Kwa kweli nakerwa sana na matangazo yanayorushwa na television ya taifa ya kupiga vita rushwa ambayo yameandaliwa na Taasisi ya Kupiga Vita Rushwa Tanzania. Hapo unaoneshwa traffic akisimamisha daladala halafu anapewa rushwa ya shs 5,000/= analiachilia. Au unaonyeshwa hakimu akimwachia mtuhumiwa baada ya kupewa rushwa ya kama shs 30,000 (kama niliziona vyema kwenye TVT) Vile vile, kuna nesi analazimisha rushwa itolewe ili mgonjwa apigwe X-Ray.
Kweli, hizi rushwa ndizo zinaonekana mbovu sana katika taifa na za kukemewa mpaka kwenye runinga? Mbona hamtuonyeshi mfano wa kigogo mmoja akiingia mkataba wa kuleta/kununua umeme Tanzania? Au wa kununua rada? Au kujenga twin towers za benki kuu? Hizi ni rushwa ambazo kila mtanzania, (pamoja na wewe unayetarisha matangazo hayo) ameathirika. Bei ya umeme imepanda, na kuna tetesi tena kuwa itapanda mwezi wa sita. Priorities zetu za kupiga rushwa ziko wapi? Mmewapigia kelele weee Hakielimu kuwa wanatoa matangazo ya kudhalilisha taaluma za wafanyakazi wa serikali, nanyi mmeanza kufanya hayo hayo. Lakini naamini kuwa mmeanza kufanya hivyo ili ku-divert attention ya wananchi kwenye hizo rushwa kubwa kubwa ambazo zinafanywa na viongozi wa serikali.
Haya, endeleeeni. Labda ndio the best approach. Mimi nayaunga mkono mawazo ya Doc. Mwakyembe wakati wa kujadili mswada wa kupiga vita rushwa.