatu yupo wapi, Wakajibu yule Kakobe, hatujui kwenye lile eneo ameondokaje,

Wakili wa Serikali Elezea huyo Mtuhumiwa Wa tatu kama Unamfahamu

Shahidi: Watuhumiwa wenzake walisema Majina yake ni Moses Lijenje. Maarufu Kama Kakobe

Akasema Hana, Mimi Nilienda kukabidhi zile Kete za Unga ambazo zilikuwa Nilidhani ni Madawa ya Kulevya, Wakati nakabidhi Kete zile Niliandika Draft la Kukamata ilitufungue Kesi kwa Unga unaodhaniwa kuwa ni Dawa za Kulevya

Wakili wa Serikali nini kilitokea Kituo cha Polisi Kati Moshi

Shahidi: Sisi na Afande RCO Tukiingia kwenye gari yetu na Watuhumiwa Na Mashahidi Wakapanda Gari ambayo ACP kingai aliagiza Kutoka Kituoni, Tulilokuwa Njiani Nilimuuliza Adam Kasekwa Kama ana Nyaraka yoyote Kuhusiana na hiyo Silaha

Wakili wa Serikali Kitu gani Kiliwafanya Muende kwenye hayo Maeneo Mliyoyataj

Shahidi: Washtakiwa walisema ni Maeneo ambayo walikuwa wanapenda kwenda, kupata Chakula au Kinywaji na Eneo kama la Aishi walieleza Waliwahi hata Kukaaa

Wakili wa Serikali Elezea zoezi hili la Kumtafuta Siku hiyo ilikuwaje

Saa Nane Dakika 20 Mpaka 30

Shahidi: Kituo cha Polisi Kati Moshi Tukarudi tena eneo la Rau Madukani, Tukaenda eneo la KCMC, Majengo, Pasua , Tulikwenda Mpaka Hotel ya Aishi ambayo ipo Machame, Tulikwenda Mpaka Boma, Lakini Kote huko hatukuweza Kufanikiwa Kumpata Moses Lijenje

Wakili wa Serikali Nini Kilifanyika na huyu Mtuhumiwa Mmoja

Shahidi: ACP RAMADHAN KINGAI aliwaukiza Mnaweza kutusaidia Kumpata huyu Mtuhumiwa Wakasema Wapo tayari Kuonyesha Maeneo waliyo amini kwamba anaweza Kupatikana

Shahidi: Tulianza zoezi la Kuanza Kumtafuta, Shahidi Lilianza Moshi,

Wakili wa Serikali Elezea hapa Mahakamani kama walipata Huduma ya Chakula

OBJECTION, Tunapinga hilo swali

Wakili wa Serikali Wakati Ufutailiaji Unaendelea nini kilitokea

Shahidi: Tukiwa tunatoka Boma tuliagiza Chakula, Sisi tukiwa Nje ya Gari na Watuhumiwa wakiwa kwenye Gari

Shahidi: Zoezi hilo la Tarehe 05 August 2020 liliisha Kwenye Majira ya Saa 4 kwenda Saa 5, Tukarudi kituo cha Polisi Moshi

Wakili wa Serikali: Mlirudi Kufanya nini

Shahidi: kuwarudisha watuhumiwa, na kuweza Kupumzika ili kesho tuendelee na Zoezi

Wakili wa Serikali: Uliwatoa kwa Madhumuni gani

Shahidi: Tuliwatoa Kwa Madhumuni ya kwenda kutusaidia Kwenda Stendi Kumtafuta Mtuhumiwa Wa tatu


Wakili wa Serikali: Mlikuwa nani na nani

Shahidi: Afande Kingai, Inspector Mahita, Detective Constable Goodluck na Detective Coplo AZIZI ambaye alikuwa ni Dereva

Shahidi: Walikuwa Ndani ya Gari bado wanasubiri Kwenda Kumtafuta Moses Lijenje Alfajiri ya 06 August 2020 Tulikwenda Kituo cha Kati Moshi, Mimi na Mahita Tulikwenda Ndani wakati ACP kingai alibaki Nje, Nilikwenda Kuwatoa Watuhumiwa wote wawili

Wakili wa Serikali: Wakati mmerudi Kituo cha Polisi pale Moshi ni nani uliwakabidhi watuhumiwa

Shahidi: Tukiwa kituoni tulimkabidhi Afande Mahita awakabidhi Watuhumiwa pale Kituoni

Wakili wa Serikali: Wakati Mnakabidhi Ule unga uzani wao Kuwa ni Madawa ya Kulevya Watuhumiwa walikuwa wapi

Lakini Maeneo yote hayo tuliyopita bado Hatukufanikiwa Kumuona Moses Lijenje, Lakini watuhumiwa waliweza Kusema Kwamba Arusha, Sakina Mtuhumiwa Moses Lijenje ana Dada yake,

Shahidi: Tulijaribu Kuangalia Mabasi yanayoenda Mikoa Mbalimbali Kama Morogoro, Dar es Salaam au Arusha, Na Maeneo ambayo tulikuwa tunaingiza na Watuhumiwa ambao tulikuwa tumewakamata. Lakini tuliondoka Kuelekea Maeneo ya Aishi Hotel

Shahidi: Tulifika Kule na Kufuatilia Maeneo hayo Kadri ambavyo watuhumiwa walikuwa wakituongoza lakini hawakuwa na Uhakika na Nyumba anayoishi Dada Yake Lijenje

Shahidi: Baada ya Kushindwa Kumpata tuliamua Kurudi

Wakili wa Serikali: Ulikuwa muda Gani?

