Sophia Simba ambwaga Anne Kilango uenyekiti UWT

Eddo Lowassa hoyeee!

EL all the way!! Mie seriously nataka EL aje aongoze!! Nilishandika sana kwanini namkubali. Msiniulize wageni hapa JF
 
wapi Anna Kilango Malecela??. imekula kwako mama??. Huna uwezo wa kushindana na Lowassa. njoo CHADEMA tukomboe nchi yetu kutoka kwa wakoloni weusi CCM. mia


Mama yake William Malecela kaangukia Pua...
Hah hah hah hah hah hah hah haha Super
 
Mama Simba ni kambi ya JK. Ina maana kambi ya JK ndio kambi ya Lowassa?

Jibu ni ndio. Sasa njia nyeupeee!
 
Eddo Lowassa hoyeee!

EL all the way!! Mie seriously nataka EL aje aongoze!! Nilishandika sana kwanini namkubali. Msiniulize wageni hapa JF

Urais wa tanzania haununuliwi, fedha anazotumia lowasa ina maana anautaka urais kuliko tunavyomtaka awe rais.
ingekuwa heri kama fedha zake angenunulia ng'ombe akagawane na wamasai wenzake ingempa sifa za ukweli, lakini nikutahadharishe Pasco, magogoni is not for sale!
 
Last edited by a moderator:
umeona eeh!!?. nashangaa 2010 Alikua akitembea na cd eti amenasa maneno wakimuundia zengwe la kumuangusha kwenye anayo ita jimbo lake. wakamdharau. akajipendekeza kwa kikwete akimchongea wiliam kwamba akienda kwake anapewa chai badala ya umeme, cha ajabu ccm aliunda baraza hajampa hata unaibu waziri. sijajua matatizo ya huyu mama. ngoja aipate na sitaki kuskia akisema rushwa. mia

Ogopa sana watu wanaoongea kwa hisia kali na machungu bila kituo kikubwa na data za zisizoeleweka na huku wanapaza sauti juu kushinda wengine (hilo ndio tatizo lake, kwa maana nyingine ni wa...fiki)
 
Mama Simba ni kambi ya JK. Ina maana kambi ya JK ndio kambi ya Lowassa?

Jibu ni ndio. Sasa njia nyeupeee!

alaah mi nilijua anna kilango ni ngome ya JK maana hata huo ubunge alioupataga mara ya kwanza wa kuteuliwa mmh tulihisi mengi...alifanya kosa alipojiingiza kwa babu malecela..kaonyeshwa nini maana ya ccm, chama cha wenyewe....
 
Kidedea wapi!! Kahonga mahela kibao halafu anajiita mshindi
Sasa si ni kidedea wa kuhonga? Ndani ya CCM wote wahongaji ila Sophia Simba kamshinda Anne Kilango baada ya kuhonga zaidi. Lowassa anazidi kupeta
 
mara zote ukisikia nani kashinda jiulize yupo kundi lipi ? hivyo hilo kundi lina nguvu
 
Kama ni hivyo heri mama simba apeperushe hiyo bendera ya wamama wa magamba, maana kilango hana msimamo. Hongera mama lioness.
 
kweli umenikumbusha! Mama sofia lion yuko kwenye kambi ya ma-mvi dam dam. Nakumbuka alivyokuwa anamsafisha.

kweli kaka lakini naomba heshima na adabu kwa sababu unatakiwa kujali sana kuwa mimi yanga na leo tumepiga 3, so hii lion hapa.........dadadiditeh

ni utani broda! EL kapanga safu yake wima kwa 2015. Hana mchezo hata Sumaye analijua hili.
 
kweli kaka lakini naomba heshima na adabu kwa sababu unatakiwa kujali sana kuwa mimi yanga na leo tumepiga 3, so hii lion hapa.........dadadiditeh

ni utani broda! El kapanga safu yake wima kwa 2015. Hana mchezo hata sumaye analijua hili.

aitishe press conference kama sumaye.
 
tunakutakiwa mafanikio mema kujenga chama chetu imara..wanawake ndio wapiga kula endelea kujenga chama hadi vijiji tena
Uchaguzi Mkuu UWT-CCM: Shy-Rose Bhanji imebidi wamtulize la sivyo...

20/10/2012

Inaelezwa kuwa katika uchaguzi huo, Sophia Simba ametetea kiti chake cha uongozi cha Uenyekiti wa UWT.

975317287.jpg
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UWT, wakiwasili mjini Dodoma kwa uchaguzi unaofanyika Jumamosi Oktoba 20, 2012 (picha, maelezo: K-VIS blog)


534807487.jpg
Makamu wa Rais, Dkt. Ali Mohammed Shein, (Kulia), Makamu wa Mwenyekiti wa CCM, (Bara), Pius Mekwa, (Kushoto), na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake, UWT, Sophia Simba, mwanzoni mwa kikao cha uchaguzi cha Jumuiya hiyo, mjini Dodoma, Jumamosi Oktoba 20, 2012


816575763.jpg
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake ya CCM, (UWT), ambaye anamaliza muda wake, Sophia Simba, akiingia ukumbi wa Mipango tayari kwa uchaguzi mkuu wa Jumuiya hiyo mjini Dodoma, Jumamosi Oktoba 20, 2012


508814281.jpg
Shy-Rose Bhanji, (Kulia), akionyesha uso wa hasira huku akitulizwa na mjumbe mwenzake, kufuatia tafrani kati yake na mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania UWT), Sophia Simba


670119287.jpg
Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji, (Aliyekaa), akitulizwa hasira na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwkezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu, wakati wa kikao cha uchaguzi mkuu wa Jumuiya ya Wanawake ya CCM, UWT, kwenye ukumbi wa chuo cha Mipango Dodoma Jumamosi Oktoba 20, 2012. Taarifa zinasema, mbunge huyo alipandwa na hasira kufuatia majibu yaliyoelekea ya kudhalilisha kutoka kwa mwenyekiti anayemaliza muda wake wa jumuiya hiyo, Sophia Simba, wakati akijinadi na kuulizwa maswali na wajumbe kabla ya uchaguzi kuanza. Sophia Simba ambaye ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela


854833065.jpg

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom