Tanzania: Utawala bora vs Rushwa

Tanzania: Utawala bora vs Rushwa

All CCM needs now ni kumeguka. hii itafanya makundi mawili mapya ambayo sasa yatakuwa on equal footing yaogopane kuharibu nchi.
 
yule mpigania haki za weusi huko America,Malcom X alipoulizwa kuhusu mauaji ya wazungu dhidi aliyofanywa na wazungu wenyewe,yaani wao kwa wao alisema (mtanisahihhisha nikikosea) "The chicken are coming home to roost" akimmanisha kuwa maouvu dhidi ya weusi yaliyolelewa na weupe sasa yanawarudia weupe wenyewe...katika hili suala la rushwa kwa CCM ni kwamb 2005,2000 there prevailed massive rigging of votes by CCM against wapinzani,eg Keenja dhidi ya Mnyika pale Ubungo etc,sasa kwa kuwa safari hii ni wao wenyewe ndo mambo hayo...tatizo ni kuwa i don't pity any of them kwani kama ni waadilifu wote basi kwa nini waendelee kulea mfumo mbovu kabisa uliooza kwa rushwa?wamo kina Mkono,Lamwai,Mwakyembe,etc...God sijui wanasheria wote hawa wanafanyia nini taaluma yao...

by the way hivi hii PCCB ipo kwa ajili ya kuisafisha CCM tu?mbona 2005 hatukuwasikia?achilia mbali Buzwagi,RICHMONDULI,Kiwira,etc?
 
Rushwa na wizi wa kura ni mtoto wa CCM, sasa mtoto amekua na kaamua kuwaibia wazazi wake.

Je JK ana ubavu? Akitaka kusafisha chama, hahitaji ushahidi, lazima awatoe kafara baadhi ya viongozi ambao wametajwa kwenye hizo rushwa. Kama hao wabunge wawili, kinachotakiwa ni kuwafuta uanachama na hivyo kuwafanya wapoteze ubunge.
 
Mwanasiasa mkongwe aitabiria mabaya CCM kwa rushwa
*Asema rushwa inakipeleka chama pabaya
*Asisitiza viongozi wa juu ndio wanunuzi wa kura

*Amtaka Kikwete kuwadhibiti wasaidizi wake

Claud Gwandu na Michael Uledi, Dodoma
Kutoka Gazeti la Mwananchi

MWENYEKITI wa wenyeviti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Pancreas Ndejembi (77) ameonya kuwa chama hicho kiko katika hatari ya kuporomoka ikiwa hatua za dhati, na za haraka za kupambana na rushwa ndani yake, hazitachukuliwa

Akizungumza katika mahojiano maalum yaliyofanyika nyumbani kwake Kilimani mjini hapa juzi, Mzee Ndejembi ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma anayemaliza muda wake, alisema rushwa ndani ya chama hicho tawala imefikia mahali pabaya na kwamba viongozi wa juu wa chama ndio wenye uwezo wa kutoa rushwa kwa ajili ya kununua kura.

“Mkulima hana pesa…ataitoa wapi? Lakini hawa viongozi wa juu na matajiri ndio wenye pesa na wanatumia pesa zao kutaka kukifikisha chama pabaya ni lazima ifikie mahali tuamue kukiokoa chama chetu, ” alisema Mzee Ndejembi ambaye amekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma tangu mwaka 1982.

Alisema malalamiko yanayotolewa katika uchaguzi wa CCM unaoendelea nchini ni dalili mbaya kwa chama hicho na kwamba wananchi hawawezi kuendelea kuvumilia vitendo hivyo vya kihalifu.

“Hakuna chama kinapendwa kama CCM lakini hii tabia ya rushwa inayoendelea itawafanya wananchi wakichukie kwa sababu wengi hawataki kuona chama chenye heshima kama CCM kinachagua viongozi wake kwa misingi ya dhuluma.

“Kelele zote za rushwa zinazosikika hivi sasa ni kutengeneza mazingira kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2010. Wanataka kuweka watu wao ili wapite kwa urahisi katika nafasi za ubunge, na hii si tabia ya CCM,” alisisitiza.

Alisema wanaweza kukabiliana na rushwa ndani ya CCM kwa viongozi wa juu wa chama hicho kuweka mikakati ya kupambana na rushwa kwa kuwakataa walioshinda katika chaguzi hizo kwa misingi ya rushwa.

“Si jambo rahisi kuimaliza rushwa mara moja lakini viongozi wa juu wakichukua hatua na kila mwanachama akaona madhara ya hatua hizo basi wengine wataogopa kuendelea na mambo ya rushwa,” alisema.

Ndejembi alisema kuwa, kama viongozi wa juu wakiacha tabia hiyo na kuhakikisha kunakuwapo na utengamano wa kimaadili, itasaidia kukirejesha chama katika mstari badala ya hali inayoelekea kujijenga hivi sasa.

Mwenyekiti huyo wa wenyeviti ambaye ameamua kung’atuka mwaka huu na kuamua kuwa mkulima wa kisasa, alisema kuwa viongozi ndiyo wanaojenga tabia hiyo ya kutoa rushwa kwani hata magari yanayozunguka huko na huko katika azma ya kuhakikisha ushindi unapatikana kwa njia zisizo halali, ni ya viongozi.

Ndejembi alisema kuwa, wengi wa watu wanaohusika na rushwa hiyo wana uwezo mkubwa wa kifedha, kitu kinachoambatana na uroho wa madaraka.

Alifafanua kuwa, watu wanaotoa rushwa na kujenga himaya mpya ya viongozi wasio waadilifu wana lengo la kuhakikisha wanawafuga baadhi ya viongozi kwa manufaa yao hususani linapokuja suala la kuondoa majina ya wenzao wanapotaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Alisema kuwa matajiri kwa upande wao wamejikuta wakitaka kuingia katika nafasi za chama hicho kwa kile alichosema kuwa ni kutaka pamoja na mambo mengine, kupata hati za kusafiria za kidiplomasia ili warahisishe shughuli zao za kibiashara na akataka hatua za makusudi kudhibiti hali hiyo zichukuliwe.

Ndejembi alisema kuwa kimsingi katika taifa hili, rais wa nchi ni mmoja tu na akashangaa kuona baadhi ya watu wanawanunua watu na akahoji wanawanunua watu hao kwa lengo lipi.

Hata hivyo Ndejembi anayeonekana kuwa na imani kubwa na Rais Jakaya Kikwete alimshauri kiongozi huyo mkuu wa nchi akisikia kuna matatizo miongoni mwa viongozi wenzake achukue hatua ikiwa ni pamoja na kuwaita ili kuwakemea na kuchukua hatua nyingine za kimaadili.

Mwenyekiti huyo wa CCM anayemaliza muda wake ana maoni kuwa tangu Mwalimu Nyerere afariki chama hicho kimekumbwa na mtikisiko mkubwa ambapo alisema:

”Wananchi hawaoni chama kingine wenyewe wanaita chama cha Mwalimu Nyerere. Sisi tunaanza kuvurunda kwani mgema akisifiwa tembo hulitia maji…mimi nadhani tangu mwalimu aondoke CCM imetikisika sana, wengine wanasema tunakwenda lakini…”

Alisema kuwa katika nchi maskini matatizo haya ya rushwa na ukosefu wa uadilifu yapo na kwamba hata akikosea huthubutu kusema ama kukosoa.

Alisema kuwa baadhi ya watu wakipata uwaziri wanajenga himaya ya kunufaisha watu wao na kwamba anachokiona katika utawala uliopo ni kuwa, Rais Kikwete amewakabidhi madaraka baadhi ya watu ambao wamekuwa hawafanyi vizuri na akashauri rais awakemee mara kwa mara.

“Mkiwa na rais mzuri mambo yanakwenda vizuri, alikuja Mwinyi baada ya Mwalimu, kisha Mkapa wote hawa walifanya vizuri na sasa kaja Kikwete anaonekana ana mawazo ya Mwalimu..ila vijana aliowakabidhi madaraka hawafanyi vizuri na kama rais akiwakemea mara kwa mara itasaidia, ”Alisema Ndejembi.

“Nadhani tuwe na kiwango fulani, lazima tuwe na limit… huko kujilimbikizia mali lazima kuwe na mipaka, ”Alisema Mwenyekiti huyo wa Wenyeviti wa CCM wa Mikoa.