Shahidi: Muda huo ulikuwa Saa 10

Shahidi: Ikiwa Muda wa Mchana kwenye Saa Nane tuliamua Kuondoka Kuelekea Arusha Kumtafuta Moses Lijenje

Wakili wa Serikali: Ni akina nani hao walienda Arusha

Shahidi: Mimi Mwenyewe, Afande Kingai, Inspector Mahita, Detective Constable Goodluck, Detective Coplo Aziz

Wakati tunasubiria Gari tuliteremka na Kuagiza Chakula, Wakili wa Serikali Hapo Himo umesema gari ilipata tatizo la Mfumo wa Umeme, Mlikaa hadi saa ngapi, Shahidi Hatukukaa sana, Saa 2 au Saa 3 Gari ililetwa aina ya FOTON na Detective Coplo AZIZI Tukimuacha na Mafundi

Wakili wa Serikali: Safari ya a kuelekea Dar es Salaam Ilianza wapi Shahidi: Ilianzia Moshi, Ambapo Njia panda Himo Gari yetu ilikuwa na Tatizo kwenye Mfumo wa Umeme, Dereva alitueleza

Shahidi: Baada ya Kushindwa Kumpata, afande Kingai alisema amepokea Maelekezo kutoka Kwa DCI wakati huo Rober Boaz Na Kwamba Shauri la Kula Njama za Kutenda Matendo Ya Ugaidi lilikuwa limefunguliwa katika Kituo cha Mjini kati Dar es Salaam

Shahidi: Afande Kingai aliomba Gari kwa Kalama da Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, na Baadae akaletewa Gari Tulianza Safari ya Kuelekea Dar es Salaam na Watuhumiwa wawili, Mom tulikuwa na Afande Kingai, Inspector Mahita, Detective Constable Goodluck na Detective Coplo AZIZI, Tulikuwa tunatumia Gari ya Afande RCO ambayo ni Toyota Landcruiser

Wakili wa Serikali: Mlikuwa na nani Kwenye hiyo Safari

Shahidi: Mimi, Afande Kingai, Inspector Mahita, Detective Constable Goodluck na Dereva wa ile Gari ya Moshi PC wembo

Wakili wa Serikali: Mlikuwa na nani Kwenye hiyo Safari

Shahidi: Mimi, Afande Kingai, Inspector Mahita, Detective Constable Goodluck na Dereva wa ile Gari ya Moshi PC wembo

Wakili wa Serikali: Ukaaji katika ile Gari ya FOTON ulikuwaje Mbele Kushoto alikaa Afande KingaiUkaaji katika ile Gari ya FOTON ulikuwaje Mbele Kushoto alikaa Afande Kingai

Na Mlango Unaofuata Kushoto nilikaa Mimi Mtuhumiwa Adam Kasekwa katika na Kulia ni Inspector Mahita na Nyuma alikaa Constable Goodluck na Mohammed Ling'wenya WS: yenu ilikuwaje Shahidi: Ilikuwa Safi, Hakuwa na Shida yoyote WS: Dar es Salaam Mlifika. Lini

Wakili wa Serikali: Wewe Ulipewa Majukumu gani

Shahidi: Nilipewa Jukumu la Kumuhoji Mtuhumiwa Mohammed Abdilah Ling'wenya

Wakili wa Serikali: Wewe Kama Askari Polisi ni Wakati gani Mtuhumiwa anatakiwa Kuhojiwa

Shahidi: Ndani ya Masaa Manne kuanzia unapomkamata

Wakili wa Serikali: Saa Moja ya Majira gani

Shahidi: Ya Asubuhi, Ya Tarehe 07 August 2020

Wakili wa Serikali: Hebu elezea ni Wakati gani tena mlikutana

Shahidi: Saa Moja Tulikutana, alikwepo Afande Kingai na Inspector Swila, Swila alikuwa anatokea Ofisi ya DCI

Shahidi: Tarehe 07 August 2020, alfajiri, Tulifika Kituo cha Polisi Pale Mjini kati Dar es Salaam, niliwakabidhi watuhumiwa pale, Ilikuwa imeshapita Saa 12 Asubuhi, Afande Kingai alielekeza Kwenda Kupata Refreshments angalau Maji ana akasema Tukutane Saa Moja pale Central

Shahidi: Kuanzia tarehe 05 Mpaka Tarehe 07 August 2020

Wakili wa Serikali: baada ya Kupewa sasa Maelekezo ya kumuandika Maelezo Mohammed Ling'wenya

Shahidi: Tulikwenda kwa Mkuu wa kituo cha Mjini Kati Dar es Salaam Ili nipate Chumba Cha Kuweza Kukaa

Wakili wa Serikali: sasa Mohammed Ling'wenya alikamatwa Tarehe 05 August 2020 Moshi, Nini kilikupeleka uchukue Maelezo Tarehe 07 August 2020

Shahidi: Ni baada ya kukosekana kwa Muda, Kwa sababu tulikuwa tunaendelea Kumtafuta Mtuhumiwa Wa tatu

Wakili wa Serikali: ni lini hiyo Mlimtafuta Mtuhumiwa Wa tatu

Kusema lolote isipokuwa kwa hiari yake Mwenyewe, Chini ya Kifungu cha 24 cha Sheria ya Kupambama na ugaidi, Na lolote atakalolisema Basi Litaandikwa hapo Chini na litaweza Kutumika Kama Ushahidi Mahakamani Kwenye Chumba Cha Mahojiano

Wakili wa Serikali: Taratibu zipi sasa ulizo chukua kwenye Chumba Cha Mahojiano Shahidi: Nilijitambulisha Kwake kwamba Mimi naitwa ASP Jumanne Malangahe Nilimuonya Mtuhumiwa anatuhumiwa kwa Kosa la Kupanga Njama za Kutenda Matendo Ya Ugaidi na hivyo alazimishwi

Shahidi: Alikuwa ajafika na baada ya Muda Akafika na Kwenye Saa 2 na Dakika 20 Asubuhi nilianza Kumuhoji Mohammed A Ling'wenya

Wakili wa Serikali: Kabla ya Kuandika Maelezo, Asubuhi hiyo ukimpata wapi

Shahidi: Nilienda Kwenye Chumba Cha Mashitaka Nikaenda Kumuomba, nikapewa na Kwenda naye

Shahidi: Lilikuwa Chini baada kuandika Particulars Zote na kumuonya Chini yake

Wakili wa Serikali: Baada ya Kumfahamisha hizo Haki alifanya nini

Shahidi: yeye alijibu kuwa ameelewa nimemuonya kwa kosa la Kula Njama za kutenda Ugaidi na Kwamba Katika tuhuma hizo halazimishwi Kusema Lolote Isipokuwa kwa Hiari yake na Lolote atakalolisema linaweza Kutumika kama Ushahidi Mahakamani.. Baada ya Kusema hivyo alisaini na Mimi Mwenyewe nikasaini

Shahidi: Pia nilimueleza anayo Haki ya Kuwepo Mwanasheria Wake, Ndugu, Rafiki au Jamaa wakati Wa Kuandika Maelezo Haya

Wakili wa Serikali: yoye hayo Unavyosema wewe Kwamba Ulimfahamisha, Ulifanya nini

Shahidi: Nilisaini Kwenye hilo Onyo na Mtuhumiwa akasaini

Wakili wa Serikali: hilo Onyo lipo wapi

Wakili wa Serikali: Kuanzia hapo saa 2 na Dakika 20 Mliendelea Mpak Saa ngapi

Shahidi: Mpaka Saa 5 na Dakika 02 Asubuhi, Ambapo Niliandika Uthibitisho akayasoma Mwenyewe, Nikayasaini na Yeye akayasaini sasa ilikuwa imeahafika Sa 5 na Dakika zake Asubuhi

Muda wake wa kuandika maelezo ulikuwa ni Saa 2 na Dakika 20 Asubuhi, Nilianza kuandika Tuhuma alizokuwa anatuhumiwa nazo, ambazo alinisimulia yeye Mwenyewe na alikiri kuhusika na Tuhuma hizo, Wakati ananieleza Mimi nilikuwa na andika Maelezo yake

Shahidi Nilimuhoji Je upo tayari Kutoa Maelezo yako, Akajibu Yupo Tayari, Nikamuuliza tena nani awepo wakati wa Kutoa Maelezo, Akajibu mwenyewe.

Wakili wa Serikali: Kitu gani kinaonyesha alibubali Mwenyewe

Shahidi: yeye a Kusaini, Mimi Kusaini, kukubali Kuhojiwa bila Wakili, Ndugu wala Rafiki

Shahidi: nilichukua na Kumrejeaha pale Chumba Cha Mashtaka

Wakili wa Serikali: Wakati anaandika Maelezo yeye alijitambulishaje?

Shahidi: kwa Majina Matatu ya Mohammed Abdilah Ling'wenya na Jina lake alimaarufu kama DOYI

Wakili wa Serikali: Maelezo uliyoandika yalikuwa ni ya nini

Shahidi: onyo

Wakili wa Serikali: Kwanini ulimpa yale Maelezo baada ya Kuandika ili ayasome

Shahidi: nilimpa Maelezo hayo ayasome ilikujiridhisha Maelezo hayo yapo sawasawa Kama amgahitaji Kufanya Marekebisho angeweza Kunieleza

Wakili wa Serikali: Baada sasa Ya Kumalizia Kuandika Maelezo haya Kwa Siku ile Ulifanya nini

Wakili wa Serikali Unamuona hapa Mahakamani

Shahidi: Namuona hapa Mahakamani

Wakili wa Serikali Kwa Ruhusa ya Mheshimiwa Jaji unaweza Kupita na Kwenda Kumuonyesha

Shahidi: Mohamed Abdilah Ling'wenya ni huyu hapa Mwenye Tshirt Nyeupe, (anaonyesha KWA kumsonta kidole)

Wakili wa Serikali: ASP Jumanne ulisema Wakati wa Briefing Pale Arumeru kwamba Uliambiwa Kikundi hiki Cha Uhalifu kinaratibiwa na Freeman Mbowe

Kibatala: OBJECTION sijasikia akisema hivyo

Wakili wa Serikali: Taarifa uliyopewa na Ramadhan Kingai Kwamba Kikundi hicho kinaratibiwa na Freeman Mbowe hatua gani
zilichukuliwa dhidi yake

Shahidi: Pamoja na Kupewa Briefing Pale Ofisni Kwangu ARUMERU kwamba Freeman Aikael Mbowe ndiye aliyekuwa anaratibu Kundi lile, Kwamba watu wanaoratibu wana mafunzo ya Kijeshi, yaani Makomandoo hatukuwa tayari tumemkamata

Wakili wa Serikali: lini

Shahidi: Tarehe 22 July 2021

Shahidi: Saa 6 Usiku

Wakili wa Serikali: Ni wakati gani sasa yeye alikamatwa

Shahidi: Tarehe 21 Mwezi July Mwaka 2021

Wakili wa Serikali: Wewe Uli husika Vipi baada ya Kukamatwa kwake

Shahidi: Nikitakiwa kuandika Maelezo yake ya Onyo

Wakili wa Serikali: Kwa Sababu gani

Shahidi: Kwa sababu za Kiupelelezi Zingine zilizokuwa zinaendelea, Ili Kujiridhisha

Wakili wa Serikali: Mambo gani mlikuwa Mkifuatilia

Shahidi: Mambo ya Forensic Yaani Uchunguzi wa Kisayansi tukiwa tumefanya Kuelekea Kuwa kamata Watuhumiwa hawa

Wakili wa Serikali: Ulipofika Central ikawaje

Kibatala: OBJECTION Hakuna Mahala Shahidi amesema alifika Central

Jaji: si ndiyo anatoa Ushahidi Wake sasa, We Ulitaka Umsikie wapi?

Kibatala: Ninachosema hiyo ni Leading Question

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji labda Usome Swali la Mwisho

Jaji: Nilijaribu kumuhoji saa 6 na Dakika 51 Usiku

Kibatala: Wapi sasa kataja Central

Jaji: Hakuna

Wakili wa Serikali: Ngoja nibadili Swali. Ulifika lini Dar?

