Tanzania National Identities

Mpango wa kuwa na vitambulisho vya kitaifa:

  • Ni Nzuri

    Votes: 205 58.4%
  • Ni Mbaya

    Votes: 147 41.9%

  • Total voters
    351
kwanini kila mara tuwe na mawazo hasi(negative?) UK kwenyewe pasport feki zipo hata nchi zilizoendelea kama Japani watu wanafoji. Pesa za dola zenyewe zinafojiwa.

Cha muhimu vitambulisho ni muhimu cha kuangalia ni utekelezaji unakuwa je ili uwe na manufaa kwa watanzania.
 
Jamani jamani mweee!

Vitambulisho ni muhimu sana! huwezi kukata majani ya ng'mbe ktk malisho bila kufahamu una ng'ombe wangapi?.
Hata mmasai wa kule ndani anaifahamu hesabu na pengine alama za mifugo yake!

Utahudumia vipi wananchi wako ikiwa unafikiria Dar kuna watu 3/m kumbe wapo 5/m ukiweka na wageni wasiokuwa na karatasi?

Tanzania tunafuga ng'ombe wa jirani jamani kazi lazima inaanza kuwatambua ng'ombe wako.
Sema tatizo ni hilo la deal. Hakuna mradi unaofanyika nchini bila kuwa na Ulaji mkubwa sana, haya maswala ya tender za serikali kama vile mtu anatakiwa kulisha jeshini Lugalo ndipo tunapozungukwa lakini vitambulisho ni muhimu sana!
 
Jamani jamani mweee!

Vitambulisho ni muhimu sana! huwezi kukata majani ya ng'mbe ktk malisho bila kufahamu una ng'ombe wangapi?.
Hata mmasai wa kule ndani anaifahamu hesabu na pengine alama za mifugo yake!..Utahudumia vipi wananchi wako ikiwa unafikiria Dar kuna watu 3/m kumbe wapo 5/m ukiweka na wageni wasiokuwa na karatasi?..
Tanzania tunafuga ng'ombe wa jirani jamani kazi lazima inaanza kuwatambua ng'ombe wako.
Sema tatizo ni hilo la deal. Hakuna mradi unaofanyika nchini bila kuwa na Ulaji mkubwa sana, haya maswala ya tender za serikali kama vile mtu anatakiwa kulisha jeshini Lugalo ndipo tunapozungukwa lakini vitambulisho ni muhimu sana!

Hao ng'ombe wa jirani tunawakaribisha wenyewe zizini na tunawahudumia kuliko ng'ombe wetu wenyewe.

Kama kuna raia wa kigeni wameweza kupata kazi sehemu nyeti bila vipingamizi na wengine wamekingiwa vifua na vigogo unafikiria watashindwa kupata hizo ID?

Hili ni wazo zuri kama maslahi ya nchi yatawekwa mbele na sio maslahi ya wachache at least ule ushenzi wa kusimamishwa na polisi anakuuliza kitambulisho kikowapi wakati anajua jamhuri haitoi vitambulisho utakwisha.
 
Wazo la kuwa National IDs ni zuri, nchi nyingi duniani zina aina fulani ya ID; najua UK wanatumia Insurance Number, Australia wanatumia Tax File Number, Marekani wa Social Security Number, Japan nao wana document yao siikumbuki jina tena ila akina-wakuja huwa wanapewa Alien Registration Card, al mradi kila nchi ina namna fulani ya kumpa namba maalum raia wake, na namba hii haina uhusino na namba ya passport yake.

Ukweli kuhusu namba hizi ni kuwa:

(a) Siyo fool proof na zinaweza kutengezwa za bandia; Marekani inasumbuliwa sana na wamexico wanaojitengezea Social security card za bandia. Wengine wao wanazitumia kadi hiz kwa muda mrefu hadi miaka kumi bila kushikwa. Kwa hiyo madai ya kuwa tukiwa na National IDs tutapunguza wazamiaji yanakuzwa tu. Document za aina hiyo ndiyo zinazoweza kufanya wazamiaji wawe wengi. Kama wanapata passport zetu itakuwaje washindwe kupata hizi IDs?

