Tanzania National Identities

Mpango wa kuwa na vitambulisho vya kitaifa:

 • Ni Nzuri

  Votes: 166 54.6%
 • Ni Mbaya

  Votes: 139 45.7%

 • Total voters
  304

Mkandara

Verified Member
Joined
Mar 3, 2006
Messages
15,472
Points
1,250

Mkandara

Verified Member
Joined Mar 3, 2006
15,472 1,250
Mpango huu tumeuzungumzia sana hapa kijiweni na hakika inaonyesha wazi wengi wetu wanachopinga sii kuwepo kwa vitambulisho isipokuwa gharama ya Vitambulisho hivyo. Binafsi baada ya kuuona mfumo mzima wa Kiutawala hapa Tanzania nadhani swala hili linahitaji kutazamwa upya kwa sababu zipo njia rahisi na muhimu kupata faida zote za Vitambulisho.
Kwa mfano hadi sasa hivi swala la wananchi kuwa na Social Security ambayo naweza kuifananisha kwa ukaribu (Tanzania) na Tin number - HALIPO. Sababu sielewi kabisa ikiwa kweli serikali yetu inataka kufanya kazi zake kwa ufanisi.

Binafsi naamini kabisa kabla serikali yetu haijafikiria kutoa vitambulisho ni muhimu kwanza ihakikishe kila mwananchi apatiwe tin number iwe wewe raia ama sii raia wa nchi hii ili kuhakikisha Ukusanyaji kodi na mafao mengine ya kitaifa yanapitia namba ya kodi ya kila mtu.
Ni maajabu ya Mussa kuona kwamba Mtanzania mwenye tin namba ni yule tu anayejihusisha na biashara ama malipo fulani ya kodi za serikali, laa kama huna uagizaji wa mali basi wewe huna ulazima wa kuwa na tin namba. Hii hakika hainingii akilini kabisa kwani umuhimu wa wananchi kupewa tin namba ni mkubwa zaidi ya hivyo vitambulisho na pengine kuna wananchi wengi wasiookuwa na tin namba kuliko waliokuwa nazo! kisha tunajisifia kwa mfumo wetu wa ukusanyaji kodi...Halooo!.

Watu hukatwa ama kupokea kodi na malipo mengnineyo kwa kutumia tin namba zao..hii ndio nguzo mojawapo kubwa ya ujenzi wa maendeleo ya nchi yeyote iweje kwetu kiwe ni kitu kisichokuwa lazima?Tin namba itarahisisha sana ukusanyaji wa kodi na kufahamu nani hajalipa au kuwakilisha claim ya kodi ya mwaka na pia mwaka gani, iwe hata watu wawili au mia wanafanana kwa majina...

Leo hii wapangishaji majumba hawalipi kodi lakini kama Tin namba itatumika kulipia pango kwa kila mpangaji sijui hao wenye kupangisha wataepa vipi kodi. Muhimu pasiwepo na urasimu maanake Bongo hakika imefika ktk hatua nyingine ya Ufisadi - Urasimu...hili ni gonjwa jipya kuliko ukimwi lisiloweza kupata tiba bila kumpata mtawala Dikteta...Wakuu zangu na wa Waheshimiwa tuwe na imani na nchi yetu, tuwe wakweli na wenye uzalendo kuweza kufuata taratibu za usajili wa wananchi ambao unaweza kufanya kazi kwa malengo bora zaidi..

Siku zote ngoma huanzia hapa kwenye vitambulisho vya kodi. Hata wale waliokwenda Ulaya watakubali na maneno yangu kwani wao pia hulazimika kwanza kupata namba ya kulipia kodi hata kama hawana vitambulisho vya kuishi nchi hizo na ndio pekee vinavywawezesha kupata ama kufanya kazi nchi hizo, pasipo namba hizi huwezi kuajiriwa kabisaaa pamoja na kwamba unaweza kuwa na kitambulisho cha Utaifa. Hivi ni vitu viwili tofauti na tin namba kwa kila mwamamchi ndio hutangulia hivyo vitambulisho vya Uraia..

Hivyo naiomba serikali yetu bila kupoteza muda, fedha na kwa urahisi zaidi kuanzisha kampeni ya wananchi kujiandikisha kupewa namba za tina iwe hata mtoto mdogo na namba hivyo ndizo pekee zitakazo mwezesha mtu kupata kitambulisho cha Uraia pindi itakapo fikia wakati wake..
Huu ndio utaratibu unaoelewaweka na wenye kugharibu fedha ndogo sana. na tusiseme haiwezekani kwani kama mashirika ya simu yameweza kuwalazimisha watumiaji wote wa simu kujisajili sidhani kama itakuwa shida kubwa kwa serikali yetu kulazimisha wananchi wote kujisajili ili kupata tin namba kwa majina yao (personal) na biashara zao, kisha ndio mpango wa vitambulisho vya Uraia vitafuata.
 

