barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi Sophia Simba,amesema kwa sasa hana mpango tena wa kugombea uongozi ktk jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi wa mwaka 2017.
Bi Sophia Simba anasema kwa sasa ameamua kukaa kando na kuwaachia wengine ili waweze kuendeleza gurudumu la umoja huo wa kina mama,huku yeye akiwa pembeni kuhakikisha anakuwa msaada kwa jumuiya hiyo kukisaidia chama kushika dola.
Anasema ni muda sasa wa kuwaachia watu wengine kuleta changamoto ktk jumuiya na kuipeleka mbele jumuiya hiyo kufikia malengo ya chama.Mama Sophia Simba anasema "kila zama na kitabu chake",hivyo kwake anaona zama zake na kitabu chake kimekwisha pita.
Itakumbukwa kuwa katika uchaguzi uliopita,Sophia Simba hakumuunga mkono JPM katika harakati za kutafuta mgombea ndani ya chama.Akiwa na wajumbe wenzake Dr Nchimbi na Kimbisa,walitoka ukumbini huku wakimshutumu Mwenyekiti wa chama kwenda na majina yake "mfukoni".
Hata mara baada ya uchaguzi Mkuu,Sophia Simba amepotea kabisa ktk siasa za nchi,kwenye majukwaa na bungeni.Hata zile nafasi ktk baraza la Mawaziri ambazo hapo awali zilitolewa kwa kutazama uwakilishi wa jumuiya za chama kama UVCCM,Umoja wa Wazazi na UWT,safari hii UWT ya Sophia Simba ambayo ilikuwa kama "tawi" la Lowassa imechinjiwa mbali.
Kwa tamko hili la Simba,ni kama namuona Mama Anne Kilango Malecela akipiga jaramba,mara baada ya uchaguzi wa 2012 kushindwa dhidi ya Sophia Simba.Tutegemee kampeni za chini kwa chini za nafasi ya Sophia Simba kwa akina Mama wa CCM.Bila shaka ktk kuelekea 2020,JPM lazima atahakikisha nafasi hii anakaa "mtu" wake.Ili yasitokee yale ya 2015 pale White House-Dodoma.