Tafsiri ya ndoto

Tafsiri ya ndoto

Joined
May 6, 2026
Posts
46
Reaction score
107
Habarini wana jamvi.... natumai mpo wazima kabisa..

Kuna kipindi nilikuwa katika changamoto fulani za kimaisha (ni kawaida katika maisha kupitia milima and mabonde). Sasa, nilipambana sana kuweka mambo sawa lakaini ngoma bado ikawa ngumu.... kwakuwa nilikuwa msomaji sana wa Biblia na vitabu vingine vya imani... nikakumbuka baadhi ya maandiko ambayo yanasema kifunga(fasting) kunaweza mfungua mtu na vifungo mbalimbali anavyopitia katika maisha.....daaah!,, nikasema sasa hapa sinabudi kurejea kwa Mungu kwa kufunga na kusali...

Basi mwanaume nikajitenga na chakula na baadhi mambo kwa muda fulani... kweli bana, baadhi ya mambo yakaanza kufunguka,

jambo la La kushangaza " nikaanza kuota ndoto ambazo nashundwa kabisa kuelewa maana yake," jambo la ajabu siku ya mwisho ya mfungo wangu niliota ndoto ya ajabu sana.. nilioata nafanya mapenzi, tena chooni, na mtu ambaye namfahamu ambapo baada ya muda watu wakapita wakiwa kwenye gari wakatuona", by the way alikuaga mchepuko.. lakini niliamua kuachana nae muda kidogo maana niliamuaga kutulia...

Sasa "minister Mshana Jr " (naomba nikuite hilo jina).... uje hebu unipe ilimu kuhusiana na hiyo ndoto maana nimejaribu kupotezea lakini bado inanisumbua sana kichwani
 
Iko hivi unapopambana kiroho unaua tabia asili za mwilini' sasa kwa vile ulikuwa kwenye kuukatalia mwili mazoea mabaya ya dhambi adui hakufurahi akakuletea mashambulizi kwa njia ya ndoto, kiroho ulitenda zinaa ndotoni sawasawa kabisa na mwilini ilihitajika uendelee na hiyo vita mpaka ushinde hadi ndotoni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom