Sophia Simba ambwaga Anne Kilango uenyekiti UWT

hongera sofia

wewe huna unafiki kama KILANGO.WOTE TU WACHAFU PAMOJA NA KILANGO SASA ANAJIFANYA YEYE YU MSAFI

SOFIA....USISAHAU AHADI YA UBUNGE VITI MAALUM NI MIAKA KUMI TUU WAONDOLEWE VING'ANG'ANIZI
usisahau "MSIMBAZI" umemwaidi bibi 2015 pia atapata ubunge wa viti maalum.
 
Nazungumza na jamaa yangu ndani ya uchaguzi wa UWT kwa kura zilizokwisha hesabiwa mama Sophia Simba anaelekea kuchukua ushindi, habari hii ni ya uhakika toka kwenye chumba cha kuhesabia kura, Anne Kilango anaponzwa na undumila kuwili wake mara anapinga ufisadi mara anametetea Ngereja , haeleweki, akina mama wamempa fundisho.

ningependa kujua vipi kuhusu mgombea wa Pasco aitwaye MayRose majinge Kavura ambaye pwana Pasco alimuanzishia thread maalum humu JF kumpamba??
 
Last edited by a moderator:
Urais wa tanzania haununuliwi, fedha anazotumia lowasa ina maana anautaka urais kuliko tunavyomtaka awe rais.
ingekuwa heri kama fedha zake angenunulia ng'ombe akagawane na wamasai wenzake ingempa sifa za ukweli, lakini nikutahadharishe Pasco, magogoni is not for sale!
Mkuu Jogi, pale palisha uzwa zamani, aliyepo is just a piper!, sasa wanasubiria tuu makabidhiano!. Kiukweli naona 2015 ni mbali sana, natamani hata kesho ndio ingekuwa 2015 ili nasi tuianze zamu yetu!.
 
Tatizo wanalalamika rushwa na taratibu mbovu katika uchaguzi ambao wanashiriki kwa hiari yao.......kwa nini wasijitoe kama taratibu mbovu?
Au kwanin wasiripoti hayo matukio ya rushwa wakati uchaguzi ukiendelea?? Why after fail ndo waje na mzigo wa lawama?
 
Nilifikiri CCM is dying?
na kwambayeyote ndani ya CCM hawezi kuwa tishio?

sasa mbona watu wako busy na Mwenyekiti wa UWT na sio BAWACHA?

au hii ni ishara ya CCM kuwa ni very strong?
Does BAWACHA still exist?!, tangu alipojiuzule yule M/Kiti ile 2010 (baada ya kutomteua mbunge wa kuteuliwa na badala yake watu wakateua watoto wao, dada zao, wake zao, wakwe zao, hadi vimada wao!,) nani ni M/Kiti sasa?.
 
ningependa kujua vipi kuhusu mgombea wa Pasco aitwaye MayRose majinge Kavura ambaye pwana Pasco alimuanzishia thread maalum humu JF kumpamba??
Huu ndio ulikuwa msimamo wangu kuhusu Uchaguzi wa UWT kwenye uzi wangu huu Uenyekiti wa UWT: Ni Vita Kati ya Ukweli na Ubatili!


quote_icon.png
By Pasco
Wanabodi,
Kipenga cha kugombea nafasi ya Uenyekiti wa UWT kimepulizwa na wa kwanza kukimbilia fomu ni Mwenyekiti wa sasa Mhe. Sofia Simba akijiaminisha atapata kwa mteremko wa kupita bila kupingwa maana CCM inatawaliwa na nidhamu ya woga kwa jina la "utii". Lakini hali haikuwa hivyo kwani Mhe. Mama Anne Kilango Malecela ametia timu kumpinga Mama Simba ambae "she is good for nothing"!. Mama Kilango ni just an opportunist mpiga kelele kila anapoongea as if ana uchungu wa kweli na anachopigia kelele!.

Ila kumlinganisha na mama Simba, Kilango ni mpiganaji wa kweli kwani baada ya kubebwa pale mwanzoni, sasa amejibeba na kubebeka zaidi wakati Simba yeye ni kubebwa tuu mwanzo mwisho!.

Leo kuna binti kijana, msomi wa haja ambaye yuko very bright upstairs kwa jina la Bi. Mayrose Kavura Majinge, naye atatupa karata yake!. Huyu ni "very promising" kuibadili UWT toka hapo ilipo na kuipaisha to the next level!.

Sasa subirini tushuhudie sarakasi za kama CCM inaendelea kuchagua "good for nothing" na kuisindikiza rasmi kaburini, au wana CCM wata opt for "oportunistic" ili kuendeleza ulaji na kupeana au this time watachagua "promising leadership" kujaribu kuiokoa CCM ambayo imeshaonyesha dalili zote za mkao wa kifo?!.

Kwa vile sio siri, its open secret kuwa members wengi wa jf ni washabiki wa CDM, wakiwa na matumaini kuwa 2015 its their time, wajue kuwa wapiga kura wengi zaidi Tanzania ni wanawake, I doubt kama BAWACHA does realy exist!, hivyo majaaliwa ya Chadema kushinda uchaguzi wa 2015, itategemea kura za wanawake hivyo ni nani anashinda uchaguzi wa UWT!. Akirudi Mama Simba au Mama Kilango, ushindi wa Chadema ni dhahiri, ila akishinda Mayrose Kavura!, amini msiamini, ikulu mtaishia kuisikia tuu!.
Mark my words!.

Pasco!.

NB. Kwa vile mimi namshabikia EL ateuliwe CCM, na kwa CDM naisupport move ya ZZK, bado nasisitiza sina chama!. Ila wale mnao amini mimi ni gamba, endeleeni kuamini hivyo kwa sababu kuwa mwana CCM sio dhambi wala kuishabikia CCM sio kosa!.



Uchaguzi umemalizika matokeo yametoka!, ubatili umeshinda!. Sasa tuendelee na mengine huku tukisubiria yatokanayo!.

P.​
 
Hao wote mama Kilango na mama Simba walikuwa hawafai. Lakini kwa vile suala la EL linazungumzwa kila mara penye chaguzi hizi za ndani ya CCM nirudie haya hapa:

Watz ni wavivu wa kufanya hata utafiti mdogo tu kama hii habari ya EL. Sikilizeni enyi msioona mbali:-


1. Kwamba EL si msafi halipingiki. Nape yuko sahihi kusema hivyo lakini pia ni kichekesho kuwa yeye na Katibu Mkuu walipiga 'U turn' ya ajabu kukana ultimatum ya zile siku 90 ambazo EL na wenzake walipaswa kujiengua wenyewe kusafisha chama. Nape na wenzake wamezidiwa kete na kuonekana chochote wanachokiongea sasa kuwa hakina ukweli kwa sababu it is ironically useme mtu si msafi na kweye CC mumpitishe hadi kugombea uNEC na hakuna mahala mmemjadili na kumchukulia hatua kichama. Hayo yataonekana kuwa majungu.

2. Utafiti wangu unanionyesha kuwa EL kamwe hataweza kupitishwa jina lake kuwa mgombea maana CCM si wajinga mnavyodhani. Kwa sasa, jina lake linatumika ili msiwafikirie wenzake ambao hamuwasemi na katika hao atatajwa mmoja na ndipo mtashangilia (mazingaombwe ya Mwanakijiji) kuwa EL amekomolewa kumbe ndivyo ilivyopangwa. Ni hivi EL hana ugomvi na Rais Kikwete wala Membe wala Migiro. Na hata siku moja hutamsikia Rais wetu wala Membe akisema hayo wazi wazi. Hawa wako pamoja sana na ndio maana ya kuwa na mikakati ya muda mrefu na ambayo huwezi kuipredict kiurahisi kama wenzetu wa CHADEMA wanavyotake political risks bila kuzichambua.

3. EL yeye hana shida ataendelea kula pension kama Ex-Premier na atakuwa ndani ya NEC, ndani ya CC na Mbuge wa huko kwao kwa hivyo yuko safe & liquid kona zote. Na atakuwa Mweyekiti Kamati ya Bunge na Bodi zenye mashiko ya posho, haitaji Urais. Sana sana wakiona hata mmepumbazika kwa kumhurumia eti jina lake kutopitishwa kwenye Urais basi Rais ajaye kwa kuwa ni mtu wake anampa uWaziri wa nguvu basi mnabaki kung'ang'aa macho kuwa kaonewa kumbe ndivyo ilipangwa!

