Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,603
Umuofia kwenu....!
Kati ya mwaka 2018 na 2020 Tanzania ilipitia changamoto za uhaba mkubwa wa Cement na bei kuanza kupanda kiholela. Lakini baada ya kulifuatilia suala lile, nikaja kugundua kwamba, kuadimika na kupanda kiholela kulisababishwa Zaidi na utekelezaji wa miradi mikubwa ya ujenzi kipindi cha utawala wa Magufuli. Kwahiyo upungufu ulijitokeza kwa sababu ‘internal capacity’ ya kutengeneza cement ilikuwa ni ndogo na isingeweza kumudu ongezeko kubwa la demand ambayo ilitokana na mahitaji ya cement kwenye miradi mikubwa ya serikali. Kwa maana hiyo, Cement nyingi ikawa inauzwa kwa makampuni ya ujenzi na kidogo sana ikawa inaenda mtaani kwa wananchi, na ndio haswa ikaleta lile janga la cement kipindi kile cha Magufuli Serikali haiwezi kukwepa lawama ya kuadimika na kupanda kwa bei ya Saruji nchini. Waziri wa Viwanda ana kazi sana, kuna janga linatunyemelea
Baada ya kutafiti matukio yaliyotokea kwenye cement, nikaja kugundua ya kwamba, uchumi wa Tanzania unakosa kitu kwenye uchumi tunakiita ‘space capacity’. Yaani kwa tafsiri ya yake ni kwamba ‘space capacity’ ni ule uwezo au utayari wa sekta za kiuchumi kama viwanda, kuweza na kuendana na kasi ya mabadiliko ya haraka ambayo yanatokea kwenye uchumi bila kuwa na mtanziko kwenye soko mfano uhaba wa bidhaa au huduma.
Ukiangalia kwa sasa, kwenye sekta ya cement, pamoja na ongezeko la haraka la uchumi kwa miaka miwili iliyopita, hali imekuwa ni ya usatahimilivu, na naweza kuvipa hongera viwanda vya cement na waagizaji wa cement kwa kuhakikisha hakuna mtanziko kwenye upatikanaji wa cement kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma.
Kwa upande mwingine imekuwa rahisi sana kwa sekta ya cement kustabilize kwasababu sekta yenyewe ni huria, kwa maana ya kwamba kuna players wengi kwenye sekta. Mtu kama Dangote ana capacity kubwa sana ya kuzalisha, na inawezekana kwa sasa Tanzania, space capacity kwenye cement industry ipo kubwa nay a kutosha, ndo maana husikii kelele za kuadimika kwa Cement. Hiyo ndio faida ya soko huria kwenye uchumi ambayo naona ndio inakosekana kwenye umeme.
Umeme
Kinachotokea kwenye umeme hakitofautiana sana na kilichotokea kwenye cement kipindi cha Magufuli kwenye miaka ya 2018 mpaka 2020. Na inatupeleka kule kule kwenye hoja ya kupishana speed kati ya mahitaji (demand) na uzalishaji (supply) kwenye uchumi.
Mwezi mmoja uliopita nilikuja na huu uzi Miezi 30 ya Rais Samia madarakani: Pamoja na kujikwaa kwenye Bandari, bado ni Rais mwenye record bora ya kukuza uchumi wa Tanzania kwa kipindi kifupi ambao nilijaribu kuchambua na kuonesha hali ya ukuaji wa uchumi kwa miaka hii miwili ya Rais Samia ambao mimi mpaka sasa, bado nashikilia msimamo kwamba kumekuwa na ongezeko maradufu kwenye shughuli za kiuchumi nchini, na hiyo inaweza uwa bayana kwa kuangalia baadhi ya viashiria vingi tu ambavyo nilivielezea kwa upana. Hata hichi cha ukuaji wa uzalishaji wa cement kikiwa pia kimojawapo.
Kwanza kabisa, kwa manufaa ya wengi, pamoja na nchi kuwa kwenye mgao mkali ambao binafsi sijawahi kuushuhudia, ukirejelea takwimu za hivi karibuni kwenye ‘supply ya umeme Tanzania’, utagundua ya kwamba, kati ya June 2021 mpaka June 2023, wastani wa supply ya umeme Tanzania kwa mwezi iliongezeka kwa asilimia 39.5% - kutoka kWh 617 millioni kwa mwezi June 2021 mpaka kWh 861 millioni kwa mwezi June 2023.
Hivo, ni wazi kabisa kwamba tatizo la umeme linalojitokeza sasahivi lipo ‘driven’ Zaidi na demand side pressure, yaani, ongezeko la mahitaji limekuwa kubwa maradufu kushinda ongezeko la TANESCO ku supply umeme ili ku meet demand. Kwamba ni kweli TANESCO wanajitahidi, lakini mbio zao ni speed ya Km 60 kwa saa wakati mahitaji yanakimbia kwa speed ya Km 80 kwa saa, lazima TANESCO atashindwa vita. Na huu ni mwanzo tu wa mbio.