Shahidi: Ilipofika Saa 6 Na Dakika 51 Ndipo Freeman Aikael Mbowe aliletwa Mbele yangu na Inspector Machota

Wakili wa Serikali: Inspector Machota alikukuta eneo gani

Shahidi: alinikuta Katika Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda ya Dar es Salaam (ZCO OFFICE)

Shahidi: Tarehe 21 Mwezi July Mwaka 2021

Wakili wa Serikali: Ulikuwa wapi

Shahidi: Nilikuwa Ofisini Arumeru nilipigiwa simu na DCI Afande Wambura akinitaka nifike Dar es Salaam kituo cha Polisi Kati, ndipo akaniambia Kuna Mtuhumiwa Freeman Aikael Mbowe Ataletwa Mbele yangu niweze Kuhojiana naye kuhusiana na Shauri tuliokuwa tunapeleleza

Wakili wa Serikali: Shauri gani

Shahidi: Shauri au Tuhuma Likiwa na Kumbukumbu namba CD/IR/2097/2020

Wakili wa Serikali: Elezea Sasa ni wakati gani Freeman Aikael Mbowe aliletwa Mbele Yako

Shahidi: Tarehe 21 Mwezi July Mwaka 2021

Wakili wa Serikali: Ulikuwa wapi

Shahidi: Nilikuwa Ofisini Arumeru nilipigiwa simu na DCI Afande Wambura akinitaka nifike Dar es Salaam kituo cha Polisi Kati, ndipo akaniambia Kuna Mtuhumiwa Freeman Aikael Mbowe Ataletwa Mbele yangu niweze

Shahidi: Nilijitambulisha Kwake Kwa Majina Yangu na Cheo changu, Nilimueleza kwamba nataka Kufanya naye Mahojiano WS: Wewe Ulimfahamu vipi Kama ni Freeman Aikael Mbowe Shahidi: alijambulisha Kwamba Yeye ni Freeman Aikael Mbowe, Akaeleza Particular zake Zote, Mahala Anapoishi

Pia anayo Haki ya Kuwepo Mwanasheria Wake, Ndugu yake, Jamaa yake au Rafiki yake ili aweze Kushuhudia Wakati Maelezo yake Yake yakiandikwa, Baada ya Kujibu Onyo hilo alisaini na Mimi nikasaini Hivyo Nilimuuliza Kama yupo tayari Kutoa maelezo yake..? Alijibu ndiyo

Namba zake za Simu, Shahidi: Nilimuonya na Yeye kwamba anatuhumiwa kwa Kosa la Kula Njama za Kupanga Ugaidi Kinyume na Sheria namba 24 ya Kupambana na Ugaidi na Kwamba Halazimishwi Kusema Lolote Kutokana tuhuma hizi, isipokuwa kwa Hiari yake Mwenyewe

Na lolote atakalosema Kitaweza Kuletwa KAMA Ushahidi Mahakamani, Vilevile nilimueleza anayo Haki ya Kuwepo Mwanasheria Wake, Ndugu yake, Jamaa yake, au Rafiki yake, Ili aweze Kushuhudia wakati Maelezo hayo yakiandikwa,

Shahidi: Nilisaini Sehemu yangu na Yeye akasaini sehemu yake, Na akajibu Onyo hilo Kwamba ameonywa kwamba anatuhumiwa Kwa Kosa la Kula Njama na Kufanya Vitendo Vya Kigaidi Kinyume na Kifungu cha 24 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambama na Ugaidi

Shahidi: Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam, KATIKA Ofisi Ya Mkuu wa Upelelezi Kanda ya Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Wewe Ulikuwa wapi

Shahidi: Nilikwepo Kituo cha Polisi palepale, kwa kuwa Muda Mfupi Mtuhumiwa Freeman Aikael Mbowe alikuwa amefika na Wakili alikuwa amefika

Shahidi: Kesho yake Tarehe 22 July 2021 Majira ya Saa Saba na Dakika 51 Mwanasheria Wake Fredrick Kihwelo aliweza Kufika Jaji: Saa Saba ya Muda Gani Shahidi: Saa Saba Mchana, Ndipo alipofika Mwanasheria Wake WS: Alifika wapi

Shahidi: Nilimuuliza angependa nani awepo Wakati Maelezo yake yakiandikwa, Akajibu kwamba angependa awepo Mwanasheria Wake wakati wa Kuandika Maelezo yake, Ambaye alitaja kwa Jina la Fredrick Kihwelo WS: Baada ya Kukueleza Kwamba angehitaji Mwanasheria Wake, wewe Ulifanya nini

Shahidi: Nilisaini na Yeye alisaini baada ya Kumueleza, Nikamuita Inspector Machota ili waweze Kumpata Mwanasheria Wake Na Ufutailiaji ulifanyika na Mwanasheria Wake hakuweza Kupatikana Kwa Usiku Ule WS: Ni Nyakati gani sasa Ka Mlifanikiwa Kumpata Mwanasheria Wake

Wakili wake akiwepo, anatuhumiwa kwa Kosa la Kula Njama za kutenda Ugaidi, Kinyume na Kifungu cha 24, Nikamuuliza Mtuhumiwa ataendelea Sasa Kutoa Maelezo Yake Mbele ya Mwanasheria Kama alivyokuwa ameomba, Akajibu Kuwa hayupo tayari Kutoa Maelezo Yake Mbele ya Afisa wa Polisi

Wakili wa Serikali: Freeman Mbowe alikuwa amefika. Kutokea wapi Shahidi: sikuweza Kujua, Aliletwa tena Mbele yangu na Inspector Machota, Baada ya Mwanasheria Wake kufika, Nilirudia tena Kujitambulisha Mbele ya Mwanasheria Wake Nika rejea Kusoma. Tuhuma zilizokuwa zinamkabili Mtuhumiwa

Shahidi: Baada ya Maelezo hayo yeye alisaini, Mimi Nilisaini na Mwanasheria Wake Fredrick Kihwelo alisaini, Tukawa Tumeishia Hapo

Wakili wa Serikali: Unasema Mwanasheria wa Freeman alifika na Ulirudia Kusoma tuhuma zinazomkabili Shahidi Mwanasheria Wake pia alisaini Katika Maeneo Yote Kuanzi nilipo Muonya, alipo Jibu Onyo, Mpaka Utayarinw kutoa Maelezo,

Wakili wa Serikali: Leo Ukiona hiyo Nyaraka hapa Mahakamani Unaweza Kutambuaje

Shahidi: Uwepo Wa Jina langu, Uwepo wa Saini Yangu, Mwandiko wangu na Yote Niliyoaandika Kuhusiana na Majibu ya Mtuhumiwa

