Tanzania: Utawala bora vs Rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania: Utawala bora vs Rushwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlalahoi, Sep 19, 2006.

 1. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2006
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Diwani CCM akiri mbunge wake kutoa rushwa

  Na Mwandishi Wetu, Mara

  DIWANI wa Chama Cha Mapinduzi, Mary Bandoma, ametoa ushahidi kuwa mbunge wake alitumia rushwa katika kampeni za uchaguzi jimboni humo.

  Alitoa ushahidi huo katika Mahakama ya Mkoa wa Mara kwenye kesi ya kupinga matokeo ya Mbunge wa Mwibara (CCM), Charles Kajege, iliyofunguliwa na mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Mutamwega Mugayhwa.


  Diwani huyo alisema Desemba 10, 2005, Kajege akiwa mgombea wa CCM kwenye jimbo hilo alifanya kikao cha ndani katika eneo la Bulamba Ginnery, ambapo baada ya mkutano aliwagawia wananchi sh 500 kwa kila aliyehudhuria.


  Alidai kuwa siku moja kabla ya Uchaguzi Mkuu kufanyika, mbunge huyo alialika watu kwenda kumsikiliza katika eneo la Kibara, wengi wao wakiwa wanawake na baada ya mkutano alianza kuwagawia kanga, vitenge na sabuni.


  Diwani huyo alisema, mbunge huyo aliwataka wananchi hao wampigie kura na kuwaahidi kuwa mambo yao yatanyooka wakimchagua kwa kuwa rais aliahidi kumteua kama waziri.


  Shahidi huyo ambaye naye alikiri kupokea mgawo huo, alipoulizwa iwapo aliwahi kumshauri au kumwonya mwana CCM mwenzake juu ya vitendo hivyo, alisema waliwahi kufanya hivyo kupitia kikao cha kamati ya siasa lakini alipingwa na baadhi ya wajumbe.


  Alisema hata mbunge mwenyewe alimwambia kuwa yeye haogopi na ametumwa na rais kugombea nafasi hiyo ya ubunge kwenye jimbo hilo.


  Diwani huyo alisema ameamua kutoa ushahidi huo ili kulinda masilahi ya chama na kuwa CCM imedhalilishwa kwa vitendo hivyo.


  Kesi hiyo inaendelea kusikilizwa leo katika mahakama hiyo mjini Musoma, ikiwa chini ya Jaji Mchome
   
 2. E

  Eric Ongara Verified User

  #2
  Oct 3, 2006
  Joined: Sep 19, 2006
  Messages: 165
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hii hali ni nchi nzima! Kwani Hii si ndio Takrima?
   
 3. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2006
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Ongara,
  Kama hiyo ni takrima au siyo, itabidi tumuulize Chenge atufafanulie.
   
 4. O

  Ogah JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2006
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  hiyo ndio tunaita NONSENSE!!

  Hizi kesi za ushahidi wa kijinga zinaligharimu taifa letu pesa nyingi sana unnecessarily.
   
 5. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2006
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Ogah,
  Hakuna ushaidi wa kijinga...ushahidi wowote ule unaweza kumuingiza mtu hatiani au kumuondoa, hivyo don't try to undermine any evedence.
   
 6. O

  Ogah JF-Expert Member

  #6
  Oct 3, 2006
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mafuchila,

  binafsi si mwanasheria, however kuna vitu viko so obvious, kiasi unahitaji common sense kuona mwisho wa kesi yenyewe

  inaelekea huijui vyema sisiem, huyo shahidi ni obviously wa kupandwa, na ukiangalia huo ushahidi ambao nimeuita wa kijinga kwa sababu shahid wa just talking about takrima (wakati huo ilikuwa rukhsa) and nothing else!!, na at the end utasikia hakuna kesi trust me!!, labda kuwe na ushahidi ambao hata sisi tusiojua sheria tutasema thats hold some water!!, ndio maana nikasema yote ni NONSENSE, ni upotevu wa pesa za wanachi na muda, its so obvious
   
 7. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #7
  Oct 3, 2006
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Navyoelewa mimi huyo sio shahidi pekee katika kesi hiyo aliyejaribu kuthibitisha matumizi ya rushwa.Last week,shemeji wa mbunge huyo said the same thing.Gharama ya demokrasia ni kubwa sana na wakati mwingine huwezi kuipima in terms of money or time.Tusubiri hukumu lakini pia ni vema kufuatilia ushahidi uliotolewa kabla na utaotolewa baadae kabla ya kui-dismiss case hiyo.
   
