Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,254
Bubu, hivi trilioni moja ni sawa na bilioni ngapi?! mbona kwenye hayo maandishi naona kama si sawa vile... dola moja hivi sasa ni wastani wa sh. 1250, je dolla milion 152 inakaribia trilion 2?!
Anyway, kwenye hii issue miye naona ni kukurupuka ki uamzi, ndiyo wanasema wamefanya uchunguzu wa kutosha na wame involve wataalam mbali mbali, lakini kwenye nchi ambayo asilimia nyingi ya raia makazi yao hayako katika ramani hili zoezi litafanikiwa kweli... hata kama linafanikiwa; je hii ni kuondokana na tatizo lipi... raia wakigeni? wataalam wa kigeni wasio na vibali? wakimbizi? au ni zoezi mojawapo lenye gharama lakini manufaa yake wala hayataonekana. Kuhusu pasipoti kwanini isiwe njia mojawapo ya kuwatambua watu, maana yake watu wenye kuleta matatizo ni wale wanao safiri safiri na siyo wananchi ambao wamejikalia kwenye vijiji vyao miaka nenda rudi, hivyo vitambulisho kwao havita kuwa na cha maaana cha kuongeza.
Hizo pesa kwa kweli ni nyingi, na zinaweza kufanya mengi...lakini zoezi la vitambulisho kwa sasa sioni faida yake ya hivi karibuni, tukisubiri hili zoezi linaweza kuwa cheaper zaidi kutokana na mabadiliko ya teknolojia pia litaleta maana zaidi kwani serikali inampango wa kupima vijiji vyote ifikapo 2015 (natumaini), hivyo hili zoezi likienda sambamba na ukamilishaji wa vipimo hivi linaweza kuleta maana zaidi. Kwani yanayowafanya wafikirie mambo ya vitambulisho hivi sasa si mengi kiasi cha kuingia gharama kama hiyo. Kule Ngara na kanda nzima ya magharibi wakimbizi wanazidi kurudishwa makwao, pia cha kukumbuka ni kuwa watu wanaopelekesha kuundwa kwa vitambulisho kama ni wageni kutoka nchi nyingine basi tujue kuwa wana uwezo wa kutafuta vitambulisho feki wakiwepo hapa nchini.
Naisihi serikali isikimbilie zoezi hili, tukisubiri kidogo hapo mbeleni litakuwa na manufaa zaidi na litakuwa bora zaidi na litakuwa rahisi zaidi.
SteveD.