4. Kosa kubwa linalofanywa na upizani ni hili.
Kwanza hamko wamoja kwa hiyo hata kwenye fair ground ikipigwa kura leo wale wasioipenda CCM wanagawanyika kati ya CHADEMA, CUF, NCCR n.k wakati wapenzi wa CCM wao watafia hapo hapo hasa WATAKAPOONA KUWA JINA LA ANAYEPEPERUSHA BENDERA YAO SI Mh. E. LOWASSA ALIYEWAUMIZA WENGI KWENYE CHAGUZI ZA NDANI BALI NI MWINGINE MSAFI ( MIGIRO, MAGUFURI, MEMBE etc) jambo ambalo si kwa sababu za mnyukano bali mpango wa muda mrefu.

Pili uchaguzi wa kumpata rais ni wa nchi yote kila kitongoji na si maeneo machache tu ya nchi. Uchaguzi Mkuu ni zaidi ya political rally za M4C mkoa fulani au kanda fulani. Unahitajika kuwa na watu wengi kila kitongoji nchi nzima ambao wanaushawishi kwa wengine na pia kuwasimamisha wagombea Ubunge kote nchini kila kitongoji kama wafanyavyo CCM. Sasa angalia CCM imepanua wigo wa ujumbe wa NEC toka mkoa hadi kila wilaya TZ nzima na hao wanaochaguliwa wanaushawishi fulani wa ama kiuiwezo au hata kifedha na pia wana marafiki wao na ndugu zao ambo ndio watawapigia debe CCM (Kimya kimya au kwa uwazi). Chaguzi za CCM Mikoani na za Jumuiya zake UVCCM, Wazazi na UWT ni mtandao tosha ambao unafanya hata CHADEMA na CUF humu wanajadili habari za mama Simba vs mama Malecela bila kujijua mpaka wanasahahu kuwa kuwa BAWACHA au baraza la wanawake wa CUF n.k.

Swali ni kuwa mbona hatuoni maandalizi ya namna hii ya mfumo wa kutafuta wawakilishi wa jumuiya za vyama vingine vya upinzani katika mtandao mpana kama huu wa CCM Tanzania nzima (haijalishi kuwa hata kama wa CCM pia una mapungufu lakini unaibua ushindani mkubwa sana).

5. Sikiliza CHADEMA, hakuna ubishi Dr. Slaa ni jembe na anapendwa lakini uchaguzi ni maandalizi ya kuwa na mtandao wa kupata watu wengi (Bara na Visiwani) wawakilishi watakaomsaidia nchi yote kuwashawishi watu wengine waone kuwa kweli huyu akipewa kuongoza nchi kama Rais basi si kwamba itakuwa yake na kakundi kake kadogo kwa Mbowe, Lissu, Mnyika, Mdee bali kwamba kuna watu wengi kila kitindoji Tz yote wenye uwezo kuendesha Wizara zote na Mikoa yote bila kutikisika.

6. Mwisho, ni bayana pia kuwa hata thread za Zitto na mikwara mbuzi yake ya kuutaka Urais ni kanya boya akitegemea kuzua tafrani CHADEMA maana anatumika. Tunashukuru kuwa hilo limejulika kwa wengi sasa maana amepwaya na ataishia kuwa looser tu kwa kuwatumikia mabwana wawili na kamwe hatasimamishwa na CCM (hata akihama leo CHADEMA) kuwa mgombea na wala hakuna mgombea binafsi anayeweza kupita kuwa rais leo Tanzania; demokrasia yetu haijafikia hatua hiyo hata Marekani bado!

EL si mgombea urais, anawaandalia watu wake makao ili naye aendelee kufurahia utukufu wa mtandao wake. WaTz hatupendi kujishughulisha na kuchambua kwa undani mambo ya juzi na kesho bali ya leo tu!!!

Mfano, leo Mh. ShyR Banji ametaka kutwangana na Mh. mama Simba kwenye uchaguzi wa UWT. Hivyo atakuwa na hasira naye na pia EL kwamba ndiye alikuwa sponsor wa mama Simba lakini kesho atasimamishwa mama Rose Migiro, msomi na hana tuhuma na Banji atakuwa wa kwanza kumpigia hata kampeni Tz yote kwa jina la kumkomoa EL hahahahahahahahahah!!!