 8. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #8
  Oct 3, 2006
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Guys, samahani Mr. Charls is my boy na hatuwakimbii marafiki zetu wanapokuwa kwenye shida,

  Huyu ni kijana mdogo sana, kati ya vijana wapya tuliotoka majuu na kuingia CCM wakati mmoja, pamoja na kina Masha, wote tulikuwa US, huyu mshikaji amesoma shule kule Florida, kwa shida mno, maana wizara yake ya nje haikuwa na hela za kumlipia shule, akisomea MA yake,

  Ninasikitika, na kwa bahati mbaya kwamba siwezi nikawaashawishi wananchi humu kwamba hii kesi ni majungu matupu, kwa sababu miezi michache kabla ya uchaguzi huyu mshikaji wangu alioa, tena hata hiyo harusi kama sio michango ya washikaji isingefanyika kama ilivyofanyika, senti tano alikuwa hana, isipokuwa tu baada ya kuona harusi inakaribia, ilibidi kuwaomba wakubwa wake wa kazi, angalau wampe vi-trip Arusha kwenye mikutano ya EAC, ili angalau awe na hela kidogo za harusi!

  Sasa hawa mashahidi uchwara, wanaposema uongo wa mchana inatia huzuni tena sana, kosa kubwa la kijana ni kuwa mdogo ki-umri, na kuwa masikini, hata siku moja siwezi kutetea uozo kwenye taifa, lakini this is unfair by any political standards, na niaamini kwamba Mr. Charles, atashinda hii kesi ingawa ni lazima ni kubali kuwa uwezekano pia ni mdogo, kutokana na kukaliwa kooni na wazee wengi wenye uwezo mkubwa kuliko alionao, sasa hivi hata hela za kumlipa mwanasheria wa kumtetea najua kuwa hana!

  Kwa wapenda maendeleo na mabadiliko, ninasema huyu kijana ni agent of change na sio corrupt, nafikiri hata ukiangalia michango yake bungeni toka aingie inajisema yenyewe, na hasa kwenye issue ya madini, nina wasi wasi kuwa kuna baadhi ya wakubwa waliochukizwa na michango yake bungeni pia,

  Kwa hayo ndugu zangu ninaomba niwaage kwa muda, kwamba ninaelekea huko Mwibara, Musoma kusimama na a friend indeed, na my boy! Nitasimama naye mpaka nione mwisho!
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Oct 3, 2006
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mzee ES, unatuonesha tatizo jingine la CCM? kuwa kwa vile mtu "your home boy" basi he can never do wrong? Kama kijana kavurunda, ni lazima alipe kwenye jamii ili baadaye awe amejifunza! Labda ni kutokana na umri wake mdogo ndo hayo yakamkuta. Vinginevyo, nakushauri ukae mbali naye hadi kesi yake itengemae ama sivyo anaishi na wezi, ana yelala na wezi, na anayekula na wezi labda na yeye ni.... Nafikiri wewe uko juu ya mambo haya.. wacha sheria ifuate mkondo wake!!!
   
 10. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #10
  Oct 4, 2006
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Siajuzuia kitu chochote ndugu yangu, lakini ni lazima tutumie common sense sometimes, shemeji yako anapokwenda mahakamani kukuumiza binadamu yoyote mwenye akili timamu lazima ujielize what is wrong?

  Huyu kijanaa aliyetoka nje kusoma kwa shida, na kuoa kwa shida, hajashika nafasi yoyote muhimu serikalni au kwenye chama, leo anaenda kugombea ubunge ambao kila anayemfahamu pale foreign alisema ni ndoto ya Alinacha kwake kuuupata, aliyekuwa anakaa chumba cha kupanga mpaka kuupata ubunge, leo uniambie eti ni mwizi? ana hela za kutoa rushwa achaguliwe?

  I mean where is busara? Huyu kijana nauli tu ya kwenda kutafuta ubunge ilikuwa tabu, sasa ameiba wapi hizo za kutoa rushwa?
   