Alipotakiwa kutoa wosia wake kwa wanachama wa CCM nchini, Ndejembi alisema kuwa, kwa maoni yake anadhani kuna umuhimu mkubwa wa kuendesha semina za uraia kwa viongozi na wanachama nchi nzima juu ya ubaya wa rushwa na juu ya tabia ya unyanyasaji kutokana na uwezo.

Alisema sanjari na hilo, semina hiyo ijielekeze katika kukemea tamaa iliyojengeka kwa baadhi ya wanachama kutaka fedha katika masuala ya kuchagua viongozi ili watambue kuwa kufanya hivyo ni kujidhalilisha.

“Ningeomba tusiharibu jina zuri, umoja wetu, mshikamano wetu. Na mengine yote ambayo ni mabaya yaachwe na kura ipigwe kwa mtu anayefaa, mwenye maadili mazuri, mkereketwa katika maendeleo ya watu,” alisema Ndejembi.

Mwenyekiti huyo alishauri pia watu wanaogombea uongozi katika chama na hata katika nyanja za kisiasa na kijamii, kuachana na tabia ya kuomba fedha kwa matajiri na kwamba kinachotakiwa hivi sasa ni kukirejesha chama katika msimamo wa kuheshimu watu.
 
Taasisi ya Kuzuia rushwa yawachanganya wana CCM
*Baadhi walalamika inakiumbua chama
*Wengi wahofu kunaswa kama itaongeza kasi

*Tuhuma za rushwa kwa wabunge zazua hisia mpya

Na Timu ya Waandishi Wetu Dar, Mikoani
Kutoka Gazeti la Mwananchi

CHAGUZI za CCM zinazoendelea, ambazo wiki iliyopita zimeibua matukio makubwa ya kihistoria hapa nchini, hususani tukio la kunaswa katika tuhuma za rushwa kwa wabunge wawili wa CCM mkoani Arusha, zinaelezwa kuzua hali tete kufuatia baadhi ya watu wenye nafasi katika chama hicho kupishana katika kauli hasa kuhusu kitendo hicho cha kutumia vyombo vya dola kudhibiti rushwa katika chama.

Taarifa za ndani kutoka CCM zinaeleza kuwa, hatua ya TAKUKURU kuanza kuonyesha makucha, ikiwa ni kuitikia agizo la Rais Jakaya Kikwete aliyewaamuru kuchunguza vitendo vya rushwa katika chaguzi za chama, hasa baada ya kuanza kuwepo malalamiko kuhusu matumizi ya fedha katika kununua kura, zimewafanya baadhi ya wanachama na viongozi wao kuwa na kauli tofauti huku wakiwepo wale wanaosema chama kinachafuliwa na wengine wakisema kinasafishwa.

Kuna taarifa kuwa, baadhi ya viongozi wa CCM hawakupenda tukio la tuhuma za rushwa kwa wabunge wao, Elisa Mollel (Arumeru Magharibi) na Lekule Laizer (Longido), tukio lililofanywa na TAKUKURU na wanaeleza kuwa, linalenga kukionyesha chama kuwa ni kichafu miongoni mwa jamii, hali inayoweza kuwanufaisha wapinzani, huku pia kukiwepo na kundi linalokubaliana na kutumika kwa TAKUKURU kunasa wala rushwa likisema, ni uamuzi sahihi wa kukisafisha chama hicho kikongwe nchini.

Kundi linaloonekana kukubaliana na agizo la Kikwete kuhusu kutumika kwa TAKUKURU, linaeleza kuwa, makali ya kudhibiti rushwa yanatakiwa kuongezeka na yasiwe na mipaka hata kama yatapewa tafsiri mbaya kama hiyo ya chama kuonekana kichafu miongoni mwa jamii.

"Matukio kama haya ya rushwa hayakuwahi kuchunguzwa na kupewa maamuzi na vyombo vya dola huko nyuma. Hii ni mara ya kwanza imefanyika na inalenga kusafisha uozo ambao umekuwa ukiwaumiza wananchi. Rais ameliona hili na ni wazi yuko nyuma ya TAKUKURU," chanzo chetu kilieleza na kuongeza;

"Kuna wengi ambao wanataka chama kiendeshwe kwa mazoea. Hawa ndio wanaotaka kufunika mambo kwa faida zao binafsi. Hatuoni kama kuna nafasi ya kupoteza katika mapambano ya rushwa, ni muhimu sasa kusikia kauli za wananchi ambao pia wanamuunga rais mkono kuhusu kudhibiti rushwa."

Chanzo kingine kililieleza gazeti hili kuwa, kuna wasiwasi baina ya wana CCM ambao wanaeleza kuwa, ni wale wasio na nguvu katika serikali na chama wanaonaswa, huku baadhi yao wakiachwa warande na kuendelea kumwaga fedha za kununulia kura.

"Hofu iliyopo ni wale ambao wanajifahamu hawana nguvu ya dola. Hawa kwa mtazamo wangu ndio wanaotafutwa na hii TAKUKURU. Lakini kama itakuwa makini bila kujali makundi, basi katika chaguzi za mikoa na zile za taifa, huko tutegemee kunaswa wakubwa wengi," chanzo hicho kilifafanua.

Taarifa kutoka mkoani Iringa zinaeleza kuwapo malalamiko miongoni mwa wagombea katika nafasi za mkoa, wanalalamikiana kuwa inaonekana TAKUKURU inalenga kuwanasa baadhi huku wengine wakiachwa kumwaga fedha.

Kitendo cha TAKUKURU kujiingiza katika chaguzi za CCM ili kuangalia na kufuatilia vitendo vya rushwa kina baraka zote kutoka kwa Rais Kikwete ambaye tayari alishatoa onyo la kufuta matokeo ya wagombea watakaobainika kujishughulisha na rushwa.

TAKUKURU ni mkono wa dola ambao Naibu Katibu Mkuu CCM Tanzania Bara, Kapteni Jaka Mwambi, alisema ahadi ya nne ya mwana-CCM inatamka wazi kwamba, "rushwa ni adui wa haki" na kisha akaonya kuwa watakaobainika kutumia rushwa, watashughulikiwa na dola na chama.

Kauli hiyo ilikuja siku moja baada ya uchaguzi wa ngazi ya Wilaya nchini kuripotiwa kugubikwa na matukio ya rushwa. Baadhi ya wachambuzi wa mambo, walifafanua hatua ya Mwambi kujitokeza na kuzungumzia rushwa haraka hivyo kama mabadiliko ya mfumo katika CCM.

Taarifa za awali kuhusu vitendo vya rushwa katika uchaguzi huo ziliripotiwa kutoka mkoani Dodoma ambako TAKUKURU, ilidai iliwanasa watu watatu wakigawa fedha kwa ajili ya kuwashawishi watu wawapigie kura wagombea wanaowataka.

Wilayani Ilala pia uchaguzi uligubikwa na hisia za rushwa hali iliyomlazimu Msimamizi Mkuu, Janeth Kahama, kuwataka maafisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Usalama wa Taifa waliokuwapo mkutanoni humo kuwakamata watu waliokuwa wakitoa rushwa kwa wapigakura.

Awali saa 8.00 mchana Kahama alilazimika kuagiza baa zote zilizopo katika viwanja vya Ukumbi wa Msimbazi kufungwa ili kuondoa wigo wa wagombea na wapambe wao kuendelea kuwakirimu wapiga kura kwa ajili ya kuwashawishi wawachague.

Kutoka Sumbawanga; Mkutano mkuu wa uchaguzi wa CCM katika Wilaya ya Sumbawanga Mjini uliingia dosari baada ya kubainika kuwa baadhi ya wagombea walijihusisha na vitendo vya rushwa siku ya mkutano huo, ikiwamo kugawa fulana za chama hicho.

Tukio hilo la wazi lilifanyika nje ya ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Chemichemi, kabla ya mkutano huo kuanza na kushuhudiwa na watu mbalimbali akiwamo Katibu wa CCM wa mkoa huo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Mkoa, Verena Shumbusho.

Kutoka Magu, katika uchaguzi huo rushwa ilidaiwa kutolewa waziwazi kwa wapigakura hali ambayo ilimfanya Afisa Msaidizi Takukuru kumkamata mjumbe mmoja wa mkutano huo akiwa katika uchochoro wa nyumba karibu na eneo la kufanyia uchaguzi 'akikata' mlungula kwa wapigakura.