Wakili wa Serikali: Ungependa Mahakama ifanye nini katika Hayo uliyoyatambua

Shahidi: Mahakama Iyapokee Kwa Utambuzi, Kama Sehemu ya Ushahidi Wangu Ninaotoa hapa Mahakamani

Wakili wa serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Kumuonyesha Shahidi Maelezo hayo

Wakili wa Serikali: Hebu angalia Nyaraka hiyo Kama umeitambua na Umeitambuaje

Shahidi: Nyaraka hii nimeitambua kwanza Kwa Mwandiko wangu, Uwepo wa Majina yangu, Sahihi Yangu, Yale Niliyoaandika ikiwemo Majina ya Mtuhumiwa

Wakili wa Serikali: Naipeleka Nyaraka hiyo Upande wa Mawakili wa Utetezi Upande wa Utetezi wanaikagua

Nashon Nkungu: kwa Upande wetu tunapinga Kupokelewa Kwa Nyaraka hii.

Jaji: Spray faili ni Kubwa Sana

Jaji: najaribu kujiuliza kama upande wa mashtaka kuna mambo mnayotaka kuthibitisha kupitia hii nyaraka

Mawakili wa Serikali, wanapekua..

Wakili wa Serikali: kwa Mujibu wa Ph mshtakiwa wa nne alikubali Personal particulars, Kwamba ni Mwenyekiti wa Chadema, Na kwamba alikamatwa Ilemela, Mwanza,

Jaji: Kama nimemuelewa shahidi hii nyaraka Ina maoni kwamba hayupo tayari kuhojiwa na Afisa Polisi na pia Ina particular zake ambazo alizikubali,

Jaji: Kama mnahisi you Neee Eeeeeeeheeeee, You Need Enheeeeeee..

Wakili wa Serikali: Sawa Mheshimiwa tunaweza kupata muda tuweze kutafakari hiyo hoja yako na Ku' respond

Jaj: turudi saa ngapi

Wakili wa Serikali: Saa nane

Jaji: tunahairisha shauri mpaka saa nane

--------

Jaji ameingia,

Kesi imetajwa

Column za mawakili pande zote zipo vile vile

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Wakati Shahidi wa nane, Anatoa Ushahidi alitoa Caution Statement ya Mshitakiwa wa Nne Kuzingatia Ushahidi ambao Imetolewa tunaondoa Maombi Yetu Ili Shahidi Wetu aweze Kuendelea na ushahidi Mwingine

Jaji: Utetezi

Mawakili wa upande wa utetezi wote wanakubaliana na Ombi lao..

Jaji: basi Mahakama imekubali Request ya Kutenda hivyo, Ili Shahidi Aendelee na Ushahidi

Wakili wa Serikali:
Umezungumzia Huyu Freeman Aikael Mbowe, Hapa Mahakamani Umemuona

Shahidi: Ndiyo nimemuona hapa Mahakamani

Wakili wa Serikali: yupo wapi?

Shahidi: Huyu aliye Vaa Tshirt ya Mistari Mistari Meusi Jirani na huyo Askari

Wakili wa Serikali: Ulielezea Kumpekua Adam Hassan Kasekwa, Yupo wapi hapa Mahakamani

Shahidi: Mtu aliye Vaa Shati Nyeusi Watatu Kutoka alipokaa Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: Ulisema Kwamba Mnamo Tarehe 07 Mwezi 08 2020 Uliandika Maelezo Ya Mohammed Abdilah Ling'wenya. Kama Ukiona Karatasi hiyo ya Maelezo unaweza kuitambuaje

Shahidi: Niliona naweza Kuutambua kwanza Kwa Mwandiko wangu, Majina Yangu,

Wakili wa Serikali: Unaitambuaje

Shahidi: Uwepo Wa Majina yangu, Sahihi Yangu, Uwepo wa Majina ya Mtuhumiwa na Sahihi Yake pamoja na Vitu Vilivyo humo ndani

Wakili wa Serikali: Ungependa Mahakama Ifanye nini Kuhusu Nyaraka hii?

Shahidi: Naomba Ipokee Kama Sehemu ya Ushahidi ninaoutoa hapa Mahakamani

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Kumpatia shahidi Karatasi ya Maelezo aweze Kuitambua

Wakili wa Serikali: angalia Nyaraka hiyo Kama Unaweza Kuitambua

Shahidi: Naweza Kuitambua Kwakuwa ndiyo nimeandika Maelezo ya Mohammed Abdilah Ling'wenya

Wakili wa Serikali anaichukua Nyaraka ile anaipeleka kwa Mawakili wa Upande wa Utetezi Mawakili wa upande wa utetezi wanaikagua

Fredrick Kihwelo: Kwa niaba ya Mshtakiwa Wa tatu tunapinga Kupokelewa Kwa Maelezo haya.. Naomba nitaje sababu...

Fredrick Kihwelo: 1. Mshitakiwa Wa tatu hakawahi Kuwa Katika Kituo cha Polisi Mjini Kati Dar es Salaam kwa tarehe tajwa wakati wa Kurekodi Maelezo 07 August 2020 au Tarehe yoyote ile

Fredrick Kihwelo 2. Mshtakiwa wa tatu aliteswa katika kutoa Sahihi yake, Katika Maelezo ambayo hajawahi kuandika Kwa Maelezo yake huko Kituo cha Polisi Mbweni, na Hakuruhusiwa Kusoma hayo Maelezo

Fredrick Kihwelo: Mateso yalikuwa kwa Vitisho, kisaikolojia Vilivyotolewa na D/C GOODLUCK MINJA ambaye alikuwa amemshikia Bastola na ASP JUMANNE MALANGAHE ambaye alimtishia Kwamba Asipo weka Sahihi yake, Mateso yatafuatia Kama alivyofanyiwa KITUO CHA POLISI MJINI KATI MOSHI.

Fredrick Kihwelo: 3. Maelezo ya Mshtakiwa wa tatu yamerekodiwa kinyume na sheria ya masaa 4 kinyume na Kifungu cha Sheria 50(1) a & b cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) Sura 20 ya Mwaka 2019

Fredrick Kihwelo: 4. Maelezo ya Mshtakiwa wa tatu yamechukuliwa kwenye Sheria ambayo Haipo ya Kifungu cha 57(3) CAP 20 Iliyofanyiwa Marekebisho Mwaka 2018 Mshtakiwa wa tatu hakuonywa Kwa Mujibu wa taratibu kwa Shahidi wa 08 KUSHINDWA Kunukuu kifungu cha sheria cha 57(3)

Wao Wameongeza Kifungu cha 24 Wakaweka Kipengele cha pili, Kwenye Maelezo halisi ambacho anataka Kutuletea Wanatudanganya Kwa kuwa Maelezo Halisi hayana Eneo lililo Andika hivyo, hivyo wanatudanganya..

John Mallya: Mheshimiwa Nitaongezea Kwa ajili ya Mshtakiwa Wa Pili Mahakama hii imeshazungumza Mara Kadhaa Kuhusu Kupatiwa Nyaraka Kwenye Committal, Kwenye Makabrasha Inaonekana Statement Ya Mohammed Abdilah Ling'wenya Kwenye ile PRE TRIAL BUNDLE Type INAONEKANA Kifungu cha 24,

John Mallya: Kwa Maneno sahihi Wame EDIT kwa Maelezo yanayotakiwa Leo Kutaka Kutolewa Mahakamani, Kwa Maana hivyo Wanatudanganya na Wanadanganya Mahakama Yako. Tusingekuwa Makini tusingejua ni Nyaraka Iliyo editiwa*

John Mallya: UONGO huu wa wazi ukitaka kuwapa Faida washtakiwa ni Kukataa hii Statement Isipolelewe Kwa Maana Nyaraka Iliyowekwa Kisutu siyo Nyaraka inayo takiwa kwa kesi hii....

John Mallya: Wateja wetu wanateseka Kwa Uongo ambao Jamhuri wameutengeneza..

Wakili wa Serikali PIUS HILA: OBJECTION Mheshimiwa Jaji anatumia Maneno Makali sana na Tuhuma Nzito Sana

Wakili wa Serikali: Maneno UONGO WA JAMHURI, Nyaraka Ina Mwandishi na Mahakama inaweza Kuangalia, Lakini Mahakama Ilisema Imuachie Aseme WAONGO WAONGO Tutaomba Mahakama Itake Utaratibu Mzuri.. Na Kama Unataka Kuipotezea Sifa Nyaraka Ipo namna Nzuri lakini siyo Kututuhumu wote

Wakili wa Serikali Robert Kidando: ananyanyuka.. Mheshimiwa Jaji pamoja na Taratibu ambazo zipo, Maombi yanayoletwa na Wakili Msomi basi yawe Ya Kisheria, Yaani Wakili anaomba Kwamba hata Nyaraka za Committal Proceedings Zibatilishwe Leo, Jamani Kweli Leo tubatilishe?

Jaji: Umeelewa Mallya

Mallya: Nimeeleza Mheshimiwa Jaji

Jaji: Umeelewaje

Mallya: Kama Wanachukizwa na Neno UONGO, basi kuanzia sasa nitatumia neno Hawakusema KWELI...

Mallya: Kwa kuwa hiki kilichopo leo sicho tulichopewa kwenye Kitita cha nyaraka kwenye hatua ya Commital, na mtu ambaye hasemi ukweli anaitwa MUONGO.. Jaji: na mimi najua kweli anaitwa MUONGO, lakini Kwa Mahakamani tumia lugha ambayo haitowaudhi basi..

Jaji: Mbele Yako Kuna Nyaraka Moja na Wewe Una Nyaraka Tayari. Leo hatufanyi Kwenye Examination ya Commital, Zungumzia kuhusu Nyaraka hiyo, Na Maneno yawe Moderate (YASIWE MAKALI)

Mallya: Mahakamani tunatumia Neno ita koleo ni Koleo (Call a Spade, spade) Siyo kijiko kikubwa

Mallya: Pale ambapo pana kuwa na utofauti kati ya nyaraka ya commital na ya leo inayoletwa Mahakamani, Jambo Jema ni KUKATAA Document, Kwa sababu content ya Nyaraka hiyo inamuingiza kila mmoja wetu..

Mallya: Hii Document Kwenye Commita haikuja ndiyo InaKuja Leo, Lakini Hoja Nyingine Ya Jambo hilohilo la Hii Nyaraka, Kwa Mujibu wa Kesi ya Hii Nyaraka, imetaja Sheria iliyotumika Kuchukua Maelezo hayo kwamba ni ya 2018

Mallya: Lakini kwenye Kitika cha Nyaraka cha Commital Nyaraka hii hii Inaonekana kwamba imechukuliwa Kwenye Sheria ya Mwaka 2019, Athari gani inapatwa na Wateja wetu na Mtu huyo huyo Mmoja anayetaka Sheria hii ipo na Sheria hii haipo??

John Mallya: Zoezi lililozaa hii nyaraka ni zoezi la Kisheria, NYARAKA inapaswa kufuata Misingi ya Kisheria, Kunukuu kwa Sheria ambayo Kwa Tanzania Haipo ni Kutokuzingatiwa kwa Sheria....

John Mallya: Swali lingine Mahakama itajiuliza Nyaraka hii Inai' move mahakama, anaomba Order Ili Mahakama Itamke ni Kielelezo fulani, Mahakama ifanye hayo inapaswa Ifuatwe Kwa Masharti Yake, Ndiyo tunapinga Nyaraka hii Isipolelewe na Tunaomba Mahakama Yako tukufu Itupilie Mbali

Adv. John Mallya.. Mimi ya kwangu ni hayo tu....