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Messages
4,141
Points
1,250

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2009
4,141 1,250
huu mradi vipi??>>>

National identity cards information


1. Utangulizi

W
azo la kuanzisha vitambulisho vya taifa kwa raia wa tanzania na raia wageni waishio nchini tanzania lilizaliwa mwaka 1968 katika kikao cha “interstate intelligence gathering” kilicho-jumuisha wajumbe kutoka nchi za tanzania, kenya, uganda na zambia. Kwa wakati huo nchi za kenya na zambia tayari zilikuwa na vitambulisho vyao vya taifa. Iliazimiwa kwamba ili kuimarisha mahusiano ya kiusalama yanayozingatia utawala wa sheria katika nchi hizo nne ni lazima nchi za uganda na tanzania nazo zikatoa vitambulisho vya taifa kwa raia wao.

Kumekuwa na jitihada mbalimbali za serikali kuhakikisha watanzania na wageni wote wanapatiwa vitambulisho vya taifa, lakini jitihada hizo hazikuweza kuzaa matunda yaliyotajariwa kwa kipindi kirefu kutokana na sababu mbalimbali. Mwaka 1986 serikali ilitunga sheria ya vitambulisho ambayo haikutumika wala kutungiwa kanuni zake.

Ni ukweli ulio wazi kwamba kwa wakati huu kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na vitambulisho vya taifa kulingana na mazingira tuliyonayo. Kuanzishwa kwa jumuiya ya afrika mashariki ambapo nchi tano zimeungana na kukubaliana kwamba watu wa nchi hizo wanaweza kutembeleana bila bughudha pia kumeongeza umuhimu wa kuwa na vitambulisho. Ikumbukwe kuwa tanzania na uganda ndizo nchi pekee katika jumuiya hiyo ambazo hazina vitambulisho vya taifa.

Upembuzi yakinifu wa vitambulisho vya taifa ulikwishafanyika na matokeo ni kwamba mradi unatekelezeka. Aidha taarifa hiyo imeainisha makadirio ya gharama za mradi na namna mradi utakavyotekelezwa ambapo teknolojia ya “smartcard” ndiyo itakayotumika kama ilivyokubaliwa na baraza la mawaziri katika kikao kilichokaa mjini dodoma mwezi februari, 2007.

Mhe. Rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania tayari ametia saini hati ya kuidhinisha kuanzishwa kwa chombo cha kusimamia vitambulisho vya taifa kinachojulikana kama mamlaka ya vitambulisho vya taifa au “national identification authority (nida)”. Hati hii imechapishwa katika gazeti la serikali, gn no.122 ya tarehe 01/08/2008.

Aidha katika kikao chake cha tarehe 3 februari, 2007 baraza la mawaziri lilitoa mwongozo kuwa iundwe kamati ya usimamizi (steering committee) ya makatibu wakuu, wakuu wa idara na vitengo vinavyohusika na mambo muhimu kuhusu vitambulisho vya taifa. Kamati hii pamoja na mambo mengine itakuwa na jukumu la kutoa mwongozo na mwelekeo wa program za mradi.

Baraza pia liliamua kuwa taarifa ya upembuzi yakinifu ya kampuni ya gotham international limited (gil) iwe ndio mwongozo wa utekelezaji wa mradi na kampuni hiyo iliteuliwa kuwa mshauri mwelekezi wa mradi.

Katika hatua nyingine, serikali ilitoa mwongozo kuwa taarifa mbalimbali za utekelezaji wa mradi ikiwemo ile ya mshindi wa zabuni ya mkandarasi wa kutengeneza mfumo wa vitambulisho vya taifa ziwasilishwe katika baraza la mawaziri ili kupata ridhaa yake.

2. Dhana ya kitambulisho cha taifa


swala la mfumo wa kitambulisho cha taifa bado ni dhana ngeni miongoni mwa watu wengi hususani umuhimu wake kwa mwananchi, taasisi mbalimbali na serikali kwa ujumla. Hata wakati mwingine baadhi ya watu hudhani ya kwamba ni kitambulisho cha uraia, au ni kitambulisho kama vilivyo vitambulisho vingine vya kazi, au ni kipande cha karatasi chenye picha, jina la mhusika pamoja na anuani yake.