Wilayani Arumeru uchaguzi ulivurugika baada ya Katibu wa CCM Wilaya kutangaza matokeo mara mbili tofauti, ya nafasi ya Katibu wa Uchumi na Fedha.

Wilayani Nzega nako uchaguzi ulivunjika baada ya wajumbe kubaini kuwako kwa wapiga kura hewa na katibu wa wilaya kudaiwa kukutwa na kura feki mkononi, akiwa amekaa meza ya kuhesabia kura.

Wilayani Ukerewe kundi la Mwenyekiti aliyeshinda, Jiyantilai Karia �Bhiku� limemtangaza 'Mbunge mpya' wa Jimbo la Ukerewe kuwa ni Ally Mambile tangazo ambalo lilitolewa na wafuasi wa Mwenyekiti aliyeibuka na ushindi katika uchaguzi huo ambao umeibua makundi yaliyokuwepo wakati wa kura za maoni ndani ya chama hicho wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.

Makundi yaliyoibuka yanadaiwa kuwa mawili, moja likiwa lile linalomuunga mkono Spika Mstaafu Pius Msekwa ambalo limefanikiwa kushinda kwa kumpata mwenyekiti wakati jingine likidaiwa kuwa lile linalomuunga mkono Mbunge wa Jimbo hilo, Balozi Getrude Mongella ambalo limeandaliwa mkakati wa kuondoka.

Katibu wa CCM mkoani Mwanza Kundya Rajabu aliliambia gazeti hili kuwa, hajapokea taarifa za kutangazwa kwa Mbunge wilayani
Ukerewe, na kudai taarifa alizonazo ni kuwa tukio kama hilo limetokea wilayani Geita na kisha akaonya kuwa, jambo hilo ni kosa kwa mujibu wa kanuni na katiba ya CCM.

Katika mkoa wa Pwani ilionekana kazi ya uchaguzi huo ilikuwa kuwashughulikia wakuu wa wilaya walioomba nyadhifa mbalimbali za uongozi katika chama hicho wilayani wasipate nafasi hizo na kugubikwa na tuhuma kuwa huenda hali hiyo ni ya kupanga.

Baadhi wa wana CCM wameibuka na kudai kuwa chaguzi hizo ziligubikwa na harufu ya rushwa iliyosababisha kuandaliwa kwa mpango wa kuwaangusha wakuu wote wa wilaya waliojitokeza kugombea nafasi mbalimbali.

"Nchi nzima inajua kuwa Mkoa wa Pwani ndipo anakotoka mwenyekiti wa CCM taifa, hivyo ulipaswa kuwa mkoa wa mfano wa kuigwa. Lakini kutokana na hali hiyo inaonyesha chama na serikali hatuna ushirikiano," alisema mmoja wa wakuu wa wilaya za Mkoa wa Pwani.

Miongoni mwa wakuu wa wilaya waliowania nafasi ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa katika wilaya zao ni Khanifa Karamagi kupitia Wilaya yake ya Kisarawe, Gilberty Dololo aliyegombea Kibaha Vijijini, pamoja na Henry Clement aliyegombea wilayani Mkuranga.

Habari hii imeandaliwa na Boniphace Makene, Boniface Meena, Julieth Ngarabali, Musa Juma, Fredrick Katulanda na Doris Mageta.
 
Mwenyekiti huyo alishauri pia watu wanaogombea uongozi katika chama na hata katika nyanja za kisiasa na kijamii, kuachana na tabia ya kuomba fedha kwa matajiri na kwamba kinachotakiwa hivi sasa ni kukirejesha chama katika msimamo wa kuheshimu watu.


Mbona hasemi alipewa hela ngapi na RA kwenye uchaguzi wa uliopita wa CCM, mkoa wa Dodoma?

Kwenye uchaguzi wa rais ndani ya CCM uliopita, alipewa ngapi na SAS? Hawa ndio viongozi wananfiki hawa, anajua kuwa sasa time yake imeisha ndio anajaribu kujiosha, wananchi tuwe macho na hawa vibaka!
 
rushwa rushwa rushwa

nchi inanuka rushwa

chama kinanuka rushwa

tukimbilie wapi?
 
Chama kimeshika utamu! (rushwa) sasa wanajimaliza wenyewe. Viongozi wa juu ndani ya CCM walikuwa wanaliona tatizo hili lakini wakafumba macho na kulibadili jina na kuhalalisha. Kutoa Takrima inaruhusiwa kwa wale wanaokuunga mkono katika chaguzi. Mhhhh! sasa linawatokea puani na wanaona haya. Walikuwa wapi Viongozi wa juu (Mkapa, Kikwete, Makamba, Malecela etc)ndani ya CCM wakati rushwa inaota mizizi ndani ya chama chao!?
 
Rushwa imekivua nguo Chama Cha Mapinduzi

Na Julius Samwel Magodi
Kutoka gazeti la Mwananchi

Unapojiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) kuna kiapo ambacho lazima uapishwe ili uweze kukamilika kuwa wanachama wake.

Kifungu hicho kinasema hivi: "Rushwa ni adui wa haki, sitatoa rushwa wala kupokea rushwa." Huo ndio msimamo wa chama kuhusu wanachama wake.

Hata hivyo, msimamo huo wa chama hicho tawala unaonekana sasa kuwa ni muziki wa zamani ambao umechuja katika masikio ya wanachama wake kuusikia.

Hakuna tena mwana CCM ambaye yupo tayari kuingia katika kinyang'anyiro cha kuomba uongozi ndani ya chama hicho au uchaguzi mwingine bila ya kuwa na fungu la kutoa takrima kwa wapigakura.

Matukio ya baadhi ya wanachama wake kukamatwa na rushwa katika uchaguzi wa viongozi unaoendelea nchini kote hivi sasa ni uthibitisho tosha kwamba ukiwa mikono mitupu huwezi kupata uongozi ndani ya CCM.

Kama kuna tukio ambalo limewahi kukiumbua Chama Cha Mapinduzi katika uhai wa maisha yake ya miaka 30 basi ni uchaguzi huu ndani ya chama unaoendelea nchini kote.

Uchaguzi huu umetoa picha kamili jinsi baadhi ya viongozi wa chama hicho wanavyopatikana kwa njia ya kutoa rushwa kwa wapigakura wao.

Wiki hii Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa Mkoa wa Arusha (Takukuru), imewakamata kwa tuhuma za rushwa wabunge wawili na viongozi kadhaa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mmoja wa waliokamatwa ambaye anadaiwa kuwa mpigadebe wa wabunge hao, alikamatwa na fedha taslimu Sh436,500 ambazo Takukuru wanadai zilikuwa ni kwa ajili ya kuwahonga wajumbe.

Mbali ya viongozi hao wa Arusha Takukuru pia mwishoni mwa wiki iliyopita iliwakamata wana CCM wengine kadhaa katika mikoa ya Dodoma, Iringa na Kagera kwa tuhuma za kutoa na kupokea rushwa kwa wapigakura.

Kukamatwa kwa vigogo hao kumekuja siku moja tu baada ya wagombea wa nafasi mbalimbali za CCM katika ngazi za wilaya kukata rufani, kupinga matokeo wakituhumu kushindwa kutokana na wenzao kutumia rushwa.

Kwa hakika kukamatwa kwa watu hao na watu wengine waliokwisha kamatwa kutoka katika mikoa mbalimbali na taasisi hiyo mpaka sasa kumeiacha hadharani uchi CCM.

Ile dhana kwamba viongozi wa wanapatikana kutokana na uwezo wao wa utendaji halipo tena, bali pesa ndiyo inayoamua mtu achaguliwa kuwa nani.

Hali hii ya uchaguzi wa chama hicho tawala kukumbwa na kashfa ya rushwa kunathibitisha madai ambayo yamekuwa yakitolewa na wanasiasa nchini kwamba kwa mazingira yaliyopo hivi sasa ni vigumu kwa mtu maskini kupata uongozi ndani ya CCM.

Hivi kweli mtu masikini ambaye hana hata Sh 5,000 za kuwapa wapigakura anaweza kupata uongozi? Ni dhahiri kuwa nafasi hiyo haipo. Nadhani CCM sasa imekuwa kama gari ambalo limekosa mwelekeo na linaelekea kuingia shimoni.

