mtafuta-maisha
JF-Expert Member
- Nov 5, 2016
- 1,982
- 2,915
Mauaji katika Fungate (je ni kweli Shrien Dewan alipanga mauaji ya mke wake?)
Tarehe 13, mwezi wa 11 mwaka 2010, wanandoa wawili wakiwa safari ya kula fungate Afrika ya Kusini baada ya ndoa yao ya kifahari iliyofungwa huko Mumbai India. Wakiwa kwenye tax, wakipita kwenye kitongoji kidogo kijulikanacho kama Gugulethu, kilichopo karibu na Cape Town, mara tax yao inavamiwa na na watu wawili wenye silaha, wanaiteka na kumwamuru dereva ateremke na kasha mmoja wao anaendesha tax kuelekea kitongoji kijulkanacho kama Harare. Huko mwanaume anaamuriwa ateremke na kumwacha mkewe ambapo watekaji wanaondoka naye.
Kesho yake mwili wa mwanadada unakutwa kwenye hiyo tax, ikiwa imeterekezwa, ambapo mwili wake ulikuuwa kwenye viti vya nyuma ukiwa na jeraha la risasi shingoni.
Msako mkali unaanzishwa kwa lengo la kuwapata wahusika wa mauaji hayo, waweze kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Upepelezi unapoendelea, polisi wa Afrika ya Kusini wanadai ya kwamba mpango wote wa kuuawa kwa mwanamama, umesukwa kwa umakini na mumewe hivyo mume anageuka kuwa ndiye mpangaji ya mauaji ya mkewe.
Historia fupi wanandoa
Shrien Dewan aliyekuwa na miaka 30 kipindi hicho, ni mfanyabiashara tajiri raia wa Uingereza mwenye chimbuko la India. Amezaliwa tarehe 29, mwezi wa 12, mwaka 1979 (age 38) huko Bristol Uingereza.
Shrien Dewan anamiliki kampuni mbalimbali huko Uingereza ikiwemo kampuni kubwa ya PSP Holdings Ltd.
Anni Ninna Dewani (Hindocha) alizaliwa tarehe; 12 Mwezi wa 3 mwaka 1982, huko Uswiss.
Familia yao yenye chimbuko la kihindi ilihamia Uswiss kutoka Uganda kipindi ambapo aliyekuwa raisi wa Uganda Idd Amin, alipowataka raia wa Kihindi kuondoka nchini humo.
Mwaka 2009, akiwa huko London uingereza alikuana na Shrien Dewan, na wakajikuta wako penzini, na aliporudi kwao Uswiss waliendelea na penzi lao wakiwa mbali mbali na walidumu katika hali hiyo kwa miezi 18, kabla ya Anni Dewan kuamua kuhamia Uingereza mwezi wa tatu mwaka 2010, kumfuata mchumba wake. Mwezi wa tano wakavalishana pete ya uchumba na tarehe 29 mwezi wa 10 mwaka 2010, walifunga ndoa huko Mumbai India.
Lakini kwa ushahidi uliopo unaonyesha katika kipindi walichovalishana pete ya uchumba, Anni alianza kuona kuwa yeye na Shrien hawaendani kwakuwa Shrien alikuwa ni mtu mwenye wivu sana na anayetaka kumtawala kwa kila namna.
Walikuwa hawaishi kugombana kulikuwa kuna mabishano na ugomvi wa mara kwa mara katika kipindi hico cha uchumba wao.
Hata baada ya ndoa inadaiwa Anni alitaka kuomba taraka siku ya tatu tu, akidai kwamba hampendi Shrien, anamchukia na anaona hawaendani maana Shrien ni mtu anayetaka mambo yake yaenda sawa kwa asilimia mia (perfectionist), wakati yeye Anni amezoea kuishi maisha ya kawaida tu.
Kuna ushahidi wa ujumbve mfupi wa simu ambao Anni alimtumia binamu yake akimuelezea kuhusu kumchukia Shrien na kuwa anajuta ni kwanini alikubari kuolewa naye.
Baada ya ndoa waliamua kuelekea kwenye fungate Afrika ya Kusini, huku wakiwa na mpango wa kuandaa tafrija kwa ajili ya ndugu na marafiki wao walioko huko Uingereza ambao hawakuweza kuhudhuria ndoa yao huko India, pindi tu watakapo rejea kutoka katika fungate lao.
Fungate
Tarehe 9, mwezi wa 11 mwaka 2010, baada ya ndoa yao huko Mumbai India. Wanadoa hao Shrien Dewan na Anni Dewan walisafiri kuelekea Afrika ya Kusini kula fungate. Walifika na kukaa siku nne katika hotel ya kifahari ya nyota tano ijulikanayo kama Chitwa Chitwa Game lodge iliyoko katika hifadhi ijulikanayo kama Kruger.
Tarehe 10, mwezi wa 11, mwaka 2010, baada ya kufika Afrika ya Kusini, Anni alimtumia tena ujumbe mfupi binadamu yake akimwambia kwamba anajaribu kuendana na Shrien kwa maana Shrien anajitahidi kumfurahisha na ni kijana mzuri tu.
Na kesho yake yani tarehe 11, alimtumia ujumbe mwingine binamu yake akidai kwamba, Shrien anazidi kuwa bora kuliko awali na akaongezaa kuwa ni ngumu kueleza hiyo hali ila atampigia simu atakaporejea Uingereza, akamalizia kwa kusema anachukua kusikia neon taraka kwa muda huo,
Hii inaonyesha kuwa fungate na ndoa yao ilikuwa inaenda vizuri na ule msuguano ulionekana awali ulikuwa unaanza kupotea na kugeuka ndoa yenye amani na furaha kwa wanandoa wapya.
Tarehe 12, mwezi wa 11, waliondoka kwa usafiri wa ndege kuelekea Capetown kwa ajili ya kuendelea kula raha na kufaidi fungate lao.
Hapo ndipo matukio mpaka kifo cha Anni dewan yanaanza.
Saa 30 kabla ya kuawa Anni dewan
Baada ya kuwasiri katika kiwanja cha ndege cha Cape Town, walitoka nje ya uwanja na kutafuta tax. Kati ya tax zilizokuwa uwanjani hapo kulikuwa na tax ya kijana ajulikanaye kama Zola Robert Tongo.
Akiwa na umri wa miaka 30 kwa kipindi hico, alikuwa amewahi kukamatwa na kosa moja tu lilimfikisha polisi na kosa hilo lilikuwa kuendesha gari pasipokuwa na leseni ya udereva.