 11. K

  Kulikoni JF-Expert Member

  #11
  Oct 4, 2006
  Joined: Aug 28, 2006
  Messages: 203
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mzee ES, kama unahakika kuwa kijana yuko innocent .. go and stand by him. As a matter of principle kuwa utastand na yeyote alie right. Nadhani mshangao ulikuja pale uliposisitiza zaidi u-'home boy', .. 'rafiki in need' etc kuliko kutokuwa kwake na hatia unakokuamini.

  Rafiki yangu akianza kuwa mwizi ndio mwanzo wa urafiki kufa, lakini nikiwa na hakika kasingiziwa I'll stand by him hata iweje!
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Oct 4, 2006
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mzee ES, nakusikia mheshimiwa ila nenda with an open eye...!kwani hakuna kitu kinachoweza kumbadili mtu kama tamaa na hamu ya madaraka!! Kuna watu wamewatoa watoto wao kwa waganga ili wapate that extra edge katika biashara!!....

  Kila la kheri though!
   
 13. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #13
  Oct 4, 2006
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji,

  Ushahidi ni tooooooooooo Gud to be true!!

  Majaji wana akili. Haiwezekani hapa duniani shemeji yako akutolee ushahidi wa kukupinga kama kosa lenyewe sio jinai. TUMIENI AKILI KIDOGO TU!

  Hamna kesi hapo, Surely Mkuu Ogah huu ni upotevu wa hela zetu!

  FD
   
 14. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #14
  Oct 4, 2006
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mshtakiwa bado yuko innoccent...ndio kanuni zetu za kisheria,innocent till proven guilty.Mshtaki na mshtakiwa wana mawakili na mashahidi,mahakama hadi kukubali kesi isikilizwe inamaanisha kuwa wameona it's worth kuisikiliza.

  Inachofanya mahakama ni kufanya haki sio tu itendeke bali ionekane imetendeka,and only way to do that is for mshtaki ku-prove hoja zake beyond any reasonable doubt,na mshtakiwa ku-prove his innocence beyond any reasonable doubt.And what a more convenient place for doing that if not in the court of law?Tusipuuze haki za wenzetu kwa vile tu hatuafikiani nazo.Wenye utaalam wa kisheria ambao unawafanya waamini kuwa kesi hii inapoteza muda wanaweza kuisaidia mahakama,wapiga kura wa jimbo hilo na Taifa kwa ujumla kwa kuupatia upande wa ushahidi (wa Mbunge) hoja za kuonyesha kuwa kesi hiy haina mantiki na ifutwe.Kama kuendesha kesi ni gharama,what about the cots of maintaining mashangingi wanayotumiwa waheshimiwa?Je wananchi wasitafute haki zao kwa vile zoezi zina ni la gharama?

  Kwanini tusisubiri outcome ya kesi hiyo badala ya kuendeleza guesswork?
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Oct 4, 2006
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Haya tusubiri!
   
 16. M

  Mr. Clean Senior Member

  #16
  Oct 4, 2006
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 195
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Rushwa zilitolewa tena saaaana tuu, hata JK kawin uraisi kwa rushwa! Msiniambie nitoe ushahidi kwani everything is clear. Sasa kama huyo shemeji kuna pahala aliahidiwa atawekezwa na Kajenge then wakaja kukorofishana ndo akaamua kuwa upande wa Mutamwega labda kamtip rushwa pia ya kiurafiki mtajuaje?

  ...........................
  :U Can't Change The Nature:
   
 17. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2006
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Nimemuona Charles kwa muda mfupi sana, lakini Yes! kesi ni ngumu, lakini ninaamini kuwa ata-come through, ila sio rahisi kutokana na wanaomlalia macho!
   
 18. C

  Chifu Ihunyo Member

  #18
  Oct 5, 2006
  Joined: Jul 3, 2006
  Messages: 62
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii ni kazi kubwa sana kama Mzee Es unaweza kutoa hukumu ukiwa US je Mahakama za CCM zitasema nini ndugu ? Duh nimechooka sana sana .
   
 19. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #19
  Oct 5, 2006
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Pengine na sisi tunahitaji Gacaca courts kama zile za Rwanda.Food for thought...:)
   
 20. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #20
  Oct 5, 2006
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mlalahoi,
  Tunahitaji GACACA nyingi tu. Tuanze na gacaca ya wala rushwa, tupate Truth Commission ili watu wajue nani anatajirika kwa rushwa na kutafuta njia za kuitokomeza rushwa. Or maybe this is an issue for another topic?
   
Loading...