Hawa Tanesco mimi huwa nashindwa kuwaelewa kabisa!

Unaenda kuomba kuunganishwa umeme, wanakuangalia tu.

Wanakupa fomu unajaza, wanakuangalia tu.

Wanakupa fundi wao akafanye tathmini, wanakuangalia tu.

Fundi wao anatoa makadirio ya gharama, wanakuangalia tu.

Wanakupa gharama unazotakiwa kulipia, wanakuangalia tu.

Unaenda kulipia, wanakuangalia tu.
Ukishalipa tu, wanakuambia nguzo hakuna, subiri miezi mitatu!
 
wanasubiri kenge azame shimoni ndio wamwagie maji ya moto!!!
 
TAARIFA KWA UMMA

Jana nimeleta uzi hapa kutoa taarifa muhimu lakini moderators wa Jamii Forum kwa utashi wao wakipumbavu wakaona waufute.

Sasa leo naleta taarifa rasmi kutoka Tanesco kuhusiana na nilicholeta jana na naomba ndugu zangu muwaambie hawa mods wa JF waurudishe uzi ule nilioleta jana haraka sana na ikiwezekana kuunganisha na huu. Asanteni

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake wote wanao tumia mita za malipo ya kabla yaani (LUKU) kuwa, kuanzia April 2, 2018 TANESCO itahamia rasmi katika mfumo wa malipo wa Serikali ujulikanao kama Government e-Payment Gateway (GePG) kama matakwa ya sheria kwa Taasisi za Serikali.

TANESCO ikiwa miongoni mwa Taasisi za Serikali, itaanza kutumia mfumo huu kwa kufanya mauzo ya LUKU kupitia ofisi za TANESCO, Kampuni za simu pamoja na Benki zote zinazofanya mauzo ya LUKU kupitia huduma za kibenki.

Serikali kwa kushirikiana na Wataalamu wa TANESCO itahakikisha kuwa mfumo huu unafanya kazi bila kuathiri manunuzi ya LUKU. Ifahamike kwamba, TANESCO ni miongoni mwa Taasisi za Serikali zitakazotumia mfumo huu mpya na hadi hivi sasa Taasisi nyingine za Serikali zimeshaanza kutumia kwa mafanikio, baadhi ya Taasisi hizo ni Polisi, Brella, Ardhi, TRA pamoja na Mamlaka za maji.

TANESCO inapenda kuwahakikishia wateja wote kuwa mbali na Kampuni za simu ofisi zote za Shirika na vituo vya mauzo ya LUKU vitaendelea kutoa huduma katika kipindi chote cha Sikukuu ya Pasaka.

TANESCO ‘‘Tunayaangaza Maisha yako’’

Kwa mawasiliano

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Tovuti: www.tanesco.co.tz, mitandao ya kijamii:

Mitandao ya kijamii

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

Facebook Tanesco Yetu

IMETOLEWA NA:

OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU

MACHI 27, 2018
Mbona TANESCO wamekanusha hii taarifa yako nyoko wewe? Unastahili kupigwa ban maana umewatukana bure hao Mods!!
 
Huo mfumu una faida zip Kwa wateja

Ngoja tusubiri tuone! Ila rekodi zinaonyesha serikali huwa inashindwa vibaya ktk kuendesha mifumo yake, soko huria inatakiwa waliwezeshe!! Sasa Kutoka 'soko' huria kwenda monopoly, yangu macho!!

By the way: id yangu haijawa hacked, msiniulize maswali.
 
sema maslah yako yameanza kuguswa unapiga yowe tulia namba zisomeke vizuri
 
Huo mfumo mpya wa malipo ya Luku unaweza kuizika kabisa Tanesco maana huenda wakashindwa kupata fedha za operations zao kwa wakati maana urasimu wa kuzipata hizo pesa unaweza kuchelewesha utendaji wa Tanesco.

Vv
 
Inatia moyo, ila huko mbeleni msikimbie maswali na malalaniko ya wadau wenu PIA kwa siku za usoni msije mkauacha HUKIWA huu uzi.

KARIBUNI.
 
Inatia moyo, ila huko mbeleni msikimbie maswali na malalaniko ya wadau wenu PIA kwa siku za usoni msije mkauacha HUKIWA huu uzi.

KARIBUNI.
 
Back
Top Bottom