Kuna kauli moja imo ndani ya hilo tamko ambalo watu wangeacha shuku wangejua hawa jamaa wametuma ujumbe gani. Lakini inaonekana baadhi ya watu badala ya kusoma substance yake na kusoma "between the lines" wanajikuta wanamiss the whole message. Sijui ndiyo ule "wepesi wepesi" wenyewe au ndio mojawapo ya madhara ya mfumo wa kifisadi; hatuamini mtu ambaye yukoo serious.. wametuharibu sana hawa.
Mzee Mwanakijiji,
Hivi waraka huo ni wa kutia matumaini na kuaminika zaidi ya kauli na ahadi za JK wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2005?Naamini jibu ni HAPANA.Kauli za JK zilileta matumaini makubwa zaidi ya contents za waraka huu wa "wapiganaji".JK alifanikiwa kuwaaminisha Watanzania kuamini kuwa yeye anaelewa WANATAKA NINI lakini akatumia ujanja wa kusema kile wanachotaka kuskia i.e. alifahamu Watanzania WANATAKA KUSIKIA NINI.Just like "wapiganaji wetu" wapendwa.
Wengi walilaghaiwa na kauli hizo za JK kwa sababu hii hii inayojirudia hapa:KUAMINI MANENO BADALA YA VITENDO VILIVYOPASWA KUTUAMINISHA MANENO HUSIKA.Call me a doubting Thomas,au mzembe wa kusoma kati ya mistari lakini sijashawishika kuwaamini "wapiganaji" hawa.
Mwanakijiji,tuirejee historia kidogo kabla ya kuwapa hawa jamaa free pass.Hivi uhuru ulipatikana kwa nyaraka za aina hii pekee au jitihada za dhati kuhakikisha mkoloni anang'oka?Hata kama sasa kuna maswali kuhusu umuhimu wa UHURU wetu,bado tunapaswa kuzithamini na kuzienzi jitihada za waliojitoa mhanga kupambana na mkoloni kwa kila jinsi.
Nduli Iddi Amini nae hakudhibitiwa kwa nyaraka kama hizi za "wapiganaji" hawa,bali kwa kujitoa mhanga na kupambana nae hadi dakika ya mwisho.
Lakini pengine mfano mzuri zaidi ni wa marehemu Edward Sokoine.Hakupambana na wahujumu uchumi kwa maneno,he truly was a man of actions.Alitenda zaidi ya kusema.Na hata kama ufanisi wa vita dhidi ya wahujumu uchumi unaweza kuwa questionable,lakini alionyesha mfano.Na kiongozi mzuri anapaswa kuwa mwingi wa matendo kuliko maneno.
Mwanakijiji,ni kweli kwamba moja ya athari za ufisadi ni kwa wananchi-hususan walalahoi-kupoteza imani kwa kile wanachosikia kutoka kwa wanasiasa.Na wana sababu za msingi katika hilo kwa vile experience inaonyesha kuwa tatizo la Tanzania halijawahi kuwa katika kuja na mawazo bora bali turning such good ideas into actions.Nyaraka hiyo ya "wapiganaji" haina tofauti na MKUKUTA,MKURABITA,Kilimo Kwanza,Mkakati wa Taifa dhidi ya Rushwa,Visheni ya Taifa 2025,na "porojo" nyingine kama hizo.Kwanini tusishtushwe na nyongeza hii ya "mikakati mwingine maridhawa" ambayo si ajabu ikaishia kwenye maandishi tu.
Hivi ni personalities za waandishi wa waraka huu au substance ya walichoandika inayoleta credibility kwao na kwa waraka husika?If it's the former,then tunaweza kuwa for a big surprise kwa vile siasa za personalities zimekuwa kikwazo kikubwa sana cha maendeleo si Tanzania tu bali barani Afrika kwa ujumla.Tusisahau mchango wa "haiba ya JK" na "rekodi yake ya kutojihusisha na rushwa" zilivyopelekea kulainisha nyoyo za wengi 2005 (japo fedha za akina ROSTAM ndizo zilizotoa mchango mkubwa zaidi).If it's the latter,then ni muhimu kurejea substance katika nyaraka nilizozitaja hapo awali.Tusisahau pia kuwa mapema mwaka 2006 JK alitoa maneno matamu sana kuhusu chuki yake dhidi ya rushwa,na akatuhakikishia kuwa NAWAFAHAMU WALA RUSHWA ILA ANAWAP MUDA WA KUJIREKEBISHA.An open deadline,I suppose...
Unless hao "wapiganaji" watatuonyesha kuwa wana cha muhimu zaidi ya "nyaraka za kuleta matumaini" binafsi ntaendelea kuwa-regard kuwa ni "wajanja" (or wahuni?) flani wanaocheza na feelings zetu.
And,final thought,kuna kitu inaitwa UZANDIKI,ambapo si lazima uwe in the form of character assassination au kuwakoroga watu bali pia exaltation.Kwanini tusi-suspect kuwa waraka huu ni kazi za "watu"?Na kama si kazi ya "watu hao" je kwa kusambaza waraka huo "mzuri" hawawarahisishii kazi "watu hao" kuwadhibiti kiulaini?Let's not forget that Tanzania is a
de-facto quasi-security state,afterall!