Utatuzi pekee hapa na wa maana ni endapo ‘space capacity’ itaweza kupatikana. Lakini ukifuatilia maneno ya serikali, ni kwamba bado wanaishi kwenye ulimwengu wa ahadi na matumaini kwamba ‘Bwawa la Nyerere likikamilika basi shida hii itatatuliwa’, au utasikia ‘Mvua zikinyesha shida hii ya umeme itatatuliwa’.
Miaka 10 iliyopita, Prof Sospeter Muhungo, alikuwa anasema maneno hayo hayo, kwamba sijui Tanzania itaanza kuuza umeme nje ya nchi. Kwahiyo, inakupa picha kwamba, serikali yenyewe kwa miaka kumi iliyopita na hata sasa bado hawana plan ya kuwa na ‘space capacity’ kwenye umeme wa uhakika, zaidi maneno matupu na mbambamba.
Lakini wanasiasa wa Tanzania wanazidi kutoa ahadi nyingi za kuboresha upatikanaji wa umeme na kusahau kwamba TANESCO yenyewe kama kampuni haipo tena kiushindani, na ni shirika ambalo tunaliita ni ‘deadhorse’ ama Farasi aliyekufa. Na itakuwa ni kuendelea kujidanganya kuwa na ndoto za kuinua uchumi wa hii nchi kwa kuendelea kuamini utendaji wa shirika dhaifu kama hili.
Ukiangalia baadhi ya hizo number hapo juu, unaona kabisa kwamba kwa hali ilivo, TANESCO haina muscles za ku kuhimili ongezeko kubwa la ukuaji wa mahitaji ya umeme, kwa sababu shirika linajiendesha bila ufanisi hata faida ni kama vile haipo.
Ukiangalia current liabilities za kampuni bado ni kubwa maradufu kuzidi current assets na hizo current liabilities zinaongezeka mwaka hadi mwaka. Maana yake ni kwamba uwezo wa TANESCO kulipa suppliers wake kwasasa ni mdogo kitu ambacho kinaturudisha kule kule kwamba, TANESCO haina tena uwezo kugharamia shughuli yake ya muhimu ya kugenerate umeme kadri inavyotaka ili kukidhi mahitaji ya soko kwasababu haioneshi uwezo wa kuwalipa wazabuni wake kwa wakati.
Kingine, ukuangalia, hapo kwenye hicho kinachoitwa free cash flow, kwa miaka mitatu imekuwa ipo negative kwa wastani wa Zaidi ya Trilioni moja kila mwaka. Hiyo inakuambia ya kwamba, TANESCO ni shirika ambalo halina tena uwezo wa kugenerate cash lenyewe kama lenyewe. Kwa kigezo hiki, japo sijui huko serikalini kunaendelea kitu gani, ni wazi serikali kwa hii miaka miwili iliyopita wameipatia TANESCO fedha nyingi sana ili ku support kampuni kujiendesha.
Performance hiyo ya TANESCO mimi ndo huwa kila siku najiuliza, inakuwaje serikali wanazidi kuona kwamba TANESCO wana uwezo wa kufanya mapinduzi kwenye sekta ya umeme? Maana kwa wenye uzoefu wa biashara, ukiwa na kampuni la dizaini hii, maana yake ni mgonjwa ambaye yupo mahutihuti. Halafu eti, mgonjwa huyo huyo unamuweka awe mlinzi wa nyumbani. Yaani hii nchi kuna watu wanastahili kabisa kupimwa akili.
Maana mimi binafsi naiona TANESCO kama kitisho kwenye uchumi kwa sasa. Suluhisho la kudumu ambalo halikwepeki, ni kuifumua TANESCO na kuisuka upya.
The best structure ninayoiona mimi na ambayo nimekuwa nikiifikiria, ni kuwepo kwa soko huria kwenye sekta nzima ya umeme. Hii TANESCO inatakiwa kumegwa na kutengeneza makampuni kama matatu.
Lakini kama watawala wanazidi kuona hakuna haja, kuna siku yaja hili shirika litaangusha huu uchumi na kuturudisha nyuma miaka 5.
Tumechoka hizi ahadi za uwongo kila siku mawaziri kuendelea kutudanganya kwamba Tanzania itauza umeme nje ya nchi bila kutuambia itawezaje.
TANESCO ni kitisho namba moja kwa uchumi na usalama wa nchi, ifumuliwe harakaaaaa.
Wasalaaaam
N.Mushi

TSh. Million | Jun-19 | Jun-20 | Jun-21 |
Revenue | 1,535,040 | 1,564,353 | 1,658,235 |
Profit before Tax | 45,094 | 43,891 | 54,845 |
Current Assets | 434,962 | 1,465,420 | 1,918,525 |
Current Liabilities | 1,972,800 | 2,884,503 | 3,250,450 |
Free cash flow | (2,229,212) | (335,011) | (1,452,405) |