Sitaki kusikia mtu akilialia baada ya uchaguzi mkuu (2015) kuwa tumeibiwa kura!!!! Mtu anajiibia kura yeye mwenyewe kuanzia sasa kutegemeana na mfumo wa maandalizi yake.

Ombudsman, niko huru na niko tayari kutoa msaada wa kweli kwa ajili ya maendeleo ya nchi yangu Tanzania.
 
Pasco!.

NB. Kwa vile mimi namshabikia EL ateuliwe CCM, na kwa CDM naisupport move ya ZZK, bado nasisitiza sina chama!. Ila wale mnao amini mimi ni gamba, endeleeni kuamini hivyo kwa sababu kuwa mwana CCM sio dhambi wala kuishabikia CCM sio kosa!.



Uchaguzi umemalizika matokeo yametoka!, ubatili umeshinda!. Sasa tuendelee na mengine huku tukisubiria yatokanayo!.
P.​
Pasco, tangu siku ulipotoa posti thread hii nilikwambia namjua vema sana huyu uliyemuita msomi na mtu stahiki UWT Mayrose. Nilikwambia namjua fika ni dhaifu kupindukia. Ningeshangaa kama hata angekuwa wa pili. Kwa wagombea waliokuwepo wote watatu, hakukuwa na mtu muafaka kwa wanawake wa Tanzania, vyote ni vinyago vilivyokuwa vnachongwa tu na hatimaye kinyago kizuri kimevishinda vingine.

Lakini kwakuwa Mshindi Sofia simba yuko katika kambi yako ya EL, naomba nikupe hongera kwa niaba yake. Mnajiandaa vema kwa 2015
 
Last edited by a moderator:
Hapa tuko pamoja, sasa Le Mutuz atafute gia nyingine ya kutongozea badala ya kuwadanganya kwamba atawaombea kwa Mama yake nafasi ya viti maalum.

Nasikia Le M, kaamua kuachana na siasa uchurwa na kuanzisha biashara ya mitumba.....LOL
 
"tunajiandaa kupanga safu kwa ajili ya ushindi wa 2015"JK katika kikao cha nec walipokuwa wakipitisha majina.

pamoja na kuwa sehemu nyingi washindi wamekuwa wakipata ushindi wa kishindo binafsi najiuliza jinsi safu iliyopangwa ilvyolalia kwenye kambi ya mtu mmoja,hii inatoa nafasi ya hata asipogombea uchaguzi 2015 ila kufanya awe na maamuzi makubwa zaidi. lakini pia ni kutengeneza visasi visivyo na msingi hasa kwa matabaka yale yasiyo na nguvu ya pesa ambao itawagharimu miaka mingi au kumalizika kwa utawala wa mtu fulani ili wao kushika hatamu.
 
Kilichombeba sofia simba tofauti na wengi mnavyodhani kwamba ni lowassa ukweli ni idea yake ya kutaka kuwepo na ukomo wa kina mama kuingia bungeni through viti maalum,kumbukeni kuna akina mama wanasiasa wapya wengi ambao wameifurahia hiyo idea kwa kuwa itawapa nafasi na wao kuingia mjengoni wakati wale wazoefu watakapolazimishwa na kanuni kuachia nafasi za viti maalum na kwenda kugombea majimboni kwa kuwa wameshakomaa.Issue yenyewe ilianzia hapa na kumpatia umaarufu mkubwa da soffy miongoni mwa wapiga kura ambao jana walimzomea shyrose bhanji

Raia Mwema: Halmashuru Kuu ya CCM imekubaliana na pendekezo la Baraza Kuu lako juu ya ukomo wa viti maalumu, lakini baadhi ya wabunge waliopita wa muda mrefu ambao wanadhani mlikuwa nao, wanadai umewatosa. Hayo manung'uniko yao wewe unayajibuje?

