Tamko la Wapiganaji CCM Feb 10, 2010

Tamko la Wapiganaji CCM Feb 10, 2010

Tamko limekuja wakati muafaka?

  • Ndiyo

    Votes: 8 57.1%
  • Hapana

    Votes: 5 35.7%
  • Sijui

    Votes: 1 7.1%

  • Total voters
    14
  • Poll closed .
hakuna wapiganaji ndani ya ccm, hawajawahi kuwapo na wala hawatakuwepo.....

ndani ya ccm kuna wachumia tumbo tu....wanachojali ni maslahi yao, washikaji zao na familia zao......hii ndiyo kweli ya hakika walau kwa ufahamu wangu.....nilisema kwenye thread moja jana nadhani...nadhani bi SS hakukosea pale alipowatolea uvivu akina Mwak.....na kuwaambia...ni njaa tu inayowasumbua....na kuwa EL ni mwanamme wa shoka...nadhani ni kweli kuwa EL ni mwanamme wa shoka walau ndani ya CCM...si tumeona Richmond ilivyoisha....mwenye macho haambiwi tazama!!!!!!
 
Karata ya mwisho mnasubiri CCM wadondeshe tonge ni report ya kamati ya mwisho; baada ya hapo msahau!!
 
Kitila Mkumbo,

..nakumbuka 1995 kulikuwa na mazingira kama haya ya Richmond. wakati ule kulikuwa na kashfa za Chavda na Loliondo.

..sasa hivi Mwinyi na Kinanan ambao ni watuhumiwa wa kashfa za 1995, wamepewa jukumu la kuchunguza migongano kati ya mafisadi na "wapiganaji" ndani ya CCM.

..Mwinyi ndiye Raisi aliyemfutia kifungo rubani wa ATC aliyekamatwa airport akitorosha dhahabu. Kinana naye alikuwa mstari wa mbele katika ugawaji/ukodishaji wa mbuga ya Loliondo.

..sijui kwanini baadhi yetu wana matumaini na CCM kwa kweli?
 
Tatizo moja la siasa za Tanzania yetu, pengine tofauti na nchi zingine hapa Afrika, ni kukosa watu wenye ujasiri wa kisiasa, ambao wapo tayari kuhesabiwa, sio kwa maneno yao bali kwa matendo yao. Pengine hii inachangiwa kwa kiasi fulani na ukweli kwamba ni wanasiasa wachache sana wanaoweza kusurvive bila mkono wa serikali. Wanasiasa wetu wengi wanaishi ama kwa kuitegemea serikali moja kwa moja, kwa kuajiriwa, kwa pensheni wanazopata au kwa kuwa wafanyabishara wakifanya biashara ambazo ufanisi wake kwa kiasi kikubwa unategemea short cut kama vile kukwepa kodi, etc., kiasi kwamba serikali ikiamua kuziba mianya sawasawa hawezi kukatiza siku mbili.

Ni kwa sababu hii wengine hatukashangazwa kwa waanzilishi wa CCJ kujificha wakipima upepo, na ndio maana na leo wanatoa nyaraka kwa kujificha. Kama unaamini unachokiongea kwa nini ufiche jina lako? Woga ni adui mkubwa sana wa maendeleo ya kisiasa katika nchi hii.

Mkuu Kitila,

Mimi naamini sana hii dossier kwani the way ilivyoandikwa inaonekana ina uzito. Inawezekana waandaji/muandaaji akawa anataka kuwavurugia watu fulani akiwa anafahamu joto lake ndani ya chama. Vile vile yawezekana ni watu kweli wanataka kuleta mapinduzi ya kweli, pia yawezekana ni kundi la watu walioondolewa kwenye utafunaji wa keki; kama wengine wanavyofaidi, so gere!!

Kwa kuangalia upande wa kuwaona kama watu wa kweli wenye kuleta mapinduzi, hii yaweza kuwa mbinu yao kwa sasa kwani ni watu wanaofahamu mbinu za ndani ya chama za kuvuruga wapinzani wake.

Nielewavjo CCM ni chama kikubwa kilichojijengea uwezo mkubwa wa kufaniliwa kwenye mambo yake tangu zamani!!! Wote tutajua yaliyomkuta Kombe, Kolimba........

Yangu macho.
 
hamna jipya mnanjaa kama viongozi wenu hatutaki huwo upuuzi kwenye jf kwakuwa kila mtu kwasasa anatambua yakwamba ccm wanaongea kama malaika ila wanatenda kama mashetani , ccm imeondoka na nyerere so ni bora uache kuongopea wananchi tafuta mada nyingine ila si ccm huna hoja na ccm yako chafuuuuuuu
 
Kitila Mkumbo,

..nakumbuka 1995 kulikuwa na mazingira kama haya ya Richmond. wakati ule kulikuwa na kashfa za Chavda na Loliondo.

..sasa hivi Mwinyi na Kinanan ambao ni watuhumiwa wa kashfa za 1995, wamepewa jukumu la kuchunguza migongano kati ya mafisadi na "wapiganaji" ndani ya CCM.

..Mwinyi ndiye Raisi aliyemfutia kifungo rubani wa ATC aliyekamatwa airport akitorosha dhahabu. Kinana naye alikuwa mstari wa mbele katika ugawaji/ukodishaji wa mbuga ya Loliondo.

..sijui kwanini baadhi yetu wana matumaini na CCM kwa kweli?
kaka tatizo watu hawajui ccm kuwa ni wakoloni weusi
 
Greetings dear friends; We received this document late last night from very reliable and impeccable sources. M has given the greenlight to release it as it is.

Kanzi, Tunashukuru sana... si mbaya. Good work
 
Wameamua kuahirisha ripoti ni sawa na kuamua kutomtibu mgonjwa ili uweze kuomba ushauri wakati ugonjwa unaendelea kwa kasi , bila kujua kuwa unatafuta ushauri ama vipi--- anayestahili dawa wangempatia tuuuu
 
CCM wana kazi,hapo ishu inazidi kuwa nzito..nashukuru ugomvi wao wanaosogeza karibia na uchaguzi.kaazi kweli
 
Mie binafsi nashangaa sana na siasa za CHADEMA.

Wao badala na kudili na matatizo halisi tuliyonayo wanajitahidi kufanya mbinu zisizofanyika.

1. CHADEMA ndio wamesajili CCJ eti wakijaribu kumuuwa kiboko kwa kumpiga kwa unyasi, ili ionekane ccm inapasuka.

2.CHADEMA ndo wameandika waraka huu eti wakijaribu kumuuwa tembo kwa kumchapa na kijiti cha mti.

Politiks za CHADEMA ndizo zinazowakatisha tamaa watanzania wenye nia na uwezo, maana propaganda wanazo propagate CHADEMA zinazidi kudidimiza matumaini ya watanzania na kuwavunja moyo. Kwa wao wakifikiri wanawavunja watanzania moyo kuipenda ccm ili wapendwe wao.

CHADEMA acheni uzushi fanyenia siasa halali , za haki na zenye tija ktk mustakbali wa Taifa.
 
Hiyo list inamgusa the comedy moja kwa moja, ni mtego anatakiwa kuruka. Ndio maana hawa wanaojita wapiganaji hawajaweka majina yao. Hawana uhakika JK yuko upande gani...Je anaweza kuwatosa? Je na yeye yuko kati ya hao kwenye list ? my 50 cents
 
Back
Top Bottom