Dhana nzima ya mfumo wa kitambulisho cha taifa ni pana zaidi ya hapo. Pia ni vyema ieleweke kwamba kadi za vitambulisho vya taifa zitatolewa kwa watu wazima kuanzia miaka 18 na sio watoto wadogo kama inavyoelezwa.

Vitambulisho vya taifa kulingana na nchi mbalimbali mfano angola, afrika kusini, bostwana na kenya, ambazo zimeweza kutengeneza vitambulisho vyao vya taifa hutengenezwa kutokana na taarifa zilizohifadhiwa kwenye daftari maalum. Daftari hilo hutunza kumbukumbu za mtu kuanzia alipozaliwa hadi mwisho wa uhai wake, huboreshwa kwa kupokea au kuongezwa taarifa za mara kwa mara za mhusika kutokana na matukio mbalimbali yanayomhusu mhusika. Taarifa hizo huhifadhiwa katika daftari moja, na mhusika hukabidhiwa kadi ambayo hutumika kama alama ya utambulisho. Aidha taasisi nyingine zinaweza kutumia taarifa zilizohifadhiwa kwenye daftari hiyo kwa makubaliano maalum.

Wakati mwingine watu hutaja kitambulisho cha uraia wakiwa na maana ya kitambulisho cha taifa. Ukweli ni kwamba taasisi hii itahusika na kutengeneza kitambulisho cha taifa ambacho kitatolewa kwa raia wa tanzaia na watu wengine ambao sio raia wa tanzania.

3. Umuhimu wa mfumo wa vitambulisho vya taifa


Mfumo wa kitambulisho cha taifa unaanzishwa kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na:-

 • kutambua mtu au mhusika.
 • kusaidia kumtambua mhusika anapohitaji kupatiwa huduma katika taasisi mbalimbali mfano benki,taasisi za mikopo, huduma za afya n.k.
 • kuunganisha mifumo mingine kwa lengo la kuwasiliana na kubadilishana taarifa muhimu ambazo zitalenga kuongeza ufanisi na kupunguza gharama za uendeshaji kuliko ilivyo hivi sasa.
 • kumtambua mtu pale anapofanya uhalifu wa aina fulani; hii itasaidia sana katika kupambana na uhalifu.
 • kutambua wakwepaji wa kurejesha mikopo kutoka kwenye mabenki hasa pale wakopaji wanapochukua mikopo kutoka katika mabenki mbalimbali.
 • kuweka kumbukumbu za matukio ya uhalifu katika daftari.
 • kutambua walipa kodi, hii itasaidia kupambana na wakwepaji wa kulipa kodi.
 • kumtambua mtu anapofanya biashara mbalimbali kwa kutumia majina tofauti.
 • kuhakikisha kuwa mtu anapata stahili zake za jamii, kwa mfano kupata malipo ya pensheni, haki za matibabu , haki za kujiunga na shule ikiwa ni pamoja na stahili zozote ambazo raia wa tanzania anastahili. Hii itasaidia kuondoa watumishi hewa kwenye “payroll “ ya serikali.
 • kuboresha utendaji kazi serikalini kwa kuwa na kumbukumbu sahihi za watumishi na malipo ya stahili zao; hasa pale wanapostaafu.
 • kupunguza gharama za mwananchi kutokana na huduma mbalimbali anazozipata kutolewa na taasisi moja.
 • kurahisisha zoezi la kuhesabu watu/sensa.
4. Maeneo yanayotakiwa kuboreshwa ili kufanikisha mfumo wa vitambulisho vya taifa

Gharama za kutengeneza vitambulisho hujumuisha gharama mbalimbali ikiwa ni pamoja na miundombinu yake, rasilimali watu, mafunzo na kuboresha maeneo muhimu yatakayokuwa yakishirikishwa katika utekelezaji wake mfano ni yafuatayo:-

 • rita (wakala wa usajili, ufilisi na udhamini) – kuboresha mfumo wa usajili wa vizazi na vifo.
 • tra (mamlaka ya kodi) – uboreshaji wa mfumo wa utoaji wa leseni za uendeshaji wa magari.
 • tawala za mikoa na serikali za mitaa (tamisemi), wizara hii ndiyo msimamizi wa serikali za mitaa na ndio wenye taarifa zote za watu mijini na vijijini.
 • polisi, kuboresha mfumo wa taarifa za udhibiti wa uhalifu.
 • mifumo ya mishahara na ki-utumishi kwa kurahisisha namna ya kuwatambua watumishi.
 • kuanzisha mtandao wa mawasiliano “networking and connectivity”.
 • kujenga vituo vya usajili vya wilaya (registration centres) na kujenga (data centre) makao makuu.
 • kutoa elimu kwa umma (public awareness) ili kuwawezesha kujua umuhimu wa dhana nzima ya vitambulisho vya taifa.
 • kuanza zoezi la usajili wa watu kwa lengo la kupata taarifa muhimu za watu.
 • taasisi za mifumo ya jamii kama nssf, ppf, gepf n.k zitaweza kupata taarifa za watu baada ya kuboresha mifumo yao. Kwa hiyo tunapozungumzia gharama za kuendesha shughuli za vitambulisho vya taifa hutumaanishi kadi tu bali ni jumla ya gharama zote za uendeshaji katika kutekeleza zoezi zima la mfumo wa vitambulisho vya taifa.
5. Hatua za utekelezaji

Utekelezaji wa mradi umepangwa kuwa katika awamu mbili ambapo awamu kwanza ni maandalizi ya mradi na awamu ya pili ni awamu ya utekelezaji wa mradi wenyewe. Ifuatayo ni taarifa ya utekelezaji wa awamu ya kwanza ya maandalizi ya mradi:-

 • jengo la ofisi limenunuliwa na kufanyiwa ukarabati pamoja na kuwekewa samani za ofisi
 • hati ya kuanzisha mamlaka (establishment instrument) tayari imesaniwa na mhe. Rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania na kuchapishwa katika gazeti la serikali gn. 122 ya tarehe 01/08/2008. Mamlaka hiyo inajulikana kama “national identification authority” (nida) au mamlaka ya vitambulisho vya taifa
 • zabuni kwa utaratibu wa pre- qualification ilitangazwa na makampuni 104 yalijitokeza kununua vitabu vya zabuni.
 • makampuni 54 yalirudisha zabuni zao
 • kamati ya uchambuzi ilitumia mwezi mmoja kufanya tathimini na kupendekeza makampuni manane (8) yaingie katika hatua inayofuata.
 • bodi ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi ilikutana na kuridhia mapendekezo ya kamati ya uchambuzi.
National Identity Cards Information
 

mageuzi1992

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2010
Messages
2,509
Points
0

mageuzi1992

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2010
2,509 0
Hii ni habari nzito iliyokuwa inasubiriwa...

Kwa kuwa tumekuwa na matatizo sana kwenye mikataba, sijui na mradi huu utasalimika!

Ni kampuni ile ile walioshinda tenda zamani wakanyimwa ikawa kesi? Au ni zabuni mpya?


Vitambulisho vya taifa Tanzania kugharimu Sh192bilioni

Na Simon Berege, Dodoma, MWANANCHI

SERIKALI imetangaza rasmi kuanza kutekelezwa kwa mradi wa taifa wa kutengeneza vitambulisho vya raia wa Tanzania walimo ndani na nje ya nchi pamoja na wakazi wasio raia waishio nchini utakaogharimu jumla ya Dola za kimarekani 152 milioni sawa na Sh192bilioni.

Waziri wa Mambo ya ndani, Joseph Mungai alisema mjini hapa jana kwamba mradi huo unaoanza mara moja ulipitishwa na kikao cha Bazara za Mawaziri kilichoketi Februari 2 mwaka huu mjini hapa chini ya Rais Jakaya Kikwete. Mchakato wa maandalizi yake ulianza mwaka 1995 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2009.

Akizungumza na Wanahabari kwenye ofisi za Bunge, Mungai alieleza kwamba vitambulisho hivyo vipya vitatumia teknolojia ya Smart Card ambayo ina uwezo wa kuingiza taarifa nyingi za muhusika zinazoweza kutumika kurahisisha huduma mbalimbali kwa mwenye kitambulisho.

“Teknolojia ya Samart Card ni ya kisasa zaidi kwani inaweza kubeba picha ya mwenye kitambulisho, alama za dole gumba, alama za kiganja, taarifa za DNA (chembechembe za urithi) , vipimo vya ndani ya macho, taarifa za elimu na nyingine,” alieleza Waziri Mungai na kuongeza kwamba teknolojia hiyo imeonekana kufanikiwa sana katika nchi ya Malaysia ambako walikwenda kujifunza.