Swali ambalo watu wengi wanajiuliza kama watu wanapigana vikumbo kuhoga na kutoa takrima ili wapate vyeo ndani ya CCM, je katika chaguzi nyingine wanatumia mbinu gani?

Ni wazi kwamba mbinu hii waliyoionyesha baadhi ya wana CCM katika uchaguzi wao wa ndani ndiyo ambavyo wamekuwa wakiitumia kucheza rafu katika chaguzi nyingine.

Ni vyema sasa CCM kama chama tawala kilichodumu madarakani kwa miongo mitatu kikatumia nafasi hii kujisafisha na kuondoa doa hili la rushwa kwa kuwaengua watu wote ambao wamethibitika kutumia rushwa.

Ni jambo lisilopingika kwamba kama kuna kiongozi atatoa rushwa kupata uongozi lazima naye ataomba rushwa akiingia madarakani ili aweze kurejesha fedha zake alizotumia wakati wa uchaguzi.

Kwa upande wa Takukuru ninawapongeza kwa kujaribu kufanya kazi yao wanayotakiwa kuifanya ingawa wamekuwa wakikamata siku zote dagaa na kuyaacha mapapa ya rushwa yakiendelea kutafuta hela za wananchi.

Hata hivyo, ninajiuliza Takukuru walikuwa wapi siku zote kufanya wanachokifanya hivi sasa katika chaguzi zilizopita. Je mpaka wapewe amri na viongozi wa kisiasa ndio wafanye kazi hiyo?

Ninashawishika kuamini kwamba kauli ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa hivi karibuni kuhusu uchaguzi wa CCM kutaka watakaotoa rushwa wakamatwe huenda ndiyo ambayo imeiamsha Takukuru.

Hivyo ninaitaka Takukuru iendelee na moto huu kwa kuwakamata papa wa rushwa badala ya kuendelea na hawa dagaa wanaokamatwa.

Mwandishi wa safu hii ni mhariri wa habari maalum. Anapatikana kupitia barua pepe; juliusmagodi@yahoo.com Simu; 0754 304336
 
CCM sasa yanuka rushwa

na Mwandishi Wetu
Kutoka Gazeti la Tanzania Daima
MWENENDO wa mambo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) sasa unaonekana kwenda kombo na unaonyesha kila dalili kwa chama hicho kutumbukia shimo katika kashfa mbaya ya rushwa.

CCM imeingia katika kashfa kubwa ya wanachama na viongozi wake kukumbwa na tuhuma za rushwa na ubadhirifu wa mali za chama licha ya viongozi wake wakuu kutokubaliana na ukweli huu.

Wachunguzi wa mambo, sasa wanaonyesha wasiwasi mkubwa wa kuporomoka kwa hadhi ya chama hicho huku kikitoa nafasi kwa kambi ya upinzani kuanza kujiimarisha.

Matukio ya hivi karibuni ya kukamatwa kwa wabunge wawili wa chama hicho na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Arusha wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa katika uchaguzi wa viongozi wa chama hicho yamekipaka matope na kuzipa nguvu hoja za wanasiasa wa kambi ya upinzani kuwa ushindi wa chama hicho hupatikana kwa rushwa.

Ingawa Kamati ya Maadili ya CCM imeonyesha kukerwa na tuhuma zinazowakabili wabunge hao pamoja na viongozi wengine na kupendekeza wasiruhusiwe kugombea uongozi, kauli ya hivi karibuni ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuph Makamba, kwamba uchaguzi huo ulikuwa safi inazidi kutoa ujumbe kuwa bado kuna viongozi ndani ya chama hicho wanaoficha tatizo linalokitafuna chama chao.

Kauli ya Makamba inatofautiana na malalamiko ya wanachama wake wengi kuhusu kukithiri kwa vitendo vya rushwa katika uchaguzi huo.

Malalamiko ya kuwepo kwa mchezo mchafu katika chaguzi mbalimbali za chama hicho sasa si geni, lakini linaonekana kuvuta hisia za wengi baada ya wanachama wake kuanza kunaswa wakihusishwa na rushwa.

Mbali na rushwa katika uchaguzi, tuhuma za ubadhirifu wa mali ya umma zinazowaandama baadhi ya makada wa chama hicho ambao wana nyadhifa kubwa serikalini, nazo zinakoleza sifa mbaya ya chama hicho.

Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, ni mmoja wa watu wanaotajwa kuiweka CCM katika hali mbaya ya kutoaminiwa na wananchi kwa kuhusishwa kwake na kusaini mkataba wa mgodi wa Buzwagi kinyume cha taratibu.

Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaeleza kuwa hatua hii ni matokeo ya kuwepo kwa makundi ndani ya chama ambapo kila kundi sasa linapambana dhidi ya kundi jingine, huku wanamtandao wakiendelea kuwa na sifa ya juu ya kuchafua wanachama wasio wanamtandao.

Jambo jingine linalotajwa kukichafua chama hicho ni utitiri wa ndugu wa viongozi wakuu kujitumbukiza katika siasa na kunyakua baadhi ya nafasi nyeti katika chama.

Ingawa ndani ya Bunge kuna wabunge kadhaa wa chama hicho ambao ni wanandoa huku wengine wakiwa na nyadhifa kubwa serikalini, ndani ya chama hilo linaonekana kuwa doa linalokigeuza chama hicho kuonekana kama cha familia zaidi.

Hatua ya mke ya Rais, Salma Kikwete kugombea nafasi ya mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wilayani Lindi huku mtoto wa Rais, Ridhiwani Kikwete na ndugu mwingine wa Rais, Yusuph Kikwete kuchaguliwa kuwakilisha Wilaya ya Bagamoyo, kunaacha maswali mengi.

Ingawa si jambo baya kwa ndugu wa viongozi wakuu wa nchi kuwa wanasiasa, historia ya chama hicho inaonyesha kuwa hakijawahi kuwa na mwenyekiti ambaye mkewe na mtoto wake ni wajumbe wa vikao vya mkutano mkuu wa taifa, wakiwa na uwakilishi wa sehemu fulani ya nchi.

Mbali na familia ya Rais Kikwete ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho, mke wa Katibu Mkuu wa chama, naye amechaguliwa kuwa mjumbe wa NEC - Taifa hivyo anashiriki moja kwa moja katika maamuzi makubwa ya chama hicho.

Vita ya kuwania madaraka miongoni mwa wananchama wa chama hicho inayoendelea sasa katika mikoa ya Mbeya na Mara, ni ishara ya chama hicho kupoteza mwelekeo.
 
cha kujiuliza je ni kwa nini siku zooote wanakamatwa viongozi ambao ni minority na ambao hawana infulence kubwa katika jamii ? ina maana akina naniii na naniii wao ndio hawakamatwi ?
 
Hili jambo si geni,leo hii bila fweza,huwezi kupata uongozi ndani ya ccm,hii imekua ni kama mojawapo ya sifa za mgombea,kutoa kitu kidogo.Ndio maana kikao kilichopita cha bunge,mbunge mmoja alisema"Zamani kuku alikua hajisaidii sehemu anayolala,lakini jogoo alivyoanza kujisaidia tu,basi leo hii hadi vifaranga wanajisaidia pale wanapolala.

Sasa hii rushwa ya CCM imeota mizizi,imeanzishwa na hao wakubwa zao,leo hii uchaguzi wa wenyeviti wa mitaa nao kuna rushwa inatembea kama karanga.Hii dhana potofu ya kitu kidogo,inasababisha watu wenye uwezo wa kuuongoza kukosa kura,na wale wasio na uwezo wa kuongoza kupewa kura,kwa kigezo cha kutoa rushwa.Nchi inadidimia,hadi leo hii sijaona hata kiongozi mmoja mwenye uwezo wa kupambana na rushwa,imekua ni methali tu.Rushwa ndio imesababisha Nigeria kuwa taifa maskini,japo ndio nchi inayoongoza kwa mafuta Afrika,sasa Tanzania tuna kila aina ya madini na vivutio chungu nzima vya kuweza kutufanya tuwe na taifa lilostawi kabisa barani Afrika,lakini kwa mchezo huu mchafu,tutazidi kuwa mkiani na omba omba tu,bila ya aibu,huku viongozi wetu wakiishi kama wapo sayari ya pili.
 