Kwa maelezo ya Tongo anadai Dewan aliwafuata, akawauliza kama anaweza kupata tax, huyu Tongo ndiye shahidi namba moja katika kesi ya mauji ya Anne Dewan. Tongo na wenzake waliongea na Dewan na ikaonekana kwamba Tongo alikuwa na bei ya chini hivyo Dewan alichukua tax ya Tongo.
Ilimchukua Tongo dakika 25, kuwatoa uwanja wa ndege mpaka kwenye hoteli ya Cape Grace. Walipofika wakati Anne alipoingia ndani ya hotel, Tongo anadai Dewan alirudi na kumwambia anahitaji kusaidiwa kuua mtu flani. Tongo anadai alimwambia kwamba yeye hajihusishi na shughuli hizo ila naweza kumpigia mtu anayemfahamu ambaye anaweza kumsaidia kupata mtu wa kufanya mauaji hayo.
Kamera za hoteli zinaonyesha Dewan akirudi ndani ya hoteli na kuangana na mkewe, kasha baada ya muda anatoka tena kwa mara nyingine kuongea na Tongo yani mara mbili ndani ya muda wa dakika tisa tu.
Lakini kwa maelezo ya dewan anadai ya kwamba yeye na Tongo walikuwa wanazungumzia mipango ya Tongo kuwazungusha sehemu mbalimbali za cape town kwa tax yake hapo baadae.
Tongo yeye anadai kwamba, dewan alimwambia kwamba yuko tayari kulipa Rand 15,000 kwa ajili ya shughui hiyo na atalipa kwa kutumia Dolla, na anadai dewan alimwambia mtu anayehitajika kuawa ni mwanamke na atafika kwa ndge jioni ya siku hiyo.
Maswali la kujiuliza hapa ni kwamba, ikiwa kweli Anni ndiye mtu ambaye Shrien alihitaji auawe, kwanini hakumwambia Tongo kuwa ni yeye ukizingatia ya kwamba alitaka mauaji hayo yafanyike usiku wa siku inayofuata.
Na swali lingine, ni kwamba inawezekanaje mtu mgeni, ndiyo kwa mara ya kwanza amefika Afrika ya Kusini, hajui mazingira hana wenyeji anawezaji kumwambia jambo zito kama hili mtu aliyekutana naye kwa mara ya kwanza ndani ya dakika 40?
Baada ya kuondoka hapo hotelini Tongo alielekea Protea Colosseum hoteli ambayo ni mwendo wa dakika 20, kutoka kwenye hoteli walikofikia wanandoa hao.
Akiwa njiani anaelekea kwenye hoteli hiyo, Tongo alipiga simu hapo kwa mhudumu wa mapokezi ajulikanaye kama Monde Mbolombo, na kwa maelezo ya polisi na ushahidi wa video na sauti baina ya mazungumzo kati ya Tongo na Monde ni kwamba Monde ndiye alikuwa mtu wa kati ya kiunganishi kati ya Tongo na muaji aliyempiga Anni Dewan risasi.
Lakini jambo la kustaajisbisha katika kesi hii, ni kwamba Monde alipewa kinga kabisa ya kutoshitakiwa ikiwa kama atashirikiana na polisi kwa kutoa ushahidi wa mipango yote na uhusika wake katika mpango wa mauaji ya Anni.
Hili ni jambo la kustaajibisha kwakuwa bila ushirika wake kama mtu kati akiwaunganisha muaji na Tongo, basi huenda Anni asingeuawa, lakini bado polisi ilimpatia kinga mtu huyu ya kutoshitakiwa.
Wakati Tongo akiwa njiani kuelekea Colosseum kukutana na Monde, kamera za ulinzi za hoteli ya Cape Grace zinamuonyesha, Dewan akitoka chumbani kwake na kuelekea nje ya hotel.
Pia kamera za ulinzi za Colosseum zinaonyesha Tongo alipowasili, Monde anaweka mikono kichwani kama akishangilia hivi kasha wanatoka nje.
Tongo anadai alimwambia Monde kuwa kuna mtu anahitaji auawe mwadada, na yuko tayari kiulipa kiasi cha Rand 15,000. Monde alimjibu ya kwamba anafahamiana na kijana mmoja hapo mjini ambaye anaweza tekereza mauaji hayo.
Kamera zinawaonyesha Monde na Tongo wanarudi ndani ya hoteli sehemu ya mapokezi na Monde anachukua simu na kuanza kutafuta namba kisha anampigia kijana mwenye umri wa miaka 25 ajulikanaye kama Mziwama Dodo Qwabe ambaye hana ajira.
Monde na Qwabe wanazungumza na Monde anamwambia kwamba kuna kazi ya kuua mtu, kwa malipo ya Rand 5,000. Qwabe anakubari kufanya hiyo kazi kwa hayo malipo.
Jambo la kushangaza zaidi katika hii kesi, polisi pia waliingia makubariano na Qwabe kama waliyoingia nayo kwa Monde wakimtaka atoe ushahidi dhidi uhusika wa Shrien Dewan katika mauaji hao kwa makubariano ya kupunguza kifungo chake kutoka miaka 15 mpaka miaka saba.
Monde anampatia Tongo namba ya Qwabe, na anamwambia kwamba atahiotaji malipo ya Rand 5,000 kwa kumuunganisha Tongo na muaji ambaye ni Qwabe.
Lakini katika utetezi wake Monde anakataa kuwa hakuhitaji pesa kutoka kwa Tongo, akidai kuwa kupokea pesa inayotokana na kumwaga damu ya mtu ni vibaya, hivyo yeye hakuwa tayari kupokea pesa ya damu bali tu alishiriki kumsaidia rafiki yake Tongo kwa kumpatia mtu wa kufanya kazi hiyo.
Baada ya Tongo kuondoka hapo hotelini, kamera za hoteli zinamuonyesha Monde akiwa mwenye furaha akicheka na kushangilia peke yake. Maswali ya kujiuliza ni je Monde alikuwa akifurahia mpango wa mauaji au alikuwa anafurahia jambo linguine tofauti ukizingatia kwamba Monde hakuwahi kuwa na matatizo yote au historia ya uhalifu, iweje jambo la mauaji limfurahishe mtu ambaye hana historia ya kufanya uhalifu?
