Taasisi ya Moyo (JKCI) yafafanuzi madai ya kuchezea mifumo ya NHIF ili baadhi ya Dawa ionekane hazipo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Awali Member wa JamiiForums.com anadai baadhi ya Maafisa wa Afya wamekuwa wakichezea mifumo ili ionekane baadhi ya Dawa na Huduma hazipo kwenye vituo vyao wakati Wanufaika wa Bima ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wanapohitaji, akitoa mfano hali hiyo imetokea katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Dar es Salaam

Kusoma hoja ya Mdau ni hapa = Maafisa wa Taasisi ya Moyo wanachezea mifumo ya Bima ionekane baadhi ya Dawa hazipo katika Bima ya NHIF
Snapinsta.app_430890789_777180504315919_3160546507527059445_n_1080.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dkt. Peter Kisenge
Akijibu madai hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dkt. Peter Kisenge amesema:

Utaratibu mpya wa NHIF unaelezea kufuata muongozo ambao umewekwa, mfano Dawa ziwe za aina fulani, baadhi ya Dawa zikaondolewa kwenye orodha na kuelekezwa nyingine, yaani kilichofanyika ni mabadiliko ya ‘brand’ ya jina tu lakini Dawa inakuwa ni ileile.

Hivyo, mgonjwa anaweza kuwa anatumia dawa X akienda Hospitali anaandikiwa Dawa XY, umuhimu wake na aina ya Dawa ni ileile kasoro 'brand name' tu ndio imebadilika.

Kingine ni mazoea, unakuta kuna mtu amezoea Dawa fulani, so akiandikiwa Dawa nyingine hata kama matumizi ni yaleyale ni ngumu kukubali.

Pia kuna Dawa ambazo zina gharama kubwa na nyingine zipo za bei ya kawaida lakini matumizi ni yaleyale, hivyo zile za gharama kubwa ndizo ambazo zimeondolewa kwa kuwa kuendelea kutumia Dawa hizo wakati zipo za kawaida ni matumizi mabaya ya mfuko.

Hali hiyo ikiendelea mfuko unaweza kuyumba na hatimaye kukwama na mwisho Watanzania wengi wataathirika. Mfuko hauwezi kununua Dawa za ghali wakati zile za kawaida ambazo nzo zinatibu ugonjwa uleule zipo.

Upande wetu (JKCI) tutaendelea kutoa somo kwa wanaohitaji huduma, kilichotokea kama kilichoandikwa na huyo Mdau inawezekana ni suala la mawasiliano kati ya watumishi na Mgonjwa.

Kuna wakati inaweza kuwa ngumu kutoa maelezo kwa watu wengi, unakuta mtoa maelezo anaweza kuwa kazungukwa na watu wengi hivyo anashindwa kutoa maelezo.

Kuhusu kuandika orodha ya dawa hospitalini, hii ipo au haipo ni vigumu kubandika matangazo ya aina hiyo kwa kuwa sio sawa kimaadili.

Kuhusu changamoto kama hizo za kuandikwa mitandaoni yataendelea kuandikwa kwa kuwa elimu bado haijawafikia wengi, hivyo ni jukumu letu sote kama taasisi kuendelea kutoa elimu lakini hilo la kundikwa haliwezi kuzuilika.
 
Long Live JF
 
Dr Peter Kisenge najua hayo maneno uliyosema hayatoki moyoni ila unalazimika kusema kwa sababu huna namna..
Pole sana
 
Inasikitisha Dr/Mtaalamu anapoongea kisiasa na kusahau kuwa kuna Dr's waliowahi kuwepo hapo yeye alipo Leo na hawezi kuwadanganya chochote kuhusu magonjwa na matibabu yake
 
Back
Top Bottom