Je, Kuna Taasisi ya ovyo Kabisa Nchini Kuizidi TANESCO?

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,547
41,058
Bila shaka hakuna asiyejua madhara ya TANESCO, iwe mjini au kijijini, awe kiongozi au raia asiye na cheo, awe kijana au mzee, awe msomi au asiyeenda shule kabisa, awe mwenye kiwanda au mmiliki wa genge.

Ni takribani miaka 250 tangu Benjamin Franklin na Michael Faraday walipoweka kanuni jinsi umeme unavyozalishwa na unavyofanya kazi, lakini mpaka leo Tanzania haielewi chochote hata kwa vile vinavyoonekana kwa macho, kuhusiana na umeme. Uzalishaji wa umeme ni kati ya tekinolojia rahisi za kiwaida isiyohitaji elimu na tekinolojia ya pekee, lakini kwa Tanzania, hata kufunga tu wire au kuchomeka nguzo vizuri ya umeme ardhini ili isidondoke, inaonekana ni tekinolojia ngumu sana!!!

Mtanisahihisha, lakini kwa mtazamo wangu, TANESCO ni taasisi muhimu sana ambayo ubora au ubovu wake unagusa kila mahali katika maisha ya Mtanzania. Lakini kwa bahati mbaya sana, taasisi hii iliyo muhimu kabisa, bila shaka wamepewa watu wa hovyo kabisa, wenye uelewa duni kabisa, watu wazembe kabisa ambao upeo wao wa kuona mambo unaishia kwenye vidole vyao vya miguuni. Ukiwaona mitaani ya yale makoti yao unaweza kudhani wanafanya kazi, lakini kwa kiasi kikubwa wanazurura tu bila kuleta matokeo yoyote chanya.

Kuanzia Wizarani ambako kuna waziri, mpaka huko chini kwa wahandisi na mafundi, kote kumejaa watu waongo wanaotaka kuficha ubovu wao kwa kutengeneza hadithi za uwongo. Badala ya kutumia muda mwingi kufikiria namna ya kumaliza matatizo ya umeme, wao muda wote wanafikiria namna ya kutengeneza uwongo.

Miezi miwili iliyopita niitembelea vijiji 4 ambavyo vinatumia umeme kutoka kwenye mradi uliofadhiliwa na Kanisa Katoliki. Katika mwezi mzima, nilishuhudia umeme kukatika mara 2, na mara zote, haikuzidi nusu saa. Mradi huo unaendeshwa na wanakijiji wenyewe, na viongozi na watendaji wote wa mradi, hakuna mhandisi wala mfanyakazi yeyote mwenye hata degree moja. Lakini umeme ni wa uhakika.

Kwa aina ya watu waliopo wizara ya nishati mpaka hao waliopo TANESCO, nawahakikishieni, hata bwawa la Nyerere lianze kufanya kazi, hakuna kitakachobadilika. Maana tatizo kubwa halipo kwenye vyanzo vya umeme bali aina ya watu waliopo.

Muda huu ninaoandika, nimewasiliana na watu mbalimbali na kuthibitishiwa kuwa maeneo mengi ya nchi hakuna umeme.

Tujiulize, hivi watu waliyopo huko TANESCO wana uhalali gani wa kuendelea kuwatesa Watanzania kiasi hiki? Na mamlaka za juu, kwa nini zinaamua kuwatesa Watanzania kupitia TANESCO kwa kuwaweka watu ambao kwa kipimo chochote, hawafai na ni hasara kwa Taifa zima? Na sisi wananchi tutaendelea kuwavumilia hawa watu mpaka lini?

Kuna haja ya kuandaa maandamano makubwa dhidi ya TANESCO na watawala. Watawala muda huu ambao sehemu kubwa ya nchi ipo gizani, watawala wamewashiwa generators. Hawana giza.
 
Hao Ndo mwanzo wa mdororo mkubwa wa kiuchumi hapa nchini pmj na viongozi wa serikalini......mbaya Zaidi wanatuaminisha kuwa nchi kuwa ya wachuuzi Ni bora Zaidi kuliko kuwa ya viwanda kisa wanakusanya kodi nyingi kutoka kwa wafanyabiashara

Nakubaliana Nawe kuwa hii Ni taasisi ya hovyo Sana sana
 
Kama kweli Tanzania itapata maendeleo bila ya umeme, basi itakuwa maajabu ya kwanza Duniani yatakayozunguzwa kwa miaka mingi ijayo, na Dunia watalazimika kuja kujifunza toka kwetu.

Wiki 3 zilizopita nimezungukia nchi 4 za Afrika, hakuna hata nchi moja niliyoiona ina hali kama hii ya Tanzania kwenye suala la umeme.
 
Tulia twiga yuko kazini

OIG1 (1).jpeg
 
Bila shaka hakuna asiyejua madhara ya TANESCO, iwe mjini au kijijini, awe kiongozi au raia asiye na cheo, awe kijana au mzee, awe msomi au asiyeenda shule kabisa, awe mwenye kiwanda au mmiliki wa genge.