Adv. Peter Kibatala; Kwa Niaba Ya Mshtakiwa wa Nne tunapinga Nyaraka hii Kupokelewa kwa Sababu hizi.. 1 Maelezo Ya Onyo hayawezi Kupokelewa bila Onyo (PRE requisite ya Adminisivity) Onyo linaonekana Kupelekwa Kwa Mohammed Ling'wenya Maarufu Kama DOYI Chini ya kifungu 24

Kibatala: Kifungu cha 24(1) kinahusiana Kula Njama Kutenda Matendo Ya Kigaidi Nje ya Tanzania Wakati 24(2) inahusiana na Kula Njama Kutenda Matendo Ya Kigaidi Ndani ya Tanzania Kwa kutokutaja Vifungu Vidogo na Kuishia 24 haionyeshi Nini hasa Onyo lililenga katika Mambo hayo..

Kibatala: 2. Hakuna Sheria Inaitwa Sheria ya Kuzuia na Kupambama na Ugaidi, HAIPO Sheria Tuliyonayo ni Sheria Ya Kuzuia Ugaidi Hapo Hakuna Onyo Kisheria kwa Sababu hizo..

Kibatala: Lakini Pia Mheshimiwa Jaji Nyaraka hii siyo Admisible kwa sababu Onyo limetolewa Kwa Kifungu Cha 57 au 58.. Kwenye Onyo Kuna Vifungu cha 57 na 58 na siyo 57 au 58 na Vifungu hivi vina mataumizi Tofauti...

Kibatala Kesi ya SEKO VS SAMUEL ilisema Vifungu hivi Vina mataumizi tofauti, Kwa Namna hiyo Kwa Niaba ya Mshtakiwa wa Nne tunapinga Kupokelewa kwa Maelezo hayo, Ni hayo tu Mheshimiwa..

Kibatala anaketi,

Anasimama Nashon Nkungu Mheshimiwa Jaji Kwa Niaba ya Mshtakiwa wa kwanza NAPINGA VIKO Kwa Nyaraka hii Kuingia kama Kielelezo Kwenye kesi hii.... Nyaraka haijafika kwenye viwango vya kukubalika Kuitwa Maelezo ya Onyo...

Mara tu Mtu anayehojiwa anapo Anza Kutubu/kukubali Kosa Kuna Onyo lake Tofauti, Kwamba Kutokana ana Uzito unaofuatia, Ndiyo panapokuwa Umuhimu wa Kumuita au kwenda Kwa Justice of Peace..

Nashon Nkungu: Nyaraka hii inatakiwa Kuchukuliwa kwa Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai na Vifungu Vya 57 na 58, Na Moja ya kigezo ni Maelezo ya Onyo Yana KUTUBU kuna mambo kadhaa yanahitajika, Kifungu cha 57(d) cha Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai chapter 20

PS: Justice of Peace... Mnajua maana yake?? ni Mlinzi wa amani, ukiwa umepigwa na makarao na wakakulazimisha kukiri makosa yako ili Uandike Maelezo na Kusaini, huyu ndiye ambaye atakusaidia huko mahakamani ili utoe Maelezo yako bila kupigwa mateke, virungu na kushikiwa bastola

Nashon Nkungu: Mara tu inapoibuka suala la kukubali Makosa au Kutubu 57,2(d), Kinasema...... ANASOMA SHERIA...., Kwamba Pamoja na Mtu anachukuliwa Maelezo, mara tu anapotubu/Kukubali Kosa Mtu huyo anatakiwa Kuonywa tena,

Nashon Nkungu: Kuhusiana na Kilicho fanyika kwa Wateja wetu, Moja ambalo linaonekana Moja kwa Moja, Ni kitu ambacho Linaonekana Ukurasa wa Wa Pili, naye akakubali Kuonyeka Kwa kifungu hichohicho, Hayo ni Madhara ya Kwanza Mteja wetu aliyapata. Katika Mashauri Mbalimbali ya.......

Mawakili wenzake wa utetezi wanansanua asitaje hiyo nondo.. Ni silaha nzito, inaonekana wanaweza kuitumia baadae, Nashon Nkungu amewasoma wenzake, anakausha..

Nashon Nkungu: Mheshimiwa Jaji Kwa hayo tunaomba Kielelezo kisipokelewe kabisa..Na Itakapokamilika ndiyo tufanye yale yanayotokana na Sheria, Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji

Nashon Nkungu: Mheshimiwa Jaji Kwa hayo tunaomba Kielelezo kisipokelewe kabisa..

Na Itakapokamilika ndiyo tufanye yale yanayotokana na Sheria, Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji nimesikia Hoja za Mapingamizi, ambayo ni ya aina Mbili 1.Kwa Maan kwamba Kuna ambayo yanakijita kwemye a kifungu cha 27 cha Sheria ya Ushahidi Sura ya 6 2.Kuna ambayo yanayo jikita kwa Kutokidhi Matakwa ya Sheria ya Mwenendo

Wa Makosa ya Jinai Kwenye Vifungu Kadhaa Kama walivyo Virejea, Kiutaratibu Mheshimiwa Jaji aina hiyo ya Mapingamizi yalitakiwa Kutatuliwa kwa Mawakili Wa pande zote Mbili Kuelezea Mahakama na iweze Kutoa Maamuzi Na yale Chini ya Sheria Ya Ushahidi Yanatakiwa yawe kwa Kesi

Katika kesi ya Msingi, Lakini Sasa Kwa aina ya Mapingamizi Yakiyoletwa hasa yale ya Kutokidhi Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai. Yanaingiliana na Yake Mengine ya Sheria ya Ushahidi, Kama Utaridhia na wenzetu Hawatokuwa na Pingamizi. Tuanze na Kesi Ndogo Katika kesi ya Msingi

Mawakili wenzake wa utetezi wanansanua asitaje hiyo nondo.. Ni silaha nzito, inaonekana wanaweza kuitumia baadae, Nashon Nkungu amewasoma wenzake, anakausha..

Wakili Peter Kibatala: tunakubali MWONGOZO wa Wenzetu lakini tunaomba Maangalizo kwamba Mashahidi tutaoleta Hawatohusika na Pure points of Law.. Na Baada ya Kesi Ndogo ndiyo tuwe na Pure Points of Law

Jaji: ni Lazima tukayachambua yapi yaangukia kwenye Kifungu cha 27 na Kisha tufanye Ya Kisheria, Mnaweza Mkapata Muda wa Kukaa Pamoja na Kuchambua

Jaji: Kuna suala la Kukaa na Kuchambua yapi Yanakuwa Katika kesi Ndogo na yake ya kisheria, LA sivyo tutajikuta tunafanya yote.. Je tutumie Njia gani Kuyachambua

Wakili wa Serikali: Pamoja na Angalizo la Mwenzetu, Kuna Maneno alikuwa anaumia kuwa Mteja alikuwa ameathiriwa, Hata Kama litatolewa Ushahidi naona Mahakama Itaona Jinsi gani itaamua..

Jaji: Mimi pia nakubaliana tufanye kesi Ndogo katika Kesi ya Msingi Bila Kutengeneza Kesi katika Kesi Ndogo, Mkutane, tuoeane Muda, Mnatizama Kipi kinaangukia wapi, Na Mimi nitakaporudi hapa Nitaona, niwape kama Dakika ngapi??

Mallya kaenda kushauriana na Mawakili wa Serikali.... Amemaliza..

Mallya: Mheshimiwa Jaji tumekubaliana Kwa Dakika 20..

JAJI: sawa Dakika 20

Jaji: basi tutarudi baada ya Dakika 20 tuone Mmefika wapi

Jaji anatoka...

--------

Jaji ameingia

Kesi imetajwa

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji tupo tayari Kibatala: pia na sisi tupo tayari.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji tumepitia Mapingamizi yale, Tumeona ambayo yanaweza Kutuongoza Katika Trial within Trial ni Mapingamizi Mawili, Yaliyotolewa na Wakili Fredrick Kihwelo Pingamizi la Kwanza na la Pili..

Wakili wa Serikali: Kwamba Hakuwahi Kuwa katika Kituo cha Polisi Central Dar es Salaam na hajawahi kuchukuliwa maelezo yoyote pale.. Na kwamba Mteja wake alilazimishwa Kuandika Maelezo, Kwa Vitisho Vya Maneno, na Vitisho Vya Kisaikolojia. Mapingamizi Mengine yote ni ya Kisheria...

10 Mwezi wa November Saa 5 Asubuhi

Jaji: Upande wa Utetezi

Kibatala: Ni sawa Mheshimiwa Jaji

Wakili wa Serikali: Ambapo yanaweza Kuwa Adressed Kwa Pande Zote Mbili Kuleta Hoja za Kisheria,

Kibatala: Ni sahihi Mheshimiwa Jaji Jaji: Mmekubaliana tutaanza na kesi Ndogo Katika Kesi Kubwa

Wakili wa Serikali: Sisi Kwa Upande wetu Tunaomba Kujiandaa, na Kwa sababu Sisi ndiyo Tunaanza tunaomba Kuanza Kesho

Jaji: Maombi ya hairisho yamekubaliwa Mpaka Kesho Tarehe 10/11/2021, Saa 5 Asubuhi, mashtaka mnaelekezwa kuleta mashahidi Washtakiwa watakuwa chini ya magereza mpaka kesho asubuhi saa 5 shauri litakaposikilizwa Jaji anatoka
 
Kesi ya mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe inaendelea kuunguruma leo mahakamani baada ya kuahirishwa jana. Leo Jaji atatoa maamuzi ya mabishano ya kisheria yaliyotokea jana kati ya mawakili wa Utetezi na Jamhuri.

Leo Jamhuri inaendelea na shahidi yule yule Jimanne . Kuwa nami.
Asante sana kwa update Mkuu Mungu akubariki macho na masikio Yako mahakamani.

Thank you.

Kazi njema sana wapenzi wa haki
 
Wacha niwahi nafasi


Sijui haji atajua na mwarobaini mtanzuka wa Jana kwa kukata sheria au maagizo ? Wacha tuone
 
Kesi ya mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe inaendelea kuunguruma leo mahakamani baada ya kuahirishwa jana. Leo Jaji atatoa maamuzi ya mabishano ya kisheria yaliyotokea jana kati ya mawakili wa Utetezi na Jamhuri.

Leo Jamhuri inaendelea na shahidi yule yule Jumanne.

Kuwa nami.
Mungu akutangulie Kwa updates zako
 
Kesi ya mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe inaendelea kuunguruma leo mahakamani baada ya kuahirishwa jana. Leo Jaji atatoa maamuzi ya mabishano ya kisheria yaliyotokea jana kati ya mawakili wa Utetezi na Jamhuri.

Leo Jamhuri inaendelea na shahidi yule yule Jumanne Malangahe.

Kuwa nami.
Jamani saa tatu si ndio Hii? Kumbe Majaji nao hawafati muda?

Tuko hapa hata supu imetushinda Kula tunasuburi Mahakama ianze kwanza ndio tunywe supu.
 
najiuliza tu kama mawakili wote upande wa utetezi wakijitoa kwa kutokuwa na imani na mahakama juu ya maamuzi ya Jaji leo, je nini inaweza kuwa mustakari wa washitakiwa ? wajuvi tafadhali.
 
Tusisahau kuwa hii ni kesi ya ugaidi, watu kuuliwa kwa halaiki. Haiwezekani jambazi huyo aachiwe huru eti kwa vile tu walikosea kifungu 38(6) badala yake wakaandika 38(7), au wakasema SIKAMOO JAJI badala ya kusema SHIKAMOO JAJI. Kama walikosea wapewe warekebishe, hi siyo kesi ya ugoni.
 
Tusisahau kuwa hii ni kesi ya ugaidi, watu kuuliwa kwa halaiki. Haiwezekani jambazi huyo aachiwe huru eti kwa vile tu walikosea kifungu 38(6) badala yake wakaandika 38(7), au wakasema SIKAMOO JAJI badala ya kusema SHIKAMOO JAJI. Kama walikosea wapewe warekebishe, hi siyo kesi ya ugoni.
Heat na eat ni viwili tofauti ingawa utamkaji wake ni mmoja.

Thomson na Thompson ni watu wawili tofauti.

Huna akili, kenge takataka kabisa.
 
Back
Top Bottom