Tanzania National Identities

Mpango wa kuwa na vitambulisho vya kitaifa:

  • Ni Nzuri

    Votes: 205 58.4%
  • Ni Mbaya

    Votes: 147 41.9%

  • Total voters
    351
Sijui basis ya maamuzi yetu inatoka wapi, maana sijakutana na taarifa yeyote ya utafiti inayohalalisha umuhimu wa huu mradi wa vitambulisho vya taifa. Lakini nimeona dada Meghji ametumia sehemu ya kutosha katika bajeti yake kuelezea hili jambo.

Kilichonichosha zaidi ni sababu za huu mradi zilizotolewa na dada Zakia. Yeye anasema sababu mojawapo ni kuimarisha demokrasia. Sasa nimekuwa najaribu kufikiria link kati ya viambulisho na demokrasia, kwa kweli sijaona. Sana sana nimeona katika nchi zingine sababu moja ya kukataa kuwa na IDs ilikuwa ni kwamba IDs zinaingilia uhuru wa watu (freedom/liberty). Sasa sisi hii kwamba IDs vinasaidia kuleta demokrasia tumeitoa wapi?

Kwa maoni yangu, hii project haina maana, ni ghali pasipo na sababu za msingi na yafaa kabisa ipigwe chini!

Nyie mnasemaje?
 
hapana hujaaangalia vyema, ID zitasaidia kwa security ya nchi, cha msingi zifanywe kwa umakini na kupewa wanaostahiki.

hata wakimbizi pia watapungua au ni rahisi kuwagundua, pia demokrasia itapanuka maana si rahisi kwa asie mtanzania kujiingiza kwenye siasa za tanzania.
 
Kitila, wazo ni zuri lakini wanatanguliza mkokoteni kabla ya punda! Vitu vya kwanza vifanywe kwanza... Jinsi ulivyo sasa ni mradi wa ulaji tu!!
 
Mojawapo ya mambo ya kwanza kufanywa ni kuhakikisha watu wanaishi katika anwani zinazoeleweka. Leo hii mitaa haina majina, wala nyumba hazina namba za kueleweka...
 
Kitila and Mzee Mwanakijiji,

Mambo yale ya Zitto/AC na siasa tuweke pembeni, lakini this argument, the argument kwamba wananchi hawahitaji vitambulisho, has to be the lowest level you have gone in any argument here at JF.

Mwanakijiji - uko Michigan, sio? Hebu jisachi hapo ulipo, kama huna ID mfukoni (State ID or Driver's licence - yenye barcode or a chip), you have the right to say Watanzania hawahitaji ID.
 
mugongo, ni wapi niliposema wananchi hawahitaji vitambulisho? Unatambulisha nini sura tu? alichosema mwanagenzi hapo juu ndio kitu cha kwanza kufanywa..!
 
National ID is an expensive white elephant project. Kama ni vitambulisho tayari tuna passport za kisasa kabisa?? pia tunavyo vitambulisho vya wapiga kura, zoezi ambalo lilighalimu pesa kibao.

Honestly hata mimi sioni huo ukuzaji wa demokrasia unaotokana na National IDs sana sana vitu kama "daftari la kudumu la wapiga kura" ndio vilikuwa adui mkubwa wa demokrasia "madudu" yaliyofanyika kule kila mtu anayajua.

Kama suala ni kuzuia wakimbizi nashindwa ku figure out how hizo IDs zitazuia wakimbizi ikiwa wanaweza kupata passport hawatashindwa kupata hizo IDs. Kubwa hapa sio uwekano wa kughushiwa laa, suala hapa ni dishonest ya watendaji wetu. Kama watu wenye hadhi ya ubunge (with all marupurupu) wanasaidia kuwapatia wasomali passports unategemea nini kutoka kwa maofisa wa uhamiaji (choka mbaya)

Kuna mtu aliwahi kugusia kuwa tatizo letu tunageuza vipaumbele, kwa mfano bajeti ya wizara ya miundo mbinu hakukuwa na fungu la fedha la kujenga barabara mpaka wajumbe wa kamati husika walipoikataa ndio ad hocly wakaanza kunyofoa huku na kule na kuweka fungu la barabara. Sasa je baina ya barabara na IDs kipi muhimu? mifano ya kisengere nyuma ya priorities ni mingi sana, kubwa hapa ni kuwa kwenye uchumi tunasema since resources are scarce then we have to plan according to scale of preferences, and to me Ids lies at the bottom of it.
 