Ni takribani miaka 250 tangu Benjamin Franklin na Michael Faraday walipoweka kanuni jinsi umeme unavyozalishwa na unavyofanya kazi, lakini mpaka leo Tanzania haielewi chochote hata kwa vile vinavyoonekana kwa macho, kuhusiana na umeme. Uzalishaji wa umeme ni kati ya tekinolojia rahisi za kiwaida isiyohitaji elimu na tekinolojia ya pekee, lakini kwa Tanzania, hata kufunga tu wire au kuchomeka nguzo vizuri ya umeme ardhini ili isidondoke, inaonekana ni tekinolojia ngumu sana!!!

Mtanisahihisha, lakini kwa mtazamo wangu, TANESCO ni taasisi muhimu sana ambayo ubora au ubovu wake unagusa kila mahali katika maisha ya Mtanzania. Lakini kwa bahati mbaya sana, taasisi hii iliyo muhimu kabisa, bila shaka wamepewa watu wa hovyo kabisa, wenye uelewa duni kabisa, watu wazembe kabisa ambao upeo wao wa kuona mambo unaishia kwenye vidole vyao vya miguuni. Ukiwaona mitaani ya yale makoti yao unaweza kudhani wanafanya kazi, lakini kwa kiasi kikubwa wanazurura tu bila kuleta matokeo yoyote chanya.

Kuanzia Wizarani ambako kuna waziri, mpaka huko chini kwa wahandisi na mafundi, kote kumejaa watu waongo wanaotaka kuficha ubovu wao kwa kutengeneza hadithi za uwongo. Badala ya kutumia muda mwingi kufikiria namna ya kumaliza matatizo ya umeme, wao muda wote wanafikiria namna ya kutengeneza uwongo.

Miezi miwili iliyopita niitembelea vijiji 4 ambavyo vinatumia umeme kutoka kwenye mradi uliofadhiliwa na Kanisa Katoliki. Katika mwezi mzima, nilishuhudia umeme kukatika mara 2, na mara zote, haikuzidi nusu saa. Mradi huo unaendeshwa na wanakijiji wenyewe, na viongozi na watendaji wote wa mradi, hakuna mhandisi wala mfanyakazi yeyote mwenye hata degree moja. Lakini umeme ni wa uhakika.

Kwa aina ya watu waliopo wizara ya nishati mpaka hao waliopo TANESCO, nawahakikishieni, hata bwawa la Nyerere lianze kufanya kazi, hakuna kitakachobadilika. Maana tatizo kubwa halipo kwenye vyanzo vya umeme bali aina ya watu waliopo.

Muda huu ninaoandika, nimewasiliana na watu mbalimbali na kuthibitishiwa kuwa maeneo mengi ya nchi hakuna umeme.

Tujiulize, hivi watu waliyopo huko TANESCO wana uhalali gani wa kuendelea kuwatesa Watanzania kiasi hiki? Na mamlaka za juu, kwa nini zinaamua kuwatesa Watanzania kupitia TANESCO kwa kuwaweka watu ambao kwa kipimo chochote, hawafai na ni hasara kwa Taifa zima? Na sisi wananchi tutaendelea kuwavumilia hawa watu mpaka lini?

Kuna haja ya kuandaa maandamano makubwa dhidi ya TANESCO na watawala. Watawala muda huu ambao sehemu kubwa ya nchi ipo gizani, watawala wamewashiwa generators. Hawana giza.
ni kweli kuna changamoto ya umeme nchini na mara kadha wahusika wameshalielezea kwa kina jambo hili na mikakati inayotekelezwa kulikabili .

ni vizuri kuwa na subra na wastahimilivu. Ni vizuri zaidi kuwapa muda wa kitosha zaidi ili walishughulikie kwa uhakika zaidi ili kuondokana na kadhia hii ya kukatikatika kwa nishati hiyo muhimu nchini..

hayo mengine yabaki tu kama maoni na mtazamo utatuzi unakuja.🐒
 
Shida ya Tanzania yetu ni ubinafsi uliopitiliza,mwizi mwenye mamlaka ya kukwiba anataka akwibe hadi vitakavyo saidia vizazi vyake mia vijavyo.Pamoja na ahadi yao isiyotekelezeka ya kusema kweli daima wameigeuza kuwa watasena uongo daima na kuwa uongo mwiko🤔
 
ni kweli kuna changamoto ya umeme nchini na mara kadha wahusika wameshalielezea kwa kina jambo hili na mikakati inayotekelezwa kulikabili .

ni vizuri kuwa na subra na wastahimilivu. Ni vizuri zaidi kuwapa muda wa kitosha zaidi ili walishughulikie kwa uhakika zaidi ili kuondokana na kadhia hii ya kukatikatika kwa nishati hiyo muhimu nchini..

hayo mengine yabaki tu kama maoni na mtazamo utatuzi unakuja.🐒
Subira wote wa Watanzania hivi sasa wamegeuka mateja,wabugia sembe kama sii wachoma nyasi waaminifu😒
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom