Tanzania: Utawala bora vs Rushwa

Tanzania: Utawala bora vs Rushwa

HIvi suala hapa ni Rushwa, ama kupatanishwa? Nadhani tunaanza kupoteza mwelekeo. Ikiwa kuna rushwa halafu chombo cha kupambana na rushwa kinasitisha uchunguzi, eti sababu mjadala umefungwa, hii ni kali na mpya. watu wataendelea kula RUSHWA na UFISADI utaendelea kama kawaida. Hii ni HATARI SANA.

Kesho Prof. Mahalu akikubaliana (pengine pia tayari) na viongozi wa Serikali, basi kesi itafutwa!????
 
Huu ni mfano wa funika kombe mwanaharamu apite!

Walipa kodi baada ya kukamuliwa mil 100 walihistahili kupata majibu ya maswali haya;

1. Mtu aliyewahonga wajumbe wa kamati ya Haki, maadili ma madaraka ya Bunge.

2. Je aliwahonga kwa sababu gani?

3. Je ni kweli Lowassa alimpigia simu Mengi? na je anamjua mtu aliewahonga wajumbe?

4. Ukweli kutoka Mengi mwenyewe ( his side of the story )


Matokeo yake tumeambiwa Mh Malima apuuzwe! Indeed nadhani Mh Spika ndio wa kupuuzwa hapa.
 
Rushwa ni sehemu ya maisha ya wana CCM akiwemo JK hakuna la kufanyika hapa.Tegemeeni nyimbo tena wakati wa kampeni .
 
Usanii mwingine! These people play with Tanzanians' minds. Sasa huyo Hesea alitangaza kulirukia suala hilo ili kutuchezea shere Watanzania! Yaani uchunguzi wa TAKURU anauhusianisha vipi na mambo ya ndani ya Bunge?
 
To me inaonekana Spika ana madaraka mengine makubwa kwamba hata akikosea vyombo vya sheria haviwezi kumgusa .Jamani tuna kazi kubwa sana sisi wadanganyika
 
Ni hatari sana

Swala hili mimi kwa mtizamo wangu naweza kufananisha na ufa katika msingi uliojitokeza katika nyumba mpya uliyoijenga wakati unajiandaa kuamia.

kuna haja ya viongozi wetu ambao kweli wanania ya kupambana na rushwa kutambua kuwa Tatizo la rushwa kuwa kubwa nchi hii linachangiwa kwa kiasi kikubwa na watendaji wenye dhamana ya kupambana na rushwa

ama kuwa na nidhamu za woga, mambo mengine wao wanahisi tu hiki nikikifuatilia nitaaribu ulaji,

ama watendaji wenyewe kutokuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu walio pewa maana watanzania tunashindwa kutambua kuwa kila binadamu anakipaji chake na sio kila mtu anaweza kufanya kila kitu irimradi kaambiwa fanya hiki. Sisi tunadhani ukimwambia ngombe alinde atalinda tu usiku, ukimwambia mbwa atage mayai atataga tu au ukimwambia kuku akamuliwe maziwa atakamuliwa tu. bila kutambua kuwa hawa kulinda ama kutoa maziwa au kutaga mayai ni kipaji cha asili kama vlivyo vipaji mbali mbalimbali vya wanadamu.

jina la taasisi mchango wake katika kupambana na rushwa ni almost zero hivyo jitihada zetu za sasa za kubadili jina la takuru hazina mantiki katika kupambana na rushwa.

katika takuru tunayoiacha sheria zilikuwepo zeye mapungufu, sasa tujiulize tatizo lilikuwa ni nini? ni mapungufu ya seria yalikwamisha upamabanaji au hata zile zilizokuwepo hazikutekelezwa?

kumtoa mbuzi katika sekta ya utagaji wa mayai ukamweka ngombe katika sekta hiyo hakuna kinachokuwa kimefanyika hivyo katika kuteua tusishabikie mabadiliko ya watendaji bali tushabikie kuwa na watendaji sahihi katika seta husika.

HOJA ILIKUWA KUNA WABUNGE WALIPOKEA RUSHWA SASA PENGINE X-TAKURU WATUELEZE KAMA KUNA UKWELI KATIKA MADAI HAYA YA WABUNGE KUPOKEA RUSHWA JE SPIKA KUFUNGA MJADALA INAMAANISHA KUHALISHA HIYO RUSHWA ILIYOTOLEWA AU ILIYOPOKELEWA.