Jambo la kushangaza, hawa wote wahusika wakuu waliingia makubariano na polisi wa Cape Town kutoshitakiwa au kupewa adhabu ndogo pale watakapo kubari kutoa ushahidi dhidi ya ushirika wa shrien Dewan katika mpango wa kumuua mkewe.
Je hii ilikuwa sawa, ukizingatia hawa walikuwa waalifu na walikuwa tayari kusema lolote na kufanya jambo lolote kuepuka mkono wa sheria baada ya kufanya mauaji hayo?
Na je kauli zao na ushahidi waliotoa ni wa kuaminika kiasi gani mpaka polisi wautumie kama ushahidi tosha wa kujenga kesi dhidi ya Shrien Dewan?
Muda huo huo ambapo Tongo aliondoka kutoka kwa rafiki yake Monde, kamera za hoteli ya Cape grace zinamuonyesha Shrien Dewan akiwa anarejea kutoka alipokuwa amekwenda, ambapo alikuwa ameenda kwenye duka la kubadirisha fedha na kubadiri pounds 800, akapewa Rands kasha alienda duka la maua na kumnunulia mkewe maua ya Rose mekundu anayoonekana akiwa ameyabeba wakati anaingia hotelini.
Dakika tano baada ya Shrien kuingia chumbani, Anni alipiga simu kwenda kwa wazazi wake na kuzungumza na baba yake..
Kwa maelezo ya baba yake anadai sauti ya Anni haikuwa sawa, alionekana ni mtu ambaye hakuwa sawa na allihisi kuna jambo haliko sawa. Lakini Anni alipoulizwa na baba yake kama yuko sawa alimwambia yuko sawa. Na hiyo ndiyo ilikuwa mara ya mwisho Anni kuzungumza na baba yake.
Ijumaa saa 12 na dakika 41
Tongo alikuwa karudi nyumbani kwake katoka kuonana na Qwabe,
Kwa maelezo ya Qwabe anadai kwamba Tongo walipoonanan alimwambia kuna mtu anataka asaidiwe kutekeleza mauaji, wakati wakizungumza mara Qwabe alipokea simu kutoka kwa rafiki yake aitwaye Kolile Mngeni, ambapo Qwabe aliamua kumshirikisha katika mpango huo kama msaidizi wake.
Kwa maqelezo ya Qwabe anadai kwamba yeye na Mngeni walizungumza kwa kina juu ya mauaji hayo, na Mngeni akamwambia yuko tayari kushiriki ikiwa dau litaongezeka mpaka kufikia Rand 15,000.
Huyu Mngeni tofauti na wenzake, ndiye pekee aliyekataa kuingia makubariano na polisi ya kupunguziwa adhabu kwa kutoa ushahidi unaoonyesha ushirika wa Shrien katika mpango wa mauaji ya Anni Dewan. Na ni Mngeni pekee ambaye maelezo yake hayamhusishi Shrien katika mpango wa kutekeleza mauaji hayo.
Ni Mngeni aliyekutwa na hatia ya kumuua Anni, na alipatikana na hatia hiyo kutokana na ushahidi aliotoa Qwabe juu yake akahukumiwa kifungo cha maisha. Na ajabu alifaariki akiwa gerezani.
Ijumaa saa 2 na dakika 13
Wakati hayo yakiendelea, kamera za hoeli ya Cape Grace zinawaonyesha wanandoa Bwana na Bibi dewan wakiwa wanatoka chumbani kwao, wakielekea kwenye bar ya hoteli hiyo, kisha baadae wanaenda kupata chakula kwenye mgahawa ulioko mwendo wa dakika chache kutoka hapo hotelini.
Kwa maelezo ya mhudumu aliyewahudumia siku hiyo, anawakumbuka na anadai kwamba amehudumu meza kadhaa za watu wanaokuwa kwenye fungate, ila siku hiyo ilikuwa tofauti kwa akina Dewan.
Anadai kwa kawaida watu wakiwa fungate uwa wanaonyesha mapenzi sana, wanashikana, wanabusiana wanatazamana wanassemezana na kuonyesha kila aina ya mahaba lakini anadai wao hawakuwa hivyo walikuwa kimya sana.
Pia anadai kuna wakati alienda kuhakikisha kama kuna kitu kingine wanachohitaji, lakini Shrien hakuwa mezani alikuwa aktoka nje ya mgahawa ni bi dewan tu aliyekuwa mezani peke yake na alimwambia mhudumu kuwa Shrien katoka nje kuzungumza na simu inayohusiana na mambo ya kibiashara.
Mhudumu anadai kuwa watu wengi pale mghahawani walikuwa wakitazama ile meza aliyokuwa kaka Anni wakimuonea huruma huku wakishangaa na kuongea juu ya mwanaume aliyemuacha Bibi yake mezani peke yake wakiwa kwenye fungate.
Ijumaa saa 3 na dakika 21
Kamera zilizo nje ya huo mgahawa zinamuonyesha Shrien akiwa anatembea kurudi hotelini, na kamera za hoteli sinamuonyesha akiingia chumbani kwake akatoka akuwa kashika simu yake mkononi, jambo linaloonyesha kuwa ni kweli alikuwa kafuata simu yake.
Na kutokana na kumbukumbu kutoka kwenye mtandao wa simu, Shrien alikuwa kuna ujumbe mfupi wa maneno kutoka kwa Tongo ambapo Shrien alimpigi Tongo na kuzungumza naye kwa dakiaka 5 na sekunde 26,
Ukitazama kwa umakini utagundua hakuna ushahidi wowote ambao unamhusisha Dewan katika mpango wa mauaji moja kwa moja, ila kitu ambacho kinatia shaka ni mpangilio wa simu nbaina yake na Tongo pamoja jinsi walivyokuwa akitoka na kuzungumza naye wakati akiwa hotelini.
Kwa maelezo ya Tongo anadai kwenye simu walizungumza na akamtaarifu kuwa ameongea na rafiki yake ambaye amemuunga na kijana anayeweza fanya kazi hiyo ya mauaji na kasema atahitaji malipo ya Rand 15,000/
Ijumaa saa 5 na dakika 23
Kameera za hoteli zinawaonyesha Bwana na bibi Dewan wakiwa wanarejea kwenye chumba chao huku Shrien akiwa anaonekana mwenye furaha akitabasamu. Akiwa katangulia mbele na Anni akiwa nyuma, Shrien anageuka huku akicheka anaonyesha ishara ya kama namlenga kwa pistol Anni kwa kutumia vidole vya mikono yake yote miwili.
Anni haonyeshi furaha wala kushtushwa na kitendo hicho cha Shrien kumuonyesha ishara ya kama anamlenga kwa pistol. Wanaingia kwenye chumba chao.
Nini lilikuwa lengo la Shrien kumuua Anni, na je nini ambacho angefaidika nacho kutokana na kifo cha Anni kwa maana Anni hakuwa na Life Insurance hivyo Shrien asingeweza kupata pesa kutokana na kifo chake.
Polisi wa Afrika ya Kusini wao wana mawazo tofauti, wanadai Shrien alipanga mauaji hayo kutokana na tama zake za kingono,
Kutokana na maelezo aliyotoa Malaya wa kiume ajulikanaye kama Leopold Leisser, anadai kwamba Shrien alikuwa ni shoga na alikuwa akimlipa kwa ajili ya kufanya naye mapenzi. Leisser alidai kwamba Shrien alikuwa kafanya naye mapenzi mara tatu na mara ya mwisho ilikuwa na mwezi mmoja kabla ya ndoa yake.
Aliendelea kusema kuwa Shrien alidai Anni ni msichana mrembo, mzuri na anampenda ila asingependa kumuoa kutokana na sababu ya kuwa yeye Shrien ni shoga na anafurahia kitendo cha kuingiliwa zaidi kuliko kumwingilia mwanamke.
Laisser anadai ya kwamba Shrien alimwambia angependa kusitisha ndoa isifungwe ila anaogopa endapo atafanya hivyo, familia itamtenga hivyo inabidi ndoa ifungwe lakini atafute njia ya kuondoa tatizo hilo.
Kutokana na maelezo ya Laisser, polisi wanaamini ya kwamba Shrien alimaanisha njia ya kuondoa tatizo ilikuwa ni kumuondoa Anni katika maisha yake ili apate kuendelea kuishi maisha yake ya siri kama shoga.
Jumamosi ya tarehe 13, mwezi wa 11 mwaka 2010 ndani ya Jiji la cape Town
Hii ndiyo siku Anni alipouawa.
Kamera za hoteli zinawaonyesha Bwana na Bi Dewan wakiwa wanatoka chumbani kwao wakielekea kwenye mghahawa wa hoeli kupata kifungua kinywa.
Tongo anadai alizungumza na Shrien ambapo Shrien alimpigia simu saa 5 na dakika 30 asubuhi, na kumwambia amfuate na kumchukua hapo hotelini. Laini kutokana na kumbukumbu zilizochukuliwa kutoka kwenye mtandao wa simu zinaonyesha kuwa Tongo anadanganya hakukuwa na simu ya aina yoyote ambayo Shrien alimpigia Tongo muda huo.
Je kwanini tongo aseme uongo juu ya kupigiwa simu? Ikiwa ameza kudanganya juu ya hilo, je Tongo ni kwanini Tongo aaminike kwa mambo mengine aliyosema juu ya Shrien?
Jumamosi saa 5 na dakika 56
Nusu saa baada ya hiyo simu ya kusadika ambayo Tongo anadai alipigiwa na Shrien, Tongo anafaika kaiwa na Tax yake kuja kumchukua Shrien. Kamera za hoteli zinaonyesha gari ya Tongo ikiingia kwenye sehemu ya kuegesha magari ya hoteli na pia zinamuoneysha Shrien akitoka hotelini na kuingia kwenye tax ya Tongo kasha wanaondoka.
Kutokana na maelezo ya Tongo anadai kwamba, Shrien alimuomba mapeleke sehemu atakapoweza kubadirisha fedha, na Tongo aliamua kumpeleka sehemu ambako hiyo biashara inaendeshwa bila uhalali (Black Market).
Tongo aliampeleka kwenye duka linalojihusisha na kuuza vito vya thamani lijulikanalo kama The Golden touch Jewellers, lakini pia linafanya shughuli ya kubadiri pesa za kigeni bila vibari.
Wamiliki wa hilo duka wanadai Shrien alibadiri 15,000$ akapewa Rand 10,200. Kwa maelezo haya ukipiga hesabu kuwa alikuwa amekwishabadiri pound 900 ambazo zilikuwa sawa na rand 11,000 , ukajumuisha na Rand 10,200 za sasa jumla utapata Rand 21,000 ambazo ni zaidi ya kiasi kinachodaiwa na Tongo kuwa kilihitajika kutekeleza mauaji hayo.
Katika upepelezi wa mauaji ya kulipiwa, mzunguko wa pesa ya malipo uwa ni muhimu, lakini kwa polisi wa Afrika ya Kusini wameshindwa kuonyesha malipo hayo yalikofanyika na niwa wapi hiyo pesa ilipo kwa hao waliolipwa. Yani hakuna sehemu yoyote kwenye mafaili ya polisi pesa Rand 15,000 ya malipo inakoonyeshwa ililipwa na wahusika waligawanaje hiyo pesa na matumizi ya kila mmoja na kiasi kilichobaki ili kitumike kama ushahidi. Kwa kifupi ni kwamba hiyo pesa ilipotea tu hata hakuna sehemu wala ushahidi wa kuoneysha Shrien alimpatia Tongo au muaji pesa hiyo.
Kutokana na kumbukumbu za minara ya simu polisi waliweza kufuatilia ni wapi Shrien alielekea baada ya kubadiri pesa, na inaonyesha kuwa alirudi moja kwa moja Cape Grace hotel ambapo ni afari kama ya dakika 10 kutoka hapo alipobadirishia pesa.
Kwa maelezo ya Tongo anadai wakiwa katika safari ya kurudi hotelini, Shrien alianza kumueleza Tongo ni jinsi gani anataka mauaji hayo yatekelezwe. Anadai Shrien alimwambia kuwa anataka ionekane kama gari limevamiwa na majambazi halafu Tongo na Shrien watupwe nje ya gari kasha watekaji waondoke na gari pamoja na anayetakiwa kuuawa.
Haya maelezo ya Tongo yana ukakasi, kwakuwa inaonyesha kwamba Shrien na Tongo hawakuwa na muda wa kutosha kujadiri utekelezaji wa mauaji hayo kwa kina. Kama tulivyoona awali Anni alikuwa anadai moja ya kitu asichopenda kwa Shrien ni mtu anayependa mambo yake yaend kwa usawa kabisa (perfectionist), je mtu kama huyo anawezaje kupanga mauaji ndani ya dakika kumi apange mpango mzima utakavyotekelezwa bila kuhofia kutokea makosa?
