Bila shaka wewe huwafahamu kabisa wanawake. Tena ni vyema ungeelewa tu kuwa moja ya vichocheo vikubwa sana vya wanaume kuwa mafisadi ni katika harakati za kuwakosha wanawake (ambao WENGI WAO hupenda matanuzi mazito bila kutaka kufahamishwa senti zimetoka wapi-kula bila kuwajibika). :wink1:
Lakini cha muhimu sana ni kwamba rushwa si suala la jinsia au kigezo chochote cha aina ya watu (demography). Ni suala zaidi la mfumo wa uongozi na utawala wa nchi. Bila wananchi kuwa na msukumo wa uhakika kupinga rushwa na kuuadhibu bila kuuonea haya uongozi unaoendekeza ufisadi badala ya kuuzawadia, mtaendelea kuliwa tu hata muweke madarakani vijana, vikongwe, watoto, maalbino, wenye chongo, waandikia mkono wa shoto, n.k. Hamtakuwa tofauti na waendao kutafuta majawabu ya maisha kwa wapiga ramli.