AU WATUELEZE NI AZINGIRA GANI YANASABABISHA RUSHWA KUWA HALALI?pengine tujue kuwa kama mtu akipokea rushwa kupitisha mambo fulani muafaka ukishafikiwa kosa la rushwa ndio mwisho wake? au linakuwepo mpaka lini
 
Hapa waliochoogopa ni kuumbuana tu hakuna kingine kwa sababu mwelekeo ulikuwa unaoonyesha kuna mkubwa/wakubwa wangeumbuka. Rushwa katika nchi hii haitaisha wala kupungua tutabaki tu kudanganyana. Viongozi waliochukia rushwa toka mioyoni mwao ni wawili tu tangu nchi imepata uhuru nao wote ni marehemu sasa - Mwalimu na kijana wake Sokoine.
Hivi inaingia akilini kwa mtu mwenye dhamana kubwa ya kusimamia chombo kama PCB kuutangazia umma wa watanzania kirahisi tu kuwa uchunguzi dhidi ya wabunge (waliokuwa wajumbe wa kamati ya bunge) waliotuhumiwa kuhongwa na mfanyabiashara mmoja umesitishwa. Hivi kazi ya PCB kuchunguza tuhuma za rushwa ina uhusiano wowote wa kiutendaji na busara za spika?
Mimi sioni kama kuna juhudi zozote makini za kutokomeza rushwa kwa sababu hata adhabu zilizopo kwenye sheria mpya ya rushwa ni kichekesho. Adhabu ni ndogo mno au kwa sababu hao watunga sheria ndio wala rusjwa wenyewe?
 
"Spika mwenyewe ametangaza kufunga mjadala huo. Wewe unataka sisi tuendelee nalo la nini," alisema Hosea alipoulizwa na HabariLeo kuhusu hatua iliyofikiwa na PCB katika uchunguzi wake.

Bwana Hosea aidha hajui kazi yake au amefanya makusudi. Anachotaka kusema ni kuwa Taasisi yake inachunguza rushwa kwa kutumwa badala ya kutumia clues kutafuta ukweli; yaani anasubiri atumwe na spika kupeleleza rushwa ndani ya bunge? Kwa maana nyingine kama kuna rushwa wizarani basi atasubiri apate kibali cha Waziri? Hajui kuwa taasisi yake ni independent ambayo haijali mamlaka ya spika au ya waziri. Sasa tutajuaje kama Spika naye hakuwa ni mmoja wa waliokula rushwa hiyo na huenda ndiyo maana baada ya Malima kuonekana na hatia ya kuliongopea Bunge bado Spika hakumwadhibu.

Hata hivyo ni afadhali ametanganza kuwa hawafanyi uchunguzi kuliko ambavyo wangefanya uchunguzi na labda kupindisha ukweli.
 
Mhe. Halisi you can't be serious! Yaani tunaanza kupoteza mwelekeo au tulishapoteza masiku mengi yaliyopita?
 
Kigogo anaswa na PCB

2007-05-01 17:33:00
Na Janneth Kiure, Kibaha


Kigogo mmoja wa Serikali mkoani Pwani amejikuta akinaswa juujuu na askari wa Kikosi cha Kuzuia Rushwa nchini, PCB baada ya kudaiwa akipokea mlungula wa maelfu kibao ya pesa za Kibongo.

Kigogo huyo aliyekumbwa na zali baya na linaloweza kumharibia kila kitu kazini kwake, ni Lucius Mulokozi, Ofisa wa Mifugo wa Kituo cha Kwala mkoani Pwani.

Anadaiwa kigogo huyo kuwa amebambwa `laivu` katika baa moja maarufu pale Mlandizi mkoani Pwani, akipokea mlungula wa Sh.600,000 kutoka kwa mfanyabiashara wa ng`ombe.

Hatahivyo, soo la ofisa huyo limeshatua kortini ambapo hivi karibuni, liliunguruma pale kwenye Mahakama ya Wilaya ya Kibaha.

Ikadaiwa mbele ya Hakimu Victoria Nongwa wa korti ya wilaya kuwa Ofisa huyo wa Mifugo, amepokea rushwa kutoka kwa mfanyabiashara mmoja wa ng`ombe.

Akisoma hati ya Mashtaka, Mwendesha mashtaka wa PCB mkoani Pwani, Thuwaiba, alidai kuwa mnamo Aprili 8 mwaka huu, mshtakiwa alidai na kupokea pesa hizo za rushwa kutoka kwa mfanyabiashara Abdallah Hemed, kupitia kwa mwenzake aitwaye Lukumano Mulungu.

``Mheshimiwa hakimu... nia yao ilikuwa awarudishie ng`ombe zaidi ya 200, aliokuwa amewafukuza katika kituo cha Kwala kilichopo chini ya Wizara ya Mifugo,`` akadai Mwendesha Mashtaka huyo.