Ni jambo la kushangaza kweli kuwa watu wawili wapange mpango mzima wa mauaji ndani ya dakika kumi bila kufanya makosa kutokana na kutokuwa na muda wa kutosha wa kuhakiki mpango mzima.
Tongo anaendelea kudai kwamba pia Shrien alimuahidi kuwa atamlipa kiasi cha Rand 5,000 badda ya kazi hiyo kutekelezwa. Na pia anadai aliikubari kuwa atamlipa kijana atakayefanya hiyo kazi Rand 15,000 taslimu.
Jambo la kushangaza ni kwamba, muajiri wake Tongo yani mmiliki wa hiyo tax anadai anashangaa kwanini Tongo alikubari kushiriki kwenye mpango huo wakati hiyo pesa aliyoahidiwa ilikuwa ni ndogo kulinganisha na mshahara wake wa kila mwezi ambao ulikuwa Rand 15,000-20,0000 mara tatu au nne zaidi ya ela ambayo Tongo anadai Shrien aliahidi kumpatia.
Tongo anadai kwamba walikubariana na Shrien kuwa aje kuwachukua saa 1 na dakika 30 jioni.
Jumamosi saa 8 na dakika 26
Baada ya Tongo kuondoka Cape Grace hoteli, alimpitia Monde, ambaye kama tulivyokwisha ona ndiye alikuwa kiunganishi kati ya Tongo na muaji Qwabe, Tongo alimpa msaada wa kumpeleka Monde kazini kwenye hoteli ya Colesseum.
Monde anadai wakiwa kwenye gari alimuuliza tena Tongo kwanini unahitaji mtu wa kutekel;eza mauaji, na Tongo alimjibu kuwa na mtu ndiye anahitaji mtu flani auawe.
Anasema mara simu ya tongo iliita na Tongo akasema kuwa huyu anayenipigia ndiye anayehitaji mauaji hayo yafanyike. Andai Tongo alipokea simu na Monde anadai alikuwa tu akisikia Tongo akijibu “Ndiyo niko njiana, niko njianai, ndiyo niko njiani, niko njiani.”. Anadai baada ya hapo aliweka simu chini na kusema “eeish, huyu jamaa haniamini”
Jambo la kushangaza kutokana na kumbukumbu za simu, inaonyesha hakuna rekodi yoyote kwenye mtandao wa simu inayoonyesha kuwa Shrien alipiga simu hiyo kwenda kwa Tongo. Hivyo kwa mantiki hiyo ni kwamba Monde alikuwa naongopa kuhusu simu hiyo.
Shrien Dewan kutokana na fedha aliyobadiri alikuwa na Rand 10,200 pamoja na pond 900. Je hii pesa yote alihitaji kwa ajilii ya shughuli gani kama siyo kuwalipa wauaji wa watakaotekeleza mauaji ya Anni?
Kwa amaelezo ya watu waliozungumza Dewan kabla, wanadai alikuwa anampango wa kumfanyia “Surprise” Anni kwa kuandaa safari ya kuzunguka mji kwa kutumia Helkopta siku inayofuata yani Jumapili. Hili polisi hawakulifuatilia kuhakiki kama ni kweli Shrien alitaka kufanya hivyo.
Jumamosi saa 8 na dakika 48
Kamera za hoteli ya Colesseum zinamuonyesha gari la Tongo likiingia kwenye eneo la kuegesha magari katika hoteli hiyo na Monde anateremka. Na pia kamera zinawaonyesha wafanyakazi wenzake Monde pale mapokeziwakiwa wanaongelea juu ya safari ya helkopta na malipo ya Rand 10,00 kwa ajili ya kuandaa safari hiyo ya mteja aliyempata Monde. Pia wahudumu wanazidi kuzungumza wakidai kuwa kuna mtu anataka kumfanyia Surprise mkewe huku wakidai ni ghali sana.
Colesseum Hotel anakofanya kazi Monde wana huduma hiyo ya kukodi helkopta kwa ajili ya safari au mizunguko, kwenye kumbukumbu za video za ulinzi wahudumu wamerekodiwa wakiwa wanazungumza na kusema kuwa atafanyiwa punguzo mpaka Rand 7,200 badala ya bei ya kawaida ya Rand 10,000 kwa safari ya saa moja..
Je hii ilikuwa bahati mbaya Monde kuzungumza juu ya Rand 15,000 za safari ya helkopta na kuom,ba apewe punguzo mpaka Rand 7,250 badala ya Rand 10,000.
Kamera bado zinamuonyesha Monde anaingia mapokezi akiwa kaambatana na Tongo, na anaoneka Monde akiwa anaendeleza mjadara wa safari ya helkopta wahudumu hao waliokuwa wakiizungumzia na wanamsifia kwamba Monde uwa anajua kukutana matajiri kweli na atapata faida kwenye safari hiyo maana kiasi kinachobaki atakichukua yeye.
Anaskika Monde akisema kuwa ndiyo nakutana na matajiri, ila huyu amekwishatapeliwa. Je hii kauli ya Monde inamzungumzia Shrien kama ndiye huyo tajiri? Na vipi juu yauli yake ya kuwa amekwishatapeliwa, je anazungumzia gharama za juu walizompa kuhusu kukodi helkopta kwamba ni Rand 15,000 kumbe ni Rand 10,000 tena hapo akiwa hajapewa punguzo?
Saa 8 na dakika 57
Baada ya dakika tano toka Tongo na Monde wafike pale hotelini, Tongo aliondoka kuelekea katikati ya mji kukutana na watekaji Qwabe na Mngeni wakiwa pamoja kwa mara ya kwanza.
Qwabe anadai walipokutana na Tongo aliwambia kuwa mhusika anataka mkewe auawe, na anataka ionekane kama ni utekaji wa gari kwa ajili ya unyanganyi katikati ya kitongoji cha mji wa Cape Town.
Jambo la kushangaza tena hakuna kumbukumbu yeyote kwenye mtandao wa simu inayoonyesha Tongo kumpigia dewan kumpa taarifa kuhusu kukutana na wauaji au hata kumtaarifu kuwa mpango ulikuwa tayari uko kwenye utekerezaji ksms eslivyopanga baada ya kukutana na Qwabe na Mngeni.