Nilipokuwa chuoni mwaka wa kwanza, zoezi la timu yetu darasani ilikuwa ni 'IWAPO MRADI WA VITAMBULISHO UNAFAA HAPA UINGEREZA AU LA'' na haya ni maelezo yangu kwa kumbu kumbu na maoni yangu:

Suala la ID CARDS duniani kote lina utata. Utata baina ya serikali na wanaodai haki za binadamu kuwa ni kuingiliwa uhuru binafsi.

Pili utata unaojitokeza ni katika suala zima la fedha kuwa kiasi kikubwa sana kinahitajika na vipi utaweza kukidhi matakwa yote ya utambulisho wa mtu ili kutetea (justify) gharama kubwa sana za Vitambulisho vya Taifa.

Hapa Uingereza hivi sasa mdahalo ni mkubwa sana wengi wakidai mradi huo hauna maana yeyote na vitambulisho walivyonavyo wahusika vinatosha kabisa, ie. Kwa Uingereza mkaazi yoyote mwenye umri wa miaka 16 na kuendelea ana kadi ya bima {insurance number} ambayo inamuelezea mchango wake katika mfuko wake wa pensheni kwa jinsi anavyofanya kazi, pia hiyo hutumiwa na BODI YA MIKOPO YA SHULE kujua mchango wake uweje na alipwe kiasi gani.

Aidha ni kadi hiyo hiyo ndio hutumiwa na mamlaka ya kodi kumtoza mhusika kodi.

Lakini kadi hiyo ina walakini kiasi kwa vile haina sura ya mtu, taarifa zake nyingi ni za siri na polisi huhitaji kadi hiyo pale tu wanapohitaji kujua baadhi ya mambo kuhusu mtu husika.


Wanaodai Vitambulisho vipya wanatoa hoja kwamba ongezeko la ugaidi duniani limezua hitajio jipya kabisa la vitambulisho vyenye nembo ya macho na pengine alama za vidole ili kumtambua mtu, na mjadala ni je hivi vitu viwe ni sehemu ya leseni ya gari ya mwenye nayo au iwe ni kadi 'stand alone'? Bado mijadala ni mingi....


Kwetu Tanzania, kwa wananchi walio wengi hawana aina yoyote ya utambulisho kuwa ni mtanzania..Passport ni kwa wenye nazo na wanaozihitajia {bado nchini mwetu Pasi ya kusafiria ni mpaka ukiihitaji sio 'haki' ya mtu husika}

Ni aghalabu kumkuta mtu anatembea na pasi bila matumizi yeyote.

Ni kweli kwamba Tanzania tunahitajia wananchi wetu wawe ni kitambulisho cha aina fulani ili waweze kuwa na uwezo wa kupata huduma za jamii vizuri na pia kujua mtanzania 'halisi' ni nani.

Kwa Tanzania nadhani Kitambulisho kitasaidia na kuwa na manufaa pale tu iwapo kitatumika kama ni moja ya nyenzo ya kurahisisha huduma za serikali kwa wananchi.

Kwa mfano, Ikiwekwa kwamba lazima mtoto anaemaliza elimu ya msingi awe na kitambulisho, na kila unapoomba kazi lazima utoe kitambulisho hicho kisajiliwe, kiwe na 'link' ya moja kwa moja na TRA na NSSF na kuweza kurekodi malipo yako ya uzeeni tangu ukianza kazi au ukijiajiri...

Kadi hiyo hiyo itumike katika fomu mbali mbali za serikali na huduma za jamii na iwe ndio kadi na utambulisho rasmi wa kutoa mikopo ya wanafunzi {ULIPAJI WAKE UTAKUWA RAHISI} kwani mwanafunzi akimaliza tu chuo akiajiriwa 'data' zake zitakuwa zinatumika kulipia madeni aliyokopeshwa....


Na vile vile kwa upande wa usalama iwe ni hivyo, ukitaka pasi basi ni lazima utoe kitambulisho, ukitaka leseni lazima utoe kitambulisho, ukikamatwa ama kwa kushukiwa au 'at random' uwe na aina fulani ya kuthibitisha kweli wewe ni saidi au kitila.

Lakini mradi huu wa vitambulisho pia kuna mambo yawe wazi:

- Uwe ni mradi mama ''super project'' utakaoweza kufanya maisha ya mtanzania yawe nafuu kwa kuunganisha huduma za serikali, kama ilivyoelezwa hapo juu.

- Ijulikane nani ataweza kulipia gharama, hapa UK imesemwa itagharimu paundi 39 kwa kila mwananchi na kelele ni nyingi.

