meningitis
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 8,464
- 4,828
- Thread starter
- #141
PASCO,Huyo mkurugenzi ni bora angekuwa alisema hivyo.Walichokuwa wanasema na kusisitiza ni wananchi wahakikishe wananunua ving'amuzi ili mitambo ya analogy itakapozimwa waendelee kupata televisheni za nyumbani bure na za ziada za kulipia.Hawakuweka msisitizo unaotakiwa kuelezea utofauti uliopo kati ya hizo leseni ya ving'amuzi mbalimbali.
Wananchi hao wakawa wananunua bora king'amuzi kama walivyoshauriwa na hao TCRA wako.Usiwatetee kwamba wametoa elimu kuhusu utofauti huu unaousema wewe wa ving'amuzi.Wao walikomaa zaidi na kuwapa elimu wananchi wasitupe tv za migongo,jambo ambalo ni rahisi sana kueleweka wakaacha yale tatanishi kama hili la makampuni.
Sasa wale waliofuata maneno ya hilo li TCRA lako wakanunua ving'amuzi walivyovichagua(sio startimes,ting wala hiyo ambayo umesema ya star tv na ITV,ambayo bado haipo sokoni na tayari wana leseni!) wakitegemea kuwa wataona free local channel kumbe hawakuambiwa kuwa hayo makampuni hayana mandate ya kurusha free channel waende wapi sasa?
Ni serikali ipi ilipaswa kutoa elimu hii kuhusu huu utofauti wa makampuni?Kuwalaumu tu kuwa wabongo ni wazito sio kuwatendea haki kwani watu wengi sana wamenunua ving'amuzi vyao kabla hata ya tangazo lenu rasmi TCRA.Wasiliana na huyo ndugu yako Mungi mwambie aje huku kujibu kwanini watu waendelee kulipia local channel kisa hawakununua ving'amuzi tajwa na wao(TCRA) wala hawakuwaambia wasinunue hivyo ving'amuzi.Kwa nini wanasema sasa ambapo watu wameshanunua ving'amuzi hivyo visivyotakiwa.Huoni kama huku ni kuibiana na kunyanyasana?
mkunashukuru kwa kuendelea kufafanua swali langu la msingi.naona pasco anahangaika sana kutoa details ambazo hatuhizihitaji kwa sasa.