Kama mnaweza kukumbuka hotuba moja ya mwalimu alisema, mwenzao mmoja alipokea rushwa na walitaka achapwe viboko akamuoneshe mke wake. lakini siku hizi mtu akipokea rushwa anaweza kualikwa na mke wake kwenye karamu kubwa. Hii ni rushwa wakati wa Nyerere na rushwa wakati wa JK.
 
Vita ya rushwa ionekane pia serikalini

Juvenalis Ngowi
Kutoka Gazeti la Tanzania Daima

SHUKRANI kwa Mungu ni moja ya utaratibu wangu wa siku hadi siku ninapowasilisha wazo langu jepesi kabisa.

Nimefanya hivi siku zote kabla ya kuanza waraka huu na leo hii natanguliza dua yangu hiyo iliyosheheni shukrani, maombi na masifu. Kisha baada ya dua hiyo tusonge mbele na gumzo letu.

Uchaguzi ndani ya chama tawala umekuwa gumzo kubwa. Kuna mengi yamefanya wadadisi wa mambo wakodoe macho katika chaguzi za ndani ya chama hicho kikongwe cha siasa.

Nitataja machache tu yanayosababisha hisia za watu wengi ziende huko. Jambo la kwanza ni hali iliyojitokeza katika miaka ya karibuni ambapo watu wengi hasa wafanyabiashara kujifungamanisha na chama hicho. Wapo wengi wanaoonyesha huba yao kwa chama tawala kiasi cha watu kuanza kujiuliza, kuna fungate gani kati ya siasa na biashara?

Kimsingi Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekuwa kikijipambanua kwa maneno kwamba hicho ni chama cha wakulima na wafanyakazi.

Lakini sasa wafanyabiashara wanapigana vikumbo kuchukua si tu uanachama wa chama hicho lakini pia kutafuta uongozi katika ngazi mbalimbali. Hali hii imesababisha kuwepo kwa watu wengi ‘maarufu’ wanaowania uongozi wa CCM, hivyo inapokuwa wakati wa uchaguzi wengi wanaangalia ni mkubwa yupi ameanguka na ni yupi amepona.

Wachambuzi wa mambo pia wana hamu ya kuona kati ya walio madarakani nani anazidi kujiimarisha katika chama. Si jambo la kushangaza kuona viongozi wengi wa serikali wakiwa katika hekaheka za kusaka nafasi muhimu ndani ya chama. Wanapenda wawe jikoni.


Si rahisi mpishi afe njaa wakati akikaangiza! Hili pia linafanya uchaguzi wa chama hicho umulikwe na wanachama na wale wasio wanachama.

Lakini katika uchaguzi wa mwaka huu jambo moja jingine limefanya gumzo liwe kubwa zaidi. Ni rushwa. Vyombo vya habari vimetangaza kwa kiwango cha juu mno kuhusu malalamiko ya rushwa hata kama Aggrey Mwanri anakataa uwepo wa rushwa hiyo. Rushwa imekuwa gumzo kila kona kwa wanaofuatilia habari hizi. Tukio la huko Arusha la kukamatwa na hatimaye kufikishwa mahakamani kwa waheshimiwa sana wabunge wawili kwa tuhuma za rushwa kumeongeza hamasa ya masikio kukaa tayari kudaka lolote linalohusiana na uchaguzi huo wa chama tawala.

Vyombo vya habari hasa vile vyenye fungate na chama tawala vimeonyesha kutoa pongezi za dhati kwa mapambano dhidi ya rushwa ndani ya chama. Isifikirike hata kwa makosa kwamba ninakasirika kusikia kuna mapambano ya haki dhidi ya rushwa ndani ya chama. Ila nina haki ya kuwaza na kuangalia pia upande mwingine wa shilingi. Ni vizuri kushangilia jambo jema linapofanywa, lakini ni vizuri zaidi unaposhangilia jambo jema lililofanywa kwa nia njema.

Rushwa si tatizo lililoanza leo wala jana. Wala hakuna anayetazamia kwamba ipo siku jamii yetu itakuwa na rushwa asilimia sifuri. Yamefanywa mengi kuhusu rushwa, lakini bado haijapungua kwa kiwango kinachotegemewa. Hata hivyo ‘umakini’ huu wa kupambana na rushwa katika uchaguzi unaoendelea unafanya wengi tukune vichwa na kujiuliza; vimeumbwa upya na nchi ikageuka?

Lengo la msingi la kupambana na rushwa ni ili kila raia apate maisha bora. Hapa ndipo tunapojiuliza, kwa nini inaelekea kuna nguvu tofauti linapokuja suala la uchaguzi ndani ya chama? Inawezekana rushwa ya ndani kwa ndani ndiyo inayowaumiza zaidi wananchi hivyo ni muhimu kuonyesha ukali zaidi kuliko hizi zinazosemwa kuwepo kwenye serikali na vyombo vyake?

Kwanini viongozi wametega masikio na mitego yao kuwanasa wala rushwa wakati wa uchaguzi huu wa chama?

Je, mitego hiyo isingeweza kufanya kazi kabla au wakati au baada ya kusainiwa kwa mikataba inayolalamikiwa kuwa mibovu?

Nguvu hizi za ndani ya chama zisingeweza kutumika kubaini manunuzi yasiyostahili yanayodaiwa? Ni rushwa ipi inamuumiza zaidi mwananchi? Hatukatai kwamba ufisadi wa aina yoyote lazima udhibitiwe. Lakini tunapaswa kuanza pale panapoumiza zaidi.

Mwananchi wa kawaida anaumizwa sana anapokwenda hospitali kutibiwa kisha anatakiwa atoe mlungula ili apate matibabu. Mwananchi huyu huyu hajali sana kama watu katika chama chao wameamua kuuziana vyeo! Hivyo katika hoja ya kwanza tunatarajia na inapaswa iwe hivyo, kwamba rushwa zinazowagusa wananchi moja kwa moja lazima zidhibitiwe haraka sana.

Ununuzi wa rada unadaiwa kutumia kiwango kikubwa cha fedha kuliko ilivyostahili huku kukiwepo tuhuma za mtu kupewa kamisheni kubwa. Watu wamehoji kuhusu mikataba ya madini kiasi kwamba rais mwenyewe akatamka kwamba kuna haja ya kuipitia upya.

Sakata la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) limeendelea kuwa simulizi inayotapakaa sehemu mbalimbali na kwa njia mbalimbali. Bado kuna kiza kinene kuhusu mkataba wa IPTL.

Kote huku hakuna uchunguzi wa wazi unaofanyika na kama umefanyika, basi wananchi hatukufahamishwa kilichogundulika. Lakini inapokuja kwenye watu kukamatwa na sufuria za pilau kwa ajili ya kugombea nafasi ndani ya chama, hawa wananaswa kirahisi na baadhi ya watu wanasifu kwamba kuna juhudi kali za kupambana na rushwa.


Bado tuna kumbukumbu namna ambavyo wakubwa hawakuipokea kwa furaha hukumu ya kishujaa ya Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga ile rushwa iliyobatizwa jina la takrima. Tulifika hapo. Ndiyo mana tunapofurahia kwamba walau kuna ujasiri wa kuwakamata uzao wa rushwa, tunalazimika pia kuhoji, kuna msukumo mwingine nyuma ya hii vita au ni hesabu zenye lengo tofauti na uelewa wetu?

Uchaguzi umekuwa ukitumia fedha kwa muda mrefu sasa. Kuna taarifa za watu kuweka poni nyumba zao. Wengine wanatumia msemo wa Waswahili kwamba mkono mtupu haulambwi. Wapiga kura walipofushwa kiasi cha kutokujua au kuamini kama mtu anaweza kupewa kura bure kama tunavyovuta oksijeni bila malipo. Ghafla kelele sasa zinasikika kwamba mara huku, mara kule kuna tatizo la rushwa. Inasemwa kwamba mwenyekiti wa chama kabariki wanaojihusisha na rushwa wachukuliwe hatua kali. Mwenyekiti huyu ni Rais wa Jamhuri ya Muungano. Tunasubiri kwa hamu ili tuone pia akiwageukia watendaji wa serikali wanaojihusisha au hata walau wanaoonekana kuwa katika mazingira ya rushwa.

TAKUKURU wameripotiwa kuwa tishio kwa wale waliokuwa wanajiandaa kutumia rushwa katika uchaguzi wa ndani ya chama. Tunafurahi na tena tunasubiri kwa hamu kubwa pia kuwaona wakitumia ujuzi na uwezo wao kuingilia na kuondoa rushwa hizi ambazo wakati mwingine zinakatiza maisha ya wanadamu. Kama inawezekana kudhibiti rushwa ndani ya chama, itawezekana pia kuidhibiti ndani ya serikali.

