TAKUKURU: Rushwa katika Taasisi za Dini hutokea wakati wa Uchaguzi wa Viongozi

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
Rushwa katika Taasisi za Kidini ipo hasa katika Uchaguzi wa Viongozi. Wanaoenda kugombea ni watu wanaotoka katika Jamii ambayo inaelekeza kwamba huwezi kuchaguliwa bila kutoa Hongo, hivyo analazimika kutoa hela ili achaguliwe.

Wakati huo huo Mgombea mwenza naye hupata taarifa kuwa Mwenzako anatoa hela, usipotoa hela hupiti, naye anatoa hela.

Viongozi au watoa Huduma katika Taasisi za Kidini wanapojihusisha na Vitendo vya Rushwa huweza kusababisha migawanyiko ambayo hukwamisha na kurudisha nyuma harakati za kutimiza malengo na Miradi ya Taasisi husika.

Aidha, Waumini wanaweza kugawanyika kati ya wale wanaounga Mkono na wale wanaopinga Vitendo vya Rushwa, na hivyo kusababisha Ugomvi na Migogoro.

 
Ndo maana mimi nimeachana na mambo ya hawa so called viongozi wa dini! Kila kuchao wanataka michango yetu tena minigi tu! Wanataka waendeshe ma V8, wajengee vimada wao majumba na kusomesha their prodigal children! Na baada ya hapo, waende kwa waganga wa kienyeji kutafuta vyeo ikiwemo pia kuhonga!

Tangu lini mambo ya Mungu yakachanganywa na wachawi na hongo?

Bora kujisalia nyumbani kwangu, Mola atasikia tu sala yangu, kuliko kwenda kwa hawa matapeli nisio na imani nao!
 
Sheria ikubali kuwa viongozi wa dini hawachaguliwi. Lakini wakiendelea kulazimisha wachaguliwe,,basi nakiri wataziharibu na wamefanikiwa kuziharibu sana hizi taasisi za kidini
 
Kiislam hakuna uchaguzi wa viongozi wa dini. Kama wapo wanaofanya hivyo, Waislam wanaofata Uislam hawatakiwi kumchaguwa yeyotekati ya hao "wanaogombea" na hawatakiwi kujihusisha kabisa na huo uchaguzi.
 
Back
Top Bottom