Mkuu Ishina, DSTV, ZUKU, Easy TV na wengine watakaokuja hawana vibali vya TCRA ku distribute local contents, the official distributer wanaitwa multiplex operators wako 3. Vituo vya TV vinabaki kuwa content provider hata sisi jf tukiamua kuwa na channel yetu, tunafungua JF TV!.
DSTV wana service licence only lakini hawaruhusiwi kupokea local contents, hata vipindi kama Wanawake live, na lots of Bingo movies kwenye DSTV Swahili, zinarushwa kutokea Afrika Kusini!. Hata hiyo TBC yenyewe kwenye DSTV, iko beamed kwa nchi za Afrika Mashariki tuu, hata ukiwa South Africa, TBC haionekani!.
Hapo ilipo hata hilo la kuonyesha 5 channels bure ni ubabe tosha!, channel ya bure ilipaswa iwe moja tuu, TBC ambayo tunailipia kwa kodi zetu, nyingine zote tulipaswa kulipia!. Kwa msio fahamu TV kama CNN, BBC, Al Jazeera na nyingine za wenzetu zilikwenda digital kitambo kidogo, ukiwa ulaya kuna ma chanell ya CNN kibao suprising, hii tunayoiona huku kwetu kule haionekani!, wakati fulani nikiwa huko ndipo nililiona Tangazo la utalii la Tanzania kwenye CCN masikini Afrika hatulioni!.
Kitendo cha kuilazimisha DSTV ionyeshe hizo chanell tano za bure, ni sawa na kuilazimisha CNN itangaze matangazo ya TBC!. Kwanza huko DSTV hakuna hata chanel moja ya bure, kule inaongea pesa tuu!, na ili kuona mechi zote, lazima kila mwezi ulipie zaidi ya laki!, kama hizi za kulipia elfu 10 kwa mwezi watu wanapiga kelele, DSTV tutaigusa?.
Pasco.