(b) Namba zinazotumika huko nje zina malengo kadhaa na mara nyingi siyo kumtambulisha mtu kuwa ni raia, kwa vile ukienda nchi ile kihalali unaweza kupata kitambulisho hicho hata kama siyo raia. Kwa nchi nyingi, namba hizi hutumika kama index ya mtu kwenye database inayotunza taarifa za kila mtu nchini kwa mfano mapato ya mtu na kodi yake, financial history ya mtu inayosadia kuelewa credit worthness yake, record ya michango yake kwa ajili ya malipo ya uzeeni, tarehe ya kuzaliwa na mahali alipozaliwa, vile vile zinatunza criminal record ya mtu. Hii inahitaji database nzuri sana ambayo sidhani kama kweli Tanzania tumeshatengeza.

(c) Ingawa namba hizo pia zinaweza kutumika kufahamu uraia wa mtu, siyo kawaida watu kutembea na kadi zile kwa vile vitambulisho vingine vya kawaida kama Drivers Licence na Passport vinaweza pia kutumika kuingia kwenye data base na kupata taarifa za mtu.

Kwa maoni yangu, pamoja na faida za vitambulisho hivyo, sidhani kama muda wake umeshafika kwa sababu hatujajenga mazingira ya kuweza kutunza record za raia na kuzipata mara moja, na vile vile kutumia record hizo kujua raia yuko wapi, yaani akitakiwa na serikali aweze kupatikana mara moja.

Nadhani kuwa serikali ingeanza maandalizi ya kutayalisha ujio wa National IDs kwa kufanya mambo yafuatayo:

(i) Kutengeneza utaratibu mzuri wa kuweka physical addresses za makazi ya kila raia. Huwezi kumtafuta mtu kwa kutumia P.O.Box, lazima kila mtaa upewe jina na kila nyumba iwe na namba. Nyumba zote zilizojengwa kiholea zitafutiwe utaratibu wa kutambulikana, na endapo nyumba itabomolewa, ni lazima serikali ijulishwe. Kwa hiyo, serikali inatakiwa iwe na data za makazi ya kila raia wake, na endapo raia akihama nyumba, ni wajibu wake kwenda kusahihisha record zake serikalini.

(ii) Kujenda database ya kuaminika kutunza record za raia wote. Database hiyo itunze record za vizazi, vifo, criminal record, mali zake na malipo ya kodi, movements na mambo mengine kama hayo. Mtu anapoondoka nchini vile vikaratasi tunavyojaza airport visiwe vinaishia pale, vinatakiwa viingie kwenye permanent record.

Katika mjadala wa katiba nilikuwa nataka kuongelea hili la majukumu ya Wizara ya Mambo ya Ndani na utunzaji wa record za raia lakini naona nimechelewa sana. Ukweli ni kuwa kwa sasa, hizi record zetu ziko shaghla baghla sana. Kuna miaka kadhaa iliyopita nilikuwa nahitaji birth certificate yangu ambayo kiukweli serikali haikuwa na record zake kwa sababu nilizaliwa wakati wa mkoloni huko vijijini ambako hakukuwa na utartibu wa kuandikisha vizazi na vifo. Lakini nilipotaka birth certificate ile nilichotakiwa kufanya ni kuandika ninavyotaka cheti kile kisomeke badala ya wao kutafuta record. Kwa bahati nzuri mimi ni mtanzania, lakini je kwa utaratibu huo unadhani mzamiaji atashindwa kupata cheti hicho? Hii ndiyo maana nasema kuwa kwanza ni lazima serikali isafishe nyumba yake kwa kutengeza data base nzuri na ya kuaminika.

Baada ya maelezo hayo machache, naungana na wale wote wanaopinga kuanzishwa kwa vitambulisho hivi kwa sasa hivi. Tutakuwa tunachezea raslimali tu. Kama serikali itasisitiza kuendelea na mradi huu, ni dhahiri kuwa lengo siyo kuwapa vitambulisho wananchi wake bali lengo ni labda ni kupeana ulaji tu kama walivyohisi wachangiaji wengine.
 
Hao ng'ombe wa jirani tunawakaribisha wenyewe zizini na tunawahudumia kuliko ng'ombe wetu wenyewe.
Kama kuna raia wa kigeni wameweza kupata kazi sehemu nyeti bila vipingamizi na wengine wamekingiwa vifua na vigogo unafikiria watashindwa kupata hizo ID?
Wewe juzi tumeona tuu wanafuzi wa kigeni wamepata mkopo kutoka body ya mikopo wakati watanzania wanakosa elimu!! Huu ni mfano tuu lakini inawezekana nchi yetu inatumia raslimali nyingi sana kuhudumia wageni.
 
