Taasisi ya moyo Jakaya Kikwete: Kunyweni angalau bia tatu tu kwa siku

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,035
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), imeshauri jamii kupenda kufanya mazoezi, kupunguza kula vyakula vya sukari, wanga na kusisitiza kwa wanywaji wa bia, kunywa angalau tatu kwa siku ili kujilinda na ugonjwa wa moyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk Peter Kisenge amesema hayo leo Jumatatu Julai 10, 2023 katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (Sabasaba).

Amesema kuna ongezeko la wagonjwa wa moyo nchini. "Asilimia kubwa ya wanaolazwa hospitali ni wagonjwa wa moyo na shinikizo la damu,” amesema

Dkt. Kisenge ameshauri jamii kuzingatia kula lishe bora hasa mboga za majani na matunda, kupunguza vyakula vya wanga na sukari. "Unywaji bia, angalau mnywaji anywe bia tatu kwa siku,” amesema.

Mkurugenzi huyo amesema Watanzania wawe na kawaida ya kucheki afya zao mapema hii inasaidia kujijua na kupunguza madhara. Kwenye banda letu tunatoa huduma hizo na elimu ya afya ya moyo.

======

1689043768177.png

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), imeshauri jamii kufanya mazoezi, kupunguza kula vyakula vya sukari, wanga na kupunguza unywaji wa pombe uliokithiri ili kujilinda dhidi ya ugonjwa wa moyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk Peter Kisenge amesema hayo leo Jumatatu Julai 10, 2023 katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), Dar es Salaam.

“Niwaombe Watanzania wazingatie kufanya mazoezi kutokuvuta sigara kutokunywa pombe zilizokithiri kwa sababu inachangia magonjwa ya moyo na kuepuka unene uliokithiri.

“Tuache kuvuta siagara na kupunguza unywaji wa pombe, tusinywe zaidi ya bia chupa tatu tusizidishe kwa siku hii itatusaidia sana kupunguza haya magonjwa ya moyo,” amesema Dk Kisenge na kuongeza, "asilimia kubwa ya wanaolazwa hospitali ni wagonjwa wa moyo na shinikizo la damu."

Dk Kisenge ameshauri jamii kuzingatia lishe bora hasa mboga za majani na matunda, kupunguza vyakula vya wanga na sukari.

Mkurugenzi huyo amewataka Watanzania kujenga tabia ya kuangalia afya zao mara kwa mara na kupata tiba mapema kwa akisema inasaidia kujijua na kupunguza madhara. "Kwenye banda letu tunatoa huduma na elimu ya afya ya moyo. Pia tunatoa huduma ya tiba utalii ambayo imekuwa ikifanyika na zaidi ya nchi 20 zimekwishaitembelea JKCI kufanya utalii huo wa matibabu.

"Taasisi ya JKCI imekuwa na uwekezaji wa vifaa vya upasuaji ambavyo unaweza kulinganisha na nchi yoyote kubwa duniani ambazo zinatoa huduma ya moyo.

"Tunapata watu mbalimbali kutoka nje na ndani ya nchi na hivi karibuni tulipokea watu kutoka Malawi waliokuja kuona huduma.

Amesema kwenye maonyesho hayo kuna nchi zaidi ya 47 na kwamba JKCI inayatumia pia kutoa huduma.

Mlele Mrisho Said ambaye ni miongoni mwa waliokwenda kupata huduma kwenye banda la JKCI amesema haikumchukua muda mrefu kupata huduma.

"Nilipewa maelekezo kwa dakika tano, kisha nikaenda kuwaona wahudumu kwa dakika tano na kupanga foleni ya kuingia kwa daktari, huduma ni bure na baadhi unalipia kidogo sana, niliamua tu kuja kucheki afya na nimekuta presha imeshuka.”

MWANANCH
 
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), imeshauri jamii kupenda kufanya mazoezi, kupunguza kula vyakula vya sukari, wanga na kusisitiza kwa wanywaji wa bia, kunywa angalau tatu kwa siku ili kujilinda na ugonjwa wa moyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk Peter Kisenge amesema hayo leo Jumatatu Julai 10, 2023 katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (Sabasaba).

Amesema kuna ongezeko la wagonjwa wa moyo nchini.

"Asilimia kubwa ya wanaolazwa hospitali ni wagonjwa wa moyo na shinikizo la damu,” amesema

Dkt. Kisenge ameshauri jamii kuzingatia kula lishe bora hasa mboga za majani na matunda, kupunguza vyakula vya wanga na sukari.

"Unywaji bia, angalau mnywaji anywe bia tatu kwa siku,” amesema.

Mkurugenzi huyo amesema Watanzania wawe na kawaida ya kucheki afya zao mapema hii inasaidia kujijua na kupunguza madhara. Kwenye banda letu tunatoa huduma hizo na elimu ya afya ya moyo.
kwenye suala la bia wakatoliki watapinga tu
ukiwa na akili iliyo sawasawa utajua mambo yao hovyo, uawaletea shida
 
Wewe utakuwa umemwelewa vibaya. Bia haziwezi kuzidi 3 kwa siku kwa mwanaume. Na ziwe zile ndogo na light...
 
stress zinaondolewa kwa bia tatu? Aloo achen masihara na simba bado hamjawapata...bora anitafune nikiwa mbwii...
 
angalau...... kwa uchache........atleast. kwahiyo ni vema tunywe zaidi ya 3 kwa siku like 5, 8 or 10 bia ili mioyo yetu iponyeke!!!!! Ufafanuzi please!
 
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), imeshauri jamii kupenda kufanya mazoezi, kupunguza kula vyakula vya sukari, wanga na kusisitiza kwa wanywaji wa bia, kunywa angalau tatu kwa siku ili kujilinda na ugonjwa wa moyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk Peter Kisenge amesema hayo leo Jumatatu Julai 10, 2023 katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (Sabasaba).

Amesema kuna ongezeko la wagonjwa wa moyo nchini.

"Asilimia kubwa ya wanaolazwa hospitali ni wagonjwa wa moyo na shinikizo la damu,” amesema

Dkt. Kisenge ameshauri jamii kuzingatia kula lishe bora hasa mboga za majani na matunda, kupunguza vyakula vya wanga na sukari.

"Unywaji bia, angalau mnywaji anywe bia tatu kwa siku,” amesema.

Mkurugenzi huyo amesema Watanzania wawe na kawaida ya kucheki afya zao mapema hii inasaidia kujijua na kupunguza madhara. Kwenye banda letu tunatoa huduma hizo na elimu ya afya ya moyo.
Ngoja tumsikie na Janabi kwanza anasemaje kuhusu hili
 
Back
Top Bottom