Je inaingia akilini kwa mtu ambaye alitazamwa na Anni, familia yake na familia ya Anni kwamba alikuwa ni mtu anayependa kutawala na anayetaka mambo yake yaende kwa uhakika bila makosa (perfectionist), angethubutu kufanya mpango wa mauaji pasipo kutaka kupata majibu ya mpango toka kwa Tongo?
Usiku wa mauaji ya Anni Dewan
Jumamosi saa 12 na dakika 17
kamera za hoteli zinawaonyesha wanadoa wakitoka kwenye chumba chao na kuelekea kwenye bar ya hoteli hiyo. Wanapigwa picha kadhaa kutoka kwa mpiga picha wa hapo hotelini kasha wanaonekana wakipigana mabusua mara kwa mara wakiwa wamekaa kwenye meza moja wapo hapo kwenye bar.
Saa 12 na dakika 35
Kamera za hoteli ya Colesseum zinamuonyesha Monde ambaye anadai yeye tu alikuwa mhusika wa kumuunga Tongo na Qwabe, ila mazungumzo yaliyonaswa na kamera yanaonyesha kuwa alikuwa anahusika zaidi ya kuwa mtu wa kati.
Kumbukumbu za simu zinaonyesha kwamba alikuwa akizungumza na Tongo, na mazungumzo yaliyonaswa na kamera za ulinzi yanaonyesha kwamnba yeye ndiye aliyekuwa mpangaji watukio zima litakavyofanyika, huku akimpa Tongo maelekezo mpaka ya jinsi gani malipo yatakavyogawanywa baina yao.
Kwa mazungumzo hayo inaonyesha Monde ndiye alikuwa kiongozi na mpangaji wa kila kitu lakini jambo la kustaajabisha ni kwamba mpaka leo yuko huru, alipewa kinga ya kutoshitakiwa na polisi kwa ajili ya kutoa ushaidi.
Katikia hoteli ya Cape Grace, ilifika saa 1 na nusu, Tongo akiwa hajafika kuwachukua akina Dewan kama ambavyo ilitakiwa, Shrien anaamua kumpigia Tongo inapofika saa 1 na dakika 45 kumuuliza yuko wapi kwanini kachelewa kuwafuata.
Lakini tongo na wanasheria wake wao wanatoa maelezo tofauti juu ya hili, wanadai Shrien alimpigia Tongo akiwa kakasirika akimuuliza yuko wapi, na akidai lazima mauaji hayo yafanyike siku hiyo na kama hayatofanyika Shrien atamuua Tongo kwa kutotekeleza makubariano yao.
Lakini kamera za ulinzi hapo hotelini zinaonyesha kitu tofauti, zinamuonyesha Shrien wakati anazungumza na Tongo hakuwa anazungumza kwa hasira na alikuwa kaka na mkewwe pembeni huku akizungumza na Tongo. Tongo anadai Shrien alizungumza kuhusu mauaji ya mkewe na kumtishia kumuua tongo kama hayatatekelezwa, Je inawezekana vipi Shrien azungumze mambo hayo akiwa kaka pembeni ya mke wake?
Inapofika saa 2 na dakika 57, Tongo ndipo anawasili pale hotelini. Kama Shrien alikuwa ni kweli ana mpango kuwa mke wake auawe, basi hakuwa kionyesha dalili yoyote ya hilo jambo kutokana na video zilizonaswa na kamera za hapo hotelini.
Alionekana ni mtu mwenye furaha na ambaye alikuwa akipiga picha kila mara yeye na mkewe kabla ya kupanda tax ya Tongo na kuondoka hapo hotelini.
Tongo mwenyewe anaunga mkono kwamba hali ya furaha na kucheka waliokuwa nayo iliendela hata wakiwa kwenye gari, walikuwa wakiongea wakibusiana na kucheka sana.
Anadai ya kwamba Shrien alimpa maelekezo ya kuendesha tax kuzunguka mji kwakuwa walitaka kuona madhari ya mji unavyofanana usiku.
Kwa maelezo ya Tongo ni kwamba utekaji wa tax ilibidi ufanyike katika kitongoji cha Gugulethu, muda mfupi baada ya Tongo kuwachukua akina Dewan kutoka hotelini. Tongo anadai kwamba alipofika hapo watekaji hawakuwepo hilo eneo na Qwabe anadai kwamba walikuwa wameamua kauchana na utekelezaji wa tukio hilo.
Lakini jambo la kushangaza ni kwamba kutoka na kumbukumbu za simu inaonyesha kwamba simu na jumbe fupi za maneno kati ya Tongo, Monde na Qwabe muda wote wakati Tongo anawazungusha akina Dewan mawasiliano baina yao yalienmdelea.
Muda mchache baadae waliwasili katika mghahawa wa Strand Beach Resort, Tongo anadai Shrien alikuwa kakasirika sana.
Tongo anadai aliongoza nao kuelekea kwenye mgahawa na walipofika sehemu ya kuingilia ndani, Anni alitangulia kuingia Shrien hakuingia alimgeukia Tongo na kumwambia kwanini mpango haujatekerezwa? Anadai kwamba Shrien alimtshia kumuua kama akishindwa timiza mpango wao.
Lakini jambo la kustajabisha ni kiwamba, kamera za mgahawa huo zilizoko ndani zinazoonyesha eneo la kuingia ndani ya mghahawa huo, zinawaonyesha wote wakiingia kwa pamoja na ni Shrien aliyekuwa katangulia na wala siyo Anni . pia mhudumu aliyewapokea anakubarina na hilo kwamba waliingia wote na Shrien ndiye alikuwa katangulia.
Ajabu, inaonyesha kwamba Tongo anazidi kudanganya na inashangaza ni kwanini polisi walikubari kuamini ushaidi wa mtu kama Tongo ambaye maelezo yake yamejaa uongo zaidi ya mara moja.
Kutokana na muda video ya CCTV inaoonyesha, sekunde 8 tu baada ya Dewan na mkewe kupotea kwenye CCTV kwa kuelekea ndani kabisa ya mghahawa, kumbukumbu za simu zinaonyesha Tongo aloimpigia Monde.
Qwabe pia anadai Tongo alimpigia akimwambia ya kwamba anataka mpango wao uendelee na kazi ifanyike usiku huo huo. Pia Tongo alipigiwa simu na Shrien akimuuliza kama ameshawapanga watekaji kwa ajili ya kazi.
Ni kweli kumbukumbu za simu zinaonyesha Shrien alimpgia Tongo saa 3 na dakika 56 na walizungumza kwa sekunde 93.