Nakubaliana nanyi ktk baadhi ya sehemu lakini nashindwa kumeza baadhi ya sababu.

Ndugu Kichuguu, huwezi tengeneza vitambulisho bila kuwa na database! kwa hiyo tunavyozungumza hivi tayari serikali imesha orodhesha vitu vinavyohitajika ktk utoaji wa hivyo vitambulisho.

Hili swala la wageni kuingia nchini lipo tu..nalitaendelea kuwepo kama ulivyosema lakini kweli tusifanye kitu ati kwa sababu wataendelea kuingia?...Ni sawa na kujiuliza hivi kweli kuna sababu ya kuwa na sheria wakati kila siku watu huzivunja na wataendelea kuzivunja!..

Tuwe na vitambulisho tusiwe navyo bado wataingia nje ya sheria lakini tukumbuke tu kwamba kutokuwepo kwa database ya vitambulisho hawa wageni leo hii wanafaidi zaidi kiasi kwamba sisi wenyewe tunashindwa kutofautisha kati ya wazamiaji na wenyeji na hata kisheria inakuwa kazi kubwa zaidi yanye gharama. Na ndi maana mnaona matatizo mengi sana leo hii yakijipanga na kuzaliana siku baada ya siku.

Kwa hiyo hao wazamiaji hata wakiishi hapa miaka 10 bado watafahamika kama wazamiaji tu. Uzuri wa Bongo wanaokuja sii watu kama Wamexico, cheap labour ni hawa watu wanaojifanya wasomi kumbe mijizi mikubwa! ambao wanachangia sana ongezeko la bei ya bidhaa nchini mwetu, ukosekanaji wa ajira na kuleta madawa feki.

Pia, Utaratibu wa kutoa pasi zetu utaimarika zaidi kutokana na kuwepo kwa vitambulisho hivi! maanake pasi haiwezi toka kama huna Kitambulisho cha uraia. Lakini kila tunavyokubali kuacha leo wakati matatizo yanazidi kuongezeka sidhani kama ni solution bali ni kuongeza kazi kubwa na ghali huko mbeleni.

Vitambulisho havihitaji address ya mtu anakoishi, Watanzania ni watu wa kuhama hama millioni 35 hadi 50 hakuna haja ya address unapoishi ila kuna kila haja ya kuorodhesha mahala ulipozaliwa na ukoo. Hizo criminal record kama zipo zitahamishiwa ktk faili lako na ndio mwanzo wa ufanisi.
Hiyo ngoja ngoja Wanyamulenge wanazidi kujazana, tuwawahi wakiwa bado wana accent.

hao ng'ombe tunaowakaribisha wanaingia kirahisi sana bila ukaribisho wa mzee. Yaani mtu yeyote anaweza kuwaingiza ndani sio lazima wapitie immigration. Nina hakika asilimia zaidi ya 70 ya wazamiaji nchini hawana hata pasi na hawana sababu ya kuwa na pasi kwani hakuna vitambulisho na wanaweza jichanganya wasiulizwe kitu.
 
Ninachoouliza, ni kitu gani serikali inataka kutambulisha? Sura, Uzawa, Utaifa, au Mahali, makazi au kitu gani? Kama ni suala la Utaifa, ni kutoa passport za kusafiria kwa kila mtanzania. Kama ni sura, hilo halina shida piga picha hadi ziungue! Kwa vyovyote vile unaweza kumtambulisha mtu ambaye hujui aliko? Ndio maana kwa ufupi huwezi kuwa na kitambulisho kimoja. Ni vizuri kuwa na aina mbili za utambulisho.

a. Kitambulisho cha nani yuko tanzania. Hapa unaweza kuwa na mfumo wa namba, za wazawa na wageni. HIvyo kila Mtanzania ana namba fulani na mgeni ananamba ya aina fulani. Vyote hivyo vinawezekana tu hadi uwe data clearance center, ambapo maelezo yote kuhusu mtu mwenye namba fulani yanapatikana. Kwenye hilo hautaji picha.

b. Kitambulisho cha makazi. Hiki ni muhimu sana na kinaonesha nani anaishi wapi. Kwa kitambulisho cha aina hii ni lazima kiwezeshe mtu kujulikana anaishi wapi, siyo mtaa au kijiji tu, bali hadi nyumba na namba ya chumba ikibidi. Hili ndilo la msingi sana.

c. Kitambulisho cha nani ni nani. Kitambulisho hiki kitaunganisha yote mawili ya kwanza na kuongezea picha.