- Ili mradi huu ufanikiwe lazima kuwe na sheria kuwa LAZIMA UWE NA KITAMBULISHO la sivyo haitokuwa muafaka.

Kwa muktadha huu nadhani binafsi naunga mkono wazo la msingi la kuwa na vitambulisho Tanzania.
 
Naam ni mdahalo mtamu sana kuoanisha Vitambulisho na Demokrasia hususan ikiwa vitambulisho vinalenga katika kuimarisha demokrasia....

will touch on them in my next posting. Hapo juu nilikuwa najaribu kujadili ID CARDS AND DEVELOPMENT IN POOR COUNTRIES...LESSON FROM UK
 
Kuna mahali ilizungumziwa kuhusu physical address(anuani ya makazi)....kama ilivyo huku ughaibuni. Hilo nadhani ni la msingi na la kwanza.

Ukiona wazo linakuja na linatekelezwa bila maandalizi ya maana (eg speed governor), ujue uwezekano mkubwa ni mradi wa kigogo fulani. Kwa vyovyote wapambe lazima watashabikia kwa sababu watakatiwa chochote. Hapa ndipo tulipo.

Ukiacha hayo, vitambulisho ni muhimu kwa sababu mbali mbali, ikiwemo usalama wa nchi. Sio kila anayeongea kiswahili ni mtanzania.

Kenya wana kipande....sisi je?
 
National ID is an expensive white elephant project. Kama ni vitambulisho tayari tuna passport za kisasa kabisa?? pia tunavyo vitambulisho vya wapiga kura, zoezi ambalo lilighalimu pesa kibao.

Honestly hata mimi sioni huo ukuzaji wa demokrasia unaotokana na National IDs sana sana vitu kama "daftari la kudumu la wapiga kura" ndio vilikuwa adui mkubwa wa demokrasia "madudu" yaliyofanyika kule kila mtu anayajua.

Kama suala ni kuzuia wakimbizi nashindwa ku figure out how hizo IDs zitazuia wakimbizi ikiwa wanaweza kupata passport hawatashindwa kupata hizo IDs. Kubwa hapa sio uwekano wa kughushiwa laa, suala hapa ni dishonest ya watendaji wetu. Kama watu wenye hadhi ya ubunge (with all marupurupu) wanasaidia kuwapatia wasomali passports unategemea nini kutoka kwa maofisa wa uhamiaji (choka mbaya)

Kuna mtu aliwahi kugusia kuwa tatizo letu tunageuza vipaumbele, kwa mfano bajeti ya wizara ya miundo mbinu hakukuwa na fungu la fedha la kujenga barabara mpaka wajumbe wa kamati husika walipoikataa ndio ad hocly wakaanza kunyofoa huku na kule na kuweka fungu la barabara. Sasa je baina ya barabara na IDs kipi muhimu? mifano ya kisengere nyuma ya priorities ni mingi sana, kubwa hapa ni kuwa kwenye uchumi tunasema since resources are scarce then we have to plan according to scale of preferences, and to me Ids lies at the bottom of it.

I got used to this type of contribution....; then all of a sudden..... I did not understand what happened.

Anyways, idea ya kuwa na vitambulisho sio mbaya, lakini kama walivyosema wahenga, 'kusuka au kunyoa,' nadhani kunategemeana na 'priorities' zako kama ulivyozipanga. Je, ni jambo la mhimu sana kuwa na vitambulisho kuliko kuwa na madarasa zaidi, dawa hospitalini, barabara?
 
the project for development of National Identity for all Tanzanians is ongoing.
Office building for the Coordinator of the Project has been secured, and the 2007/08 budget has set aside funds for hiring of key staff, procurement of
office equipment and rehabilitation of the building.

This project is coordinated by the Immigration Department. Citizen Identity Card is vital too for
facilitating tax collection, accessing bank credits, and in war against crime and in building political democracy etc.

Haya ndiyo maneno ya mama Meghji. Mimi naona kuwa na kitambulisho ni muhimo ila sasa tatizo ni utaratibu mzima na tumejiandaaje kwa zoezi zima hili na si kukurupuka. Wana JF kama kenya kunasehemu kama huna national ID huwezi kuingia wala kupata huduma.

Nchi karibu zote duniani zinatumia vitambulisho na wala sio lugha tuu. Wachina na vimacho vyao na lugha yao lakini bado wanavitabulisho. Kitambulisho ni muhimu ila tuangalie je huu mradi nifeasible? je hu mradi ni kwa masilahi yanani?
 
