Pasco, tangu siku ulipotoa posti thread hii nilikwambia namjua vema sana huyu uliyemuita msomi na mtu stahiki UWT Mayrose. Nilikwambia namjua fika ni dhaifu kupindukia. Ningeshangaa kama hata angekuwa wa pili. Kwa wagombea waliokuwepo wote watatu, hakukuwa na mtu muafaka kwa wanawake wa Tanzania, vyote ni vinyago vilivyokuwa vnachongwa tu na hatimaye kinyago kizuri kimevishinda vingine.
Lakini kwakuwa Mshindi Sofia simba yuko katika kambi yako ya EL, naomba nikupe hongera kwa niaba yake. Mnajiandaa vema kwa 2015