Madai ya kutumika kwa rushwa wakati wa uchaguzi huu yamekuwa mengi na makubwa mno katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Hata hivyo tuwe makini. Katika siasa kuna kitu kimezuka miaka ya karibuni kinajulikana kama kamati ya fitina. Inawezekana pia rushwa inatumiwa na moja au zaidi ya kamati hizi za fitina si kwa lengo la kuondoa na kupambana na rushwa bali kama daraja la kumdondosha mtu na kujipa upenyo wa kupita. Ndiyo maana awali nilisema ni vema kupiga makofi kwa jambo jema, lakini kubwa zaidi ni nia njema ya jambo linalofanywa. Tunaweza kushangilia kwamba kuna pambazuko, kumbe ni mbinu chafu za kutumia uchafu wa wengine ili kukwea.

Tukumbuke mpinzani wako kuwa mchafu haina maana wewe u-safi. Katika mazingira haya ndipo ninapojiuliza, je, chama kina mkakati kabambe wa kujisafisha? Kama ndiyo, je, mkakati huo utaanza kutekelezwa lini serikalini?

Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa simu: 0784 265 072 au barua pepe: kevinmakyao@hotmail.com
 
Kauli za wananchi kuhusu rushwa ndani ya CCM

Wasemavyo Wasomaji
Kutoka Tanzania Daima

Gazeti hili sasa linachapisha maoni yenu yatakayotumwa kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS), kujadili mjadala utakaokuwa unaanzishwa na gazeti hili.

Mimi ni mwanaCCM hai. Nasikitishwa na matendo ya wanaCCM wachache wanaokiaibisha na kukipaka matope chama. Namuomba Mwenyekiti Rais Jakaya Kikwete awachukulie hatua kali wale watakaothibitika kutumia rushwa katika chaguzi mbalimbali (yaani chaguzi za chama na zile za kiserikali kama ubunge). Kinyume na kuchukua hatua, Mwenyekiti Rais Kikwete atakiweka chama na yeye mwenyewe katika mazingira magumu katika uchaguzi mkuu wa 2010 (0754 695 662)

Kwa kitendo cha CCM, tena chama tawala na viongozi wake waliochaguliwa na wananchi kukamatwa kwa rushwa na TAKUKURU ni aibu kubwa sana kwa Serikali ya Kikwete, tutaonana katika uchaguzi wa mwaka 2010 – S. Mtunu, Kilombero, Mkamba, Kidatu (0786 011 060)

Rushwa ndani ya CCM haijaanza leo, wameshazoea, si unajua ukiwasha moto ndani ya shimo halafu ukafunika nini kitatokea? Tufumbuke macho. Tujiulize, kama angekuwa Zitto Kabwe amekamatwa anatoa rushwa unadhani wangemfanya nini, kama si kumfunga gerezani miaka hata kumi? Lakini ya kwao watafichiana, yatapoa. Binafsi najua wa kumpa kura mwaka 2010, lakini si mla rushwa –Mercy, Kawe, Dar es Salaam (0714 833 583)

Yanayotokea CCM yanadhihirisha wazi ‘sampuli’ ya viongozi wa kitaifa tulionao, ingawa hawataki kukubali ukweli huu. Ikumbukwe kuwa wengi wao walipata madaraka kwa takrima! Ila za mwizi ni arobaini. Tunazidi kuwatambua - Godwin, Tegeta, Dar es Salaam (0787 232 942)

Kwa maoni yangu, ili rushwa iishe, TAKUKURU ibinafsishwe, kwa sasa haiwezi kufanya kazi vizuri, serikali na TAKUKURU viwe vitu viwili tofauti, vinginevyo rushwa ndani ya CCM haitakaa iishe - Edwin Tillya, Babati, Manyara (0717 766 608)

Waliotuhumiwa kuhusika na rushwa waadhibiwe, vinginevyo hata anayefuatilia TAKUKURU wananchi nao wataona wamepewa rushwa wazibe mdomo – Johnson Materu, Arusha (0754 217 318)

Iliyobaki Watanzania tusiwe wajinga, kwani hata Mungu ameamua kutuonyesha madhambi ya chama tawala, kwamba CCM hali si shwari na wala hawatujali sisi, je, iweje sisi tuwajali wao? Hebu tuamke (0754 856 672)

Kama kweli CCM imedhamiria kwa dhati kuondoa rushwa ionyeshe mfano kwa watu ambao tayari wameshabainika, isiishie tu kwa madiwani wanyonge waliouza viwanja wakawatimua. Mfano katika uchaguzi uliofanyika Kiteto, mgombea mmoja anadaiwa kununua mchele kama chakula kwa wajumbe na mgombea huyo alipita kwenye nafasi aliyowania. Kwa hali hiyo, uongozi wa kuchaguliwa ndani ya chama utabaki kwa wenye fedha tu. Kama dhamira ya kuondoa rushwa ni kweli, basi serikali iiondoe TAKUKURU Ikulu, iwajibike kwa Bunge, japokuwa Bunge lenyewe ni walewale wanaoonekana kuikumbatia mikataba feki (0786 029 170)

Rushwa imezidi sana kwenye chama tawala kuanzia ngazi ya ubalozi wa nyumba kumi ni rushwa hadi wabunge wao, rushwa inatoa harufu mbaya CCM. Jamani, tuwabwageni kwenye uchaguzi ujao – Veneranda, Mwanza (0717 494 943)

Rafu za CCM zimepita ukomo. Katika kiwango cha rushwa kilichopo CCM, sioni uwezekano wa Watanzania kubadili serikali yao kwa kura za kawaida, lazima tuungane kuonyesha haturidhiki. Yanayoendelea kwenye serikali hii ya CCM mengine ni aibu hata kuyazungumzia hadharani (0787 442 559)

Rushwa ndani ya CCM si jambo jipya, inaonekana ndivyo walivyozoea na kuzoeshwa kupata na kutoa uongozi, kwani nani kasahau habari za takrima? Ndiyo maana matajiri na ‘wahuni’ wa kisiasa wote wanakimbilia huko, kwani ni rahisi kununua uongozi ukiwa huko. Hili jinamizi linaloonekana kukitafuna chama ni kama danganya toto tu kwa jamii. TAKUKURU kama kweli iko huru, kwanini isubiri agizo la “Mkubwa” ndipo ifanye kazi? Bado tunadanganywa tuone eti sasa kazi imeanza, hakuna kitu hapo, wanaibiana, kwanini tusiamini tukiambiwa wanawaibia wananchi kura zao kwenye uchaguzi mkuu? – Mkwanzania (0754 422 518)

Ama kweli mwisho wa mfanyabiashara ni hasara. Wanajua tujue wakati mwingine Mungu naye ana makusudi yake. Ipo siku Mungu atatusaidia, amina (0754 327 103)

Rushwa imekithiri CCM, cha kufanya ni kuwanyima kura mwaka 2010 ili tuwashikishe adabu (0717 494 943)

Kusema kweli rushwa ndani ya CCM ni sawa na donda ndugu kwa sababu wala rushwa wanafahamika, lakini wanashindwa kunyooshewa kidole kwa sababu ya kulinda maslahi, lakini wakipatikana watu kama Zitto, naamini tutapiga hatua – Gazza Muzungu, Dar (0756 396 991)

Nafikiri kuhusu suala la rushwa ndani ya CCM, Mungu sasa ameamua kuwaumbua, umefika wakati sasa kazi iwe kwetu kuamua kukizika chama hiki, maana wanayotufanyia sasa yametufika shingoni – Abbas Ahmed, Dar es Salaam (0755 826 210)

CCM kimekuwa chama cha wanaotaka kufanya biashara bila usumbufu, ndiyo maana wanatoa rushwa na mara kadhaa tumesikia ukitaka mambo yako yakuendee sawa, uingie CCM! – John Kalalu (0763 484 900)

Rushwa ndani ya CCM. Kama CCM wao kwa wao wanaibiana na kutumia rushwa namna hii! Vipi inapokuwa CCM na upinzani, si ndiyo balaa kabisa? Hii imetudhihirishia Watanzania kuwa kumbe ushindi wa CCM wa kishindo siku zote huwa unatokana na mchezo mchafu. Serikali ya CCM haiwezi kuipiga vita rushwa - (0713 502 497)

Rushwa CCM inatupa ukweli juu ya uozo uliomo ndani ya chama hicho na jinsi viongozi walivyo, kwa ujumla tujifunze kuwa chama kimeoza – Mwasanga David, Mbeya (0713 650 765)

Jasiri haachi asili, CCM imezoea kushinda kwa rushwa, Mungu amewafichua kutokana na dua za wapinzani – Saktay, Karatu (0754 958 254)

Kwa kushikwa wabunge wa CCM na TAKUKURU, hata kama hawajathibitika, ukweli ni kwamba, mambo si shwari – Magagula S. Magagula, Korogwe, Tanga (0786 107 240)

Rushwa na CCM ni sawa na Kulwa na Dotto, kwani viongozi wote wa CCM hupatikana kwa njia ya rushwa hivyo hakuna wa kukemea ndani ya chama – M.G.G, Musoma (0784 794512)

Rushwa ndani ya CCM ni kielelezo tosha kinachothibitisha kwamba chaguzi zote kuu pamoja na ndogo zilizopita ziliambatana na rushwa. Hii ni aibu kwa chama kikongwe. Mwalimu Nyerere aliwahi kutamka kwamba, mficha maradhi, kifo kitamuumbua, hayo ndiyo yanayoitokea CCM kwa sasa – (0784 688 333)

Rushwa ni suala baya kila pahala, hivyo chama kinachoongoza kuwa na kashfa ya rushwa ni dhuluma ya haki ya wananchi, hivyo bora watoa rushwa ndani ya CCM wafutwe uanachama, na wakabidhiwe kwenye chombo husika kwa hatua zaidi. Wananchi tujue viongozi wanaotoa rushwa ili kupata viongozi, lazima nao watatoa huduma kwa kuomba rushwa ili kufidia fedha zao walizohonga. Kamwe tusilee maovu ya rushwa kwenye CCM – Gumbo Zacharia, Mahenge (0787 531 615 )

Ndugu mhariri, binafsi sishangai, yaani inaonekana kama vile rushwa imekuwa kama ibada CCM kuanzia balozi hadi ngazi za juu, ni aibu kubwa sana kwa chama kikongwe, kama CCM kufikia hatua kama wewe ni kandambili ndani ya CCM hupati nafasi ya uongozi. Wananchi kama hao wanatafuta uongozi kwa malengo yao wenyewe dawa yao ni 2010 tu, hakuna kulala – Hassan Kibari, Musoma (0787 763 559)

Mwenye macho haambiwi tazama. Watanganyika tunashuhudia ‘live’ uozo wa rushwa ndani ya chama tawala. Mambo yaliyotokea bungeni na yanayoendelea katika chaguzi za CCM yanatosha kutuamsha Watanganyika. Mungu katufichulia uozo unaotendeka, saa ya kujikomboa ni sasa - Sallu Chamungwana (0755 538 720)

Tusitegemee rushwa kwisha au kupungua CCM kwa sababu imeshaota mizizi mikubwa na kusababisha nyufa tangu pale walipoamua kuwakumbatia mabepari, sisi walalahoi tuombeleze – A. Said (0754 378 226)

Naunga mkono kwamba, suala la rushwa limekithiri ndani ya CCM. Chama tunakipenda, lakini tunawaachia wenye pesa, haki haipo kwa wanyonge – Wanyonge, Sikonge, Tabora (0787 971 789)

Rushwa CCM haiwezi kutoweka kwa sababu TAKUKURU ni kama jibwa lisilo na meno mbele ya vigogo. (0717 090 892)

Sahani chafu haiwezi kuwekewa chakula safi, rushwa ndani ya CCM inaanzia mbali, kuanzia kwenye mtandao hadi ufamilia kwenye chama – Daudi Samson, SUA, Morogoro (0756 683 553)

Ni rushwa tu iliyokithiri katika serikali yetu na Zitto kawaumbua na ndiyo sababu wamemtimua bungeni. Na wote waliochangia hoja ya Zitto kusimamishwa shughuli za Bunge ndio wale wale wala rushwa – Salum, Tabora (0754 408 502)

Rushwa kwisha ni ndoto za alinacha, labda tuungane kukisakama chama tawala katika uchaguzi mkuu ujao. Angalia kilichotokea Arusha, wabunge wanaotuhumiwa kwa rushwa wamefikishwa mahakamani na kuachiwa kwa dhamana, ingekuwa sisi walalahoi si tungefia mahabusu? - Andrew William, Sumbawanga (0754 069 205)

Kwisha kwa rushwa ndani ya CCM sijui! Kwa sababu ndani ya chama hakuna anayekemea rushwa kwa dhati na isitoshe, matajiri wanapewa nafasi kubwa kama ilivyo kwa watoto wa wakubwa. Nani amfunge paka kengele? – Kea Baba, Kasumulo, Kyela (0754 244 547)

Kama wao CCM wanaonyeshana ujuzi wa kuibiana kura na kutoa rushwa, wananchi hatuwezi kuwa na imani na serikali ya chama tawala – Kocha (0784 480 025)

CCM na rushwa, rushwa na CCM. Hivi viwili haviwezi kutenganishwa, hata Mwalimu Nyerere aliwahi kutamka kwamba CCM imeoza na inanuka rushwa, ni kama pete na chanda. Wabunge wa CCM huko Arusha wamekamatwa kwa tuhuma za rushwa, pesa hizi za kununua kura zinatoka wapi au wenzetu wana mashamba ya fedha? - Issa Mtuli, Dar (0714 515 747)

Ukiwauliza CCM watakuambia hakuna rushwa, ukimuuliza mtu kama Mudhihir atakuambia chama ni safi kabisa. Waingereza hunena, ‘time will tell’. Watanzania tuamke jamani (0786677046)

Mungu hamfichi mnafiki. Rushwa inayorindima katika chaguzi za CCM ni kivuli cha yaliyotokea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. Hata zile tambo za ushindi wa tsunami bila shaka ulikuwa na mkono wa rushwa. Rushwa ndani ya Tanzania haiwezi kuondoka kwa sababu ndiyo inayoonekana kuwa staili ya viongozi wetu. Dawa pekee ni Watanzania kuzinduka na kuwakataa matapeli wa kisiasa – Douglas Sallu (0755 538 720)

Wakubwa wengi ndani ya chama tawala, wana harufu ya rushwa, lakini hawayaoni haya, wanayaona ya Zitto Kabwe tu (0713 481 383)

Rushwa ilionekana kama sehemu ya imani ya chama, lakini sasa ndiyo wanaanza kujisafisha. Ile dini yao ya takrima waliyotumaliza nayo mwaka 2005 sasa wameanza kuisahau na Mungu atawalaani kwa kuwaumbua kama hali inavyoanza kuonekana sasa – Kimaro Raphael (0754 449 256)

Mimi naona sasa chama hiki kinastahili kikae pembeni ili kijipange upya, kimechoka hiki – Tamtam, Tarime (0784 500 974)

CCM ninayoifahamu si hii inayonuka rushwa. Haikuwa ya kiukoo, familia au hata ya kirafiki. Ni dhambi ya mauti kwa CCM kufanya uchaguzi wowote bila rushwa. Ogopa watu wa chama hicho kinachotawala nchini wanapojaribu kutumia kila njia kupata uongozi. Tusidanganyane, hakuna mtu ndani ya CCM anayeweza kukemea rushwa, kwani wengi wamepita katika tanuru hilo. Kama Mwalimu Nyerere akifufuka, atawatawanya karibu wote CCM (0784 329 918)


Kutokana na wingi wa ujumbe wa wasomaji, tumeshindwa kuuchapa wote, hivyo utaendelea katika toleo lijalo – Mhariri
 
Mkutano wa CCM waalika Kikosi cha kuzuia rushwa Mwanza
Na Frederick Katulanda, Mwanza
Kutoka Gazeti la Mwananchi

KATIKA kuhakisha uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mwanza unakuwa huru na haki, maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Usalama wa Taifa, wamealikwa kushiriki kufuatilia nyenyendo za wajumbe na wagombea.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Katibu wa CCM mkoani Mwanza, Kundya Rajabu zimeeleza kuwa maofisa wa Usalama wa Taifa na wale wa Takukuru wamepangwa katika ukumbi wa CCM Kirumba, ambako uchaguzi huo utafanyika.