Akifafanua zaidi Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Lawrence Masha, alisema kwamba uzuri wa teknolojia hiyo mtu anaweza kuamua ni taarifa zipi zisomwe na nani kama zile zinazohusu DNA, Afya, Uhalifu, Elimu, Benki na nyinginezo.

“Kwa mfano alisema si lazima mtu wa benki ajue kwamba una-typhoid, au ukienda polisi si lazima wajue mambo yako mengine” alieleza Masha na kuongeza kwamba teknolojia hiyo pamoja na kuwa nzuri kuliko ile ya Barcode ambayo ilitumika katika kutengeneza vitambulisho vya kupigia kura ni ya gharama nafuu.

“Kama tungekuwa tumetumia smart card kuandikisha kadi za kura ingekuwa rahisi sana kutekeleza mpango huu kwa sasa...kwa kutumia Smart card unaweza kuongeza taarifa wakati wowote tofauti na barcode” alifafanua Waziri Mungai na kubainisha kwamba Benki ya dunia imeshakubali kusaidia Dola 20 milioni kufanikisha mpango huo.

Mungai alieleza kwamba katika mradi huo raia waishio nchini na wale wanaoishi nje ya nchi watapewa vitambulisho na wasio raiai ambao wanafanya shughuli mbalimbali hapa nchini watapewa vitambulisho vitakavyowatambulisha wao na utaifa wao.

Alisema mradi huo utakuwa wa kitaifa kama ulivyo wa uchaguzi mkuu na wa sensa ambao utapewa vyenzo za kuukamilisha kwa kuzingatia ratiba maalum ya utekelezaji inayoanza mwezi huu na kukamilika mwaka 2009.

Katika kuhakikisha kwamba utekelezaji wake unakwenda vyema Waziri huyo alisema kwamba utaundwa Wakala wa Usimamizi wa Vitambulisho (National ID Management Agency) unaojitegemea kwa ajili ya kuendesha mradi huo chini ya Wizara ya Mambo ya ndani kwa kushirikiana na wadau wengine.

Alisema Mradi huo utaongozwa na Kamati ya Usimamizi ya Makatibu Wakuu na Wakuu wa Idara na vitengo vinavyohusiana na mambo muhimu kwa vitambulisho vya taifa ambayo pamoja na mambo mengine itatoa mwongozo na mwelekeo wa programu za mradi.

Kazi nyingine ya kamati hiyo itahusu ufuatiliaji wa mchakato wa mabadiliko ya menejimenti, kuidhinisha bajeti ya mipango ya utekelezaji, kuhakikisha kwamba fedha zilizotengwa kwa ajili ya programu husika na kufanya mapitio ya utekelezaji wa mipango kamambe wa shughuli mradi.

Waziri Mungai alieleza kwamba kutokana na makisio yaliyomo kwenye bajeti ya mwaka 2006/07 jengo maalum limetengwa kwa ajili ya mradi huo na watendaji wakuu wa Wakala wa usimamizi wa vitambulisho watateuliwa bila kuchelewa.

“Wizara ya mambo ya ndani inachukua fursa hii kutoa wito kwa wananchi waliopo ndani na nje ya nchi na wageni waliopo nchini kutoa ushirikiano ili kufanikisha utekelezaji wa mradi huu muhimu kwa taifa” alitoa rai Mungai na kubainisha kwamba vitambulisho hivyo vitatolewa bure.

Mradi huo utatekelezwa katika hatua mbili ambazo ni ya maandalizi na nyingine ni ya utekelezaji. Ratiba ya awamu ya kwanza inaonesha kwamba shughuli ya uanzishaji Wakala wa Usimamizi wa Vitambulisho na uteuzi wa watendaji wakuu na uimarishaji wa kiutendaji wa kuazimwa watumishi wengine kutoka idara za serikali vinapaswa kukamilika katika kipindi cha Februari na Aprili mwaka huu.

Kwa upande wa ukamilishaji wa makusanyo ya fedha zinazohitajika kutoka bajeti ya Serikali, wahisani na vyanzo binafsi utatekelezwa kati ya Marchi na Mei mwaka huu wakati Kampeni ya kufahamisha umma kupitia vyombo vya habari, mikutano ya hadhara, semina na mikutano ya ndani itafanyika kuanzia Aprili mwaka huu hadi Juni 2008.

Ratiba hiyo inaonesha kwamba mapitio (review) ya sheria husika na kufanya marekebisho inapobidi yatafanyika katika kipindi cha Februari hadi Mei 2007 wakati jukumu la kujenga uwezo katika ngazi mbalimbali litafanywa na ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma kati ya Julai na Desemba 2007.

Hatu ya pili ambayo ni ya utekelezaji wa mradi itahusisha utambuzi na uandikishwaji itafanyika kati ya Julai na Desemba mwaka huu ikihusisha ukusanyaji wa taarifa mbalimbali, uundaji wa kamati za utambuzi, Uchapishaji wa kadi za vitambulisho, usambazaji na utoaji wa kadi za vitambulisho na uanzishaji wa rejista za utambuzi.
Nasikitika kuwa majority ya watu wamevote kuwa mpango wa vitambulisho ni mbaya!!!! Nahisi watu wanashindwa kuelewa swali vinginevyo kama ni kweli wadau wengi wanafikiri kuwa mpango huu ni mbaya basi hawaelewi faida ya mpango huu au faida halisi ya kuwa na vitambulisho vya taaifa.!!
 

Makaimati

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2011
Messages
462
Points
0

Makaimati

JF-Expert Member
Joined Apr 4, 2011
462 0
Nasikitika kuwa majority ya watu wamevote kuwa mpango wa vitambulisho ni mbaya!!!! Nahisi watu wanashindwa kuelewa swali vinginevyo kama ni kweli wadau wengi wanafikiri kuwa mpango huu ni mbaya basi hawaelewi faida ya mpango huu au faida halisi ya kuwa na vitambulisho vya taaifa.!!
Sioni kuwa mpango wenyewe ni mbaya ila matumizi yake ndio mabaya.

Mfano mzuri ni wa Zanzibar ambako tunazo hizi ZAN ID lakini wamepewa mpaka watu wa Msumbiji ili waipigie kura CCM

Najaribu kuwatafutia picha niwapatie ushahidi
 

Steve Dii

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2007
Messages
6,417
Points
1,225

Steve Dii

JF-Expert Member
Joined Jun 25, 2007
6,417 1,225
Sijui basis ya maamuzi yetu inatoka wapi, maana sijakutana na taarifa yeyote ya utafiti inayohalalisha umuhimu wa huu mradi wa vitambulisho vya taifa. Lakini nimeona dada Meghji ametumia sehemu ya kutosha katika bajeti yake kuelezea hili jambo. Kilichonichosha zaidi ni sababu za huu mradi zilizotolewa na dada Zakia. Yeye anasema sababu mojawapo ni kuimarisha demokrasia. Sasa nimekuwa najaribu kufikiria link kati ya viambulisho na demokrasia, kwa kweli sijaona. Sana sana nimeona katika nchi zingine sababu moja ya kukataa kuwa na IDs ilikuwa ni kwamba IDs zinaingilia uhuru wa watu (freedom/liberty). Sasa sisi hii kwamba IDs vinasaidia kuleta demokrasia tumeitoa wapi?

Kwa maoni yangu, hii project haina maana, ni ghali pasipo na sababu za msingi na yafaa kabisa ipigwe chini!

Nyie mnasemaje?
Ni project ya muhimu lakini ilitakiwa isubiri mipango mingine ya kimaendeleo yenye umuhimu wa haraka imalizike kwanza. Na siyo tu imalizike kwanza, bali imalizike kwa ubora na viwango vya juu, maana hela ambazo zingeelekezwa kwenye vitambulizo zingeliweza kuelekezwa kwenye ubora wa mipango ambayo tunahitaji sasa hivi. Zoezi kama hili la vitambulisho lingeweza kuletwa hata mwaka 2030, ambapo lingekuwa rahisi zaidi kufanyika, kuanzia gharama na hata teknolojia inakuwa imebadilika na kuoana na mazingira yetu ya kimaendeleo ya wakati huo.
 

Tiger

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2007
Messages
1,751
Points
1,225

Tiger

JF-Expert Member
Joined Nov 30, 2007
1,751 1,225
Kwa wanaofahamu, wilaya ya Temeke ndiyo ilikuwa ya kwanza kuanza kuandikisha vitambulisho vya uraia.
Swali:
Inakuwaje kama mtu alijiandikisha na wakati anapewa taarifa ya kwenda kuchukua kitambulisho, anakuwa mbali na eneo lake kwa muda uliopangwa kwenda kukichukua?
Msaada tafadhali.
Vipi kuhusu usalama wa kitambulisho kama hakikuchukuliwa kwa muda uliopangwa?
 

Forum statistics

Threads 1,380,739
Members 525,856
Posts 33,778,363
Top