Kwa maoni yangu tunahitaji national ID ili kupunguza raia wa nchi nyingine kujifanya na wao pia ni Watanzania. Kula lazima wanene wale lakini kama kawaida ya nchi yetu hili pia litakuwa na matatizo chungu nzima na hatimaye wataliboronga.

Wale ambao si Watanzania watahonga hata mamilioni na wao wawemo katika wale wanaostahili kupata ID hizo.

Pia zinaweza kuibiwa kwa wingi na zoezi zima likaingia dosari pamoja na kuwa mabilioni yatakuwa yametumika.
 
hili suala ni zuri ila linahitaji maandalizi na utayarifu wa dhati na sio kisiasa.

mfano kule zanzibar wametoa vitambulisho wa mzanzibari ukifuiatilia zoezi zima utacheka, utahisi jinsi tulivyopoteza pesa nyingi na kufikia zoezi kutokuwa na maana yeyote.

vitambulisho mwishowe walipata mpaka waburundi wakenya warwanda na wengineo seuze watanganyika.

cha msingi ww uwe unasapport CCM mambo bomba.

ile iwe case study ya kutorejea uzembe. hili ni suala muhimu umakini unatakiwa uchukulie kwa hali ya juu.

tuangalie utaifa na tuwape wanaostahiki. maana bila ya hivyo tutapoteza pesa nyingi halafu lengo halifikiwi.

nnaomba kuwasilisha
 
the project for development of National Identity for all Tanzanians is ongoing.
Office building for the Coordinator of the Project has been secured, and the 2007/08 budget has set aside funds for hiring of key staff, procurement of
office equipment and rehabilitation of the building. This project is coordinated by the Immigration Department. Citizen Identity Card is vital too for
facilitating tax collection, accessing bank credits, and in war against crime and in building political democracy
etc.

Kweli ku-spin kunataka ufundi! Kumbe Meghi kataja faida kadhaa! Kitila yeye ka-imply kwamba sababu pekee aliyotaja Meghi ya kuanzisha huu mradi ni kwa ajili ya kuimarisha demokrasia!
 
Na kuna mtu hapa kasema hatuhitaji vitambulisho kwasababu tayari kuna passport. Well, that is a contradiction kwasababu kwa kuitaja passport unakubali umuhimu wa vitambulisho. Kama passport ndo iwe kitambulisho, fine: basi Watanzania wote wapewe passport ili wawe na haki ya utambulisho kama Raia.

Kuna mtu hapa kasema tukiwa na vitambulisho, hata Wakenya watachukua vitambulisho vyetu. I think that is a twisted thinking. I think kama hatuna vitambulisho Wakenya ndio wanapata urahisi wa kujitambulisha kama Watanzania.
 
Kweli ku-spin kunataka ufundi! Kumbe Meghi kataja faida kadhaa! Kitila yeye ka-imply kwamba sababu pekee aliyotaja Meghi ya kuanzisha huu mradi ni kwa ajili ya kuimarisha demokrasia!

Mugongomugongo: ukisoma post yangu vizuri utagundua kuwa nilisema sababu mojawapo ni ..,hakuna niliposema "sababu pekee" naamini unajua kiswahili vizuri, wewe ndiye unayeleta spinning.

halafu pia sio vizuri kuita watu wenye mawazo tofauti kuwa wapo "lowest"! nafikiri ni mtazamo tu tunatofautiana. Hata nchi zilizoendelea kama UK wana mawazo tofauti kabisa kuhusu vitambulisho. In fact katika YouGov opinion poll ya leo, 52% ya waingereza hawakubaliani na idea ya vitambulisho! Sidhani kama hawa nao wapo low kama mimi!

nikirudi kwenye mada, unajua najaribu kujiuliza maswali kadhaa kuhusu hii project: kama leo tunashindwa kudhibiti passpaort zetu hadi tunawapa hata warundi na wanyarwanda, tena passport ni kiduchu tu, tutaweza kweli kudhibiti ugawaji wa vitambulisho?

Je, hii project ni sustainable? tunauliza haya maswali maana tunauzoefu ile nchi ni mabingwa wa kuja na miradi ambayo hufia pasipojulikana-vidhibiti mwendo viko wapi? mabasi ya wanafunzi yako wapi? mabasi yaendayo kwa kasi dar es salaam yako wapi? mabwawa ya kumwagilia yako wapi? umeme wa mvua uko wapi?

tuendelee na mjadala.
 
Back
Top Bottom