Ukiwa na kitambulisho chenye mambo hayo matatu basi utakuwa umepata kitambulisho cha kitaifa.
 
Mkandara,

Ninaamini kuwa vitambulisho hivyo havisaidia lolote kama havitakuwa verifiable; jamaa watavichonga tu. Kama watu wanafyatua noti za dola hawatashindwa kabisa kufyatua hivyo vipande vya karatasi au plastic hata kama vitakuwa na picha ya mhusika.

Ukishajenga utaratibu kuwa kitambulisho hicho ndiyo haki yako ya uraia, basi hao "ng'ombe" kama unavyowaita watavipata na watadai haki hizo kwa nguvu wakati huna database ya kuverify kama vitambulisho hivyo ni halali.

Nimeshaona wasomali wakimbizi wengi wana passport za zamani za Tanzania aisee; wamekwama tu baada ya passport zetu kubadilishwa. Inabidi kweli serikali iwekeze kwenye kujenga database ya raia wake. "Ng'ombe" wakiingia kinyemela tutaishi nao ndiyo, lakini hawakuwa kwenye database yetu.

Baadaye tutaweka sheria za kuwataka waajiri wote wapate verification ya uraia wa mtu kutoka kwenye databse hiyo kabla hawajamwajiri.
 
Jamani swala la ID ni zuri sana kwa sasa hivi kwa sababu moja kubwa ambayo ni kumsaidia MTZ kutoka kwenye Ufukara.

Pamoja na sababu nyingine ambazo wachangiaji wengine wamesema, naona niongeze hili la kuweza kukopa pesa kutoka Benki. Hiyo itakuwa ni moja ya gurantee ya serikali kuweza kuwapa Benki kwamba huyu mtu mkopesheni kiasi fulani n.k. – Kwani serikali inakuwa inamtambua.

Sasa hivi watu wengi wananyimwa credit kutokana na kutokuwa na aina yoyote ya ID. Ukimpa credit as a banker hata hujui utampata wapi lakini kukiwa na ID itasaidia sana. (Tusisahau wako watu wengi ambao wanaziibia benki kwa kutumia majina mengi bila kutambulika) Kisheria aki-default mahakama inabidi itoe judgement pale anapoishi sasa hebu niambie utampata nani Dar uswahilini ambako namba hamna.

Hilo la ID ni muhimu sana na vile vile kuwa na mipango ya nyumba kuwekwa number – Halmashauri za wilaya na mikoa zianze hili kwani number zipo lakini haziandikwi.

Anyway vitambulisho vitatolewa hilo limepita la msingi ni kufahamu vitakuwa kiasi gani kwa WTZ wa kawaida. JK alipokuwa UK alisema vitagharimu approx. $70 million. Uthibiti mkali uwekwe huko isiwe kama passport ambapo wageni tayari wengi wanazo.
 
Kwenye issue ya database nadhani inabidi waanze na kutoa namba kwa kila mwananchi. kwenye hili zoezi nadhani taasisi zote za umma na binafsi zishirikishwe I.e waajiri, mifuko ya pensheni, tume ya uchaguzi kwa kuanzia.
 
Nimepata tetesi kwamba zabuni ya kutengeneza na kusambaza vitambulisho vya kitaifa imetolewa kimizengwe.

Je, kuna mwenye taarifa juu ya tuhuma hizi?

Zabuni imetolewa kwa nani (kampuni gani)?

Nani aliyehakikisha watu hao wanapewa?

Je, waliopewa wana uwezo wa kutimiza masharti hayo?


Tafadhali, mwenye taarifa kuhusu haya awasiliane nami kutumia Ujumbe Binafsi (Private Message).

P.S. Hizi taarifa ni nyeti sana, na ni za hatari. Anaweza kuondoka mtu hapa!
 
MwanaHaki,

Just for your information:-

Serikali haijateua mzabuni kutengeneza vitambulisho

na Mwandishi Wetu, Dodoma


SERIKALI bado haijateua mzabuni wa kutengeneza vitambulisho vya taifa nchini na kwamba kazi hiyo itasimamiwa na taasisi ya vitambulisho vya taifa iliyoanzishwa nchini.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, alieleza hayo katika mkutano ulioitishwa na Waziri Mkuu, Edward Lowassa, mjini Dodoma kumuaga Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini, Bibi Judy O'Connor.