Mama Sophia Simba:
Nafurahi kupata nafasi hii nijibu hilo. Suala la ukomo wa viti maalumu halikuanza na mimi. Suala la ukomo wa vitu maalumu tumeanza kulizungumzia mwaka 1998 au 1999. Lakini kwa sababu sisi wenyewe tuko mle mle kwenye baraza Kuu, likaminywa.
Likarudi tena 2000 hadi 2005. Likazungumzwa tukiwa Arusha, likazungumzwa tukiwa Moshi. Watu wanalipooza kwa sababu kila binadamu tuna kitu kinaitwa choyo, unajifikiria wewe. Kwa hiyo, lile jambo ni jambo la siku nyingi. Hao wote wanaolalamika wanalijua, wanaiongopea jamii.
Suala la ukomo halikuletwa na Sophia Simba, suala la ukomo lililetwa na Baraza Kuu, isipokuwa kwenda kwenye NEC ndiyo limepelekwa safari hii.
Tatizo ni kwamba siku zile tulikuwa tunalizungumza kwenye Baraza Kuu lakini halitoki kwenda NEC. Hivi sasa limekwenda kwenye NEC, na kwa bahati mbaya sana hao wanaolalamika wengine wameshakuwa wabunge miaka 15, wengine miaka 10.
Baraza Kuu lilisema kuwa nafasi za vitu maalumu ambazo ni za upendeleo, siyo wapendelewe hao hao tu kila siku. Ziliwekwa ili kumuwezesha mwanamke aweze kupambana na vile vigezo ambavyo tumesema vinatufanya wanawake tushindwe kuingia kwenye majimbo nao kwa sababu ya kuwapo mfumo dume.
Tumesema wanawake kwa sababu ya mfumo dume tuna aibu, hatuwezi kuongea kwenye majukwaa. Kwa sababu ya mfumo dume wanatutukana (eti) tunaogopa lakini tunasema pia kwamba mwanamke hana pesa za kwenda kwenye kampeni.
Sasa Baraza Kuu linasema huyu mwanamke au mama baada ya miaka kumi amekaa bungeni amekwenda kwenye mikutano, ana pesa anashindwa nini? Aende zake kwenye jimbo.
Hiyo ndiyo concept tuliyozungumza kwamba tayari ile kazi ya upendeleo imeshafanya kazi. Imeshamtengeneza huyu mwanamke kuwa mwanasiasa.
Sisi shida yetu tunakata tuwe na wanawake wanasiasa wengi. Sasa hawa wanakuwa kama selfish, wanaona wao. Kuna mwingine anathubutu anasema ‘he mimi kule kwangu nikitoka mimi, sina jimbo kule. Lakini kama huna jimbo wewe ukitoka mwanamke mwingine atachukua nafasi yako, kaa pembeni.
Kwa hiyo mimi wananionea kusema kwamba nimewacha kwenye mataa. Na hao kwanza waliokaa wanaosema kwamba nimewatosa, mimi UWT nimechaguliwa na wanawake wa Tanzania yote.
Na nimechaguliwa; hivyo siyo kazi yangu kulipa fadhila. Nimechaguliwa niwahudumie wanawake wa Tanzania na kwa kufanya hivyo, kwa kuweka ukomo baada ya miaka kumi tutaona majimbo mangapi wanawake watachukua.
Watajitokeza tu, sisi wanawake tunapenda sana kusukumwa. Sasa nenda hapa, sasa nenda pale. Mama Anna Abdallah aliweza mwaka 2005 kutusukuma. Aliniambia Sophia nenda Ilala, wewe fulani nenda pale.
Isitoshe siku hiyo kwenye Baraza Kuu ajenda ya kuwe na ukomo haikutoka kwenye kamati yangu ya utekelezaji, ilitoka pale pale barazani.
Hilo ndilo lililotokea kwa hiyo kina mama popote walipo naomba wasilichukulie hilo kama ni langu binafsi isipokuwa hofu ya wale wanaotaka waendelee na wasiotaka wenzao wengine wapata hizo nafasi ndiyo iliyofanya waende wakapeleke hadithi hizo.
Lakini siku moja wataniona shujaa. Kwa suala hili kulipeleka kwenye NEC ilikuwa kazi kubwa, lakini imewezekana. Hata hivyo, NEC imesema lisianze mwaka 2010, litaanza mwaka 2015. Mwaka 2015 ni keshokutwa tu panapo na uhai. Kwa hiyo tutaona sura mpya zinaingia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom