Taasisi ya moyo Jakaya Kikwete: Kunyweni angalau bia tatu tu kwa siku

Kizazi hiki bana. Si wawarahihishie tu wanywaji kua wanywe tani yao au wasinywe kabisa. Sasa bia tatu ndio Nini sasa
 
Asilimia kubwa ya wanaolazwa hospitali ni wagonjwa wa moyo na shinikizo la damu,” amesema

Dk Kisenge ameshauri jamii kuzingatia kula lishe bora hasa mboga za majani na matunda, kupunguza vyakula vya wanga na sukari.

"Unywaji bia, angalau mnywaji anywe bia tatu kwa siku,” amesema

Mkurugenzi huyo amesema Watanzania wawe na kawaida ya kucheki afya zao mapema hii inasaidia kujijua na kupunguza madhara. Kwenye banda letu tunatoa huduma hizo na elimu ya afya ya moyo

Katika banda hilo pia wanatoa huduma ya tiba utalii ambayo imekuwa ikifanyika kwenye Taasisi na zaidi ya nchi 20 zimekwisha itembelea JKCI kufanya utalii huo wa matibabu.

"Taasisi ya JKCI imekuwa na uwekezaji wa vifaa vya upasuaji ambavyo unaweza kulinganisha na nchi yoyote kubwa duniani ambazo zinatoa huduma ya moyo.

"Tunapata watu mbalimbali kutoka nje na ndani ya nchi na hivi karibuni tulipokea watu kutoka Malawi waliokuja kuona huduma, kwenye maonyesho haya kuna nchi zaidi ya 47 hivyo tunayatumia pia kutoa huduma”

Mlele Mrisho Said ambaye ni miongoni mwa waliokwenda kupata huduma kwenye banda la JKCI amesema haikumchukua muda mrefu kupata huduma.

"Nilipewa maelekezo kwa dakika tano, kisha nikaenda kuwaona wahudumu kwa dakika tano, na kupanga foleni ya kuingia kwa daktari, huduma ni bure na baadhi unalipia kidogo sana, niliamua tu kuja kucheki afya na nimekuta presha imeshuka.”

Gazeti la mwananchi 10/07/2023
 
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), imeshauri jamii kupenda kufanya mazoezi, kupunguza kula vyakula vya sukari, wanga na kusisitiza kwa wanywaji wa bia, kunywa angalau tatu kwa siku ili kujilinda na ugonjwa wa moyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk Peter Kisenge amesema hayo leo Jumatatu Julai 10, 2023 katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (Sabasaba).

Amesema kuna ongezeko la wagonjwa wa moyo nchini.

"Asilimia kubwa ya wanaolazwa hospitali ni wagonjwa wa moyo na shinikizo la damu,” amesema

Dkt. Kisenge ameshauri jamii kuzingatia kula lishe bora hasa mboga za majani na matunda, kupunguza vyakula vya wanga na sukari.

"Unywaji bia, angalau mnywaji anywe bia tatu kwa siku,” amesema.

Mkurugenzi huyo amesema Watanzania wawe na kawaida ya kucheki afya zao mapema hii inasaidia kujijua na kupunguza madhara. Kwenye banda letu tunatoa huduma hizo na elimu ya afya ya moyo.
MMH N BEER JAMAAN SIO SMARTGIN WALA DOUBLE KICK XENU AMA HI GH LIFE NARUDIA BEEER
 
1689043768177.png

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), imeshauri jamii kufanya mazoezi, kupunguza kula vyakula vya sukari, wanga na kupunguza unywaji wa pombe uliokithiri ili kujilinda dhidi ya ugonjwa wa moyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk Peter Kisenge amesema hayo leo Jumatatu Julai 10, 2023 katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), Dar es Salaam.

“Niwaombe Watanzania wazingatie kufanya mazoezi kutokuvuta sigara kutokunywa pombe zilizokithiri kwa sababu inachangia magonjwa ya moyo na kuepuka unene uliokithiri.

“Tuache kuvuta siagara na kupunguza unywaji wa pombe, tusinywe zaidi ya bia chupa tatu tusizidishe kwa siku hii itatusaidia sana kupunguza haya magonjwa ya moyo,” amesema Dk Kisenge na kuongeza, "asilimia kubwa ya wanaolazwa hospitali ni wagonjwa wa moyo na shinikizo la damu."

Dk Kisenge ameshauri jamii kuzingatia lishe bora hasa mboga za majani na matunda, kupunguza vyakula vya wanga na sukari.

Mkurugenzi huyo amewataka Watanzania kujenga tabia ya kuangalia afya zao mara kwa mara na kupata tiba mapema kwa akisema inasaidia kujijua na kupunguza madhara. "Kwenye banda letu tunatoa huduma na elimu ya afya ya moyo. Pia tunatoa huduma ya tiba utalii ambayo imekuwa ikifanyika na zaidi ya nchi 20 zimekwishaitembelea JKCI kufanya utalii huo wa matibabu.

"Taasisi ya JKCI imekuwa na uwekezaji wa vifaa vya upasuaji ambavyo unaweza kulinganisha na nchi yoyote kubwa duniani ambazo zinatoa huduma ya moyo.

"Tunapata watu mbalimbali kutoka nje na ndani ya nchi na hivi karibuni tulipokea watu kutoka Malawi waliokuja kuona huduma.

Amesema kwenye maonyesho hayo kuna nchi zaidi ya 47 na kwamba JKCI inayatumia pia kutoa huduma.

Mlele Mrisho Said ambaye ni miongoni mwa waliokwenda kupata huduma kwenye banda la JKCI amesema haikumchukua muda mrefu kupata huduma.

"Nilipewa maelekezo kwa dakika tano, kisha nikaenda kuwaona wahudumu kwa dakika tano na kupanga foleni ya kuingia kwa daktari, huduma ni bure na baadhi unalipia kidogo sana, niliamua tu kuja kucheki afya na nimekuta presha imeshuka.”

MWANANCHI
 
View attachment 2684451

Ahsante kwa ushauri swala la idadi tuachie sisi
 
"Tuache kuvuta sigara na kupunguza unywaji wa pombe, tusinywe zaidi ya bia chupa tatu tusizidishe kwa siku hii itatusaidia sana kupunguza haya magonjwa ya moyo,” amesema Dk Kisenge na kuongeza, "asilimia kubwa ya wanaolazwa hospitali ni wagonjwa wa moyo na shinikizo la damu."

Kwenye hayo maelezo ya daktari ni wapi kasema tunywe angalau chupa tatu kwa siku?
 
Back
Top Bottom