Hili swali la tariff hawajibu sijui kwa nn?nimeshauliza mpaka page yao ya Facebook hawajibu
Swala hili tumelitolea ufafanuzi mara kadhaa ni kwamba hakuna mteja wa nyumbani anaweza kuwekwa kundi la viwanda na hakuna kilichobadilika kwenye makundi ya watumiaji
 
Swala hili tumelitolea ufafanuzi mara kadhaa ni kwamba hakuna mteja wa nyumbani anaweza kuwekwa kundi la viwanda na hakuna kilichobadilika kwenye makundi ya watumiaji
Ujue unapojibu kumbuka kuwa unajibu watu wazima?mm nipo tariff 1 kuna jirani yangu nae alikuwa tariff hyo sasa yeye kahamishwa miezi mitatu iliyopita kawekwa tariff 4,mm nimeenda Tanesco ili nihamishwe na ona mizengwe mingi wakati nakizi vigezo,alafu wewe unasema umeme wa majumbani wote tariff zinafanana ,kivp?alafu huwa unajibu hivi but nikiendelea kukupa ufafanuzi unakimbia hii mara 10 sasa,
 
Niliuliza humu kama eneo nipo pekeyangu ninaehitaji umeme nitafungiwa kwa wakati au mpaka wateja waongezeke kadhaa.Nimelipia tar 11/9/2018
 
Niliuliza humu kama eneo nipo pekeyangu ninaehitaji umeme nitafungiwa kwa wakati au mpaka wateja waongezeke kadhaa.Nimelipia tar 11/9/2018
Bado upo ndani ya muda kama ambavyotulivyokujibu hapo awali
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)*

TAARIFA KWA UMMA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawaomba radhi Wateja wake wote wa Mikoa iliyounganishwa katika gridi ya Taifa kwa kukosa huduma ya umeme leo Alhamisi, Septemba 27, 2018, majira ya Saa 7:42 Mchana.

Sababu: Hitilafu katika Transfoma ya 220/33 kV ya kituo cha Kupoza na Kusambaza umeme cha Kidatu (Kidatu switch yard).

Wataalamu wetu na mafundi wanaendelea na jitihada za kurejesha umeme katika hali yake ya kawaida.

Tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza.

Kwa mawasiliano

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Tovuti: www.tanesco.co.tz,

Mitandao ya kijamii

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetultd/

*IMETOLEWA NA:*
OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU
 
Kwanini mnabadilishia watu tarrif kutoka tarrif ndogo kwenda kubwa wakati matumizi ni ya kawaida sana na kudai kuwa ni ukaguzi wakati mnatuibia ina maana hizo mitters si zimefungwa system ambayo mnaweza kujua matumizi ya kawaida ya kila mteja? Huku ni kuibia wananchi toka august mnakagua nini? Na hizi mitter ni digital sio kama zile manual za catout
 
Weka maelezo ukionyesha namba yako ya mita kwa kuwa hii inahusiana na matumizi yako wewe binafsi.wateja wote wanakaa.kwenye makundi yanayoendana na matumizi yao
 
*SHIRIKA LA UMEME TANZANIA TANZANIA TANZANIA (TANESCO)*

*SEPTEMBA 28, 2018*

*MABORESHO YA MIUNDOMBINU YA UMEME DAR ES SALAAM, NJOMBE, MBEYA, RUVUMA NA ZANZIBAR*

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake wa Dar es Salaam, Njombe, Mbeya, Ruvuma na Zanzibar, Siku ya Jumapili Septemba 30, 2018 kuanzia Saa 3:00 Asubuhi hadi Saa 11:00 Jioni kutakuwa na maboresho katika kituo cha Kupoza na Kusambaza Umeme cha Kunduchi (Kunduchi Sub- station) na njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovolti 220 Iringa-Mufindi.

Lengo ni kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme katika maeneo hayo.

Kutokana na kazi hiyo baadhi ya maeneo katika mikoa tajwa yatakosa huduma ya umeme.

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.

Kwa mawasiliano

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Tovuti: www.tanesco.co.tz,

Mitandao ya kijamii

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetultd/

*IMETOLEWA NA:*
OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU
 
Naomba kufahamu waya za umeme kutoka nguzo moja kwenda nyingine au kuingia kwa mteja zinatakiwa kuwa umbali (minimum height) gani toka ardhini?
 
Weka maelezo ukionyesha namba yako ya mita kwa kuwa hii inahusiana na matumizi yako wewe binafsi.wateja wote wanakaa.kwenye makundi yanayoendana na matumizi yao
miter number yangu ni 24210087060,natumia nane kwa mwezi zikizidi ni units kumi,niko moshi
Mitter no yangu ni 24210087060,
 
hiki kizungu mkuti cha makundi ya tarif kila mteja anajibiwa kivyake vyake na mtu huyo huyo mmoja
Vigezo na masharti ni mteja anaetumia umeme chini ya unit 75 kwa mwezi

Ndani ya miezi 6 asivuke hiko kiwango
Yaani matumizi yake ni unit 60,59 na kushuka chini huyu anatakiwa awe kundi la matumizi madogo tarif 4

Tarif 1 ni yule anaevuka matumizi kutoka 75 kwenda 76 na kuendelea

Sisi wateja ndio tunafahamu hivyo
Kama utaratibu umebadilika si mseme tu

hizi ngonjera za serikalini zipo mbaka kule wizara ya afya
Watoto chini ya miaka mitano matibabu bure ukienda hospital dawa unakwenda kununua pharmacy hiyo bure yenu ni nini hapo?.
 
Tunaomba namba yako ya mita na ya simu tupitie manunuzi yako.Swala la tariff ni la mtumiaji wa umeme wa mita husika hivyo tunataraji mtu akilet ombi au lalamiko liwe la mita yake
 
mimi nataka kuhama na mita yangu ya luku..naiomba kufahamu je nitalipia kiasi gani ili tanesco waweze kuja kuiondoa hii mita ya hapa nyumbani na kwenda kufunga kule ninapo hamia...na huku ninapoondoka wafunge nyingine
 
Ndugu mpendwa mteja
Mita ikishafungwa haihamishwi kwenda nje ya eneo husika tunachokushauri ni kuomba umeme upya kwa eneo husika na inapobaki uje ujaze fomu iwe jina na anayebaki
 
Niliomba kuunganishiwa umeme nimeambiwa gharama ya kufungiwa umeme iko teyali na nimeorodheshewa na bei nahitajika nikalipe je nikilipa inachukua mda gani Kuja kufungiwa umeme?
 
Niliomba kuunganishiwa umeme nimeambiwa gharama ya kufungiwa umeme iko teyali na nimeorodheshewa na bei nahitajika nikalipe je nikilipa inachukua mda gani Kuja kufungiwa umeme?
Inategemea na umbali uliopo kutoka kwenye miundombinu ya umeme na waliokutangulia
 
Back
Top Bottom