Spika Ndugai: Nitawalinda wabunge wa Viti Maalumu CHADEMA kwa nguvu zote, Mnyika akajifunze kwa Dkt. Bashiru kazi za Katibu Mkuu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,975
Spika Ndugai amesema kanuni za bunge zinamtaka kuwalinda wabunge walio wachache na maslahi yao naye atafanya hivyo kwa nguvu zake zote.

Ndugai amesema wabunge 19 wa CHADEMA wameteuliwa kihalali na kama CHADEMA wana matatizo nao walipaswa kuwaita kwa heshima na kuwasikiliza badala ya kuwahukumu na kuwafokea kupitia vyombo vya habari.

Spika Ndugai amesisitiza kuwa Mnyika bado hajakomaa kisiasa hivyo amemshauri aende kwa Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru akafundishwe namna Katibu mkuu anavyopaswa kutenda kazi zake kwa ufanisi.


Chanzo: TBC Aridhio

Maendeleo hayana vyama!

NOTE: Ilishadokezwa tangu juzi kuwa Ndugai ana mkakati huo > Ofisi ya Spika ‘kuwalinda’ wabunge wa Viti Maalum wa CHADEMA - Imevuja!
 
Spika wa bunge Job Ndugai amemtaka katibu mkuu wa CHADEMA akajifunze namna ya kuwa katibu mkuu kwa Bashiru Ally ambaye ni Katibu Mkuu wa CCM.

Ndugai amesema kitendo cha Mnyika kuwasema hadharani, kuwahukumu na kuwashutumu wabunge wa viti maalum kwenye vyombo vya habari inaonesha wazi Mnyika hafai kuwa Katibu Mkuu.

Ndugai ameshauri mambo kama hayo huongelewa kwenye vikao vya ndani na kisha katibu mkuu hutoka na taarifa za kikao na kuwaambia wananchi sio kupayuka hadharani.

Sambamba na hilo Ndugai amesema kwamba yeye majina hayo kumi na Tisa(19) ya viti maalumu ya CHADEMA amepewa na Tume ya uchaguzi yeye kazi yake ni kuwaapisha tu Wabunge hao na ameshafanya hivyo. Na ameapa kuwalinda Wabunge hao hivyo amewataka wawe na imani kabisa.

Source: TBC ARIDHIO.
 
Back
Top Bottom