Habari zilizopatikana jijini hapa zimedai kwua kutokana sifa ya Mkoa wa Mwanza na hali halisi ya uchaguzi, ikiwa ni pamoja na kukamatwa kwa makada watano wa CCM mkoani hapa kutokana na kujihusisha na vitendo vya rushwa, Ofisi ya chama iliamua kuwaalika maofisa wa Takukuru na Usalama wa Taifa kuwa waangalizi wa karibu katika uchaguzi huu ambao umeonekana kuzaa upinzani mkali.

Rajabu alikiri kuwa chama chake kimeamua kuhusisha vyombo hivyo kutokana na vuguvugu halisi la uchaguzi na mvutano makali uliopo ili kuhakikisha uchaguzi huo unakuwa wa huru na haki.

"Ndiyo tumewaalika PCCB na Usalama wa Taifa, lakini lengo letu ni zuri tu, ambapo watakuwa waangaliazi katika uchaguzi huu...," alieleza.

Katika hatua nyingine, habari kutoka Takukuru zimedai ili kuhakikisha wajumbe hao wa CCM hawajihusishi na vitendo vya rushwa, maofisa wa wake wamepangwa kusafiri na wajumbe katika mabasi, meli na maroli ili kuwadhibiti wagombea wenye tabia ya kuhonga wajumbe.

Rajabu alisema hatua hiyo imefikiwa baina ya makubaliano ya ofisi yake na Takukuru, kutokana na baadhi ya wagombea kupendelea kutoa rushwa ili washinde.

Alisema wagombe wengi wamekuwa wakijaribu kuwanunua wajumbe nyakati za mwisho wanaposafiri kwenda kwenye uchaguzi, hivyo kudhoofisha nia ya kuwa na uchaguzi huru na wa haki.

Wakati huo huo, Rajabu aliwatangaza wasimamizi katika uchaguzi huo kwamba watakuwa Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye, mkuu wa wilaya Jackson Msome, ambao pia ni wajumbe wa NEC na Katibu Mkuu Msaidizi wa Idara ya Itikadi wa Uenezi, Simoni Nchimbi.
 
Waanze na Mkapa, Manji, Sumaye n.k.

Taasisi ya kuzuia rushwa sasa kuchunguza wenye mali nyingi
Na John Stephen
Kutoka Gazeti la Mwananchi

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imesema baada ya kumaliza kupambana na rushwa katika Uchaguzi Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaoendelea hivi sasa nchini, itaanza kuwashughulikia watu wote wenye nyumba za kifahari na mali nyingine kuliko uwezo na kipato chao.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari katika Hoteli ya Movenpick, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Eward Hoseah, alisema baada ya kukamilika kwa uchaguzi huo, wataanza kuwachunguza watu wenye mali ambazo hazilingani na kipato au mishahara yao.

Hoseah alisema watu hao wataanza kushughulikiwa kutokana na mabadiliko ya sheria ambayo sasa inaipa Takukuru uwezo wa kisheria wa kuwachunguza, pamoja maeneo mengine ambayo awali haikuweza kuchunguza, kutokana na sheria hiyo kutowapa nguvu.


Mkurugenzi huyo alisema watu wa aina hiyo, watapaswa kutoa maelezo ya kutosha mahakamani ili kuthibitisha jinsi wanavyohishi maisha ya juu na jinsi walivyopata mali zao.

Alisema katika mabadiliko hayo, mtu yeyote anayemiliki mali kwa niaba ya mtuhumiwa wa rushwa au kumiliki mali kama zawadi baada ya kupewa na mtuhumiwa huyo, itaeleweka kuwa ni mali ya mtuhumiwa wa rushwa na kwamba ni kosa kisheria.

“Baada ya uchaguzi wa CCM tutaanza kuwachunguza watu wanaomiliki mali ambazo hazina uwiano na kipato chao. Tutawataka watueleze wamezipata wapi na jinsi walivyozipata,” alisema Hoseah.

Alisema mtu atakayepatikana na kosa la kijihusisha na rushwa baada ya kushindwa kujieleza jinsi alivyozipata mali zake, atatakiwa kulipa faini isiyopungua Sh410 milioni au kutumikia kifungo cha miaka saba gerezani.

Hoseah alisema Takukuru, imepewa pia meno ya kuwashughulikia wabadhilifu wa mali na kwamba mtu atakayepatikana na kosa atatakiwa kulipa fadia isiyopungua Sh10 milioni au kutumikia kifungo cha miaka saba jela.

Alisema mtu atakayebainika kuhusika kwa namna moja au nyingine kumsaidia mtu mwingine kupata zabuni kwa kupewa malipo fulani, atapaswa kulipa fadua ya Sh15milioni au kutumikia kifungo cha miaka saba gerezani.

Alisema mbali ya kuchunguza mali za vigogo pia baada ya uchaguzi huo wa CCM, wataanza kuvichunguza vyama vingine vya siasa ili kudhibiti rushwa kama walivyofanya kwa chama tawala katika uchaguzi unaoendelea.

Mkurugenzi huyo alitoa kauli hiyo baada ya Mwenyekiti wa Wamiliki wa Nyombo vya Habari (MOAT, Reginald Mengi kutaka kujua mikakati ya Takukuru katika kuendelea kupambana na rushwa ambapo Hoseah alifafanua kuwa wamepata uzoefu wa kutosha wakati wa kupambana na watoa na wapokea rushwa katika chaguzi mbalimbali za CCM zinazoendelea.


Hoseah alisema: “Tumeshapata uzoefu. Tukimaliza kudhibiti rushwa katika chama tawala tutaelekea katika vyama vingine. Pia tutaelekea katika vilabu vya mpira wakati wanapofanya chaguzi mbalimbali.”

Hata hivyo, Mhariri Mkuu wa Mwananchi Communications Ltd (MCL),Theophil Makunga, alionyesha wasiwasi jinsi Takukuru inavyofanya kazi zake kutokana na kutokuwa na vitendea kazi madhubuti wakati wa kupambana na watoa na wapokea rushwa.

“Napata mashaka kama Takukuru wataweza kutekeleza kazi zao. Ukiangalia katika uchaguzi uchaguzi wa CCM, baadhi ya watu wanatumia magari aina ya VX, sasa Takukuru itamkamataje mtu wa namna hiyo wakati anatumia Vitara,” alihoji Makunga.

Naye Mhariri wa Sunday Citizen, Sakina Datoo, alishauri vyombo vya habari kuisaidia Takukuru katika harakati zake za kupambana na rushwa nchini pamoja na kuandika changamoto inazozipata wakati wa kupambana na wala rushwa.

Akichangia mada katika mkutano huo, Mhariri wa Tanzania Daima, Abloson Kibanda, alisema kama mabadiliko ya sheria hiyo yatafanyiwa kazi ipasavyo, yataleta mafanikio makubwa katika kupamba na rushwa nchini.
 
Bahati mbaya sheria yetu siyo retroactive na haiwezi kuwa retroactive.. hivyo yeyote aliyejipatia mali kabla ya julai mwaka huu hanasi!
 
..hivi vita dhidi ya rushwa ndo ishaanza au akili na fikra zangu zinanitega?

..logically,jinsi hali ilivyo[kwa wenye mali za....]hii vita haitawezekana!

..maana hao wenye mali hizo ni vigogo,asije akajikita na kuumia vibaya....maana ukigonga gogo ajali yake ina kishindo!

..nadhani picha sahihi ni kuwa this was just another talk shop!
 
Mwanakijiji,

Sheria mpya ni ile inayowapa TAKUKURU mamlaka ya kufanya uchunguzi huo. Lakini sheria dhidi ya kujipatia mali kwa njia za udanganyifu ni ya siku nyingi. Kulingana na Bwana Hosea, tatizo lililokuwapo ni kuwa TAKAKURU haikuwa na mamlaka ya kuchunguza makosa ya namna hiyo hadi hivi majuzi tu kwa hiyo akina Mkapa wakifumwa na makosa hayo, wembe utakuwa ni ule ule tu. Kitu sijui ni kama Bwana Hosea anasema kweli kuwa atawafuatilia wote. Aisje kuwa anafuatilia akina fulani tu na kuwaacha vigogo wenyewe.
 
Back
Top Bottom