Tamko la Wapiganaji CCM Feb 10, 2010

Tamko la Wapiganaji CCM Feb 10, 2010

Tamko limekuja wakati muafaka?

  • Ndiyo

    Votes: 8 57.1%
  • Hapana

    Votes: 5 35.7%
  • Sijui

    Votes: 1 7.1%

  • Total voters
    14
  • Poll closed .
Kuna swali la msingi ambalo limeulizwa na mlalahoi, kwamba hawa wapiganaji walikuwa wapi siku zote?!
Kwa upoe wangu wa ufikiri, nadhani walikuwa wanajipanga. Ni ngumu sana kupata wafuasi ndani ya chama ambao watakuwa wanapingana na uongozi wa chama, na inabidi kuwe na umakini wa hali ya juu katika kuwapata hao wafuasi.
Mchakato wa kuwapata wapiganaji wa kweli lazma utakuwa umechukua muda mrefu sana, na mipango ya kuanza kufanya vikao vya siri ili kuja na njia sahihi za kukabiliana na uongozi wa chama nao utakuwa umewachukua muda mrefu sana ukizingatia lazma kulikuwa na kutofautiana kwa mawazo ya nini kifanyike/njia ipi ni sahihi kuifuata katika kupambana na uongozi wa chama.

Na mwisho wa yote, ndo wamekuja na hili tamko ambalo kwa vyovyote, limewachukua muda mrefu sana kuliandaa.

Naamini kwasasa watakuwa tayari kukiacha chama kama tamko lao hili halita tekelezwa.

I wish them the best of luck
 
Kuna kauli moja imo ndani ya hilo tamko ambalo watu wangeacha shuku wangejua hawa jamaa wametuma ujumbe gani. Lakini inaonekana baadhi ya watu badala ya kusoma substance yake na kusoma "between the lines" wanajikuta wanamiss the whole message. Sijui ndiyo ule "wepesi wepesi" wenyewe au ndio mojawapo ya madhara ya mfumo wa kifisadi; hatuamini mtu ambaye yukoo serious.. wametuharibu sana hawa.
 
With what is happening unagundua ni kwa nini waraka wa kanisa katoliki ulikuwa muhimu na tishio kwa establishments za CCM.
 
Ok. Less waraka, tamko, azimio, etc and more action. Wale makarani wote kwenye ofisi za serikali wanaopoteza/wasioweza kupata mafaili bila kunywa maziwa wafukuzwe kazi mara moja.

Tukianzia hapa ndo ntajua tuko serious. Ntaamini kuna wapambanaji kweli.

Mpambanaji gani asiyeweza kuua hata mende afu anatoa tamko la kuua nyati?
 
Mpambanaji gani asiyeweza kuua hata mende afu anatoa tamko la kuua nyati?

labda mende atauliwa na watu wenye uwezo na means ya kumuua na huyo nyati ndiyo saizi yao? Au unataka aliyeshika gobore la kumtungulia nyati alilengeshe kwa mende ndiyo ujue yuko serious!?
 
sehemu iliyonigusa mimi na kunifanya niwape nafasi tuone ni hii (hasa ukizingatia kuwa masaa machache baadaye, wengine hawakutokea kuchangia kabisa upuuzi uliotokea Bungeni!!!)... I know people missed that part.. Hamjajiuliza kwanini wengine hawakuzungumza kabisa ambao walikuwa ni interested part kwenye Richmond?

Kwamba, kama wana CCM tuliokolea itikadi ya chama na makada wazuri na waaminifu wa siasa za Chama chetu tunakataa mara moja, daima na milele kuwa na ushirika wowote na wana CCM wengine ambao wanatuhumiwa, kutajwa, kushukiwa na hata kuhusishwa na kashfa zote kubwa ambazo zimeligubika taifa kwa karibu miongo miwili sasa.

to me thats whatsup!!
 
I am not convinced at all kwamba kuna "wapiganaji" ndani ya ngazi za juu za CCM.

Mpaka nitakapoona vitendo - na huu usanii haufikii kiwango cha kuitwa vitendo- ndipo naweza kuanza kuamini.

Otherwise hizi ni propaganda za "circuses" kama alivyosema Juvenal.
 
sehemu iliyonigusa mimi na kunifanya niwape nafasi tuone ni hii (hasa ukizingatia kuwa masaa machache baadaye, wengine hawakutokea kuchangia kabisa upuuzi uliotokea Bungeni!!!)... I know people missed that part.. Hamjajiuliza kwanini wengine hawakuzungumza kabisa ambao walikuwa ni interested part kwenye Richmond?



to me thats whatsup!!

Unakataa ushirika na viongozi wa CCM ambao hawajawajibishwa na hawatawajibishwa halafu bado unabaki kuwa mwanachama? Unataka tukuamini kwamba umekataa ushirika kweli au unazuga?

Wewe unataka kumpinga papa na makadinali wake halafu bado unaji identify kama mkatoliki?

Either unamkubali papa na makadinali wake na kubaki mkatoliki, or unawakataa na kutoka katika ukatoliki.There is no grey area here.
 
Hii imekaa vizuri sana na inatia moyo ila sijajua kuwa anapelekewa nani? NEC ya CCM au Kamati kuu au ni kwa raisi au itatolewa kwenye public media? Maanake kama hakuna chombo kitakachokua responsible kufanyia kazi huo waraka au kuujibu itakua haina maana.
 
Dr. Slaa
"Kuna mambo mengi ya msingi humu kwenye ripoti hayamo, kumwacha Hoseah kisa eti anafanya uchunguzi wa posho mbili dhidi ya wabunge ni jambo ambalo halina maana, kwa sababu hivi ni vitu viwili tofauti kabisa,"

Dr. Slaa
"Kama ni uchunguzi wao kuhusu posho mbili waendelee na yeye kama ni kuwajibishwa hilo ni jambo jingine, kuliacha jambo hili katika mamlaka ya juu wakati Bunge ni chombo chenye nguvu na kushusha heshima ya Bunge."

Pwenti

Ole Sendeka

"Serikali yetu ni sikivu, Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano Jakaya Mrisho Kikwete ni mtu mwenye dhamira njema ndiyo maana ameruhusu kujiuzulu waziri mkuu (Lowassa), tusiiseme serikali yote ina mafisadi, mafisadi ni mtu mmoja mmoja, na kama ni huyo Hoseah naamini Rais Kikwete atamwajibisha tu."

Mh! Haeleweki
 
Ok. Less waraka, tamko, azimio, etc and more action. Wale makarani wote kwenye ofisi za serikali wanaopoteza/wasioweza kupata mafaili bila kunywa maziwa wafukuzwe kazi mara moja.

Tukianzia hapa ndo ntajua tuko serious. Ntaamini kuna wapambanaji kweli.

Mpambanaji gani asiyeweza kuua hata mende afu anatoa tamko la kuua nyati?

I would like to adopt a top down approach, hao makarani wengi sana kuwakamata wote kazi, halafu impact yao wote inaweza kuwa sawa na kina Rostam na Chenge watano tu.

Unaanza na kina Chenge na Rostam, unaonyesha mfano kwamba nobody is invincible, hivyo vikarani vitashika adabu vyenyewe hata bila ya kuwa policed.

Ukiendekeza kukimbizana na makarani ndio kina Msabaha watakwambia unawatoa bangusilo.
 
Slaa kaongea Pwenti tupu lakini Sendeka hata Simuelewi kwa Kweli
 
Greetings dear friends; We received this document late last night from very reliable and impeccable sources. M has given the greenlight to release it as it is.
waache usanii, kama kweli wao ni wapiganaji watoke CCM na waingie upinzani! Hizi kelele chura hazizuii ng'ombe kunywa maji
 
“If fighting is sure to result in victory, then you must fight, even though the ruler forbid it; if fighting will not result in victory, then you must not fight, even at the ruler's bidding.”
 
Wewe ndio umeruhusu itoke? Maana naona imetolewa na Enigma.

Hii inaitwa DIVORCE PAPER

Kwa style ya uandishi na hata nukuu hii kitu ni ya kutoka kwa wenyewe kabisa. Sasa kama ni mtu mmoja au kakundi miongoni mwao ni lingine. Hii ikiwekwa vizuri ni Ilani tosha ya uchaguzi.

Sasa wameweza kuwataja watuhumiwa bila kujitaja wao? Huu ni upungufu mkubwa sana kuacha statement iliyosheheni uzalendo kama hii mpaka damu inachemka bila ya kuweka majina.

Hapo ndipo inapoonyesha ukosefu wa kujiamini wa wanasiasa wa Tanzania. Toka uhesabiwe kwa mema au mabaya na sio kujificha ficha!

Ukisoma kwa makini utaona kuwa hayo yaliyoandikwa ni majumuisho ya threads nyingi zilizotoka humu ndani ya JF. Most likely, 'aliyeruhusu' ndiye anayejua huu waraka umeandikwa na nani.

Ama baada ya hapo, huo waraka ni hauna jambo jipya, kana kwamba haitoshi hauelezei kuwapo kwa nguvu au muunganiko wa watu ambayo ni serious kama picha inavyotakiwa tuelewe.


Mambo ya Uchaguzi, tutaona mengi!!!!
 
Wakuu,Najaribu kufungua file lakini inasomeka damaged, nimeshindwa kujua content ya document hii
 
Back
Top Bottom