Akifafanua hoja kuhusu taratibu za utengenezaji wa vitambulisho vya taifa, Masha, alisema aliyeteuliwa ni mshauri wa kitaalamu kuhusu utengenezaji wa vitambulisho vyenyewe.

Alisema mshauri atatoa ushauri kuhusu aina gani nzuri ya kitambulisho, kama ni cha kadi ya plastiki au vinginevyo na aina gani za takwimu zitaingizwa kwenye kitambulisho hicho.

Kumekuwa na hoja mbalimbali kuhusu utengenezaji wa vitambulisho vya taifa ambavyo ndivyo vitakuwa vinavyomtambulisha Mtanzania. Miongoni mwa hoja hizo ni kwamba tayari amekwishateuliwa mzabuni.

Baadaye katika karamu ya chakula cha mchana katika Hoteli ya New Dodoma, Waziri Mkuu, Lowassa alimsifu Bibi O'Connor kwa kuwa mwakilishi mzuri wa Benki ya Dunia katika Tanzania.

Lowassa alisema katika kipindi cha O'Connor kumekuwa na ushirikiano mzuri kati ya pande hizo mbili na kwamba kuna miradi mingi ambayo Benki Kuu imeisaidia Tanzania.

O'Connor anaondoka nchini wiki hii baada ya kumaliza kipindi chake cha miaka minne. Nafasi yake inachukuliwa na John Mcintire ambaye alifuatana na O'Connor Dodoma katika sherehe za kuagana.
 
Kwanini Taarifa Hiyo Imetolewa Na Mwandishi Wa Habari Wa Waziri Mkuu? Pamoja Na Kuwa Alikuwapo, Je,kwa Kawaida Kama Zabuni Haijatolewa Hakukua Na Sababu Ya Kuzungumziwa Hapo Na Mwandishi Wa Habari Wa Waziri Mkuu Kuisambaza Kwa Waandishi Wa Habari Jioni
 
MwanaHaki,

...........Kumekuwa na hoja mbalimbali kuhusu utengenezaji wa vitambulisho vya taifa ambavyo ndivyo vitakuwa vinavyomtambulisha Mtanzania. Miongoni mwa hoja hizo ni kwamba tayari amekwishateuliwa mzabuni.


Kwanini Taarifa Hiyo Imetolewa Na Mwandishi Wa Habari Wa Waziri Mkuu? Pamoja Na Kuwa Alikuwapo, Je,kwa Kawaida Kama Zabuni Haijatolewa Hakukua Na Sababu Ya Kuzungumziwa Hapo Na Mwandishi Wa Habari Wa Waziri Mkuu Kuisambaza Kwa Waandishi Wa Habari Jioni

kuiangalia kwa umakini utaona umuhimu wa kutolewa habari hio
 
Je ile contract aliopewa yule Mdosi au Muhindi wa Kenya enzi za Alhaji Hassan Mwinyi kupitia Foreign Affairs ya imeishia wapi na Fedha tulisha lipa.
 
Unakumbuka Ule Mradi Wa Vitambulisho Kwa Nchi Ya Tanzania


Huu Mradi Ulitungwa Na Jamaa Fulani Wa Hapa Hapa Tanzania Kampuni Yao Haina Jina Maalumu Lakini Mkurugenzi Wake Aliwahi Kufanya Kazi Kiwanda Cha Kutengeneza Karatasi Enzi Hizo Na Kukifilisi Kiwanda Cha Kutengeneza Karatasi Offisi Zake Zilikuwa Pale Daily News Azikiwe .

