TAKUKURU, kwenye leseni za biashara online na za Wizara ya Fedha kuna rushwa inatolewa kwa nguvu

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,013
8,369
Kuna wakati niliwahi kuja na uzi hapa nikimlalamikia Waziri wa Fedha kutwa na usiku anasaini mikataba ya kuomba mikopo ilihali kwenye data base yake ya kuhusu watu wanao omba leseni za biashara mbalimbali wamewasilisha Maombi ili waweze kukata leseni na kufanya biashara.

Binafsi nilikuwa mhanga Mkubwa wa mfumo wa kuomba leseni ya baishara online, maana nilikuwa kila nikijaza form correctly kabisa maombi yanakuwa rejected, na anae reject unaona kabisa kuwa hana customer care kabisa maana ukifanya mawasiliano naye yeye ni mtu wa kufoka badalaya kutambua yakuwa anatakiwa kuwa msaada kwako, ili ukate LESENI ufanye biashara ili ulipe kodi.

ili jambo lilinifkisha hatua nikaamua kuacha kabisa ile biashara na kuipotezea serikali yangu pendwa mapato.

Tambua sheria za Tanzania zilivyo za ovyo, ujaanza biashara unatakiwa kukata LESENI, ukianza biashara utatakiwa kulipa KODI.

SASA unakuta mtu unapata kazi ya kufanya unaandaa pesa ya kukata leseni ili ufanye biashara ulipe kodi, UNAKWAMISHWA NA ANAYETAKIWA KUKUPA LESENI TENA ANA KUKWAMISHA NA MANENO YA VITISHO ili hali mtu huyo kesho na kesho kutwa anaenda lipwa mshahara kwa kodi hiyo hiyo uliyolipwa wewe.
haya mambo yanaumiza watu wengi,

Yaani UTOE RUSHWA WAKATI WA KUKATA LESENI, UTOE RUSHWA WAKATI WA MAKADILIO TRA, UTOE RUSHWA.

Nina wasi wasi sana na watendaji wa Takukuru katika kuhakikisha wanawakamata watendaji waliopo kwenye Halimashauri hasa wale wanao kata Leseni za Biashara lakini pia watendaji waliopo chini ya wizara ya fedha idara ya leseni, bado ukienda TFDA, YAANI POTE AMBAKO serikali imesema tukate leseni online kuna UKIRITIMBA WA HALI YA JUU SANA NA UKIRITIMBA HUO UNAPELEKEA MTU KUSHAWISHIKAKUTOA RUSHWA.

WAZIRI WA FEDHA UPO HAPA TAFADHALI SHUGHULIKANA HILI , WATANZANIA HAWANA SHIDA NA KULIPAKODI TATIZO UKIRITIMBA WENU NI KIKWAZO KIKUBWA.

Takukuru njooni PM tuwasanue wala rushwa maana kama mmeshindwa zinazo tuolewa mkononi hizi za through electronics mtaziweza.
 
"kila nikijaza form collectly kabisa maombi yanakuwa rejected,

Kwa mwandiko huu hata mimi ninakukaanga kisawasawa ba leseni hupati.
 
Hawa wafanyakazi serikalini wasio na maadili na waomba rushwa ndio adui namba moja kwa taifa. Yaani wanakwamisha maendeleo vibaya sana.

Hawa ilifaa tuige mfano wa China, yaani akitambulika na ushahidi kamili basi ni risasi kichogoni. Hii ndio dawa ingepunguza ujinga huu.
 
Back
Top Bottom