Geita: Watu 500 wafanyiwa vipimo vya magonjwa ya moyo, kati yao 290 wagundulika kuwa na changamoto

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) tayari wamewapima watu 500 ambapo kati ya hao 290 wamegundulika kuwa na changamoto mbalimbali za magonjwa ya moyo.

Takwimu hiyo ikiwa ni siku ya sita toka kuanza kwa maonesho ya madini ya Teknolojia yanayofanyika katika viwanja vya Bombambili mkoani Geita.
IMG-20230927-WA0257.jpg

Mwananchi wa Mkoa wa Geita na mikoa ya jirani akipata huduma katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa maonesho ya sita ya kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita. JKCI inatoa huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo, Sukari kwenye damu na shinikizo la damu katika maonesho hayo. Picha zote na: JKCI

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo JKCI, Dk. Saleh Mwinchete ndiye aliyetoa taarifa hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika banda lao.
IMG-20230927-WA0256.jpg

Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Salehe Mwinchete akimpima jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiograph – ECHO) mkazi wa Geita wakati wa maonesho ya sita ya kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita. JKCI inatoa huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo, Sukari kwenye damu na shinikizo la damu katika maonesho hayo.

Dk. Mwinchete amesema wanashiriki katika maonesho ya madini kwaajili ya kliniki maalum ya watu mashuhuri kwa lengo la kutoa huduma na elimu kwa washiriki na wananchi.Amesema JKCI wanafahamu kuwa kuna changamoto ya uelewa wa maradhi ya moyo katika nchini na visababishi vinavyosababisha maradhi ya moyo.
 
Vipi mbona trending ni moyo, figo, mifupa, kansa na kisukari, vipi mbona hatusikii trending ya UKIMWI? Au hali ni mbaya inatisha maambukizi yako juu kiasi cha kutotangazwa ni kitisho kwa watu?
 
Back
Top Bottom