TAKUKURU kuwakamata na kuwachukulia hatua watu wote watakaojihusisha na vitendo vya rushwa kuelekea Uchaguzi Mkuu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,283
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali imewaagiza Makamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) nchini wahakikishe wanawakamata na kuwachukulia hatua watu wote watakaojihusisha na vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi mkuu.

“Watu wamezoea vitendo vya rushwa kwenye uchaguzi, Serikali tumeagiza kwa kamati za ulinzi na usalama zishirikiane kuhakikisha kwamba hakuna vitendo vya rushwa katika uchaguzi na yeyote ambaye anajihusisha na rushwa asiachwe.”

Alitoa kauli hiyo jana jioni (Jumamosi, Juni 20, 2020) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Lindi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Nachingwea akiwa njiani kuelekea wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikazi.

Waziri Mkuu alisema kitendo cha kutoa na kupokea rushwa ni kosa, hivyo viongozi hao wa TAKUKURU nchini hawana budi kuwachukulia hatua watu wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo

Vilevile, Waziri Mkuu amewataka Makamanda wa TAKUKURU katika wilaya zote nchini wahakikishe wanawakamata watu wote watakaojihusisha na vitendo vya rushwa wakiwemo na wapambe ambao ndio wachochezi wa vitendo hivyo

Waziri Mkuu alitoa maagizo hayo ili kuhakikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu unakuwa huru na wa haki, hivyo kuwawezesha wananchi kuchagua viongozi wanaowahitaji na si kwa msukumo wa rushwa

Katika hotuba yake aliyoisoma Juni 15, 2020 bungeni jijini Dodoma wakati akihitimisha mkutano wa 19 wa Bunge, Waziri Mkuu aliwataka viongozi wa vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi wazingatie katiba, sheria, kanuni na miongozo iliyopo katika uendeshaji wa shughuli za uchaguzi

Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwasihi viongozi na wanachama wa vyama vyote vya siasa na wananchi kwa ujumla waendelee kulinda amani na kuendeleza mshikamano katika kipindi hiki na wakati wa Uchaguzi Mkuu

Mapema asubuhi jana Mheshimiwa Majaliwa alikweda Zanzibar ambako alishiriki katika tukio la Kuvunja Baraza la Wawakilishi liliyofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein kwenye ukumbi wa Baraza hilo. Pia tukio hilo lilihudhuliwa na Spika wa Bunge Job Ndugai.
Mwisho.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
 
hio rushwa ningeipata mimi aliyenipa ningempigia kura hata mara mbili mbili kuliko kura yangu kwenda bure
 
Hivi kuna mtu anawaamini hao Takukuru? PM aache siasa nyepesi maana rushwa haiondolewi kwa matamko.
 
Wabunge wa ccm ambao wanategemea kutoa rushwa zamu hii kazi mnayo,kinachofanywa hapo hata kama unakubalika kwa wajumbe utakatwa tu
 
Msi mubali kudangaywa kwa kupewa hongo ili kumchagua kiongozi fulani.hakikisha unamchagua kiongozi bora mwenye sifa na mwenye uchungu na nchi yake .na mwenye kutaka maendeleo ya nchi yetu na watanzani wote bila kubagua wa kujali kabila fulani wa dini.usi mchaguwe kiongozi mwenye kupenda kula bata.mchaguwe kiongozi mwenye kujali kazi kazi hakuna maendeleo bila kufanya kazi kazi kazi kwanza kula bata huja baada ya mafakiyo.nimalize kwa kuwatakieni maisha bora na Afya njema muwe na uzima mungu ibariki tanzania ipate viongozi bora na siyo bora kiongozi.
 
Unataka jusema nini hasa?
Jaribu kuielewa falsafa ya kazi na Bata kwanza kabla ya kuanza...
 
Msi mubali kudangaywa kwa kupewa hongo ili kumchagua kiongozi fulani.hakikisha unamchagua kiongozi bora mwenye sifa na mwenye uchungu na nchi yake .na mwenye kutaka maendeleo ya nchi yetu na watanzani wote bila kubagua wa kujali kabila fulani wa dini.usi mchaguwe kiongozi mwenye kupenda kula bata.mchaguwe kiongozi mwenye kujali kazi kazi hakuna maendeleo bila kufanya kazi kazi kazi kwanza kula bata huja baada ya mafakiyo.nimalize kwa kuwatakieni maisha bora na Afya njema muwe na uzima mungu ibariki tanzania ipate viongozi bora na siyo bora kiongozi.
Pia msikubali kuchagua NDULI.
 
Wakiamua kuwa siriazi na kazi yao,kufuata sheria zao,basi nikuhakikishie hakuna yeyotr aitwaye mwanasiasa atapona,narudia tena..MWANASIASA YEYOTE hatasalimika.
 
CCM haijawahi kufanya uchaguzi bila rushwa. Wala hawajawahi kuwa na dhamira ya kuwa na uchaguzi huru na wa haki.
 
Rushwa nchi hii haiwezi isha Labda itungwe sheria ya kunyonga mtu akipatikana na kesi hiyo

Ova
 
Hakika kila Mtanzania atakubaliana nami kuwa TAKUKURU inafanya kazi yake kikamilifu, tunashuhudia kamata kamata za watiania wa Ubunge na udiwani wanaojihusisha na utoaji wa Rushwa wakikamatwa bila kujali sura, hadhi, umaarufu wala chama

Hii inathibitisha kuwa TAKUKURU inatekeleza majukumu yake bila kuingiliwa na mtu yeyote wala uoga. Hakika kwa mwendo huu nchi yetu itapiga hatua zaidi na tutapata viongozi wenye uchungu wa kweli na wananchi wao, wananchi walio wengi hawapendi kabisa viongozi watoa rushwa.

Ahsanteni TAKUKUKURU kwa kazi nzuri, endeleeni hivyo hivyo kwa maslahi ya watanzania na Tanzania.

Wananchi wenzangu ktk kila kona ya nchi yetu tuwape ushirikiano wapambanaji wetu ktk vita hii ya rushwa.
 
Hakuna ubishi ya kwamba malalamiko kipindi hiki yamekuwa makubwa pengine kuliko wakati wowote ule...Ninaomba kujua ni lini TAKUKURU (wazee wakufanyia kazi taarifa mbali mbali mnazopewa kuhusu tuhuma mbali mbali za rushwa bila kuchelewa) mtauarifu uma kuhusu kuanza zoezi zima la kuwahoji viongozi wakuu wa chama cha mapinduzi kama ambavyo mmekuwa mkifanya kwa taasisi nyingine na kikubwa zaidi kabla hamjaanza uchunguzi tutarajie mtaitisha "Press conference" kuelezea adhima yenu ya kuwahoji CcM. Na hili ni jambo zuri saana kwani ni utaratibu mzuri unaowajengea wananchi hali ya kufuatilia matokeo ya uchunguzi wenu baadae kama vile wanavyosubiria kwa hamu uchunguzi mlioufanya hivi karibuni kwa chama kimoja cha siasa kuhusu tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za wabunge wao....
 
Back
Top Bottom