Dr Count Capone
JF-Expert Member
- Feb 7, 2017
- 1,875
- 3,237
CountCapone
Kabla ya mwaka 1961 hakukuwahi kuwa na nchi inayoitwa Tanzania kwenye ramani
1-1885 Ardhi ya Tanzania haikua na dola moja inayotawala bali jamii nyingi zilizogawanyika
1885-1919 Deutsch-Ostafrika (Afrika Mashariki ya Ujerumani
1919-1960 British East Africa Protectorate (Eneo-lindwa la Uingereza)
1961-1964 Tanganyika (Tanzania ya leo bila Zanzibar)
1964-2022 Tanzania
Hayati Baba wa taifa, Mzee Karume, Bibi Titi Mohammed,Oscar Kambona na mashujaa wetu wengine walioshiriki kupigania uhuru wetu walitamani kuwaona watanzania ni wamoja na wanaoishi kwenye viwango vikubwa vya maisha.
Wakati wanabargain mipaka ya nchi walifanya kila namna kuhakikisha rasilimali nyingi zinawekwa Tanzania ili tuweze kujitosheleza.
Vivutio vya utalii kama Mlima Kilimanjaro, na visiwa vyenye mvuto wa kipekee duniani Zanzibar, vyanzo vya maji kama ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa Mito Ruvu, Pangani, Wami, Rufiji, Matandu, Lukuledi, Mbemkuru, na Ruvuma yote inayomwaga maji yake kwenye bahari ya Hindi ipo Tanzania.
Migodi ya dhahabu huko Geita, Almasi huko Shinyanga, Uranium na makaa ya mawe huko kusini, Tanzanite huko Arusha bado sijataja Chuma, Nickel n.k,
Ukanda wa bahari unaosambaa kwa zaidi ya 800 km, toka mpakani na Kenya upande wa Kaskazini mpaka mpakani na Msumbiji huko Kusini, Fukwe tulivu zenye michanga laini na Visiwa lukuki vyenye watu karimu.
Muhimu kuliko yote Tanzania ina amani sana tangu Uhuru mpaka sasa ukilinganisha na nchi nyingine.
Ili kuleta maendeleo na maisha mazuri kwa Watanzania Mwalimu alijaribu Ujamaa lakini ikashindikana, akabadili na kuurudia ubepari ambao bado haujatupa matokeo tunayoyataka mpaka leo.
Rushwa, kutokuwajibika, Kukosekana kwa nia thabiti kwetu Viongozi na wananchi, mfumo kandamizi wa dunia, kukosekana mitaji, Elimu mbovu, Fikra mbovu, Afya duni, Maendeleo hafifu ya kisayansi YOTE HAYA YANATUKWAMISHA SANA KUPIGA HATUA.
Ni lazima tukubali ukweli kuwa tangu uhuru hatua za kuendeleza nchi hii zimepigwa ila si kwa kiwango tunachostahili Watanzania, ujenzi wa barabara alichotuachia Mkoloni si sawa na kiwango cha sasa, usambazaji wa umeme enzi za uhuru si sawa na sasa ambapo inashuhudiwa chini ya vijiji 2300 pekee ndiyo havina umeme nchi nzima, madarasa, walimu, hospitali na wahudumu wa afya wameongezeka kwa kiwango kikubwa.
Lakini pia ni ukweli kuwa bado hatujafikia kiwango cha kusema tumeendelea, Ajira zimekuwa changamoto, Rushwa si mchezo, Uwajibikaji hakuna, Viwanda na pato la mtu mmoja mmoja bado viko chini sana.
Kwa zaidi ya miaka 60 sisi kama Watanzania tumeshindwa kabisa kuja na mpango mkakati wa kutatua matatizo ya msingi ya watu wetu, tumeshindwa kupambana na rushwa, tumeshindwa kuwawajibisha wanaotuibia, tumeshindwa kutumia rasilimali zetu kwa faida yetu kikamilifu, tumeshindwa kuwapa watu wetu Demokrasia na kubwa la yote tumeshindwa kupunguza umasikini wa watu wetu.
TUPIGE KURA KUJIUNGA NA MAREKANI
Tumejaribu sana kujiendeleza sasa suluhu yetu ni hii hapa, Imefika wakati sasa Watanzania tupige kura (Referendum) kuamua kujiunga Marekani.
