Fursa ya kwenda kufundisha Kiswahili Marekani

Jimena

JF-Expert Member
Jun 10, 2015
25,857
95,808
Habari wana jamvi,

Serikali ya Marekani kwa mara nyingine tena imetoa fursa kwa watanzania kwenda kufundisha lugha ya kiswahili nchini Marekani kwa kipindi cha mwaka mmoja, ukipata nafasi hii basi utaenda kufundisha katika chuo kikuu,

Hii ni njia nzuri kwa wale wanaopenda kutoka nje ya Tanzania na kwenda kufanya kazi abroad. Sababu haihitaji connection wala msaada wa mtu.

Muombaji anatakiwa awe na umri usiozidi miaka 30 na awe na elimu ya kiwango cha degree (sio lazima iwe ya ualimu)
Mwisho wa kutuma maombi ni 03 May 2024

Link ya kuomba kujiunga na programu hii ni Foreign Language Teaching Assistant Program (FLTA)
 
Ndio waache ubaguzi wa umri sio kitu kizuri kwani Biden ana umri gani na ni Rais wa wapi? Sasa kwanini wanabagua umri mwisho miaka 30?
Ndio maisha mkuu maana kuna zingine huwa wanaweka above 30 au hata gender au dini fulani.

Hii haiwezi kwisha maana kila Job description lazma ibague watu flani ili kupata mtu sahihi
 
Ndio waache ubaguzi wa umri sio kitu kizuri kwani Biden ana umri gani na ni Rais wa wapi? Sasa kwanini wanabagua umri mwisho miaka 30?
Hii programu ya fulbright ni ya vijana mkuu😆😆😆
Hata huyo Biden hana vigezo vya kunufaika na programu hii
 
Ndio maisha mkuu maana kuna zingine huwa wanaweka above 30 au hata gender au dini fulani. Hii haiwezi kwisha maana kila Job description lazma ibague watu flani ili kupata mtu sahihi
Ila hii discrimination sio nzuri kidogo below 30 kweli?
 
Ila hii discrimination sio nzuri kidogo below 30 kweli?
Hii fursa imekuwepo toka miaka mingi iliyopita, labda hukuwa unaifahamu tu. Na ni fursa endelevu, share na watu wenye vigezo ili wachangamkie fursa.
 
Kufundisha kiswahili ni rahisi sana alafu mtihani unawapa swali kuwa
Fasihi ni kuku mnyonyoe
Mkuu hii wala hufiki huko😆😆😆
Unaenda tu kufundisha a,e,i,o,u, baba, mama yani kile kiswahili rahisi cha kuongea
 
Back
Top Bottom