Hati ya mashtaka ikaendelea kudai kuwa, katika baa moja maarufu pale Mlandizi, mshtakiwa alipokea rushwa bila kujua kuwa maafisa wa PCB walikuwa tayari wamemuwekea mtego maalumu na hatimaye kufanikiwa kumnasa.

Ikadaiwa kuwa mtuhumiwa aliomba pesa hizo kutoka kwa mfanyabiashara Hemed ili amrudishie ng`ombe wake katika kituo cha Kwala ambacho ng`ombe huhifadhiwa kwa muda kwa ajili ya chanjo kabla ya kupelekwa Jijini Dar es Salam kwa kuchinjwa.

Hata hivyo, ilidaiwa kuwa mtuhumiwa alifukuza ng`ombe hao akiwa na vijana wa mfanyabiashara Hemed na kutaka kiasi hicho cha fedha ndipo awarudishe kituoni hapo.

Mshtakiwa amekana shtaka lake kwa nguvu zote, hadi Mei 8, mwaka huu na kuswekwa lupango baada ya kukosa wadhamini.

SOURCE: Alasiri

Jamani hebu angalieni vigogo wanaokamatwa na PCB!!. Pamoja na kuwa kweli mtuhumiwa alikuwa akipokea rushwa na anastahili kuchukuliwa hatua, rushwa inayosumbua watanzania siyo hii na wala PCB hawakauwa na haja ya kutangaza "mafanikio yao haya" kwa mbwembwe vile.
Mtu huyu siyo Kigogo kama PCB wanavyodai hata kidogo; vigogo ni wabunge, mawaziri na maofisa wakuu serikalini ambao wanapokea rushwa kubwa kubwa lakini PCB inawafumbia macho hadharani kabisa.

Kwa jumla mimi nadhani PCB siyo ya lazima hapa nchini, napendekeza maofisa wake wapewe kazi nyingine tu.
 
Kichuguu.. nilipoisoma hiyo habari nilitegemea kuona "Waziri", "Mkurugenzi Mkuu wa...".. Kumbe neno kigogo limepoteza maana!! Napendekeza neno jipya... "Vijiti"!!
 
credibility ya waandishi wetu sijui ipo wapi????na wao kwa macho yao wameona huyu ni kigogo, kwa nini hawatangazi rushwa kubwa kubwa. Za mikataba? n.k
 
Jamani mimi napendekeza PCB ivunjwe maana haina kazi kabisa. PCB haina meno ni kama vibaraka tuu sasa inafaida gani kwetuu? Napendekeza PCB ivunjwe na hizo pesa zipelekwe kwenye maendeleo ya jamii kama elimu na afya. Garama ya kuwa na PCB ni kubwa mmno ukilinganisha na faida. PCB wamekuwa kama kikundi cha maigizo wanamkamata hata mlizi kwa kupokea sh 100 wanatangazi ni vigogo. Sisi hatutaki watutangazie hiz rushwa za kueana zawadi ya mlo wa jioni ila watutangazie Rushwa za mikataba etc. Napendekeza PCB ivunjwe au ibinafsishwe.

Hawa waandishi wetu nao sijui tuwafanye je maana huwa wanaandika habari kupotosha watu ili wauze magazeti na si kuwahabarisha wananchi
 
Kichuguu, yaani afisa mifugo ndiyo kigogo? Mimi nadhani huyo ni dagaa na si samaki.
 
Shadrack Sagati
HabariLeo; Wednesday,May 02, 2007 @00:05

SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta amesema hakuituma au kuiambia Taasisi ya Kuzuia Rushwa (PCB) kuacha uchunguzi wa tuhuma za rushwa kwa wabunge kwa sababu taasisi hiyo haiko chini ya mamlaka ya Bunge.

Aliiambia HabariLeo jana kuwa anachofahamu yeye ni kwamba alifunga mjadala huo bungeni na siyo kwa vyombo vingine vilivyopewa jukumu la kuchunguza tuhuma za rushwa. Alisema aliufunga mjadala huo ili wabunge wapate fursa ya kujadili mambo mengine yenye maslahi ya taifa.

“Ule mjadala niliufunga bungeni, hayo mengine sina mamlaka nayo na wala siyo wajibu wangu kuamuru PCB kuacha kutekeleza majukumu yake,” alisema Sitta.

Tuhuma kuwa wajumbe wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge walipokea rushwa kutoka kwa mfanyabiashara Yussuf Manji wakati wa kusikiliza shauri la Mbunge wa Mkuranga, Adam Malima na Mwenyekiti wa IPP Reginald Mengi, yalitolewa na Mbunge wa Moshi Mjini, Phillemon Ndesamburo.

Spika alitoa ufafanuzi huo baada ya kuombwa na gazeti hili kueleza hatua ya PCB kutangaza kufunga uchunguzi dhidi ya tuhuma za rushwa dhidi ya wabunge zilizotolewa na Ndesamburo.

Akifunga mjadala huyo wakati wa mkutano wa Bunge uliopita, Sitta alisema kuna matatizo mengi yanayowakabili wananchi ambayo yanapaswa kujadiliwa na wabunge.

Mkurugenzi Mkuu wa PCB , Edward Hoseah, baadaye alinukuliwa na gazeti hili akieleza kuwa taasisi yake haina haja ya kuendelea na uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo baada ya Spika kufunga mjadala huo.
 
hawa pcb ni kambi ya wanamtandao,kwa mantiki hiyo basi wanacheza mduwara.wananikumbusha enzi za chuu chuu
 
Hiyo ngoma Hosea lazima uchomoe, suala zima lina direct link na Lowassa. Kama ni kuhojiwa na Lowassa nae ahojiwe kwani ndie alienukuliwa na Ndesamburo kuwa EL alimpigia simu Mengi kumtahadharisha kuwa wabunge wamehongwa.

Kwa Hosea kukomolia jmabo hili ni sawa na kumtosa Lowassa. Ukizingatia ndio kwanza kakalia kiti asije akaonekana hajui jinsi ya "kuishi" za wazee.

At the end of the day nae kaangukia kwenye busara zake.

Tunaomba basi Hosea na yule "kigogo" afisa wa mifugo mlie mkamata baa Mlandizi akichukua mlungula wa 600,000 mjadala wake muufunge. Acheni double standards, tumechoka!
 
Kichuguu.. nilipoisoma hiyo habari nilitegemea kuona "Waziri", "Mkurugenzi Mkuu wa...".. Kumbe neno kigogo limepoteza maana!! Napendekeza neno jipya... "Vijiti"!!


I like that one...Vijiti is a proper.

Kichuguu

Unajua hata hao wabunge sio wote ni VIGOGO, vigogo wenye kustahili hadhi hiyo hawazidi hata 150 au sana sana 200.

Vigogo ni wale ambao Mkandara alisema hata Mtikila mwenyewe anawaogopa...!!

Wale ambao wanamfanya JK aendelee kutabasamu tu na kutoa maonyo kila siku badala ya vitendo....mfano wale waliochukua Hela BoT na kujenga kiwanda cha kusafisha Dhahabu Dar.
 
Death penalty for China official

Zheng Xiaoyu was accused of accepting some $850,000 in bribes
China has sentenced the former head of the State Food and Drug Administration to death after he was convicted of corruption, state media has reported.
Zheng Xiaoyu was convicted on charges of taking bribes and of dereliction of duty, Xinhua news agency reported.

The sentence is unusually harsh for a senior figure, but Zheng could have his sentence reduced to life on appeal.

The verdict came as the government announced plans for the first ever recall system of unsafe food products.

Beijing has been under pressure to act over increasing concern both at home and abroad about the poor standards of Chinese-produced food and medicines.

Name poisoned

State television showed footage of a grey-haired Zhang - who was expelled from the Communist Party earlier this year - appearing in court in Beijing flanked by police officers.

He had been accused by an official investigation last month of accepting more than 6.5m yuan ($850,000) in bribes to approve hundreds of drugs.

One company, Kongliyuan Group, allegedly paid Zhang bribes in return for approving 277 drugs, mostly antibiotics.

Zheng's former secretary, Cao Wenzhuang, also faced trial, accused of accepting bribes.

Thirty-one other people were also alleged to have been involved in the scandal, including Zheng's wife, Liu Naixue, and his son, Zheng Hairong.

Following Zheng's sacking in 2005, the Chinese government announced a review of about 170,000 medical licences that were awarded during his tenure at the agency.

Dozens of people have died in China because of poor quality or fake drugs.

Last year, a sub-standard antibiotic, Xinfu, which was not properly sterilised, caused the deaths of 11 people.

Thirteen babies died of malnutrition in 2005 after being fed powered milk that contained no nutritional value.

The Chinese government recently announced an urgent review of industry food standards after public alarm over a recent spate of cases.

US inspectors blamed exported Chinese pet food ingredients, contaminated with melamine, for the deaths of cats and dogs in North America.

And they recently halted shipments of toothpaste from China to investigate reports that they may be contaminated with toxic chemicals.

On Tuesday, as Zheng was sentenced, the government said a new recall process targeting "potentially dangerous and unapproved food products" would be brought in by the end of the year.

"All domestic and foreign food producers and distributors will be obliged to follow the system," Wu Jianping, of the General Administration of Quality Supervision, Inspection and Quarantine, was quoted as saying.
 
Back
Top Bottom