TANESCO
Official Account
- Jul 12, 2014
- 4,584
- 2,104
- Thread starter
- #5,681
Tunachokusihi mpwendwa mteja wetu pamoja na wateja wengine ni kupenda kupokea taarifa na kutoa taarifa sehemu husika.njoo ofisini utajaza fomu wataalamu wetu watafika kwako na kufanya savey kisha tutakupatia gharama halisi kumbuka kuhamisha mita kinyemela ni kosa kwa mujibu wa sheriaNimekusudia kukarabati nyumba yangu, mafundi wamenishauri kuwa ili kazi Yao iende vizuri ni vyema aitwe fundi wa umeme kwa ajili ya kuisogeza MITA YA LUKU, upana wa mita mbili tu kutoka mahali ilipo sasa katika ukuta huohuo.
Fundi alipofika akaniambia kuwa kwa kawaida natakiwa kuwajulisha TANESCO na gharama za kuhamisha MITA YA LUKU kihalali eti ni shilingi laki mbili (200,000) isipokuwa kama nataka nimuachie yeye aihamishe hiyo mita mwenyewe kwa malipo ya shilingi laki moja tu. Nimemwambia nitamjibu kesho!
Kwa hiyo naomba wajuzi mnijuze kama ni kweli gharama ya kusogeza mita ya LUKU ni shs 200,000?? Maana mimi nilidhani ni bure isipokuwa nilipe gharama ya ufundi tu.
Au nimpe hiyo laki moja ili kukwepa mlolongo wa kwenda TANESCO kama anavyodai, na kazi hiyo aifanye mwenyewe?
Naomba mnijuze ili niendelee na zoezi au la
Sent using Jamii Forums mobile app