Suala la Achraf Hakimi na Mke wake: Watu ni wepesi kuongea, hawataki kufanya reasoning

PakiJinja

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
7,661
15,800
Baada ya Mahakama kutamka kuwa Hakimi hamiliki pesa wala mali yoyote, Hakimi akaanza ku trend mitandaoni. Watu wakampatia sifa zenye rangi, harufu na maumbo yote.

Ikumbukwe kwamba, suala hili halijaisha wakati ndiyo kwanza game ipo mapumziko.

Inathibitishika kuwa Hakimi ni muajiriwa, hivyo basi chini ya jina lolote ambapo hela na mali zake zinaenda kuhifadhiwa inakuwa ni salama kwa masuala mengine ya kisheria lakini si kwa mke wake.

Kesi itakayofuata, Hakimi anaweza akahitajika kutoa maelezo ni wapi ambapo pesa na mali alizozipata kutokana na kazi yake amekuwa akizipeleka, maana pesa ile ni mali halali ya familia yake, inakuwaje familia ijikute haina umiliki wa kitu chochote kile?

Vyovyote itakavyokuwa, kesi itakayofuata itamuweka Hakimi mahala pabaya zaidi. Mama yake atahitajika kuelezea chanzo cha mapato cha pesa na mali zilizo chini ya jina lake.

Hii kesi ya kwanza imeishia hapo na ndiyo ina-trend kwa sasa, ila kesi ya pili nabashiri itakuwa mbaya zaidi na huenda Hakimi akajikuta mahala pagumu kuliko Emmanuel Eboue.
 
Kama kawaida Yetu wazee wa kuruka na Track!

Yes....tunaruka na story balaa!
Kuna vipawa hatuna ila sio kwenye trending issues!
Yani kikubwa huwa ni headline tu, story tunaandika wenyewe!
Ukisikiliza simulizi ya ajali toka kwa watu watatu tofauti na wewe unaibuka na story yako!

Ndio ni ka mfumo ka maisha tulikojichagulia na kana burudani yake sana tu! Nieleweke Sina tatizo na hilo maana waumini tupo wengi! Tena wengi sana, ila nina shida ni namna tunavyoshupalia mambo kwa kutake sides easily!

Ndio.... nazungumzia u-team kwenye kila jambo! Hujanipata bado? Nataka kuzungumzia sakata la 'Dogo' Achiraf Hakimi kidogo tu! Kuna wana wameanza kusema mwamba ajengewe sanamu! Kuna wadau wameanza kulalama mshikaji kuwa ni mtoto wa mama (mamaz boy)

Kuna wana wamezua utani wa Jamaa ametuwakilisha vema wanaume! Na kuna wana wanasema ndio dawa ya wadada wanaoanzisha mahusiano ili kuchuma mali! Mimi nitazungumzia hili la mwisho! Ni nani amewaambia ex wake hakuwa na pesa!?

Ni nani amesema ex wake alifata pesa! Anyway, Chukua dakika chache tu m-google mwanamama Hiba Abouk! Ni yeye ex wa 'Dogo' Hakimi!

Utaona Hiba kamzidi Hakimi miaka 12.... Yes miaka 12... she is now 36 years old na dogo ndo kwanza ana miaka 24. Kumbukumbu zinatuambia 'sister' HIBA kazaliwa Oktoba 1986 (miezi kadhaa baada ya goli la mkono la marehemu Diego Maradona)

Wakati kumbukumbu hizo hizo zinatuambia Hakimi kazaliwa November, 1998 (miezi kadhaa baada ya Zinedine zidane kuwaua Brazil).

Nitaruka mengine!

2008 Hakimi akiwa na miaka 10, Hiba ambae alikuwa na miaka 22 alikuwa anaigiza pale Hispania.

Kwa uchache tu unaambiwa kahusika kwenye El syndrome ya 2008, la isla 2010, Cheers 2011, Con el Culo 2012, pegada 2012, Aire 2013, el corazon 2014, tere bluee 2014, el principe 2016, tiempo 2017, malek 2019, Caribe 2020 na madres 2021. Which means she has been working!

Au ndo tunadhani waigizaji wa kule pato lao ni la kwenye 'max na zembwela'???

Namaanisha nini Hiba hana njaa ya pesa! (ingawa anaweza asiwe tajiri)

Geukia Couple yake na Hakimi!

Mahusiano yake na hakimi yaliwekwa wazi 2018, yes Hakimi akiwa ndo kwanza ana miaka 20 (hapa unaweza ukaelewa kwanini mama anatajwa kwenye hakimiliki za dogo hakimi). He was so young!

To cut the story short, Hakimi ni mmoja wa wachezaji ambao kwa umri wake kabahatika kuwa na Profile kubwa kweli kweli (Kapita Real Madrid, kacheza Dortmund, Inter Milan na sasa PSG)

Tufupishe stori UNIELEWE!

wameoana 2020.

Katika ndoa yao wamepata watoto wawili.

Mmoja 2020.

Mwingine 2022.

Zogo na Saga za kutengana zimehit 2023.

kabla mwanetu Hakimi hajapata ile Scandal ya ubakaji

Tuiweke kando maana sitaki kutake sides pia!

Mama akathibitisha wametengana!

Hapa ndipo jamii yetu ya Soka ikatake side sasa!

Kimsingi ni kawaida mahusiano yanapofika mwisho yanakuwa na wafuasi wa tulijua, tulikwambia n.k

Ila nachoona si haki ni namna wengi wanavyomchukulia kama Bi Hiba alikuwa anadanga ama alifata pesa!

Yeye na Hakimi ni familia ambayo tayari ina watoto wawili

Kuwalinda watoto na kuhitimisha ule muunganiko wao ilikuwa lazima sheria ihusike!

Najua ni bhati mbaya Hakimi ana support kubwa kwny footbal industry kuliko Bi. Hiba! Wachache wana muda ni mambo ya filamu!

ila niulize maswali machache!

Kwa kutengana kule na wana watoto wawili tulitegemea mtalaka wake asiombe mgawanyo wa mali??

Ni nani anapinga nguvu ya 'companiship' kwenye utafutaji??

Sheria inampa mtalaka nafasi ya kuomba nafuu zipi bila kujali kama atazipata?

Nimekusudia kusema nini!??? Lengo ni kusema wagapi tumewaza madhara ya talaka (divorce)?

NB: Dini na Sheria zina-discourage sana Divorce! Tchao
 
Kesi itakayofuata, Hakimi anaweza akahitajika kutoa maelezo ni wapi ambapo pesa na mali alizozipata kutokana na kazi yake amekua akizipeleka, maana pesa ile ni mali halali ya familia yake, inakuwaje familia ijikute haina umiliki wa kitu chochote kile?
Hebu toa vifungu vya sheria ya ufaransa ambavyo vinatibitisha hayo maneno.
Mahakama haiwezi kuhoji MALI UNAPELEKA/UNATUMIA WAPI.

Issue kubwa ni matunzo ya watoto tuu.
Hapo Mahakama ndio itahakikisha watoto wanapata matunzo yote.

 
Pole dada... Naona umeumia kwa mwenzako kuambulia patupu...

Jamaa ana wanasheria na wala hakukurupuka.... Na wanaume wote tupo tayari kumtetea....
Wanawake wanamambo ya kingese sana na hasa hapo kwenye kutaka mali za wanaume kwa kigezo cha ndoa bora kuto oa tuu maana tuna oa mashetani yanayo omba ufe wakati wowote yamiliki mali ili waenjoy na ma ex wao

Dawa ni kuzalisha tu kam MONDI kila mtu akae kwao swala oa kufua DOBI wapo ,swala la kula SHISHI FOOD yupo , usafi wa nyumba wapo wanao toa huduma hiyo

Swala la nyege MALAYA wapo tu tena wakali sana na wanakupa huduma haswaa roho inafurahi mnakutana lodge mnaachana huko imeisha hiyo ili nizeeke kwa amani

Usha wahi jiuliza kwa nini wanaume wakistaafu wanakufa mapema sana mara tu baadabya kukamilisha kuchukua oensio na viinua mgongo, wengi wanatangulizwa na wanawake zao ili wai wabaki na wafahidi pensions ya marehemu mume wake .
 
Nikuulize, kama huyo mwanamke hakua mdangaji/Gold digger/Opportunist alifuata nini kwa kijana mdogo aliyemzidi miaka 10+ ??
Unadhani alikua anampemda kweli?? Laiti Hakimi angekua hana Status aliyonayo unadhani angekubali kua na kijana mdogo aliyemzidi ambaye hana kitu/Pesa????

niulize maswali machache!

Kwa kutengana kule na wana watoto wawili tulitegemea mtalaka wake asiombe mgawanyo wa mali??

Ni nani anapinga nguvu ya 'companiship' kwenye utafutaji??

Sheria inampa mtalaka nafasi ya kuomba nafuu zipi bila kujali kama atazipata?

Nimekusudia kusema nini!??? Lengo ni kusema wagapi tumewaza madhara ya talaka (divorce)?

NB: Dini na Sheria zina-discourage sana Divorce! Tchao
 
Kwa kutengana kule na wana watoto wawili tulitegemea mtalaka wake asiombe mgawanyo wa mali??
Kikubwa angefungua madai ya talaka na swala la child support lingeisha .
Kwa nini aende kudai half of the wealth kama sio gold digger?
Kanye west kaachana na kim kadarshian kwa talaka kabisa, je umesikia kim akidai half of Ye's wealth?

Na kama anajiweza na angekuwa smart upstairs basi hili swala lilikuwa linaishia kwa wanasheria wao wenyewe tuu halafu makaratasi yanapelekwa mahakamani kwa ajili ya formality.
 
Back
Top Bottom