Wapendwa TANESCO, mimi nawakumbusha tu kwa nia njema kuhusu suala la umeme wa REA kitongojini kwetu maana tuliambiwa tuzid kusubiria sasa hadi binafsi nachoka, tafadhali sema chochote kuhusu ombi langu la kupatiwa Umeme wa REA huko kwenye kitongoji cha KIJUKA kijiji Mabuye kata Kassambya wilaya ya Missenyi mkoani Kagera.
Kama ambavyo tulikupatia ufafanuzi hapo awali wataalamu wetu wamepokea swala hili kwa hatua zaidi
 
Hivi inachukua muda gani kusajili mita mpya? Nmefungiwa umeme tangia trh 21/10 hadi leo hii siwez nunua umeme naambiwa mita bado haijasajiliwa
 
Ndugu mpendwa mteja wetu

Ilitokea hitilafu kwenye transfoma letu na wataalamu wetu wamechukua hatuaa stahiki kuhakikisha mnafurahia huduma
Mkuu TANESCO hivi ninavyoandika jtatu hii kuanzia saa 12 jioni hadi saa hizi saa mbili usiku kuanzia Manzese hadi Kimara mwisho hakuna umeme.Tatizo ni nini?mbona umeme umeanza kusumbua tena wakati ulishaanza kutuliatulia maeneo hayo?
Hizo hitilafu mbona tukiwa Cairo,Pretoria,Amsterdam hatuzishuhudii?Sisi tunashindwa wapi jamani?Anyway,nisiwakatishe tamaa,tangu Magufuli ashike nchi,umeme Dar umepungua kero,sasa msilianzishe balaa tena.Nawapongeza mwaka huu,naomba msimalize vibaya,rudisheni umeme stable Dar es salaam.Hizi wiki mbili tatu kumeanza shida tena.
 
Siku ya tatu hatuna umeme tukipiga simu tunaambiwa tuwe na subira.sasa hii subira ya kukaa na giza na kazi haizfanyuki nani alaumiwe?
Mashine tatu zimesimama kwa nini hamjali wateja wenu?
0654229464
Location
Kwekitui Mbelei Lushoto-Tanga
 
Pongwe tanga tanesco wanatuonea wanatufanya wateja sisi wasenge, tunakopa hela tujaribu ujasiliamali ununue fridge ubangaize na vijuice kuutwa umeme hakuna
 
Mbona sasa imekuwa kama ni mazoea kukata kwa umeme kila siku shida ni nini? Maana maemeo mengi ya Airport kila baada ya Siku moja lazima umeme ukatike kwa Siku nzima.
 
NAOMBA KUULIZA (NIMEANDIKA KWA HEREFI KUBWA ILI SASA TUPATE KUELEWA).

NGUZO ZA UMEME ZINALIPIWA AU NI BURE .

MAANA KILA MTU ANASEMA LAKE.
 
Siku ya tatu hatuna umeme tukipiga simu tunaambiwa tuwe na subira.sasa hii subira ya kukaa na giza na kazi haizfanyuki nani alaumiwe?
Mashine tatu zimesimama kwa nini hamjali wateja wenu?
0654229464
Location
Kwekitui Mbelei Lushoto-Tanga
Hili hamjalifanyia kazi
 
Mkuu TANESCO hivi ninavyoandika jtatu hii kuanzia saa 12 jioni hadi saa hizi saa mbili usiku kuanzia Manzese hadi Kimara mwisho hakuna umeme.Tatizo ni nini?mbona umeme umeanza kusumbua tena wakati ulishaanza kutuliatulia maeneo hayo?
Hizo hitilafu mbona tukiwa Cairo,Pretoria,Amsterdam hatuzishuhudii?Sisi tunashindwa wapi jamani?Anyway,nisiwakatishe tamaa,tangu Magufuli ashike nchi,umeme Dar umepungua kero,sasa msilianzishe balaa tena.Nawapongeza mwaka huu,naomba msimalize vibaya,rudisheni umeme stable Dar es salaam.Hizi wiki mbili tatu kumeanza shida tena.
Hudum imerejea mpendaa mteja wetu
 
NAOMBA KUULIZA (NIMEANDIKA KWA HEREFI KUBWA ILI SASA TUPATE KUELEWA).

NGUZO ZA UMEME ZINALIPIWA AU NI BURE .

MAANA KILA MTU ANASEMA LAKE.
Yaani hapa huwezi kupata jibu japo Mh Kalema anahubiri hivyo kila uchao, lakini wataalamu wa Tanesco hawapambanui ukweli wa jambo hili. Naungana na wewe kuwataka Tanesco watuweke wazi juu ya hili. TANESCO NGUZO NI BURE AU TUNALIPIA???
 
hii inategemea na maombi ya mteja mfano kama akiomba kuunganishiwa bila kuwa na nguzo ni siku 30 za kazi, kama kuna nguzo 1 ni siku 60 za kazi na kama kuna nguzo 2 ni siku 90 za kazi lakn hii inategemea na uwepo wa vifaa kama vifaa vipo tunafunga umeme hata ndani ya siku 2 lakn kama vifaa havipo kama kwa sasa tunachangamoto ya vifaa kama nguzo na waya hivyo basi tunawaomba radhi wateja kwa kucheleweshewa huduma na kuwaambia kuwa vifaa vikipatikana vitatumika kuwaunganishia wateja kwa kufuata mtililiko wa kwanza kulipia ndio anakuwa wa kwanza kufungiwa (FIFO)
Sasa hapo hiyo pesa yangu itakua ina kaa muda wote huo ni kwanini taratibu zisiwepo kama vile unavyo fuata kanuni zingine za kutoa fedha ndipo upatiwe bidhaa maana unakuta mtu anatoa fedha yake halafu muda wa kupata huduma una kua nimuda mrefu wa kusubiria nanyi
Pia mjivishe wajibu juu ya wateja wenu bilashaka fedha yake siokwamba imekaa tuu bilshka inafanya mambo mbalimbali n.k..
 
Maana tumesikia kuwa ukitaka umeme hata km panahitaji nguzo 3 unalipa gharama ya umeme tu 27000.Jeni kweli?
 
Maana tumesikia kuwa ukitaka umeme hata km panahitaji nguzo 3 unalipa gharama ya umeme tu 27000.Jeni kweli?
Hili swali wameulizwa muda mrefu humu ndani lakini hawalijibu bali wanakwepa, sijui kwanini. Tanesco mkuje huku mtuweke wazi hili suala la nguzo....
 
Back
Top Bottom