Pole mteja zinapatikana muda wote, pia tupo katika mitandao ya kijamii
Mjumbe auwawi
Izi namba za watu wa Kanda mbali mbali na wenyewe, kwa nn? Wasiwepo katika Jamii Forum wakajibu baadhi ya majibu. Na wakijibu wajitambulishe kwamba mfano Tanesco ILALA, ili iwe Raisi kujibu maana Tanzania ni kubwa mfano mtu wa Tanesco ubungo awezi kujua tatizo la Igogo Mwanza
Ushauri wangu naomba ufanyiwe kazi
 
Proof of address kwa mteja ni taarifa muhimu sana hasa katika utandawazi. Kama mteja akitaka kupewa lisiti ya aina hiyo ni vema akapewa au kukawa na utaratibu wa kutoa lisiti za aina hiyo Mara moja kwa mwezi au kwa maombi ya mteja.

Lisiti hizo kazi yake sio kusomea unit za umeme tu lakini wakati mwingine hutumika kumthibitisha mteja katika juu ya anuani yake. Hii kitu katika utandawazi ni mandatory requirements. Proof of address inafanywa kwa kutumia bili za utilities kama Maji, umeme na Gesi. Hivyo ni vema mkaliangalia hili Kama hitaji LA wateja wa katika ulimwengu wa utandawazi.

Mathalani, ukitaka kufungua akaunti za ebay, amazon, perfect money, okpay, adv cash etc, kwenye mitandao huwezi kuthibitishwa kama huna proof of address kutoka ama umeme au Maji. Na mnaweza kujaribu hili. Kwa dunia ya sasa hili ni hitaji muhimu kwa ajili ya online transactions. Ndio maana nasema matumizi ya lisiti yameongezeka na mtusaidie kuziboresha.

Maana sio kazi ngumu kuongeza field hizo kwenye report husika.
 
Huku Kawe Siku hizi Mbona hawakati Umeme Kama zamani? Kama Switch ya kukatia Umeme ni mbovu watujulishe tuwachangie!
 
"Tumepokea ushauri wako Tutaufanyia kazi" Usipojibiwa hivyo unitag. Maana hapa ndo penye chanzo chao kikuu cha rushwa. Kwenye kesi za namna hii huwa wanakuja faster.
 
TANESCO
Naomba kuuliza kuwa hivi umeme wa bei nafuu (REA) huku Geita mtaupitisha katika vijiji VP hapa Geita

naomba majibu yenu.
 
Tatizo lenu ni lipi hasa.

hamna mita au nguzo sababu nimelipia umeme tangia january mpaka leo cjafungiwa umeme
 
Haka kapicha nimekutana nako kwenye mitandao mingine lakini kanatoa picha ya hali ilivyo katika shirika letu la umeme la taifa. Hii picha ni ya Kibondo, lakini hata hapa Dar Tanesco hawako vizuri katika kutoa huduma ya uhakika ndani ya masaa 24. Kila siku umeme hukatika mara mbili au tatu kwa siku pamoja na tambo za boresho. Kuna tatizo Tanesco si bure!.
17554534_1896274220652193_3438994188772859632_n.jpg
 
hii inategemea na maombi ya mteja mfano kama akiomba kuunganishiwa bila kuwa na nguzo ni siku 30 za kazi, kama kuna nguzo 1 ni siku 60 za kazi na kama kuna nguzo 2 ni siku 90 za kazi lakn hii inategemea na uwepo wa vifaa kama vifaa vipo tunafunga umeme hata ndani ya siku 2 lakn kama vifaa havipo kama kwa sasa tunachangamoto ya vifaa kama nguzo na waya hivyo basi tunawaomba radhi wateja kwa kucheleweshewa huduma na kuwaambia kuwa vifaa vikipatikana vitatumika kuwaunganishia wateja kwa kufuata mtililiko wa kwanza kulipia ndio anakuwa wa kwanza kufungiwa (FIFO)

Mbona mimi nililipia ili nifungiwe nguzo 1 (tarehe 05.01.2017 kwa hiyo siku 60 ulizotaja zimepita) lakini mpaka leo sijafungiwa umeme? Naomba jibu tafadhali.
 
Najua TANESCO kama shirika mna nia ya dhati kabisa ya kuhakikisha mnatoa huduma bora kwa wateja wenu kama kauli mbiu yenu isemavyo "TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO".

Lakini kumekuwepo baadhi ya watumishi wasio waaminifu, wenye lugha chafu na wasumbufu ambao wamekuwa wakilipaka matope shirika zima kwa ujumla.

Mfano ni wilaya ya kilolo mkoa wa iringa. Line inayoanzia Kidabaga kupitia Bomalang'ombe, Mwatasi, Ng'ingula hadi Isanga imekuwa ikisumbua mara kwa mara. Wakipewa taarifa baadhi ya watumishi hao wamekuwa wakishindwa kutatua matatizo hao kwa wakati kwa kisingizio cha ubovu wa gari na wakati mwingine wamekuwa wakigoma kuja kufanya marekebisho kwa kisingizio kuwa gari lao halina uwezo wa kumudu kupita kutokana na ubovu wa barabara.

Imefikia wakati wanawaambia wateja wenyewe watoe magari yao ili mafundi wa Tanesco waweze kufika site na kufanya matengenezo. Je hii ni haki? Mfano mzuri ni leo tar 21/04/2017 mteja mmoja aliambiwa atoe gari iwafuate mafundi hao na alipofika sehemu waliokubaliana akaambiwa muda umeenda arudi tu hadi kesho. Je ni sawa? Kama wateja watakuwa wanakatishwa tamaa kiasi hiki na watumishi wachache waliokosa uzalendo tutafika?

Niko tayari kutoa ushahidi na ushirikiano kwa mamlaka zinazohusika endapo nitahitajika kufanya hivyo. Nawasilisha.
 
Haka kapicha nimekutana nako kwenye mitandao mingine lakini kanatoa picha ya hali ilivyo katika shirika letu la umeme la taifa. Hii picha ni ya Kibondo, lakini hata hapa Dar Tanesco hawako vizuri katika kutoa huduma ya uhakika ndani ya masaa 24. Kila siku umeme hukatika mara mbili au tatu kwa siku pamoja na tambo za boresho. Kuna tatizo Tanesco si bure!.View attachment 499132
 
Tanesco mbona mnatupa shida Wateja wapya? Mfano nililipia kupewa Huduma ya umeme tangia January hadi sasa sijafungiwa umeme. Niko kwembe
 
Anzisheni platform yenu ya kupokea maoni bosi wenu 'Dereva wa Lori' hataki habari za mitandao..
 
kuna tatizo gani tena
mbona mmekata umeme huku Mkoa wa Geita Lwamgasa-Geita?

Yaani Tanesco mnatunyima raha kabisa.
 
Kuna maeneo mnakata sana umeme, tena bila taarifa. Imefikia hatua tunaona kawaida umeme kukatika karibia kila siku.

Hili swala linakera sana ukizingatia ukienda maeneo mengine umeme upo mda wote.

Hata kama hayo maeneo ya wakubwa basi angalau kuwe na mgao, mkikata kwetu siku mbili huko mnakata siku moja.

Hii nchi yetu sote. Haiwezekani tunaumia swala la umeme wakati wengine wanasema mgao hakuna tena.
 
Back
Top Bottom