Lakini maelezo ya Shrien anadai ya kwamba alimpigia kumwambia aje kuwafuata baada ya nusu saa na aliwakuta wakiwa nje ya mghahawa wakimsubiri.
Saa 4 na dakiak 40.
Tongo anadai wakiwa kwenye gari alimtumia ujumbe mfupi Shrien akimwambia kuwa asisahau kuhusu pesa ya malipo na anadai Shrien alimjibu kuwa pesa iko kwenye bahasha nyeupe kwenye pochi nyuma ya siti ya abiria ya mbele.
Japo ni kweli inaonyesha katika kumbukumbu za polisi kuwa ni kweli Tongo alimtumia ujumbe mfupi Shrien, lakini haionyeshi ni ujumbe gani aliandika na wala haionyeshi kama Shrien alijibu huo ujumbe.
Kwa hiyo utaona ushirika wa Shrien unatokana na ushahidi unaotolewa na hawa wauaji lakini hauna kitu chochote cha kuonyesha kuunga mkono ushahidi wanaotoa. Hakuna sehemu inayoonyesha ni nini kilikuwa kwenye ujumbe wa maneno wala hakuna namna ambayo mazungumzo ya simu baina yao yalikuwa yamerekodiwa ila tu maelezo ya Tongo ndiyo polisi walikuwa wanayaamini, maana kwa teknolojia ya mtandao wa simu kipindi cha mwaka 2010, Afrika Kusini ilikuwa haiwezekani kuona ujumbe uliotumwa wala nini kiliongelewa kwenye simu. Ila tu ilikuwa inaonyesha simu ilipigwa muda flani kwenda namba flani na ujumbe ulitumwa muda flani kwenda namba flani.
Tongo aliendesha tax kueleke akatikati ya kitongoji cha Gugulethu, akiwapeleka kwenye mikono ya watekaji Qwabe na Mngeni.
Tongo anadai alipofika eneo ambalo walikuwa wamepanga kuwakuta watekaji alipunguza mwendo na mara ghafla watekaji walijitokeza wakiwa na bunduka na kuamuru asimame. Anadai waliamuru afungue milango akafungua .
Anadai Qwabe alishika usukani na ndiye akaanza kuendesha gari, huku Mngeni yeye alikaa nyuma akiwa kaelekeza bunduki kwa akina Dewan. Qwabe anadai alijifanya anaogopa lakini ukweli aliujua yeye akiwa kaka mbele siti ya abiria.
Shrien anadai mkewe alianza kulia yeye akawa kamkumbatia, ila anadai mkewe hakutaka kuwaachia pochi yake na pete yake ya uchumba na ndoa iliyokuwa na thamani ya Euro 25,000. Anadai yeye alikuwa akiwambia watekaji wachukue chochote wanachotaka waondoke wawaache tu.
Pia andai ya kwamba yeye aliwakabadhi pesa yote aliyokuwa nayo ambayo ilikuwa ni kiasi cha Rand 400, nah ii inathibitishwa na ushahidi wa Mngeni ambaye yeye ndiye alikataa kuingia makubariano na polisi ya kutoa ushaidi juu ya ushiriki wa Shrien.
Ukitazama video iliyorekodiwa wakati akifanya mahojiano na polisi kabla ya Shrien kuwa mtuhumiwa wa kushiriki mauaji ya mke wake, Mngeni anasikika akisema kuwa Shrien alitoa pesa yote aliyokuwa nayo kaisi cha Rand 400, akasema tafahdali msimuue wala msiniue chukua chochote mnachotaka. Anadai kuwa yeye alimjibu kuwa hapana hamtouawa.
Walipofika sehemu, walisimamisha tax na kumtoa Tongo nje ya tax na aliwaelekeza pesa ilipo kasha wakamwacha hapo na kuendelea kuzunguka nagari wakiwa wamewashikiria mateka Shrien na mke wake.
Waliendesha gari mpka kwenye kitongoji cha Kariche na Shrien anadai waliwaambia kuwa hawatowadhuru wao wanachohitaji ni gari yeye wakamwambia ateremke hapo na kumwambia mkewe atateremshwa mbeleni wakidai kuwa hawataki wateremke pamoja wanataka kila mmoja wamuache eeneo tofauti na mwenzake.
Lakini Shrien anadai kuwa alikataa akawambia kuwa Yule ni mkewe naomba wawaache waondoke wakiwa pamoja.
Qwabe anaamfokea Shrien na kumwamuru kuwa atoke kwenye gari akisema toka, toka , toka.
Haya maelezo bado yanaungwa mkono na maelezo ya Mngeni ambaye alikataa kuingia makubariano na polisi. Anadai kuwa Qwabe alidai kuwa hakuna atakayeumizwa ni kwamba tu anamshusha Shrien eneo moja na mkewe naenda kumshusha mbeleni wao wanaondoka na gari. Pia anaunga mkono kuwa Shrien aligoma kuteremka akidai kwamba hawezi kumuacha mkewe.
Kumbuka Shrien na Mngeni hawakuwahi zungumza wala kuonana kabla na maelezo ya Mngeni yalitolewa kabla hata Shrien hajawa mmoja kati ya watuhumiwa katika upangaji wa mauaji hayo, lakini maelezo yao bado yanaendana.
Je inawezekana vipi Shrien akatae kuteremka atake ateremke na mkewe kama kweli alikuwa kapanga mauaji ya mkewe?
Shrien anateremka na kuachwa katikati ya kitongoji ambacho na maarufu kwa uahalifu wa kutumia bunduki, kwa amelezo yake anadai baada tu ya yeye kuteremka gari liliondolewa kwa kasi ya ajabu.
Kwa bahati nzuri anakutana na na mkazi wa eneo hilo ambaye ni mhasibu ajulikanaye kama Simbonile Natakazi ambaye anamuona Shrien akipiga kelele kama kicha analia na kukimbia ovyo.
Simbonile anadai alimpigia binamu yake simu ambaye ni askari polisi, anadai pia Shrien alikuwa hakai na alikuwa anapandwa hasira kwakuwa iliwachukua muda mrefu mpaka polisi kufika pale.
Simbonile anaendelea kusema siku zambele baada ya kusikia kuwa Shrien anatuhumiwa kwa kushiriki mauaji ya kupanga dhiodi ya mkewe, alishangaa kwa kuwa haamini kama kweli Shrien alishiriki katika mauaji ya mkewe kwa jinsi alivyokuwa kachanganyikiwa sana siku ile.
Saa 7 usiku
Baada ya kumtafuta Anni Dewan na utafutaji kutozaa matunda, polisi waliamua kumrudisha hotelini Cape Grace. Kamera za hoteli zinamnasa Shrien akiwa anapita peke yake kwenye korido ya hoteli akilia akiwa kama mwendawazimui, anaingia chumbani kwake na kutoka kila mara akiwa analia kama kapagawa na kuwafuata akiwafokea polisi waliokuwa kwenye chumba cha internet cha hoteli hiyo akiwauliza kwanini hawafanyi juhudi za kumtafuta mkewe bado wamekaa tu hapo.
Jambo la kushangaza Tongo naye alikuwa pale pale hotelini, na anadai alimsikia Shrien akiwa anawambia polisi kanini hawamtafuti mkewe na anadai ndipo kwa mara ya kwanza aligundua kumbe Shrien na Anni walikuwa wanandoa na kumbe Shrien alikuwa anataka mkewe ndiye auawe.
Inashangaza kuwa Tongo anadai kuwa hakujua kama Shrien na Anni walikuwa wanandoa japokuwa ni yeye aliyewatoa uwanja wa ndege, nay eye alikuwa akiwaendesha kwa tax yake muda wote. Ajabu kweli..
Mngeni anadai baada ya kumteremsha Shrien waliendela kuzunguka huku Anni akilia sana nyuma ya gari, anadai kuwa Qwabe alitaka kumnyanganya Anni pochi ambapo Anni ailing’ang’ania ndipo Qwabe aliegesha gari pembeni akateremka na kwenda mpaka kwenye dirisha la mlango wa nyuma akampiga risasi ya shingoni bahati mbaya wakati bato wakigombea ile pochi. Hivyo kwa maelezo ya Mngeni ni kwamba hawakuwa na lengo la kufanya mauaji ilikuwa tu wana lengo la kufanya wizi.
Anadai alimuuliza Qwabe kwanini umempiga risasi, Qwabe hakujibu.
Ila Qwabe anadai kwamba aliyempiga risasi Anni ni Mngeni na alimpiga akiwa amekaa siti ya mbele uoande wa abiria kama walivyokuwa wamekubarina mpango wa kumuua Anni ulikuwa umekamilika. Ila anadai wakati anampiga risasi yeye Qwabe ambaye ndiye alikuwa akiendesha gari hakutarajia maana hakumwambia wala kumpa ishara kuwa anamaliza kazi waliyotumwa.
Waliterekeza gari wakiwa wameuacha mwili wa Anni ukiwa umelala kwenye siti ya nyuma ya gari, wakaondoka na pochi ya Anni, simu zao, saa na bangiri za thamani pamoja na vito vingine vya thamani.
Polisi wanathamanisha kwamba vito walivyochukua vina thamani ya 8,600 pounds huku pete yake ya uchumba polisi waliikuta kaililia na pete yake ya ndoa yenye thamani ya Euro 25,000 akiwa kaificha kwenye mfuko wa kuifadhia vitu nyuma ya siti ya abiria ya mbele.
Swali la kujiuliza kama kweli hili lilikuwa tukio la mauaji lenye lengo lionekane kama wizi, kwanini hawakuchukua hizo pete maana zilikuwa na thamani mara sita zaidi ya vitu vingine walivyochukua.
Na kama kweli lengo ilikuwa ni tukio la mauaji, kwa maelezo ya Mngeni hawakuangalia kuhakikisha kama kweli Anni kafariki ila tu wao walichukua walichoweza wakaterekeza gari na kukimbia.
Polisi wa Afrika ya Kusini wanadai Ushahidi (Forensic evidence) unaonyesha kuwa kweli Anni alikuwa kaka siti ya nyuma akiwa ameegemea sit, na alipigwa risasi kutoka mbele upane wa abiria, huku aliyempiga akiwa kampiga kimakusudi mdomo wa bunduki ukiwa karibu ya shigo la Anne kati ya sentimita 5-10, hivyo wanadai kifo chake hakikuwa cha bahati mbaya.
Mtaalam wa Forensic Science, DR. Richard Shephered, alipitia ushaidi wote, nay eye anapingana na hoja ya polisi. Yeye anadai haiwezekani Anne apigwe risasi toka siti ya mbela ya abiria, pia anadai haiwezekani Anne awe kapigwa risasi makusudi kwakuwa mauaji ya makusudi mtu ulenga kichwani, au sehemu ya moyo kwakuwa ndizo sehemu amabzo mtu akipigwa muaji anakuwa na uhakika kuwa aliyempiga hawezi kupona na siyo shigoni.
Pia anadai kama kweli angekuwa amekaa kuegemea siti ya ngum, alipopigwa risasi kungekuwa na damu imeruka na kutapakaa sehemu alipokuwa kaegemea shingo lake kitu ambapo hakipo.
Yeye anadai Anni atakuwa alikuwa kaegemea mbele aidha kaegemea mapaja yake, akiunga mkono maelezo ya Mngeni kuwa Anni alikua akilia huku kakumbatia pochi yake amejikunja. Pia anadai au kama hakuwa kajikuja kwa kulalia mapaja yake basi alikuwa kaka kwenye kingo za siti yani hajaegemea nyuma bali kasogea sana mbele.
Inaendelea kwenye comment #10 na #17 na #35

Attachments
-
shren.jpg54.5 KB · Views: 152
-
anne.jpg19.4 KB · Views: 170
-
chitwa chitwa.jpg328.8 KB · Views: 138
-
tongo.jpg36.3 KB · Views: 169
-
grace.jpg247.9 KB · Views: 146
-
protea.jpg10 KB · Views: 141
-
mbondo.jpg25.8 KB · Views: 157
-
qwabe.jpg30.6 KB · Views: 164
-
father.jpg45 KB · Views: 148
-
mngeni.jpg5.6 KB · Views: 133
-
table.jpg30.6 KB · Views: 143
-
gun sign.jpg80.2 KB · Views: 152
-
leopold-560650.jpg32.7 KB · Views: 145
-
bar breakfast.jpg37.9 KB · Views: 147
-
jewwelers.jpg41.2 KB · Views: 140
-
mbondo cct v.jpg31.9 KB · Views: 141
-
last day shren and anne.jpg93.3 KB · Views: 155
-
guglethu.jpg246.8 KB · Views: 123