Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
918
1,994
Umofia kwenu wakuu,

Wapo watu ambao wanapenda kujua maana au tafsiri za ndoto kwa kuwa nyingi huwa zinakuja kwa mtindo wa mafumbo. Wapo wanaoamini kuwa ndoto zina taarifa zenye miongozo au kutoa tahadhari kwenye mwenendo wa maisha yao ya kila siku. Hivyo kuzielewa kuna maana kubwa sana kwao.

Nimeona ni jambo jema kukusanya mada ambazo zimeshawahi kujadiliwa kwa kina humu JF kuhusiana na Ndoto na Tafsiri zake, ili kuweka urahisi kwa wale ambao wanataka kujua tafsiri ya ndoto zao walizoota, pasi na kuwa na haja ya kuanzisha uzi mpya kuulizia kitu cha aina moja kila uchwao..

Zifuatazo ni mada zenye maswali na majibu kuhusu ndoto mbalimbali ambazo zimeshawahi kujadiliwa humu JF:

Hizi ni ndoto hatari sana maishani mwako..

Ndoto za kupaa na kuelea hewani zinaashiria nini?

Jinamizi ni nini? Kwanini hutokea wakati wa kulala tu?

Msaada: Nimeota nimeenda eneo nisilolijua na kukutana na vitisho

Ndoto za Mapenzi zinanitesa, nifanyeje?

Kuna mahusiano kati ya ndoto na maisha ya kawaida?

Ndoto: Sehemu muhimu kwa afya ya hifadhi ya akili

Ni kipi kilichojificha kwenye ndoto zetu?

Nini tofauti na maana kati ya ndoto na maono?

Kufanya mapenzi ndotoni

Jinsi ya kupata majibu ya swali lolote kirahisi ndotoni...

Tofauti na tafsiri ya kula na kulishwa nyama ndotoni
 
Usiku wa kuamkia leo nimeota ndoto ambayo siyo nzuri sana na imenitisha sana.

Nimeota nimekufa niko ndani ya jeneza kwenda kuzikwa na watu wanalia sana. Ghafla nikashtuka toka usingizini. Nikajaribu kuinua kichwa kikawa kizito baada ya muda kichwa kikaniuma sana.

Naomba unipe tafsiri ya hii ndoto maana imeninyima raha kabisa.

Nawasilisha.
 
Ni ishara ya kufa kiroho kwa mtu aliyekua amesimama katika imani ya KRISTO pia wakati mwingine yawezekana kuna vitu vya shetani vimekufunga ambavyo umewahi kuingia navyo maagano mfano matambiko au kwenda kwa waganga wa kienyeji au hata kurogwa.

Hivyo unapoota uko kwenye jeneza ina maana uko kwenye kifungo fulani ambavyo kinasababisha kushindwa kutimiza lengo la MUNGU kwako hivyo unapewa taarifa ili kwa njia ya maombi wewe mwenyewe au kwa kutumia watumishi wa MUNGU waaminifu ufunguliwe kutoka kwenye maagano hayo ya shetani.

Pia ishara ya kufa ni kuonyesha huwezi kufanikiwa maana shetani amekufunga hivyo hadi utoke kifungoni au kwenye hilo jeneza.

Wapo watu wengi wanashindwa wako kwenye majeneza ya shetani ya magojwa , wengine wako kwenye majeneza ya mikosi, wengine wako kwenye majeneza ya kukataliwa na wachumba yaani kila akipata mchumba wakitaka tu kufunga ndoa anamkataa , wengine wapo kwenye majeneza ya kuonekana wabaya mbele za watu kwa sababu jini shamsu anakua amevaa sura ile ndio maana mke wake au mme wake anampenda kwa muda tu na baada ya muda ni vita, wengine wako kwenye majeneza ya hasira, uongo n.k. na hii chanzo chake ni shetani ambaye katika Yohana 10:10 huwa anakukuja kwa watu ili kuvunja, kuharibu na kuua na kwa kusudi hilo ndio maana Mwana wa MUNGU, YESU KRISTO alidhihirishwa ili azivunje kazi zote za shetani (1 Yohana 3:8b).

Ndugu nenda kwenye maombezi na utakuwa huru mbali na kuonewa na shetani na kwa wewe uliyeokoka ukiona yanakutokea hayo basi tambua kuwa kuna mlango umeufungulia ndio maana unaonewa maana pia kumbuka kuwa MUNGU ni mtakatifu.
 
Dah!! Chief hiyo ndoto maana yake ni ONYO.

1. Kama una deni lipa mara moja kwani mdai wako ameishachoka na ahadi zako sasa anapanga akufanyie kitu mbaya.

2. Kama unamchapia mtu acha mara moja kwani mwenyewe ameanza kunusa hilo.

Kwa niaba ya Profesa mshana jr
 
ni ishara ya kufa kiroho kwa mtu aliyekua amesimama katika imani ya KRISTO pia wakati mwingine yawezekana kuna vitu vya shetani vimekufunga ambavyo umewahi kuingia navyo maagano mfano matambiko au kwenda kwa waganga wa kienyeji au hata kurogwa hivyo unapoota uko kwenye jeneza inamaana uko kwenye kifungo fulani ambavyo kinasababisha kushindwa kutimiza lengo la MUNGU kwako hivyo unapewa taarifa ili kwa njia ya maombi wewe mwenyewe au kwa kutumia watumishi wa MUNGU waaminifu ufunguliwe kutoka kwenye maagano hayo ya shetani. Pia ishara ya kufa ni kuonyesha huwezi kufanikiwa maana shetani amekufunga hivyo hadi utoke kifungoni au kwenye hilo jeneza. Wapo watu wengi wanashindwa wako kwenye majeneza ya shetani ya magojwa , wengine wako kwenye majeneza ya mikosi, wengine wako kwenye majeneza ya kukataliwa na wachumba yaani kila akipata mchumba wakitaka tu kufunga ndoa anamkataa , wengine wapo kwenye majeneza ya kuonekana wabaya mbele za watu kwa sababu jini shamsu anakua amevaa sura ile ndio maana mke wake au mme wake anampenda kwa muda tu na baada ya muda ni vita, wengine wako kwenye majeneza ya hasira, uongo n.k. na hii chanzo chake ni shetani ambaye katika Yohana 10:10 huwa anakukuja kwa watu ili kuvunja, kuharibu na kuua na kwa kusudi hilo ndio maana Mwana wa MUNGU, YESU KRISTO alidhihirishwa ili azivunje kazi zote za shetani (1 Yohana 3:8b). Ndugu nenda kwenye maombezi na utakuwa huru mbali na kuonewa na shetani na kwa wewe uliyeokoka ukiona yanakutokea hayo basi tambua kuwa kuna mlango umeufungulia ndio maana unaonewa maana pia kumbuka kuwa MUNGU ni mtakatifu.
mkuu big up umemjibu vizuri mnooo
 
Usiku wa kuamkia leo nimeota ndoto ambayo siyo nzuri sana na imenitisha sana.
Nimeota nimekufa niko ndani ya jeneza kwenda kuzikwa na watu wanalia sana.Ghafla nikashtuka toka usingizini. Nikajaribu kuinua kichwa kikawa kizito baada ya muda kichwa kikaniuma sana.

Naomba unipe tafsiri ya hii ndoto maana imeninyima raha kabisa.

Nawasilisha.

Kwa asili ya kabila niliyotoka, ndoto mbaya ni ile unaota upo kwenye sherehe!

Pengine hiyo ndto ni kama onyo, kwa jnsi mdau alivyosema ila kwa mwono wangu siyo mbaya!
 
ni ishara ya kufa kiroho kwa mtu aliyekua amesimama katika imani ya KRISTO pia wakati mwingine yawezekana kuna vitu vya shetani vimekufunga ambavyo umewahi kuingia navyo maagano mfano matambiko au kwenda kwa waganga wa kienyeji au hata kurogwa hivyo unapoota uko kwenye jeneza inamaana uko kwenye kifungo fulani ambavyo kinasababisha kushindwa kutimiza lengo la MUNGU kwako hivyo unapewa taarifa ili kwa njia ya maombi wewe mwenyewe au kwa kutumia watumishi wa MUNGU waaminifu ufunguliwe kutoka kwenye maagano hayo ya shetani. Pia ishara ya kufa ni kuonyesha huwezi kufanikiwa maana shetani amekufunga hivyo hadi utoke kifungoni au kwenye hilo jeneza. Wapo watu wengi wanashindwa wako kwenye majeneza ya shetani ya magojwa , wengine wako kwenye majeneza ya mikosi, wengine wako kwenye majeneza ya kukataliwa na wachumba yaani kila akipata mchumba wakitaka tu kufunga ndoa anamkataa , wengine wapo kwenye majeneza ya kuonekana wabaya mbele za watu kwa sababu jini shamsu anakua amevaa sura ile ndio maana mke wake au mme wake anampenda kwa muda tu na baada ya muda ni vita, wengine wako kwenye majeneza ya hasira, uongo n.k. na hii chanzo chake ni shetani ambaye katika Yohana 10:10 huwa anakukuja kwa watu ili kuvunja, kuharibu na kuua na kwa kusudi hilo ndio maana Mwana wa MUNGU, YESU KRISTO alidhihirishwa ili azivunje kazi zote za shetani (1 Yohana 3:8b). Ndugu nenda kwenye maombezi na utakuwa huru mbali na kuonewa na shetani na kwa wewe uliyeokoka ukiona yanakutokea hayo basi tambua kuwa kuna mlango umeufungulia ndio maana unaonewa maana pia kumbuka kuwa MUNGU ni mtakatifu.
Mkuu asante Sana. Hapo labda kurogwa hayo mengine sidhani.
 
Dah!! Chief hiyo ndoto maana yake ni ONYO.
1. Kama unakajipu basi kakamue mwenyewe kabla ya JPM hajatia timu kwani yupo njiani anakuja.
2. Kama una deni lipa mara moja kwani mdai wako ameishachoka na ahadi zako sasa anapanga akufanyie kitu mbaya.
3. Kama unamchapia mtu acha mara moja kwani mwenyewe ameanza kunusa hilo.

Kwa niaba ya Profesa mshana jr
Mkuu sina jipu,sidaiwi wala sitembei na mke wa mtu. Labda Kama kuna mtu ananichezea tu.
 
Kwa asili ya kabila niliyotoka, ndoto mbaya ni ile unaota upo kwenye sherehe!

Pengine hiyo ndto ni kama onyo, kwa jnsi mdau alivyosema ila kwa mwono wangu siyo mbaya!

Wewe ni mtu wa tatu unaniambia hili. Shukrani.
 
Una vita kubwa katika ulimwengu wa kiroho ni ishara kuna watu wanapambana na wewe ili kukuangamiza kwa maana ingine kuna roho ya mauti inakutafuta, dunia tunayoishi ni hatari kuliko tunavyodhani ila kila kitu kwa wenye imani ya kikristo inakuwa rahisi sana kwa kufanya yafuatvyo...Mkabidhi Bwana Yesu maisha yako kwani yeyey ndo muweza wa yote kabla hujalala fanya sala fupi tu ya kujitakasa na kuomba ulinzi kutoka kwake...Asubuh kabla hujaamka mshukuru Bwana Yesu kwa ulinzi wa usiku pia mkabidhe siku yako hiyo mpya aweze kuwa kiongozi wako...Hakika hutoota tena ndoto hizo.
 
mwamini sana MUNGU mwambie MUNGU apambane naye anaye pambana na wewe. sawa kibinadamu lazima uwoga ukushike kutokana na ulichoota lakini ndoto isikunyong'onyeze ukakosa furaha kwani tayari umesha ota.
 
Similar Discussions

10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom