Dr Count Capone

JF-Expert Member
Feb 7, 2017
1,875
3,236
CountCapone
C22038AA-1BC9-4894-A870-FD2980127284.jpeg


Kabla ya mwaka 1961 hakukuwahi kuwa na nchi inayoitwa Tanzania kwenye ramani
1-1885 Ardhi ya Tanzania haikua na dola moja inayotawala bali jamii nyingi zilizogawanyika

1885-1919 Deutsch-Ostafrika (Afrika Mashariki ya Ujerumani

1919-1960 British East Africa Protectorate (Eneo-lindwa la Uingereza)

1961-1964 Tanganyika (Tanzania ya leo bila Zanzibar)

1964-2022 Tanzania

Hayati Baba wa taifa, Mzee Karume, Bibi Titi Mohammed,Oscar Kambona na mashujaa wetu wengine walioshiriki kupigania uhuru wetu walitamani kuwaona watanzania ni wamoja na wanaoishi kwenye viwango vikubwa vya maisha.

Wakati wanabargain mipaka ya nchi walifanya kila namna kuhakikisha rasilimali nyingi zinawekwa Tanzania ili tuweze kujitosheleza.

Vivutio vya utalii kama Mlima Kilimanjaro, na visiwa vyenye mvuto wa kipekee duniani Zanzibar, vyanzo vya maji kama ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa Mito Ruvu, Pangani, Wami, Rufiji, Matandu, Lukuledi, Mbemkuru, na Ruvuma yote inayomwaga maji yake kwenye bahari ya Hindi ipo Tanzania.

Migodi ya dhahabu huko Geita, Almasi huko Shinyanga, Uranium na makaa ya mawe huko kusini, Tanzanite huko Arusha bado sijataja Chuma, Nickel n.k,

Ukanda wa bahari unaosambaa kwa zaidi ya 800 km, toka mpakani na Kenya upande wa Kaskazini mpaka mpakani na Msumbiji huko Kusini, Fukwe tulivu zenye michanga laini na Visiwa lukuki vyenye watu karimu.

Muhimu kuliko yote Tanzania ina amani sana tangu Uhuru mpaka sasa ukilinganisha na nchi nyingine.

Ili kuleta maendeleo na maisha mazuri kwa Watanzania Mwalimu alijaribu Ujamaa lakini ikashindikana, akabadili na kuurudia ubepari ambao bado haujatupa matokeo tunayoyataka mpaka leo.

Rushwa, kutokuwajibika, Kukosekana kwa nia thabiti kwetu Viongozi na wananchi, mfumo kandamizi wa dunia, kukosekana mitaji, Elimu mbovu, Fikra mbovu, Afya duni, Maendeleo hafifu ya kisayansi YOTE HAYA YANATUKWAMISHA SANA KUPIGA HATUA.
F954580D-A2C0-46F2-B772-2F0CDFEBA31A.jpeg

Ni lazima tukubali ukweli kuwa tangu uhuru hatua za kuendeleza nchi hii zimepigwa ila si kwa kiwango tunachostahili Watanzania, ujenzi wa barabara alichotuachia Mkoloni si sawa na kiwango cha sasa, usambazaji wa umeme enzi za uhuru si sawa na sasa ambapo inashuhudiwa chini ya vijiji 2300 pekee ndiyo havina umeme nchi nzima, madarasa, walimu, hospitali na wahudumu wa afya wameongezeka kwa kiwango kikubwa.

Lakini pia ni ukweli kuwa bado hatujafikia kiwango cha kusema tumeendelea, Ajira zimekuwa changamoto, Rushwa si mchezo, Uwajibikaji hakuna, Viwanda na pato la mtu mmoja mmoja bado viko chini sana.
2BE2D154-BD32-465E-A2D6-57DCCBCAC223.jpeg


Kwa zaidi ya miaka 60 sisi kama Watanzania tumeshindwa kabisa kuja na mpango mkakati wa kutatua matatizo ya msingi ya watu wetu, tumeshindwa kupambana na rushwa, tumeshindwa kuwawajibisha wanaotuibia, tumeshindwa kutumia rasilimali zetu kwa faida yetu kikamilifu, tumeshindwa kuwapa watu wetu Demokrasia na kubwa la yote tumeshindwa kupunguza umasikini wa watu wetu.

TUPIGE KURA KUJIUNGA NA MAREKANI
E736DD84-E350-4C94-9E19-3A55B02C5A96.jpeg


Tumejaribu sana kujiendeleza sasa suluhu yetu ni hii hapa, Imefika wakati sasa Watanzania tupige kura (Referendum) kuamua kujiunga Marekani.

Faida za kujiunga na Marekani

  1. Uhuru wetu
Mchakato huu mzima utakuwa na swali juu ya Uhuru wetu kama nchi, hili lisiwatie mashaka Watanzania Kwa maana mambo yote yatakayohusu sera za kimataifa na ulinzi yatashughulikiwa na serikali kuu na mambo mengine madogo madogo tutayashughulikia wenyewe Tanzania kama jimbo.