Mkurugenzi Huyu Ni Rafiki Mkubwa Wa Lowasa , Mke Wake Ni Katibu Mkuu Wizara Moja Ya Kikwete Na Ni Kada Wa Siku Nyingi Wa Ccm , Amefilisi Kiwanda Cha Karatasi Mpaka Leo Hajawahu Kuulizwa Wala Kushitakiwa Na Hamna Mtu Mwenye Mpango Wa Kumuuliza Wala Kuhoji Na Mke Wake Kupandishwa Cheo Kikwete Alivyoshika Hatamu

Mtoto Wake Mmoja Wa Kike Anasoma Uingereza , Rafiki Yake Mwingine Wa Karibu Anaitwa Ole Yeye Ni Engineer Huko Afrika Kusini , Aliwahi Kuwa Mkurugenzi Wa Taasisi Ya Mawasiliano Tanzania , Alipomaliza Hapo Aliamua Kwenda Kuishi Na Kuanzisha Biashara Afrika Kusini Na Nchi Zingine Za Ulaya Ili Asigundulike Kama Bilali Anavyofanya Na Viongozi Wengine Wanavyoiba Na Kuhamisha Mali Za Ummah Nje Ya Nchi

Hapo Chini Niattach Proposal Ya Mradi Huu , Naomba Kuusome Kwa Makini Na Kuangalie Je I Faida Kwa Taifa Letu Changa Kama Tanzania ? Yule Mtu Ambaye Anaishi Shinganya Atafaidika Nini Na Vitambulisho Vya Uraia ?

Je Hawa Watu Wasio Jua Kusoma Wala Kuandika Nao Watafiaidika Nini Na Hivi Vitambulisho Vya Uraia ? Serikali Haijawahi Kusema Au Kutamka Hadharani Faida Za Vitambulisho Hivi , Kiafya , Kuchumi Na Kimaendelea Na Kaya Kusika Vyote Hivi Hatujui

Leo Tunaletea Vitambulisho Hii Kasheshe

Kama Inawezekana Watu Wafanya Mgomo Wa Kutojiadikisha Au Kutochukuwa Vitambulisho Hivi , Pesa Inayotumika Kwa Mradi Huu Inaweza Kujenga Shule Zaidi Na Kuajiri Watu Zaidi Au Kukopesha Wajasiria Mali Wafanyie Mambo Makubwa Zaidi

Angalia Attachement Nimeweka Jambo Fulani Hapo
 
Hapa wanaweza kuboronga tena vikaja vitambulisho vyenye low quality havina maisha ya muda mrefu halafu waanze blah blah zao kama kawaida maana katika nchi yetu hakuna kinachofanyika bila kuwa na matatizo.


Vitambulisho vya taifa kugharimu Sh2 trilioni
Na Tausi Mbowe
Mwananchi

SERIKALI imesema kuwa mtengenezaji wa vitambulisho vya Taifa atapatikana kwa njia ya zabuni itakayotangazwa kitaifa na kimataifa na kwamba mradi huo utagharimu dola za Marekani 152 milioni ( zaidi ya Sh1.9 trilioni).

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uhamiaji Wizara ya Mambo ya Ndani, Cunibert Sambalyegula alisema jana kuwa upembuzi yakinifu wa mradi huo umeshakamilika na ushauri wa kitaalamu kutokana na upembuzi huo unaonyesha kuwa mradi huo unatekelezeka.

"Upembuzi yakinifu umekamilika, ushauri wa kitaalamu kutokana na matokeo ya upembuzi huo unaonyesha kuwa mradi huo unatekelezeka na vitambulisho hivyo vitaanza kutolewa na kugawiwa kwa wananchi mwaka 2009," alisema Sambalyegula.

Alisema kuwa kwa mujibu wa upembuzi huo imependekezwa kuwa vitambulisho hivyo vitolewe kwa njia ya teknolojia ya smartcard.

Sambalyegula alisema tayari jengo la ofisi za mradi huo limepatikana na mipango ya ukarabati mdogo na upatikanaji wa samani za ofisi unaendelea kufanyika.

Alisema ununuzi wa jengo hilo limegharimu sh bilioni 2.5 liko Upanga Sea view Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, ambapo katika mwaka huu wa fedha watalifanyia ukarabati jengo hilo na kununua magari na pikipiki kwa ajili ya kurahisisha utekelezaji wa zoezi la utambuzi na uandikishaji wa watu katika Kanda.

Alisema kuwa kwa sasa Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi ya Umma)zipo katika mchakato wa kuunda wakala, ambapo utakuwa na jukumu la kusimamia na kuendesha zoezi zoezi zima la utoaji wa vitambulisho hivyo na tayari imeshaundwa iliyopewa jukumu la kuandaa nyaraka muhimu za uanzishwaji wakala vitambulisho.

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani imeandaa mpango maalumu wa kutoa vitambulisho kwa raia wote waliofikisha miaka 18 ambavyo vitamwezesha mwananchi kujulikana kuwa ni raia wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom