Nadhani kuna watu wanamiss pointi kubwa sana ya ujumbe huu; ndani ya CCM kuna wapiganaji wa kweli na wapiganaji uchwara; wapiganaji wa kweli hawajali wabunge wa CCM wanafanya nini Bungeni au wanachama wengine wanafanya nini; wao wanapigana.
Ninavyoelewa ni kuwa mstari umechorwa ardhini sasa kati ya wale wanaCCM walioweka Chama kwanza kwamujibu wa ibara ya 14:1 na wana CCM ambao wameamua kujitenga 'nao'. Ukiniuliza mimi I'll stand with these people than their opponents. CCM has been put on notice.
Nimemuuliza mmoja wao leo anasema mambo ya Ngoswe mwachie Ngoswe, wanajua wanachofanya na tamko hili ni kuwapa notice JK na uongozi wa juu wa CCM. Ati wamefunika kombwe mwana haramu apite.. lakini "haendi kokote"!
Mzee Mwanakijiji,
Naheshimu sana mchango wako.Lakini katika hili naomba kutofautiana nawe hasa kuhusu hao unaowaita "wapambanaji wa kweli".Kwanza,kama ni wapambanaji wanapambana na nani?Mafisadi au mfumo wa kifisadi?Pili,kama wanapambana,je ni kwa ajili yetu au wanatetea maslahi yao ya kisiasa?
Mwandishi mahiri wa makala,Padre Privatus Karugendo alishawahi kuwakosoa hao wanaoitwa "wapiganaji dhidi ya ufisadi".Alitoa mfano wa padre anayetangaza kupinga mafundisho ya kanisa lakini bado anamsujudia Papa (or something like that).Nilivyomuelewa,alikuwa akiwakemea baadhi ya wabunge wa CCM wanaojitambulisha kama wapambanaji wakati wao ni sehemu ya mfumo dhalimu unaodumishwa na CCM hiyohiyo.Kwa wanaofahamu masuala ya vita,watakubaliana nami kwamba vita ya ndani inaweza kuwa ngumu zaidi kuliko ya nje.Kinachowafanya hao "wapambanaji wa kweli" waendelee kuwa ndani ya CCM hadi leo ni nini kama si ubinafsi wao?Hata kwenye Maandiko Matakatifu tunausiwa umuhimu wa kujikana sisi wenyewe kama tunahitaji kuuona ufalme wa mbingu
Hata hizi nyaraka wanazokuja nazo wakati huu zinapaswa kuangaliwa kwa mashaka.Walikuwa wapi siku zote hizi wakati taifa linateketea?Kwani iwe sasa miezi michache kabla ya uchaguzi?Hivi hawa hawajitengenezei mazingira kuwa wakibwagwa huko CCM waje na hadithi kuwa "siku zote tulikuwa nanyi kiroho japo kimwili tulikuwa na CCM". Wanachofanya ni sawa na kupuuza afya ya mgonjwa hadi inakuwa mahututi na kuanza "kutangaza severity ya ugonjwa husika".Kwanini tusihisi kuwa hawa ni matapeli wa kisiasa wanaojaribu kujitengenezea mazingira mazuri pande zote mbili?Hapa namaanisha kuwa wanaonekana wana-CCM waaminifu kwa kushiriki kuunga mkono hoja za kifisadi kama hiyo ya Richmond lakini pia wanatuzuga huku pembeni kwa kutoa nyaraka za kukemea kilekile wanachokitumikia!
Lazima tufahamu kuwa si lazima kwa wao kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi (if we were to believe them) wakiwa ndani ya CCM.By the way,Mtanzania halazimiki kuwa mwanasiasa,let alone mbunge wa CCM,kuweza kushiriki mapambano ya kuleta "ukombozi wa pili".Wewe Mwanakijiji ni mfano sahihi kabisa katika hili.Wewe si mbunge au mwanachama wa CCM lakini harakati zako zinaonekana kuwatikisa CCM hadi wanakuchukia.Kwani tuwaamini wanafikia hawa wanaoogopa "lawama" au "kuchukiwa"?Askari anayefaa kuwamo vitani ni yule tu aliye tayari kumwaga damu kwa ajili ya taifa lake.Sasa kwa hawa "wazushi" kuendeleza mapambano yao nje ya CCM wala hakutapeleka umwagaji damu as such hasa kwa vile wamekuwa sehemu ya adui kwa muda mrefu.
Historia inatukumbusha pia kuwa hata baadhi ya waliopigania uhuru wetu hawakuwa ndani ya bunge la mkoloni.Na kwa wale walioingizwa serikalini au katika bunge la mkoloni waliendelea kujitoa mhanga kuhakikisha uhuru unapatikana.
Mbona Mrema aliweza kujitoa ndani ya CCM na ku-mount upinzani nje ya mfumo huo (licha ya ukweli kwamba mafanikio yake in long run yamekuwa disappointing)?Sasa kwanini hao "wapambanaji wa kweli" wasijiondoe CCM na kuanzisha mapambano ya dhati nje ya mfumo dhalimu?
Tunawatenganishaje na maamuzi kama hayo ya jana huko Dodoma hata wakijitetea kuwa "kusapoti kwao ni sehemu ya mkakati wa harakati zao"?Na kwanini tuwaamini ilhali hakuna ushahidi japo kidogo wa kututhibitishia kuwa kauli zao za "chuki" dhidi ya ufisadi ni za dhati kweli,na sio kutupumbaza?Actions speak louder than words.Na kwa hapa,matendo yao ndio yanapaswa yawahukumu badala ya vijinyaraka vya kutupumbaza kuwa ni 'notice kwa CCM na JK.Unatoaje notice kwa mwenye nyumba kama huna dhamira ya kuhama?
Let's imagine wangekataa KATAKATA kuunga mkono azimio hilo,nini kingetokea?Wangefukuzwa uanachama wa CCM?I don't think so kwa vile CCM inafahamu vizuri sana kuwa laiti ingewafukuza wangeivua nguo hadharani kuwa wamefukuzwa ili azimio la kuwalinda mafisadi lipite.
Mwanakijiji,wababishaji hawa hawana excuse hata moja ya kutoonyesha upinzani dhidi ya azimio hilo la kifisadi.Wameshiriki kurefusha mjadala wa Richmond only for them to give in dakika ya mwisho.Si bora wangekubali yaishe mapema tu!
Walichofanya ni sawa na kumbaka mtoto kisha kujitetea mahakamani kuwa ubakaji huo ulikuwa sehemu ya tambiko la kumsafishia mafanikio mtoto huyo.