  1. Demokrasia yetu itakua
Hiki kimekuwa kilio cha muda mrefu cha wanaharakati wetu, lawama kwenye chaguzi, mienendo ya jeshi la polisi, mijadala ya kisiasa na ufuataji wa sheria vyote vimekuwa havifanyiki kikamilifu.
Kwa kujiunga na Marekani mfumo mzima wa kisiasa utabadilika kuendana na Demokrasia, jambo hili litawahakikishia wananchi uhuru ambao wanao kama binaadamu.
Uwajibikaji wa viongozi- chini ya serikali mpya Tanzania kama jimbo tutaweza wawajibisha viongozi wetu kikamilifu kama nchi ya kidemokrasia.

  1. Ulinzi na Usalama
Tanzania tangu Uhuru tumepata vitisho vikuu viwili tu
  1. Mgomo wa wanajeshi 1964
  2. Vita vya kagera 1978
Lakini dunia imebadilika na vitisho vipya vimeongezeka, vikundi vya kigaidi vimetapakaa kila kona kuanzia kwenye mpaka wetu wa kusini na Msumbiji, majirani zetu Kenya, Vurugu na sintofahamu Congo DRC na Sudan Kusini. Hivyo basi kwa kujiunga na Marekani tutanufaika na uzoefu wao wa kupambana na magaidi na vitisho vya amani pia na jeshi lao imara na Intelijensia yao ya hali ya juu katika kuilinda amani yetu.

4) Elimu bora
B483542E-7CB0-4F21-B28D-4BA7D0C82C24.jpeg


Mbali na kuwa na Mabadiliko ya mfumo wa elimu watu wetu watakuwa na fursa sawa na WaMarekani kusoma katika vyuo bora zaidi duniani kama Harvard na Massachusetts Insitute of Technology, jambo ambalo ni la faida kubwa sana kwa watu wetu.

5) Ajira na viwanda
Teknolojia ya Marekani itawekezwa kwenye ardhi yetu katika kujenga viwanda na kufungua biashara wakati huohuo watu wetu watapata fursa za kazi na mwishowe wataongeza mapato yao.

Hayo ni machache kuna mengi kama Kilimo, Ufugaji, Uvuvi, Madini, Miundombinu ya usafiri na sekta zote zinazohitaji teknolojia zitanufaika moja kwa moja na uwekezaji toka kwa waMarekani wenzetu.

Faida kwa Marekani

A43CCD85-7300-4B66-841E-3AD642E5B989.jpeg


Marekani haitatukubali kwa kutuonea huruma ila itatukubali kwa sababu tuna rasilimali nyingi sana hapa kwetu, kwa msaada wao tutazitumia vizuri kutufaidisha sisi kama jimbo na serikali yetu kuu ya Marekani kwa ujumla.

  1. Marekani itanufaika kwa kupata eneo la kimkakati (HII NI KUBWA),
Urusi ni fallen power, Uchina ni Superpower on the rise na ni wazi sasa dunia inaelekea mashariki na hasimu mkubwa wa Marekani ni Uchina.

Kwa kuwa Uchina imewekeza sana Afrika, Tanzania kujiunga na Marekani itaipa Marekani eneo la kimkakati katika kuikabili Uchina.

Pia Marekani itapata fursa kuweka kambi zake za kijeshi hapa ukiacha ile kuweka Kenya na nchi nyingine kwa masharti itaweza weka kambi Tanzania bila masharti na kambi hizo kuwa kama ziko nyumbani Washington.

  1. Maeneo mapya ya malighafi, uwekezaji na masoko kwa wafanyabiashara wa Marekani
Nchi yetu hii kubwa kwa ardhi, yenye rasilimali za kila aina na idadi kubwa ya watu. Hii ni fursa kubwa sana kwa watu wanaopenda biashara kama wamarekani.

Watanzania wenzangu na hili nalo tukalitizame.
CB979B7A-12C4-40DB-ACD1-415E5099ABB8.jpeg
 
Ningekuwa na muda ningeandika paragraph ndefu sio kupinga bali kuonyesha uhalisia ambao wenyewe ni kipingamizi tosha.

Mkuu hivi unajua/umeona jinsi gani Black Americans wanavyoishi kwa tabu Marekani?
Ndio wana uhakika wa kula na kulala vizuri, miondombinu mizuri na wapo kwenye taifa lenye nguvu duniani, kwa wale wenye status kubwa basi usalama wa uhakika vilevile.
Lakini wanakosa kitu kimoja ambacho ndio kinadefine binadamu na kuleta amani ya ndani ambayo ndio ya msingi kuliko usalama na amani ya nje. Thamani ya Utu.
Ndio, Utu. Binadamu asiyethaminiwa utu wake waziwazi ni anaishi kwa tabu zaidi ya mnyama zaidi ya hapo kuna Ukandamizaji kifursa, Ubaguzi wa rangi, Police-brutality, Genocide n'k...
Kama hayo yote yanafanyika kwa waliozaliwa hukohuko unadhani itakuaje kwa mtu aliyetoka nje kabisa?

Na sio hapo tu, bali umeona ni jinsi gani Caucasians wanavyodispise na kudharau Waafrika? Hapo haujafika kwao sasa unadhani itakuaje ukienda kwao?
Kama hata hao weusi waliozaliwa huko wanawafanyia yote hayo. Je unadhani watakubali kuona Taifa lao linaungana na nchi wanayoiita third world country? Tena iliyojaa watu weusi?
Hiyo haitoshi, hata hao Black Americans wenyewe wanawadharau waafrika vilevile, Kama kwa idadi yao ndogo na wanakosa vingi, je unafikiri watakubali kuona wengine kama wao tena million 60 waongezeke kwenye nchi yao?
Bado haitoshi, watafuja rasilimali zetu zote ambazo hata wenyewe million 60 hazitutoshi na kwenda kujinufaisha wao million 300, rasilimali ambazo sasa hivi wanangaika kila namna kuzipata kwa malipo ya kijiko. (Ukisikia mbuzi kafia kwa muuza bucha ndio hii)
Na hiyo bado haitoshi, hapohapo watataka kupitisha propaganda za ajabuajabu ili kucontrol population sababu rasilimali hazitoshi. Kubomoa maadili mubashara na kuharibu vizazi vyote vijavyo kwa sababu zao nyingine zisizojulikana.

Caucasians wanasema "Waafrica ni wavivu wanaopenda vya vikubwa na vya bure bila kufanya kazi, wanashindwa kuendeleza mataifa yao wanaenda kwao kutumia vyao walivyotafuta kwa kuhangaika na jasho.
Hivyo Waafrica wabaki barani kwao kila mtu abaki nchini kwake." Mimi nasema wako sahihi na hawajakosea.
Mkuu hicho ulichoandika hakiwezekani na ni ndoto.
Na kuliko kupitia yote hayo na kuishi kama mnyama na kuwa muoga kama kunguru kwa kutukanwa, kudharauliwa kubaguliwa na wamagharibi ni vizuri kubaki nyumbani kwenye amani ya kweli na kuhangaika na kuboresha nyumbani sababu nyumbani ni nyumbani tu.
Ni vizuri Tanzania iwe moja ihangaike na isimame yenyewe kama yenyewe kwa jasho lake lenyewe kama mataifa mengi makubwa duniani. Wananchi wa Tanzania waache Ujinga, Uvivu, Ukabila na Udini na wasimame kuwa kitu kimoja na kuendeleza taifa kama taifa moja. Ikiwemo kuchagua viongozi bora na kuweka mifumo imara, sababu hapa ndip kikwazo na tatizo kuu lilipo.
Na siku zote kumbuka mtafuta kwa jasho na kula jasho lake mwenyewe hueshimiwa.

Mkuu hakuna mtu mweupe anayempenda mtu mweusi. Hizo International Relations na Public Relations zisikuongepee na kukuchanyanganya mpaka kufikia kuficha na kushindwa kuona uhalisia. Moyo wa binadamu ni kichaka lakini moyo wa mzungu ni msitu.
 
Naunga mkono hoja Kwa sababu hata Korea Kusini na Nchi zote za Western baada kufilisika vita ya pili ya Dunia zilinyenyuliwa na America..

Pia Egypt na Saudia au Israel nk zinapata mamilioni ya dola kutoka kwa America..

JK angeendelea kuwa Rais hata ule mradi wa Kigamboni ungeshakuwa realised na Tzn tungekuwa hatukamatiki hapa EAC.
 
Naunga mkono hoja Kwa sababu hata Korea Kusini na Nchi zote za Western baada kufilisika vita ya pili ya Dunia zilinyenyuliwa na America..

Pia Egypt na Saudia au Israel nk zinapata mamilioni ya dola kutoka kwa America..

JK angeendelea kuwa Rais hata ule mradi wa Kigamboni ungeshakuwa realised na Tzn tungekuwa hatukamatiki hapa EAC.
Nashukuru mkuu ni laZima tuendelee
 
kwamba hatujiwezi na tunachotegemea sana ni sisi kufaidika na ulinzi wao na akilizao za kutumia utajiri wetu ... napinga Most of countries in Africa wanajalibu kusimama nchi kama nchi bila kutemegemea msaada maaana misaada yao ina malimbikizo ya itikad za kijinga na masharti makali sana
Mfano kama Libya angalia nchi ilikua inajitegemea na wanchi walikua na Aman na walikua wanaishi kama ulaya juu ya utawala wa Mohamed Gaddaf wakaletewa mashushu na figisu za ao ao unasema tuungane nao na kuvuruga aman na kuicha Libya as Africa Country iwe omba omba na wakimbizi wao hivo ndo wanapenda yan waendeleee kuchukua wanavo taka

White pipo never Love us and can do anything ili wao wa survive na kizazi chao na ao ndo shetani wetu wa kwanza
 
Back
Top Bottom