Faida za kujiunga na Marekani
Kwa kujiunga na Marekani mfumo mzima wa kisiasa utabadilika kuendana na Demokrasia, jambo hili litawahakikishia wananchi uhuru ambao wanao kama binaadamu.
Uwajibikaji wa viongozi- chini ya serikali mpya Tanzania kama jimbo tutaweza wawajibisha viongozi wetu kikamilifu kama nchi ya kidemokrasia.
4) Elimu bora
Mbali na kuwa na Mabadiliko ya mfumo wa elimu watu wetu watakuwa na fursa sawa na WaMarekani kusoma katika vyuo bora zaidi duniani kama Harvard na Massachusetts Insitute of Technology, jambo ambalo ni la faida kubwa sana kwa watu wetu.
5) Ajira na viwanda
Teknolojia ya Marekani itawekezwa kwenye ardhi yetu katika kujenga viwanda na kufungua biashara wakati huohuo watu wetu watapata fursa za kazi na mwishowe wataongeza mapato yao.
Hayo ni machache kuna mengi kama Kilimo, Ufugaji, Uvuvi, Madini, Miundombinu ya usafiri na sekta zote zinazohitaji teknolojia zitanufaika moja kwa moja na uwekezaji toka kwa waMarekani wenzetu.
Faida kwa Marekani
Marekani haitatukubali kwa kutuonea huruma ila itatukubali kwa sababu tuna rasilimali nyingi sana hapa kwetu, kwa msaada wao tutazitumia vizuri kutufaidisha sisi kama jimbo na serikali yetu kuu ya Marekani kwa ujumla.
Kwa kuwa Uchina imewekeza sana Afrika, Tanzania kujiunga na Marekani itaipa Marekani eneo la kimkakati katika kuikabili Uchina.
Pia Marekani itapata fursa kuweka kambi zake za kijeshi hapa ukiacha ile kuweka Kenya na nchi nyingine kwa masharti itaweza weka kambi Tanzania bila masharti na kambi hizo kuwa kama ziko nyumbani Washington.
Watanzania wenzangu na hili nalo tukalitizame.

- Uhuru wetu
- Demokrasia yetu itakua
Kwa kujiunga na Marekani mfumo mzima wa kisiasa utabadilika kuendana na Demokrasia, jambo hili litawahakikishia wananchi uhuru ambao wanao kama binaadamu.
Uwajibikaji wa viongozi- chini ya serikali mpya Tanzania kama jimbo tutaweza wawajibisha viongozi wetu kikamilifu kama nchi ya kidemokrasia.
- Ulinzi na Usalama
- Mgomo wa wanajeshi 1964
- Vita vya kagera 1978
4) Elimu bora
Mbali na kuwa na Mabadiliko ya mfumo wa elimu watu wetu watakuwa na fursa sawa na WaMarekani kusoma katika vyuo bora zaidi duniani kama Harvard na Massachusetts Insitute of Technology, jambo ambalo ni la faida kubwa sana kwa watu wetu.
5) Ajira na viwanda
Teknolojia ya Marekani itawekezwa kwenye ardhi yetu katika kujenga viwanda na kufungua biashara wakati huohuo watu wetu watapata fursa za kazi na mwishowe wataongeza mapato yao.
Hayo ni machache kuna mengi kama Kilimo, Ufugaji, Uvuvi, Madini, Miundombinu ya usafiri na sekta zote zinazohitaji teknolojia zitanufaika moja kwa moja na uwekezaji toka kwa waMarekani wenzetu.
Faida kwa Marekani
Marekani haitatukubali kwa kutuonea huruma ila itatukubali kwa sababu tuna rasilimali nyingi sana hapa kwetu, kwa msaada wao tutazitumia vizuri kutufaidisha sisi kama jimbo na serikali yetu kuu ya Marekani kwa ujumla.
- Marekani itanufaika kwa kupata eneo la kimkakati (HII NI KUBWA),
Kwa kuwa Uchina imewekeza sana Afrika, Tanzania kujiunga na Marekani itaipa Marekani eneo la kimkakati katika kuikabili Uchina.
Pia Marekani itapata fursa kuweka kambi zake za kijeshi hapa ukiacha ile kuweka Kenya na nchi nyingine kwa masharti itaweza weka kambi Tanzania bila masharti na kambi hizo kuwa kama ziko nyumbani Washington.
- Maeneo mapya ya malighafi, uwekezaji na masoko kwa wafanyabiashara wa Marekani